Speed ya Mabasi Ipi Inatufaa abiria, KM/HR 80 au 100

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Jana nilikuwa naangalia kipindi cha Runinga cha ITV cha usalama barabarani ambapo walikuwa wanahojiwa abiria na madereva kuhusu speed za mabasi. Baadhi ya abiria waliohojiwa walikuwa wanakubaliana na kikomo cha speed ya km 80 kwa saa kilichopo sasa, lakini kukawa na aina fulani ya kuchomekea kuiomba serikali iangalie uwezekano wa kuongeza ukomo huo ili ufikie km 100 kwa saa kwa msingi kwamba kukaa kwenye basi kwa muda mrefu nako kunachosha abiria.

Ni nini maoni yenu wanaJF juu ya hili? kuna haja ya kuongeza ukomo huo au tubakie na uliopo wa km 80 kwa saa?
 
Barabara za bongo zina ruhusu km ngapi kwa saa?

inategemea na mahali/sehemu, ukipita sehemu hakuna katazo la speed limit inamaana wewe kamua tu mpaka mwisho. ila kwa mabasi ndio hiyo 80km/h lakini naamini mengi yanakamuliwa zaidi ya 100km/h.
nadhani serikali inatakiwa iangalie umbali wa basi linapokwenda, mfano basi linakwenda kyela, tunduma, songea, etc kwakweli kwa 80km/h litafika leo kweli??
usalama uzingatiwe, wenye mabasi wafanye checkups za mabasi yao mara kwa mara, madereva wawe wawili, abiria wafunge mikanda, matuta yapunguzwe(yanasababisha uharibifu wa magari) etc hayo yakifuatwa nadhani hata 120km/h haitasumbua kuleta ajali(kwakua ndani ya 80-120km/h dereva unaweza kucontrol in case ajali inatokea)
 
Jana nilikuwa naangalia kipindi cha Runinga cha ITV cha usalama barabarani ambapo walikuwa wanahojiwa abiria na madereva kuhusu speed za mabasi. Baadhi ya abiria waliohojiwa walikuwa wanakubaliana na kikomo cha speed ya km 80 kwa saa kilichopo sasa, lakini kukawa na aina fulani ya kuchomekea kuiomba serikali iangalie uwezekano wa kuongeza ukomo huo ili ufikie km 100 kwa saa kwa msingi kwamba kukaa kwenye basi kwa muda mrefu nako kunachosha abiria.

Ni nini maoni yenu wanaJF juu ya hili? kuna haja ya kuongeza ukomo huo au tubakie na uliopo wa km 80 kwa saa?

Na hao walioandaa kipindi ni watupu ajabu.. hakuna haja ya kutafuta maoni ya abitia na madreva. Haya ni mambo ya kitaalamu. Kwa nini wasiongee na wataalamu.
 
Back
Top Bottom