Spesho kwa Dada Zetu

AK-47

JF-Expert Member
Nov 12, 2009
1,373
199
Inasikitisha sana dada zetu wamekuwa wakipata ushauri unaochanganya kiasi cha kufanya vitu vya ajabu ili kuwavutia wanaume. Kibaya zaidi ushauri huo unatolewa na wanawake wenzao kwenye majarida eti utakuta jike limeandika makala “Mambo 100 ya kumridhisha mwanaume”. Hivi kweli mwanamke anajua nini kinachomridhisha mwanaume kuliko mwanaume mwenyewe. Hakuna mambo 100 ya kumridhisha mwanaume, mwanaume anamambo machache mno ya kumridhisha na hayazidi hata matano lakini wenzenu wanawapotosha kiasi cha kujihisi si wazuri lakini mie napenda kuwaambi wanawake nyie ni wazuri mno hivyo mlivyozaliwa. Msichanganywe na ma-columnist wanaojifanya wataalam wa mapenzi wanacheza na akili zenu na kuathirika kisaikolojia na kiafya na hata kushindwa kujua nini hasa cha kufanya ili kudumisha mahusiano yenu. Ushauri huu ni maalum katika kuonyesha upendo wangu kwenu wakati huu tukielekea kwenye Valentine Day.
 
Hakuna tatizo na columnist!wanawake wamepewa pia akili ya kujua lipi wachukue na lipi waache,wana uwezo wa kufanya maamuzi yao baada ya kusoma,ingekuwa iko kama hivyo unavyosema ungekuta wote tuna tabia za kufanana na wanachoandika.acha waandike,yapo mengi tumejua na tukasaidika kupitia hizo kazi zao.ni wajibu wa mwanamke kusoma katikati ya misatri na kuamua.asante kwa warn,Happy Valentine!
 
Akili ni nywele na kila mwanamke ana zake, wengine ni ndefu wengine ni fupi. Katika yote akili ya mtu inatakiwa itumike.
 
asante kwa ushauri,
kwa kuongezea tu ni vizuri mtu kumfahamu mpenzio apenda nini na kumfanyia hivyo siku zote ili muwe na maisha yenye furaha.
hii ni kwa pande zote mbili.mwanamke na mwanaume.
 
Nafikiri si kila kitu kinachoandikwa unakibeba kama kilivyo sanasana kati ya hivyo mia utakuta mume wa muhusika fulani ana vitu sita tu vinavyomuhusu, na mwingine na mwingine, so at the end of the day utakuta vyote vilivyoandikwa vina wahusika mbalimbali
 
Nafikiri si kila kitu kinachoandikwa unakibeba kama kilivyo sanasana kati ya hivyo mia utakuta mume wa muhusika fulani ana vitu sita tu vinavyomuhusu, na mwingine na mwingine, so at the end of the day utakuta vyote vilivyoandikwa vina wahusika mbalimbali

hivi mbona wakaka wanatupa TUITION/COURSE KWA HILI KWANI WAO HAWAACHIKI? muelekezeni JAFARAI mambo matano yakumvutia mdada ili asiachike tena
 
Hakuna akili ni nywele kila mtu ana zake wala nini!! kwa nini kina mama wanaamini sana third parties kama magazeti, mashost n.k. Hii ni kwa sababu hawajiamini.
 
hivi mbona wakaka wanatupa TUITION/COURSE KWA HILI KWANI WAO HAWAACHIKI? muelekezeni JAFARAI mambo matano yakumvutia mdada ili asiachike tena
Marytina wewe ni Shyrose nini hili la Jafarrymes umelishupalia sana lol!
 
<p>
Inasikitisha sana dada zetu wamekuwa wakipata ushauri unaochanganya kiasi cha kufanya vitu vya ajabu ili kuwavutia wanaume. Kibaya zaidi ushauri huo unatolewa na wanawake wenzao kwenye majarida eti utakuta jike limeandika makala “Mambo 100 ya kumridhisha mwanaume”. Hivi kweli mwanamke anajua nini kinachomridhisha mwanaume kuliko mwanaume mwenyewe. Hakuna mambo 100 ya kumridhisha mwanaume, mwanaume anamambo machache mno ya kumridhisha na hayazidi hata matano lakini wenzenu wanawapotosha kiasi cha kujihisi si wazuri lakini mie napenda kuwaambi wanawake nyie ni wazuri mno hivyo mlivyozaliwa. Msichanganywe na ma-columnist wanaojifanya wataalam wa mapenzi wanacheza na akili zenu na kuathirika kisaikolojia na kiafya na hata kushindwa kujua nini hasa cha kufanya ili kudumisha mahusiano yenu. Ushauri huu ni maalum katika kuonyesha upendo wangu kwenu wakati huu tukielekea kwenye <font color="red">Valentine Day.</font>
</p>
<p>&nbsp;</p>


niko siriazi napenda nijue sana ili niweze kumrudisha jamaa, nikodokezee bas hayo 5
 
mambo matano, 1,2,3,4,5 best unauhakika ni matano????????????????????? hembu tutajie kwanza hayo 5, then i will comeback to u!!!!
 
Back
Top Bottom