Spika aahirisha safari ya Marekani

Kumbe hii safari ilikuwa inawezekana kuahirishwa from the beginning kwanini hakuahirisha mpaka alipositisha kutokana na makelele? Spika hana heshima kwa Bunge ambalo ni taasisi anayopaswa kuilinda.
 
nafikiri wanzuki anayo kunywa sio nzuri ( sio ya Asali) ni hizi za mjini za Sukari na Tetracycline na inawezekana ana pepa ili aweze ku-face wabunge matokeo yake ndio hayo anakurupuku na kuongea upupu.
Solution wmuajibishe au ajiadabishe. Ajiuzulu
 
ina bidi hawa wabunge wa rangi ya kijani na njaro watambue kuwa wananchi wamewachoka kwa wao kuisapot sirikali.hivyo ktk hili la richard wa monduli inabidi waangalie wasije wajizika kabisa.hapo walipoanza jana washikilie hapo hapo wasije wakapigwa bitwa ktk kikao cha kesho wakalegea ka mlenda na kujikuta wakiwaachia kazi akina zitto na slaa na wao kuitetea siri kali ambayo siyo iliyowatuma bungeni.
 
Kesho naamka na suti na tai kuzengea yatakauo jiri . Hali si shwari na Spika kaingia Dodoma kimya kimya akiuliza pembeni atmosphere iko vipi .Yuko kimya ila hana haya kama mnavo jua na sura lake zito kama kaanguka majini mzee yule .Kesho ni siku ya kujifungia and is going to be a big test kwa wale walio fungua vinywa vyao majuzi juu ya Karamagi.Yule wa kuomba kufa kesho anaweza kufa kweli . Nitajitahidi kuwapeni lolote litalalo nifikia toka sirini .
 
mwanakiji makubaliana na wewe ,ninahisi kuna jambo kubwa linakuja hapa karibuni hususani kesho, jumatano na alhamisi.na moja kati ya vitu ninavyovihisi ni aidha el kujiuzuru au baraza kustep down, so tukaeni mkao wa kula mana kuna lolote linaweza kutokea soon. na muungwana ataenda dodoma wiki hii.
 
SITA asema

"Ni jambo la kawaida la uwajibika Ibara ya 84 ya Katiba inasema kukiwa na jambo zito ni lazima Spika asimamie," alisema Bw. Sitta na kuongeza kuwa hicho ndicho amekifanya.
HABARI ZAIDI MAJIRA
 
mwenzenu napiga mluzi tu.

a. Baraza lisipojiuzulu ndani ya wiki ya mjadala wa Richmond basi Lowassa kasalimika a.k.a uchunguzi ulishindwa kumhusisha moja kwa moja na Richmond.

b. Kama Baraza litajiuzulu au Rais atalivunja lengo ni kuhakikisha mtu mmoja tu hatolewi kafara bali itauhusiana na kuwaondoa baadhi ya watu ili kifo cha wengi kiwe harusi.

c. Kama Baraza halitajiuzulu basi mjadala utakuwa moto moto lakini usioenda mahali popote pale lengo lake ni kujenga maneno makali na porojo zitakazoandikwa magazetini, lakini wakifika mwisho, "wataunga mkono hoja". Hivyo wabunge wa CCM watajitengenezea umaarufu kwa kukaripia lakini itakapofika kuwawajibisha watapiga kura upande wa serikali.

d. Siyo maslahi ya Kikwete kumuondoa Lowassa hata kama anataka hasa mwa vile anayo miaka mitatu imebakia. Akimuondoa Lowassa sasa hivi atakuwa amejitengenezea adui namba moja Bungeni. Lowassa hatokubali kuwa Waziri wa Kawaida (itakuwani demotion) hivyo atabakia kuwa Mbunge.

Akiwa Mbunge, Lowassa ataichachafya serikali na kuonesha makali yake na kuwa "mtetezi wa wananchi". Ataonekana akitetea maslahi ya wananchi na kuziba nyota za kina Zitto na Slaa na hivyo ataimega CCM toka ndani kuelekea 2010.

Akijipangia kulipiza kisasi, Lowassa atasimama kugombea dhidi ya JK na asipoangalia JK ataangushwa na hivyo kumfanya kuwa Rais wa Muhula mmoja. Mtu pekee anayeweza kusababisha hilo ni Lowassa, lakini ataweza kufanya hivyo endapo tu ataondolewa Uwaziri Mkuu.

g. Hata hivyo, endapo ataona kuwa viongozi wenzie serikalini na kwenye chama wako kinyume naye Waziri Mkuu mwenyewe anaweza kujiuzulu na hivyo kujipa nembo ya kuwajibika na kuonesha mfano na huo ukawa mtaji wa kisiasa.

Atapita na kuomba radhi na kukiri kufanya maamuzi mabaya hasa watu walio chini yake na ataonesha kweli hakujua RDC ilivyo kwani hadi hivi sasa ile "smoking gun" inayomfunga Lowassa na RDC haipo. Kinachoonekana ni moshi tu. The gun itself is no where to be seen ( I mean I know where it is.. but they don't) Does this remind you of Dito's gun..??

i. Hata hivyo kwenye mjadala huu wa BoT na Richmond tarajieni maneno makali ya wabunge wa CCM (ndiyo makubaliano ya kesho yatakavyokuwa) na kina Kaboyonga, Selelii, na wengine watapiga kelele mno na kupigiwa makofi.

Lengo ni kuteka nyara hoja ya wapinzani ili wapinzani watakapopiga kelele waonekane wanaiga CCM. Hivyo, ni kweli upinzani mkubwa kwenye suala hili la BoT na Richmond utatoka CCM.


j. La mwisho angalieni watakachomtenda Msabaha.

f.
 
Kweli ushindi ni lazima lakini wapinzani haya wanayajua na naamini wanapanga namna ya kuwakabili. hata wakiiteka hoja is too late maana wananchi wamesha jua kunani .
 
Na kwa mujibu wa gazeti hilo la majira, spika atarejea ijumaa wiki hii...so which is whic, ameahirisha safari au ameondoka? leo alikuwa kweli bungeni?
 
mwanakiji makubaliana na wewe ,ninahisi kuna jambo kubwa linakuja hapa karibuni hususani kesho, jumatano na alhamisi.na moja kati ya vitu ninavyovihisi ni aidha el kujiuzuru au baraza kustep down, so tukaeni mkao wa kula mana kuna lolote linaweza kutokea soon. na muungwana ataenda dodoma wiki hii.

Nyie JF members sijui nini kimewapa hii imani tele kwamba hawa wawakilishi wa CCM wanaweza kuwa na ubavu wa kuisurubu sirikali.Huu ni upepo wa Baloon tu.Wakikalishwa mbele ya Bwana Jakaya na Luwasha tu upepo wote unatoka na wanaufyta.Sasa hivi wanajifanya kutingisha kiberiti kwa Naziri 'Karumogi' wakija akina Luwasha na Kibwete wote wanaobweka sasa na kujifanya kuongea kwa ukali watabadili kauli badala ya kusema TUNATAKA watasema TUNAOMBA na Supika atasema wanaoafiki RICHIMONDI iletwe wataibuka akina Slaa na kundi lake mwisho SUPIKA atasema wanaopinga Richimondi isiletwe wameshinda,..Mwisho wa mchezo hakuna cha kilango wala mlango, si-reli wala mwanakiembe wote wanajikosha tu kujaribu kupoza hasira za wananchi na inawezekana ni kwa amri maalum.Ngoja tusubiri baada ya muda tutajua tofauti ya upepo na Kimbunga
 
Nadhani huu ukali wa Wabunge wa CCM ni "DANGANYA TOTO" yakiwa ni maandalizi ya kuwadanganya wana-Kiteto kuwa CCM imejivua gamba la ufisadi. Baada ya maneno hayo makali, wabunge watapewa sifa kibao, na kama wananchi wa Kiteto watalikubali Changa hili la macho; baada ya uchaguzi kupita ;CCM itarejea kwenye "Business as usual"
 
Atapita na kuomba radhi na kukiri kufanya maamuzi mabaya hasa watu walio chini yake na ataonesha kweli hakujua RDC ilivyo kwani hadi hivi sasa ile "smoking gun" inayomfunga Lowassa na RDC haipo. Kinachoonekana ni moshi tu. The gun itself is no where to be seen ( I mean I know where it is.. but they don't) Does this remind you of Dito's gun..??

Hii gun kweli ni ya Dito!

tahadhali wanaJF usisome thread ya siasa mida hii toka kwa wachangiaji walioko US (ambao wengi wametoka lunch break zao na wameshiba) kwani unaweza kufukuzwa kazi kwa kucheka kupindukia ukiwa kazini......
 
kwa vile Rais bado ana nafasi mbili za kuteua wabunge, miye naomba hako kanafasi kamoja. Hiyo inaweza kuninyamazisha hapa JF na kunifungulia Bungeni.
 
kwa vile Rais bado ana nafasi mbili za kuteua wabunge, miye naomba hako kanafasi kamoja. Hiyo inaweza kuninyamazisha hapa JF na kunifungulia Bungeni.

kwi kwi kwi...

Kinachonichekesha ni huu utaratibu wa anonymous... sasa atajua je kwamba huyu ndiye Mzee Mwanakijiji na wala sio Kasheshe... Je ataangalia hiyo picha ya kumenya muhindi au atatumia simu yako,,, au inabidi atumie Usalama wa Taifa kughamua huyu kweli ndiye Mzee Mwanakijiji.,,, very interesting?
 
kwi kwi kwi...

Kinachonichekesha ni huu utaratibu wa anonymous... sasa atajua je kwamba huyu ndiye Mzee Mwanakijiji na wala sio Kasheshe... Je ataangalia hiyo picha ya kumenya muhindi au atatumia simu yako,,, au inabidi atumie Usalama wa Taifa kughamua huyu kweli ndiye Mzee Mwanakijiji.,,, very interesting?

Hiyo picha sio muhindi huo bali ni "mjani" fulani...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom