Spika abariki mbunge Nkasi Ally Kessi kuikashifu CHADEMA

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,885
6,885
KATIKA hali ya kushangaza jana Spika wa Bunge Anna Makinda alimruhusu Mbunge wa Nkasi, Ally Kessi Mohamed (CCM), kusema kuwa angepata ubunge kwa tiketi ya CHADEMA ingekuwa kashfa kubwa kwake.
Mbunge huyo alisema hayo bungeni jana alipokuwa akichangia hoja kuhusu mjadala wa hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 10 Novemba mwaka jana.
Akizungumza awali alianza kwa kuwapongeza wapigakura wa Nkasi na kuweka bayana kwamba alikuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo kwa muda wote aliokuwa huko hakufanikiwa kupata ubunge hadi alipoingia CCM.
“Nawashukuru wapigakura wa jimbo langu la Nkasi kwa kunichagua mimi; nilikuwa mwana CHADEMA lakini sikufanikiwa kupata ubunge hadi nilipoingia CCM nimeokoka sasa nimepata ubunge nikiwa CCM… ingekua kashfa kubwa kwangu kama ningechaguliwa kuwa mbunge kwa CHADEMA,” alisema mbunge huyo aliyetumia zaidi ya dakika 5 kujinasibu badala ya kuzungumza hoja za msingi.
Baada ya kauli hiyo Mbunge wa Kawe Halima Mdee (CHadema) aliomba utaratibu wa Spika kuhusu kauli za mbunge huyo kupitia kifungu cha 64 cha Kanuni za Bunge toleo la mwaka 2007 ambapo alimtaka mbunge huyo kuomba radhi ama kufuta kauli yake.
“Kuhusu utaratibu mheshimiwa Spika kwa mujibu wa Kanuni ya 64 kifungu kidogo (g) kinasema bila kuathiri masharti ya ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge; Mbunge hatatumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha watu wengine.
“…Mheshimiwa Spika CHADEMA ni chama kilichosajiliwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za nchi, ni chama makini chenye watu makini hivyo mchangiaji aliyepita kusema ingekuwa kashfa kubwa kwake ni lugha ya kuudhi namtaka afute kauli yake au aombe radhi au turuhusiwe kusema lugha za maudhi,” alisema Mdee.
Baaada ya kauli hiyo, Spika wa Bunge alimwambia Mdee kuwa yeye ndiye mwenye kuruhusu wabunge kuongea lugha za kuudhi na sio mtu mwingine kisha akamruhusu mchangiaji huyo kuendelea.
“Mimi ndiye mwenye uwezo wa kuwaruhusu mzungumze lugha za kuudhi siyo mwingine naomba ukae chini mtoa mada endelea,” alisema Spika huyo akimweleza Mdee aliyeonyesha kutoridhishwa na majibu hayo kisha mjadala huo uliendelea.
Source: Tanzania daima
 
Kuna haja kubwa kwa katiba yetu kuzuia spika kuwa kwenye uongozi wa chama cha siasa. Hivi sasa Makinda ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM; bila shaka katika nafasi hiyo inakuwa vigumu kwake kujizuia kushabikia chama chake.
 
Sheria hajui, eti wanamchagua kwa kuwa mzoefu kuwa bungeni bila kuwa mhitimu wa sheria, kazi kweli kweli
 
To me huyu mama si tu ni mtu asiyefaa kuliongoza bunge letu bali pia ametumwa kusafisha njia ya mafisadi kupitia kuwazuia CDM katika kila kitu bungeni.Bunge limekuwa kama uchafu halina matumaini tena,limepoteza dira.
 
Tatizo ni kuwa na wao Chadema wangesimama na kuyarudia maneno yale yale na kuona kama mbunge wa CCM angetumia kifungu kile kile kupinga!
 
Dah kweli Makinda anacheza makida!Kwahiyo kuwa kwake pale mbele ndo aruhusu kashfa kwa chama kingine?Anaudhi!
 
BUnge letu naona lipo lipo tu,hakuna mambo ya maana ya kuzungumzia hawa jamaa ambayo yanaweza kusaidia taifa zaidi ya kurushiana maneno yasio kuwa na msingi kila siku?
 
Sasa mnaelewa kwa nini Samuel Sitta alifupisha safari yake Marekani kurudi kusimamia suala la Richmond badala ya kumwachia mama huyu kipenzi cha mafisadi kulisimamia suala hilo bungeni.
 
1. Umri -- Uzee
2. Upeo mdogo
3. Unazi-ushabiki wa kichama
4. ufisadi -kuwekwa kwa maslahi ya mafisadi

5. Personal chuki na Halima Mdee
6. Matatizo na ex-mume wake.
Ndo maana maandiko yanakataza wanawake kuwa viongozi
 
Sasa mnaelewa kwa nini Samuel Sitta alifupisha safari yake Marekani kurudi kusimamia suala la Richmond badala ya kumwachia mama huyu kipenzi cha mafisadi kulisimamia suala hilo bungeni.

true alijua anaacha mtu asiye na akili bali matope
 
Kila siku nasema,na ntaendelea kusema hapa jf kuwa pale bungeni kinachoendelea ni COMEDY,nothing else,suala la cpka liangaliwe kwenye katiba kama suala la tume ya uchaguzi,yani tutegemee upuuz mwing toka kwa makinda,na mwisho wapga kura huku uraiani watasema,subirini june kwenye BUDGET!
6 atakumbukwa na atatajwa sana!wachangiaj wamekuwa waimba taarabu,kanuni zme2pwa kinachofuata ni ku2kanana na kupgana
 
Hivi kuna mtumishi yeyote wa umma akihamishiwa NKASI atashangilia au atolalamika? Kama kuna mtu kafika NAMANYELE makao makuu ya Wilaya ya NKASI atoe maelezo kwa wadau wajue hiyo NKASI ilivyo. Nashangaa kwa mtu ambaye JIMBO lake limetopea kwa UMASKINI kiasi watumishi wa serikali wakipelekwa huko inajulikana ni ADHABU, Na aliyesababisha umaskini huo ni CCM leo mtu huyo anasema kujiunga kwake tena na CCM ni sawa na KUOKOKA ! Ukisikia wabunge wanaojali MASLAHU yao na si MASLAHI ya Wananchi ndio hao yeye aliitaji kuingia BUNGENI TU, bila kujali anatumia CHAMA gani, hajali kama chama hicho ndio chanzo cha matatizo ya Wanankasi na Rukwa kwa ujumla na wana KATAVI pia. YEYE kwake ni UBUNGE ndio maana anaona raha kama vile KAOKOKA sasa cjui kaokoka na nini? KAOKOKA na UMASKINI au na KUHUKOSA UBUNGE?

SHAME ON U ALLY KESSI
 
Back
Top Bottom