Spika akalia kuti kavu

Kwani hawa wabunge wa Zanzibar ni wazamiaji ili wawahi kwenda kupiga mbizi na kuokoa watu au wanataka kwenda kuuza sura kwa wapiga kura wao?
 
Yule Mabumba wa Zanzibar naye alitoka nje? maana naye akikaa kwenye hicho kiti huwa haambilki, pengine sasa ameonja machungu ya uongozi wao wa kibabe.

Mimi wazenji siwapendi and everything about them
 
Akawii kusema hili sio suala la muungano au hatuwezi kujadili litaenda mahakamani kesho.....!!
 
Alichoharibu ni hapo kwenye RED...subiri watakuja kumjibu hapa.....

Poor Anna Makinda bila kufikiri akaota waliokufa ni wana CDM; CCM's nemesis!! kwa hiyo hakuna haja ya kuahirisha kikao cha bunge; it is business as usual si Chadema tu hao! salala! kalikoroga la ulanzi alinywe mwenyewe; wazenj wapole lakini sio vilaza kiasi hicho, kawabeep sasa wanapanga kumpigia.
 
Mnataka awe na uchungu kwani ameshawai kujifungua au kuwa na mtoto?

Kwa kauli yake ya jana inaonyesha jinsi alivyokuwa na roho mbaya, roho iliyokosa utu.

Pia, hata akalie ncha ya hilo 'kuti kavu', kwa mfumo wa kimagamba huyu bibi koroboto hawawezi kumng'oa uspika, tuhesaba tumeshalamba garasa, tusubiri 2015...

Kwani zenj, ni Tanganyika jamani alikuwa sahihi, kwa hili hakuna cha umagamba anastahili pongezi hata wao ingetokea Tanganyika wasingeahirisha baraza la wakilishi
 
From very early nilijua wazi huyu mama hana competency inayohitajika kuliongoza bunge hili la mikikimikiki...ni mara nyingi amekua akigonganisha mambo mpaka aandikiwe 'kibomu' cha ki-memo kuwa adese mwongozo upi ndio anakurupuka majestically na kuanza kufoka...niliamini na nitaendelea kuamini Mzee Sitta was one of the guys who deserve to run the house!
 
Alichoharibu ni hapo kwenye RED...subiri watakuja kumjibu hapa.....

Kaka, nakubaliana na wewe kabisa, hapo kwenye hiyo Red uliyo highlight, simuungi mkono kabisa mama Makinda kwa maamuzi yake mengi ambayo kwanza hua yupo so Bias, na ninadhani huwa anasubiri apewe SMS from a certein person, sijui nani? labda Ikulu, not sure but I am sure she is driven by remote with somebody!

Hapo kwenye hiyo RED ndo walipo haribu, kwanini watuchagulie spika watu wa Zanzibar? ina maana na wao ikitokea ajali yeyote huku Bara na wao huwa wanaahirisha Bunge huko kwao? hiyo point ni ni very poor kwenye kutoa hoja, kimsingi nimechukizwa nao, wanaonekana wapo Kizanzibari zaidi kuliko kitanzania zaidi, nani asiye jua waliopanda Boti hiyo wapo na wabara wengi tu, may be hata wazungu?
 
Huyu Anna Makinda siyo spika wa bunge bali ni spika wa serikali. Ndiyo picha ninayoipata kwa jinsi kiti cha spika kinavyotumika.
 
Mimi nina swali moja tu. Huo udhaifu wa spika ndiyo wanauona leo? Yani mambo mengine yote hovyo aliyo yafanya ambao yaliwakwaza wengine hawakuyaona leo ndiyo wanaona hafai kisa wamekwazika wao? Kwa wengine mkuki wa nguruwe leo ndiyi wameyasikia maumivu eh? Nawaonea huruma kwa sababu huyo mama hatatolewa hata wafanyaje.
 
Back
Top Bottom