Spika amtwisha Zitto Kabwe zigo la UDA

Nadhani jamaa wamepatia sana kumkabidhi Zitto jukumu la kuongoza uchunguzi wa UDA natumaini atatutendea haki watz kwa kuweka ukweli na uwazi
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

9/08/2011
BUNGE KUCHUNGUZA UFISADI UDA

Ndugu Wanahabari, Suala la Ubinafsishaji wa Shirika la UDA limeibua hisia kali miongoni mwa Wabunge, vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla. Suala hili limekuwa tata na kuzusha kila aina ya maneno. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma imeona ipo haja ya msingi ya suala hili kuchunguzwa kwa kina na mhimili wa Bunge.

Kwa hiyo, imemuandikia barua Spika wa Bunge, ikimuomba aridhie mapendekezo ya wabunge watakaoundakamati ndogo ya Bunge chini ya Kamati hii ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, ili ichunguze sakata zima la uuzwaji wa Shirika la UDA.

Uchunguzi huu umependekezwa kufuatia hisia kwamba taratibu za kuuza Shirika hili pamoja na mali zake hazikuzingatia Sheria za nchi na hivyo kupelekea Taifa kuwa katika hatari ya kupoteza mali.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Toleo la mwaka 2007, nyongeza ya sita kifungu cha 13(e), Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ina jukumu la kufuatilia ‘Utekelezaji wa Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma' na kanuni ya 13(d) ‘kufanya tathmini ya ufanisi wa Mashirika ya Umma'. Ili kutekeleza majukumu haya, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma imemuomba Mhe. Spika aridhie kuundwa kwa kamati ndogo ili kufanya uchunguzi wa suala la Shirika la UDA.

Hadidu Rejea

Hadidu rejea za Kamati ndogo ya uchunguzi inayopendekezwa ni kama ifuatavyo:

i.
Kuchunguza kama katika zoezi la kubinafsisha Shirika la UDA taratibu zote za Sheria zilifuatwa.

ii.
Kuchunguza kama Ofisi ya Msajili wa Hazina na Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) walitimiza wajibu wao ipasavyo katika zoezi zima la ubinafsishaji wa Shirika la UDA.

iii.
Kuchunguza kama Bodi ya Shirika la UDA ilifuata sheria na kanuni katika kuuza hisa zilizouzwa za Shirika la UDA na kama walikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo bila kuhusisha wana hisa. Pia kuchunguza nafasi ya Bodi kwa umoja wake na mjumbe mmoja mmoja wa Bodi katika zoezi zima husika.

iv.
Kuchunguza nafasi (role) ya wana hisa (Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali) katika zoezi zima la kuuzwa kwa hisa (unalloted shares) za UDA kwa Kampuni ya Simon Group.

v.
Kuwaita mbele ya Kamati wadau wote wa suala la UDA hususani Bodi ya UDA iliyokuwepo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UDA, Mmiliki wa Kampuni ya Simon Group ltd, Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mkuu wa CHC, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na mtu mwingine yeyote yule itakavyoonekana inafaa.
vi. Kufanya tathmini ya Shirika la UDA katika mazingira ya sasa ya biashara ya usafirishaji Jijini Dar es Salaam.

vii.
Kutoa Mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya watakaobainika kuwa na makosa katika zoezi zima la Ubinafsishaji wa Shirika la UDA.

viii.
Kupendekeza namna bora ya kuendesha Shirika la UDA.

Ukomo
Kwa kuwa mamlaka nyingine za Uchunguzi zinaendelea na uchunguzi wake, Kamati hiyo ya Bunge itajikita katika maeneo yaliyoainishwa hapo juu tu na haitahusika na suala kama la rushwa au Mahesabu ambayo yanashughulikiwa na TAKUKURU na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Isipokuwa Kamati inaweza kuhitaji msaada wa Taasisi hizi katika kutimiza wajibu wake wa uchunguzi wa kibunge. Bunge, kwa namna yoyote ile, halitazuiwa kuendelea na uchunguzi wake wakati Serikali (Executive) ikitimiza wajibu wake. Izingatiwe kuwa uchunguzi huu pia unahusisha Taasisi za Serikali zenye mamlaka ya masuala ya Ubinafsishaji na utunzaji wa Mali ya Umma (hivyo Serikali pia inachunguzwa).

Muda wa Uchunguzi

Nimependekeza kuwa uchunguzi huu uchukue jumla ya Siku 14 (kumi na nne tu) na kuwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na kisha kwa Spika ambaye ataelekeza hatua zitakazofuatia.

Wajumbe wa Kamati Ndogo ya Uchunguzi.

Kwa kuwa Uchunguzi huu unahusisha mambo mengi, nimependekeza kamati hiyo ndogo ihusishe Wabunge wengine katika uchunguzi huu badala ya wajumbe wa Kamati ya Mashirika ya Umma peke yake.

Wajumbe wafuatao wanapendekezwa kuunda Kamati ndogo.

1.
Mhe. Murtaza Mangungu, Kilwa Kaskazini (Kamati ya POAC) – Mwenyekiti

2.
Mhe. Esther Bulaya, Viti Maalum (Kamati ya POAC)

3.
Mhe. Amina Mwidau, Viti Maalumu (Kamati ya POAC)

4.
Mhe. David Kafulila, Kigoma Kusini (Kamati ya LAAC)

5.
Mhe. Angellah Kairuki, Viti Maalumu (Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala)

6.
Mhe. Herbert Mtangi, Muheza (Kamati ya Miundombinu)

7.
Mhe. John Mnyika, Ubungo (Mwakilishi Wabunge wa Dar es Salaam)
Katibu wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma na Katibu wa Kamati ya Sheria ndogo wanapendekezwa kuwa Makatibu wa Kamati ndogo ya

Uchunguzi wa Ubinafsishaji wa Shirika la UDA.
Ni matarajio yangu na ya wenzangu kuwa Spika wa Bunge, Mhe.Anne Makinda ataridhia kuundwa kwa Kamati hiyo, ili Bunge liweze kuchukua wajibu wake
wa kiuchunguzi na wa kuisimamia Serikali.

Ninaamini, uchunguzi huo ndio utakaokata mzizi wa fitina kuhusu nani amehusika na achukuliwe hatua gani zichukuliwe kwa maslahi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Taifa zima kwa ujumla.

Nashukuru kwa kunisikiliza.


Kabwe Zuberi Zitto (Mbunge)

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma
 
Safi sana wakombozi wa Tanzania, hakuna njia nyingine ya kuwaonyesha wezi kuwa wameshagunduliwa jinsi wanavyotafuna nchi.Heko ndugu zetu wa Washington DC.
 
Sikubaliani sana na huu utaratibu wa mamlaka nyingi kufanya uchunguzi wa kitu kimoja kwa wakati mmoja

Labda watasema CAG na PCCB Watafanya hii kazi kama sehemu ya kazi yao ya kila siku,kwa hyio hawatalipwa cha ziada

Lakini hadidu za rejea ya kamati ya bunge zimetulia
 
Nchi inyoendeshwa kwa Kamati. Hivi hakuna njia nyingine ya kuchukua maamuzi dhidi ya watuhumiwa mpaka ziundwe kamati?? Hivi kamati kama hiii itatumia mamilioni mangapi kuchunguza kashfa hii??

Mbona enzi za Mwalimu tulikuwa hatusikii kamati za bunge kuchunguza tuhuma zozote na maamuzi yalikuwa yakichukuliwa tu?? Huu ni uoga wa viongozi kuchukua maamuzi kwa walio chini yao, ni kuogopa kuwajibika. Nini kazi ya serikali??
 
Kwa nini hawakumpa Uenyekiti Mnyika ambaye analifahamu hili swala la UDA vizuri na ndiye aliyeibua mjadala bungeni? Baadhi ya majina kwenye hii list sina uhakika nayo - too friendly na watuhumiwa!
 
kamati hizi zinamanufaa gani, kila siku kamati, kama zilishindwa kumwondoa JAIRo basi nifeki
 
Jamani HIVI ZIMESHAUNDWA KAMAT NGAPI NA BUNGE?????MNAIKUMBUKA YA MWAKYEMBE???6 AKAIZIMA NA HOJA ZAKE,MNAIKUMBUKA ILIYOENDA KUDAI CHENJI ZA BAE'???,SIJASIKIA KAMA ZIMEKUJA,HATA HII HAITAKUWA NA TIJA,PESA ZETU ZINAKWISHA JAMAN,AAARGGGGH
 
Zitto,

Ni vyema haya mambo mnayoandika muweke na bajeti pia... Ahsante sana kwa kazi nzuri... my next President.
 
Mh. Zitto,
Kwanza pongezi nyingi zikufikie pamoja na kamati yako kwa kupewa jukumu hili na nina hakika kazi mtaifanya maana hapa ndipo napokupendea.. Ila ningekuomba kitu kimoja tu ktk utekelezaji wa uchunguzi huu uufanye kwa njia ya uwazi zaidi na ningeshauri tu mfanye kama wanavyofanya huku majuu.

Kwanza ni kuwaita viongozi wote wanaohusika ktk kikao maalum cha bunge chini ya kamati yako kujibu maswali yote yanayoambatana na scvandal hii..Na na itolewe live ktk luninga.

Itasaidia zaidi kuanzisha utamaduni wa uwazi ktk vyombo vya bunge dhidi ya Ufisadi na hujuma zozote za uchumi wa nchi yetu kuonekana live ili kesho wasipate sababu ya kusema walionewa.
Ni ushauri wangu tu....
 
Katika hizo taasisi 1 - 5 ulizotaja ipi unaiamini/inaaminika na kwa kiwango gani?

Issue sio ipi inaaminika. Issue ni inaonyesha hatuaminiani Kwa nini taasisi 5 zichukunguze the same issue. umeona wapi hiyo?
 
Issue sio ipi inaaminika. Issue ni inaonyesha hatuaminiani Kwa nini taasisi 5 zichukunguze the same issue. umeona wapi hiyo?

Taasisi zingine zinajulikana ni geresha tu. Hii itasaidia baadae tusiambiwe vielelezo havikutosha kuwatia wahalifu hatiani. Ukumbuki tulisha ombwa vielelezo vya kumtia hatiani mtuhumiwa mmoja ambaye ubadhilifu wake upo wazi na wao walihusika kufanya uchunguzi? Tupime na hili sasa?
 
Mh. Zitto,

Umeibua la PPF lakini sasa umeifanya menejimenti ifukuze wale wanaodhaniwa kukupa taarifa za ufisadi na uizi wa mabilioni ya Group Endowment scheme. Sita wanaandaliwa kufukuzwa maana kwa sasa wamesimamishwa kazi bila ushahidi kamili.

Hii PPF inaenda wapi? Zitto mzigo wako, damu za wafanyakazi zitakulilia wakifukuzwa kwa kusingiziwa kukupa taarifa.

Tunasubiri tuone unavyowatetea au unavyoangalia wakiangamia bila makosa maana si wote na inawezekana chanzo chako sio wao lakini wametwishwa zito.




Hapo sasa mwenye kipele kapewa kucha! Kamati ya Zito ni ya mashirika ya umma likiwemo shirika la UDA. Kwahiyo kamati yake ndio ilistahili hasa kufanya huo uchunguzi na sio vinginevyo! Haya maoni kwamba wanadivert hoja yake ya meremete, Zito ndiye aliyeibua au Zito anapendwa na spika sio sahihi sana. Kamati ya Zito ndio inayokagua hesabu za mashirika ya umma na ndio maana amepewa hiyo kazi yeye kama M/kiti.
Tusubiri matokeo sasa maana kipele kimeshapata mkunaji!
 
Back
Top Bottom