Spika aahirisha safari ya Marekani

Mimi nataka kuisikia sababu iliyomfanya aahirishe. Vinginevyo, aidha kuna kujiuzulu kwa baraza la mawaziri au kujiuzulu kwa Waziri Mkuu.

Kuna kitu unakijua lakini hutaki kukisema, sie tuliokula chumvi nyingi tushajua.....

Anyway check ur PM kuna kuna some clue sitaki kumwaga kuku kwenye mtama mwingi oooppps sorry! should be other way round
 
Ni ajabu na kweli kwamba "Habari Leo" wameandika habari hii, maana wao ni chombo cha sirikali na wamekuwa wakishabikia kila upumbavu wa sirikali. Inakuwaje leo wanamgeuka Karamagi (sirikali)?

Idimi,
Ni kweli kabisa, hawajamaa wanapolish news kijinga kila siku to the benefit of sisiem na serekali mpaka wakati mwinginew wanajipofua wenyewe....Naona kaupepo ka sisiem..kubadili misingi yao fulani..unasikia raisi anasema..ni mwaka wa sisiem kujenga mahusiano na wapinzani..Ameyaona ya KIBAKI? ..unaona hao wabunge...wamebadili mwelekeo..!!!!
 
Kuna kitu unakijua lakini hutaki kukisema, sie tuliokula chumvi nyingi tushajua.....

Anyway check ur PM kuna kuna some clue sitaki kumwaga kuku kwenye mtama mwingi oooppps sorry! should be other way round

Sasa nyie wakuu mbona mnaanza kutubagua watu wa chini? Mnapeana ulaji kwenye PM? Sawa mkuu tutaonana huko mbele!

Ila hata mimi nahisi Mwanakijiji ana ujumbe mzito ambao hataki kuutoa.
 
Sasa nyie wakuu mbona mnaanza kutubagua watu wa chini? Mnapeana ulaji kwenye PM? Sawa mkuu tutaonana huko mbele!

Ila hata mimi nahisi Mwanakijiji ana ujumbe mzito ambao hataki kuutoa.

Mtanzania,

Mkjj kwa siku za karibuni amekuwa anasubiri mpaka chakula kinapoa ndio anakileta hapa JF! inabidi apewe a lit visit this weekend kujua nini kinaendelea huko kijijini!
 
Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM wamekaa leo kuanzia saa nane hadi saa kumi na nusu jioni na ilikuwa inaongozwa na Lowassa akishirikiana na makamba ,na jua kuwa wajumbe wa kamati ya uongozi ni wabunge wote wa CCM ambao ni wajumbe wa kamati kuu ya CCM.
 
The good thing i can see fm the way Mr. Six plays the game as Speaker ni kuwa anajitahidi kwa njia zote kulinda masilahi ya mafisadi ndani ya CCM lakini at the end anajikuta anapoteza kwa faida ya opponent side. Ukiangalia sakata la BOT na BUZWAGI, the man refused to form Kamati ya Bunge kwa ajili ya kuchunguza akifikiri kwa kufanya hivyo atakuwa amemaliza soo kumbe watoa hoja walikuwa na vision ya mbali zaidi yake kwani waliporudi kwa wananchi mambo yalibainika zaidi kuliko kama yangefanywa ndani ya Bunge, Sitta na CCM wakawa defeated totally. Kwa hili la ziara ya Marekani na kuzuia mijadala ya mambo nyeti mpaka atakaporudi, nahisi kuna watu ndani ya CCM wameshtuka kwa ukubwa wa reaction ambayo ingetokea sio tu ndani ya Bunge ila hata nje ya Bunge hivyo wakaamua kumkataza asiondoke ili kupunguza impact ya huo mlipuko. "LET'S KEEP SHOUTING ALTHOUGH THEY'RE PRETENDING TO BE DEAF BUT THE STRENGTH OF OUR NOISES WILL KEEP THEIR BODIES SHAKING ALL THE TIME..."
 
Ebwana weee
Kwani Sita tangia lini alikua na safari ya US??

Jamaa alikua anakwepa asiombwe ripoti ya Richmord na akiwategeshea wabunge wapitishe kimeo kingine cha tanesco.

Sasa wabunge wamemchunguria ikabidi atoke mafichoni fasta
 
Mtanzania,

Mkjj kwa siku za karibuni amekuwa anasubiri mpaka chakula kinapoa ndio anakileta hapa JF! inabidi apewe a lit visit this weekend kujua nini kinaendelea huko kijijini!

Mwafrika wa Kike,

Nina wasiwasi kweli na Mwanakijiji maana toka aseme anaacha kuandika makala za Lowassa, amekuwa sio mtu wa data tena. Labda mwenzetu kisha katiwa kidogo zile za BOT.

Siku hizi anaongea na Meghji na Ballali, kuna usalama hapo kweli?
 
mawazo na mambo yote Kiteto...haya mengine yanakuja pole pole.. ila bi mdogo sitajali sana kupata special visit maana wakati mwingine hata togwa huzimuliwa.
 
Mwafrika wa Kike,

Nina wasiwasi kweli na Mwanakijiji maana toka aseme anaacha kuandika makala za Lowassa, amekuwa sio mtu wa data tena. Labda mwenzetu kisha katiwa kidogo zile za BOT.

Siku hizi anaongea na Meghji na Ballali, kuna usalama hapo kweli?

Kwi kwi kwi

Issue ya BoT iko kwenye very thin line, ni prisoner dilemma hapa kama umecheza game theory. Inaonekana hicho kinachokusanywa kuhusu Lowasa ni kikubwa mno au inawezekana pia Bi senti 50 (sijui yuko wapi siku hizi) amefanikiwa kumshawishi aachane na issue za Lowasa!

Hayo ya Meghji na Balali we yaache tu kwa sasa maana usalama kwa kweli inaonekana haupo kabisaaaaa! Naomba tu wasijempa sumu mzee wetu wa kijiji!
 
Mimi nataka kuisikia sababu iliyomfanya aahirishe. Vinginevyo, aidha kuna kujiuzulu kwa baraza la mawaziri au kujiuzulu kwa Waziri Mkuu.

Labda alikuwa anakwenda kufanya shopping au naye alikuwa anakwenda kumuona "mgonjwa".
 
Speaker calls off his US trip
LEONARD MWAKALEBELA in Dodoma
Daily News; Monday,February 04, 2008 @18:02
Also in the News

THE Speaker of the National Assembly, Mr Samuel Sitta, has called off his planned trip to the United States, amidst growing pressure from Members of Parliament who want immediate and in-depth debate on Parliamentary team report on Richmond power deal.

The Deputy Speaker, Ms Anne Makinda, told the House today that the Speaker who was scheduled to travel today has cancelled the trip and would today lead parliamentary session.

She could not however give further details including reasons behind the cancellation. Mr Sitta could not be reached for comments today. Last Thursday the Speaker announced in the House that he would be travelling to the US for an official tour, and that he would return next week.

When handing over the chair to the Deputy Speaker, he directed that all sensitive debates especially on Richmond power deal and BoT report were supposed to wait until he comes back.

"He hasn't given me the reasons but he's coming back to lead Parliamentary businesses. He has already informed his hosts over the cancellation, and they have agreed to fix another date for the tour," the Deputy Speaker told this paper outside the House.

Information had it that the Speaker was forced to cancel the trip after consultation with other top leaders so that he would lead the House to debate on the two much awaited reports. Some MPs who talked to this paper commended the Speaker's decision saying the decision was wise and patriotic.

"He has made a wise decision and I commend him for that because the MPs want the reports to be critically debated now in the interest of the nation. The trip could have delayed the debates and that would not be healthy," commented Dr Wilbrod Slaa (Karatu-Chadema) and the Secretary General of Chadema party.

Last Saturday, the MPs refused unanimously to listen to Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi at a seminar convened to discuss The Electricity Act, 2007 and the Petroleum Supply Act, 2007. Among other things, the MPs demand to see the report of the probe team on the controversial Richmond contract before they discuss the Bills.
 
Naam, moto umeanza. Ikiwa Lowassa na makamba walijifungia kwa masaa matatu wakitupa cheche, ujue mkao wa kuungua waja!


Habari za kawaida Posted Date::2/4/2008Bunge: Fukuto la Richmond,Spika aahirisha ziara ya Marekani* Waziri Mkuu, Makamba wateta kwa saa tatu
* Wabunge CCM kukutana leokuweka mkakati
* Yadaiwa kuna mpango wa kuzuia mjadala


Na Tausi Mbowe, Dodoma

SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta ameahirisha safari yake ya kwenda Marekani.

Taarifa ya kusitishwa kwa ziara hiyo ilitolewa jana na Naibu Spika, Anna Makinda na kufahamisha kwamba leo Spika atakuwepo Bungeni kuendelea na shughuli za Bunge.

Hata hivyo katika tangazo hilo la Naibu Spika Makinda hakutaja sababu ya
Spika kuahrisha safari hiyo.

"Wabunge kama mnakumbuka, Spika alitangaza kuwa atasafiri leo na kurudi siku ya Alhamisi, ameniagiza kutangaza kuwa amesitisha safari hiyo ya Marekani na kwamba kesho (leo) atakuwepo bungeni kuendelea na shughuli za Bunge kama kawaida," alisema Makinda.

Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa Spika amefikia uamuzi huo ili kuokoa jahazi kutokana na hali ya kisiasa kuchafuka kufuatia msimamo ulionyeshwa na wabunge kutaka ripoti ya Richmond iletwe bungeni kwanza kwaajili ya kujadiliwa.

Wakati anawaaga wabunge, Spika Sitta alimuagiza Naibu Spika, Anna
Makinda asije akakurupuka na kuyavamia mambo yote ?nyeti? na kuyazungumza au kuyatolea maamuzi katika bunge hilo wakati yeye hayupo.

Sitta alisema kuwa mambo yote 'nyeti' yatasubiri mpaka atakapokuwepo na kwamba Naibu Spika asije akarudhusa kujadili mambo makubwa wakati hayupo.

Spika alitolea mfano wa sakata la ufisadi la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na la Richmond na kusisitiza kuwa ili kujadili masuala hayo lazima yeye awepo.

Kauli hiyo ya Spika ina maana kuwa ripoti hiyo isingejadiliwa mpaka yeye yaani wiki ya mwisho ya kikao cha 10 cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma.

Juzi wabunge walisusia semina iliyoandaliwa na na Wizara ya Nishati na Madin ikwa lengo la kuwaelimisha kuhusu muswaada wa Sheria za Umeme na Biashara ya mafuta ya Petrol wakidai wapewe kwanza ripoti ya Kamati ya Richmond ili waijadili kabla ya kuupitisha muswada huo.

Wabunge hao pia walisema kuwa hawana imani na wizara hiyo pamoja na Shirika lake la Umeme Tanesco kwa kuwa taasisi hizo zimejaa uchafu na kwamba hawawezi kujadili masuala ya mikataba mengine mpaka wajisafishe.

Taarifa zilizopatikana kutoka miongoni mwa wabunge mjini hapa, zilieleza kuwa ili kuua mjadala bungeni, serikali inataka kutumia Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (Takukuru), kukamata baadhi ya maafisa na kuwafikisha mahakamani.

Chanzo chetu cha habari kilisema, juhudi zilikuwa zikifanyika tangu mwishoni mwa wiki kwa viongozi wakuu wa serikali kuwasiliana na Takukuru kwa ajili ya kuchukua hatua hizo.

Inadaiwa kuwa, kupelekwa kwa maafisa hao kuwatanyima haki wabunge kujadili suala hilo kwasababu ya utaratibu wa kuheshimu utawala wa sheria, lengo likiwa ni kuwaziba midomo wabunge hasa kutokana na cheche walizoonyesha mwishoni mwa wiki.

"Viongozi wanahaha kuhusu Richmond. Zimeenea habari kuwa viongozi wanaotaka kuua hoja hiyo bungeni wataitumia Takukuru kuwafungulia kesi maafisa kadhaa wa serikali kuwa walikula njama za kuihujumu Tanesco, iliwa na lengo la kuzuia mjadala bungeni," alisema Mbunge mmoja wa CCM na kuongeza:

"Upo uwezekano mkubwa watu hao watakamatwa kabla ya kikao cha wabunge wa CCM kinachofanyika leo."

Hata hivyo, Takukuru iliwahi kutoa taarifa za kuwasafisha maafisa waliohusika na kwamba hakuna rushwa iliyotumika kwenye mchakato mzima wa kufikia utoaji wa zabuni yenye mashaka ya Richmond.

Taarifa hiyo ya Takukuru ilipingwa na wananchi, huku Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Edward Hosea akisimama kidete kuwa hisia za rushwa ni juu ya mkataba huo ni majungu.

Kwa mujibu wa maelezo ya awali ya Spika, safari ya nchini Marekani ilikuwa na lengo la kuliongezea Bunge uwezo katika masuala mbalimbali yanayohusu shughuli zake na kwamba ingekuwa ya muda mfupi na kuahidi kurudi siku ya Alhamisi na kuendelea na shughuli kama kawaida na kujadili mambo hayo nyeti.

Siku hiyo pia Spika aliliambia Bunge kuwa bado mashauriano baina ya ofisi yake na serikali yanaendelea kuhusu ripoti nzima ya Mahesabu ya Akaunti ya Nje ya Nchi (EPA), kupelekwa bungeni kwaajili ya kujadiliwa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yussuf Makamba jana walikutana kwa dharura kuweka mikakati itakayowezesha Wabunge wa CCM kuwa na kauli moja kutokana kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa kwa wabunge hao dhidi ya ripoti ya Richmond.

Viongozi hao wajuu wa chama hicho walikutana jana kwa zaidi ya saa tatu katika
Ofisi za Bunge ili kuokoa jahazi kutokana na mgawanyiko huo unaonekana kutokea wazi wazi.

Habari zaidi zinasema kuwa wabunge wote wa CCM watakutana leo kwa ajili ya kuweka mkakati kabambe ikiwa ni pamoja na kuwa na kauli moja katika sakata hilo lilosababisha Spika Sitta kukatisha safari yake ya Marekani. Kwa upande wa wabunge wengi walionekana kuwa na shauku kubwa kutaka ripoti hiyo ifikishwe bungeni kwanza ili wapate fursa ya kuijadili kwa undani ripoti hiyo
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4327
 
Kwi kwi kwi

Issue ya BoT iko kwenye very thin line, ni prisoner dilemma hapa kama umecheza game theory. Inaonekana hicho kinachokusanywa kuhusu Lowasa ni kikubwa mno au inawezekana pia Bi senti 50 (sijui yuko wapi siku hizi) amefanikiwa kumshawishi aachane na issue za Lowasa!

Hayo ya Meghji na Balali we yaache tu kwa sasa maana usalama kwa kweli inaonekana haupo kabisaaaaa! Naomba tu wasijempa sumu mzee wetu wa kijiji!


LOL, lakini katika prisoner dilemma, inajulikana ni wapi penye unafuu..wa win-win situation. Katika hili, challenge ni kuwa je waliomo kwenye game wanatambua watokeje? manake wakikosea kidogo tu ndo ivo tena they are in for it
 
Kitendo cha Supika Sitta kuacha kwenda safari ghafla na huku alisha tangaza hali mbaya Bungeni naamini kina Jambo. Niko Dodoma najaribu kuzitafuta sababu za kuvunjwa kwa safari yake lakini sijapata lolote .Usiri na wasi wasi vimetanda sana hapa Dodoma .Lowasa hana raha kabisa na sijui kuna nini hasa .
 
Back
Top Bottom