Spika Amuonya Waziri Mkuu Bungeni

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Spika wa Bunge la Jamhuri Mh. Anna Makinda amemtaka Waziri Mkuu kutoongea na wabunge pamoja na mawaziri wakati kikao kinaendelea ndani ya bunge. Spika amesema kwa kuwa Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anapaswa kusikiliza na kufuatilia mijadala kwa makini. Amesema kama hali hiyo inaendelea hakuna maana kuwa na kiongozi wa wa shughuli za serikali bungeni.

Katika siku za hivi karibuni wabunge na mawaziri wamekuwa na tabia ya kwenda kunong'ona na waziri mkuu wakati kikao cha bunge kinaendelea. Hata hivyo wakati Spika anatoa onyo hilo, Mh. Mkulo alikuwa anaongea na Waziri mkuu na baadaye Mh. Wasirra akajisogeza na kuanza kuongea na Mh. Pinda.
 
Pinda ni waziri mkuu kimeo kuliko wote waliotokea tanzania
Asikilize nini wakati hatumii ubongo kuchambua???
bora asafiri nje ya nchi amwachie mnafiki Sitta usukani atukane tena
 
Tatizo huwa wanakuja bungeni wakiwa hawajajiandaa. Hivyo huwa wanashauriana na kutunga uongo upi wautoe kwa wakati huo kuwahadaa watz. Ndiyo zao hizo vilaza wakubwa!!
 
Spika wa Bunge la Jamhuri Mh. Anna Makinda amemtaka Waziri Mkuu kutoongea na wabunge pamoja na mawaziri wakati kikao kinaendelea ndani ya bunge. Spika amesema kwa kuwa Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anapaswa kusikiliza na kufuatilia mijadala kwa makini. Amesema kama hali hiyo inaendelea hakuna maana kuwa na kiongozi wa wa shughuli za serikali bungeni.

Katika siku za hivi karibuni wabunge na mawaziri wamekuwa na tabia ya kwenda kunong'ona na waziri mkuu wakati kikao cha bunge kinaendelea. Hata hivyo wakati Spika anatoa onyo hilo, Mh. Mkulo alikuwa anaongea na Waziri mkuu na baadaye Mh. Wasirra akajisogeza na kuanza kuongea na Mh. Pinda.
dalili ya serikali kupwaya.
 
Makinda ameanza kubadilika. Amesoma mood ya watu. Bora yeye kuliko kilaza Job Ndu...
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hapo mama amenena ukweli. Bungeni ni sehemu ya kusikiliza mijadala ila kwa hivi karibuni wabunge wa kawaida na mawaziri wameanzisha kamtindo ka kwenda kupiga soga na PM sijui kwa manufaa ya nani. Huenda wanamhujumu PM hadi anashindwa kufuatilia mijadala kwa makini na mwisho wake kuishia kutoa kauli tata.
 
Pinda ni waziri mkuu kimeo kuliko wote waliotokea tanzania
Asikilize nini wakati hatumii ubongo kuchambua???
bora asafiri nje ya nchi amwachie mnafiki Sitta usukani atukane tena

Mkuu sijui kama Pinda atamuachia tena 6 uwaziri mkuu. 6 naye si haba anaweza akang'ang'ania u PM!!
 
Makinda ameanza kubadilika. Amesoma mood ya watu. Bora yeye kuliko kilaza Job Ndu...

Ameshawashtukia hawa wakubwa hawabebeki, mbeleko inakaribia kukatika hivyo ama atue mzigo au aache mbeleko ikatike.
 
yule mwanamke haleweki kabisa.....kesho utakasikia kamekuja kivingine
 
Hapo mama amenena ukweli. Bungeni ni sehemu ya kusikiliza mijadala ila kwa hivi karibuni wabunge wa kawaida na mawaziri wameanzisha kamtindo ka kwenda kupiga soga na PM sijui kwa manufaa ya nani. Huenda wanamhujumu PM hadi anashindwa kufuatilia mijadala kwa makini na mwisho wake kuishia kutoa kauli tata.
inawezekana huwa wanaenda kudai bahasha nasikia bungeni linaongazoa kwa kugawa bahasha....
 
Mmmh!! kwa onyo hilo, inaweza ikachukuliwa kama kigezo cha mwanamke kuweza kuwa rais 2015.

na kuwakemea mafisadi na hata kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.

Good trial.
 
Back
Top Bottom