Speed 120km/hr ya pikipiki na 120km/hr ya gari?

unafkiri walioweka speed meter hawajui yote hayo?? Kua tairi ya scania ni kubwa, na tairi ya starlet ni ndogo??? Ngoja nikuulize swali, je ndege zikiwa hewani, moja kubwa na ingine ndogo, na zote zinaenda at 120km/h lets say, kwahiyo ndege kubwa itamzidi ndege ndogo???? Ama labda tuchukulie meli, mv skagit na speed boat ndogo, zote zikawa katika 120km/h, yupi atakaemzidi mwenzie???? Msilete mambo ya tairi kubwa na ndogo, ishu ni km/h, ni SI unit worldwide, iende gari, iende meli, akimbie swala, iende ndege, iende bodaboda, ukiweza hata ukimbie wewe, the speed will b the same, since it is km/h..

Kwa gari au pikipiki diameter ya tairi ni kigezo muhimu sana. Maana speedometer sensor imefungwa kwenye tairi linaloendeshwa (a driven tyre) na speed sensor inahesabu mizunguko (revolutions) ya tairi. Tairi ndogo inazunguka mara nyingi zaidi kuliko tairi kubwa kwa umbali uleule. Kwa hiyo wachangiaji waliochangia hapo juu kwamba tofauti ya ukubwa wa matairi unacontribute kwenye tofauti ya actual speed wapo sahihi.
 
Rafiki hapo umekosea sana, Mimi ninauzoefu wa mambo ya magari.

Kwa mfano Suzuki ina tairi ndogo Scania ina tairi kubwa kama mara mbili ya tairi ya Suzuki kama kwenye Scania mshale wa speed utakuwa kwenye 120 na Suzuki 120 lazima Scania itampita Suzuki hiyo haina upishi kabisa.
Pia Sensor ya speed iko kwenye gearbox iko wazi mzunguko wa gear box ya gari ndogo ni tofauti na gari kubwa

Speed=distance moved/time taken. Haijalishi tairi ni kubwa au dogo kiasi gani or speedometer sensor imefungwa wapi kinachopimwa ni umbali kwa muda. So mzunguko wa tairi is proportional to distance covered
 
speed ni sawa kwa sababu quantity ni sawa ila watu wengi wasichoelewa ni factor ya acceleration ina contribute vipi katika kufikia speed fulani? physics ya kukariri na ya kuelewa ni tofauti kabisa!
 
Mzee utachekwa !
Tunaposema Km/h tuna maanisha umbali wa barabara na muda unaotumika ku cover huo umbali na siyo vinginevyo.
usichanganye rpm, revolution per minute ya engine.
Hivyo, 120km/h iwe ya ndege, baiskeli, pikipiki treni, lori, chui zote ni sawa.
Kama wanaenda umbali wa Km 120 wote watatumia saa 1 wakiwa katika spidi hiyo ya 120km/h.

je tofauti ya rpm/accelaration havina impact kwenye speed?
 
Kwa gari au pikipiki diameter ya tairi ni kigezo muhimu sana. Maana speedometer sensor imefungwa kwenye tairi linaloendeshwa (a driven tyre) na speed sensor inahesabu mizunguko (revolutions) ya tairi. Tairi ndogo inazunguka mara nyingi zaidi kuliko tairi kubwa kwa umbali uleule. Kwa hiyo wachangiaji waliochangia hapo juu kwamba tofauti ya ukubwa wa matairi unacontribute kwenye tofauti ya actual speed wapo sahihi.

sawa, sjakataa,,, but what we r talking about here is that both the bus n the small car are moving at a speed of 120 km/h,, izo factorz za tairi izunguke mizunguko mingapi kwa sekunde ili speed iwe 120km/h zimeshakua considered na walioweka hiyo sensor, soo at the end of the day 120 km/h, will b the same no matter ni chombo gani cha usafiri kimetumika, hata kama punda wako anaweza kukimbia 120 km/h atafika sawasawa na bus, treni, baloon, bajaj au chochote kile kiendacho at that speed
 
Sijui watu wanabisha nini..wanaleta yale mambo ya kilo ya mawe na kilo ya pamba
 
zile speedometer zikitengenezwa ayo ya tairi yalifikiriwa jamani.Hapa suala ni la momentum.Gari dogo linakuwa linapata resistance zaidi katika upepo, friction na air na mengine yanahusian na aerodynamics.Kwa vile gari dogo halina momentum, patahitajika mara nyingi speed iongezwe ili hucompesate hayo.Pia gari dogo katika speed kubwa linapoteza energy kubwa kwa vile linakuwa jepesi na halishiki barabara vizuri .Hivyo linakuwa si efficient sana.Ni magari machache madogo yenye ubile linalosaidia gari kujishindilia zaidi linapopata speed kubwa.

Gari kubwa likishapata mwendo unaweza achia mafuta na bado likaenda kwa kasi kubwa kabla upepeo haujaweza lipunguza speed.Tofauti kwamba kupata ubali sawa gari dogo linakuwa na number kubwa ya revolutions/sec ,wakati kubwa litakuwa na pungufu.Ila kukeep the same distance dogo linahitaji kuendelea accelerate kucompesate loss.Wakati kubwa linakuwa compesated kwa momentum.
 
hivi liter moja ya gongo na lita ya konyagi na liter ya serengeti lager na liter ya castle lager??!!
ipi inalewesha??!!
 
Wakuu nahisi tofauti haipo. Tofauti ni mzunguko wa tairi kwa saa (# of rev/hr) i.e. tairi ndogo itaenda mizunguko mingi kwa saa ukilinganisha na tairi kubwa.
 
Kipepeo kama anaweza kwenda km 3oo/h na jongo vilevle pamoja na vx v8 vyote vitafika iringa at the same tym bila ya kuvukana njiani na kwa sekunde ileile
 
Wandugu hapa kuna kitu kimoja mna ki-overlook,kinaitwa CALIBRATION,vipimo vingi vinafanyiwa calibration ili vitoe readings correct katika mazingira tofauti......kama speedometer ya lorry inasoma 120kph na ya VITS inasoma 120 kph gari zote zitakuwa na mwendo sawa......

Speedometer za haya magari zinafanyakazi sawa na ni kweli wheel diameter/flywheel(gearbox) zina affect speed lakini SPEEDOMETER ZINAFANYIWA CALIBRATION KULINGANA NA FACTORS HIZO ndio maana 120kph ya lorry ni sawa na 120 kph ya vits

Najua wengi wenu humu mnajua SPEED CAMERA ambazo huwa zinaandika max speed 70kph(mfano)....je ushaona SPEED CAMERA ilioandikwa MAX SPEED LORRY 60KPH,SALOON CAR 90KPH? kwasababu mnaosema 120kph ya vits ni ndogo kuliko ya lorry then lorry zingekuwa zinakamatwa kwa kuzidi speed limit!
 
Unajua kuna kitu kimoja hapa, haya magari makubwa malori na mabaus kwenye gia kuna button, ya LOW na HIGH, ina maana kwamba magari makubwa yakienda katika HIGH yatafanana na magari madogo kwa speed barabarani?

Kuna siku nilisafiri na basi speed kubwa tu, likaja Land Cruiser likaliovertake basi na hatukuliona tena mpaka tunafika mwisho wa safari, na mara nyingi matukio kama haya yanatokea sana na si siku hiyo tu hata safari zingine nishashuhudia hilo...

Hii ina maana tairi siyo kigezo tosha, na sijawahi kuona lori lenye matairi makubwa likaliovertake magari madogo kwenye mwendo wa kasi!!!!
 
dash board calibration si standard, inaonyesha wastani wa juu wa chombo husika ikilinganishwa na mwendo wa wastani wa hicho chombo.
Speed meter za pikipiki zipo kwenye mzunguko wa tairi ilhali zile za magali zipo kwenye gear box.
Tena speed meter digital iko karibu zaidi na standard kuliko dynamic/mechanical.
Pia suala la acceleration kabla ya kufika constant speed lina mashiko.
 
Mm ni dereva na ni fundi pia. Aliyo andika Ukwaju ndiyo jibu. Ila nawapa hongera mmesugua sana vichwa. Hili somo lilikuwepo shuleni darasa tano kwa wale walio soma miaka1992 kama mtakumbuka. Ukubwa wa tyre au udogo siyo kigezo.
 
je tofauti ya rpm/accelaration havina impact kwenye speed?

vina affect speed lakini havifanyi 120kph ya lori iwe kubwa 120kph ya vitz......rpm ni engine revolution per minute kwa gari yenye engine ndogo ita-rev higher kuattain 120kph,gari ya engine kubwa itarev-lower kuattain 120kph but once they both do 120kph the will arrive at a distance of 120km at the same 1hr time....

mfano rahisi l/cruiser v8 ikiwa at 2500rpm inapata 120kph but vitz has to be at 4000rpm to attain 120kph(at correct gear,if it is manual)
 
Nyie mnaleta utani, hebu chukulia speed ya basi 140 km/hr, likitambaa na hizo speed, hata land kruz yenye spd 220, kuliona ni ishu nyingine. Kwahiyo spd 120 ya gali iko juu ukilinganisha na ya pikipiki, pikipiki ikifika 120 inakuwa nyepesi na haikanyagi chini ipasavyo, gali ni tofauti.na ndo maana wanafizics wanasema ACCEleration due to GRAVITY.

Haya ndo matatizo ya kukimbia masomo ya science mapema.......speed inapatikana kwa kuchukua distance covered per time.....
 
Kwa kuwa umebarikiwa kujua Physics chukuwa tape pima tairi ya gari kubwa inakokanyagia baada ya hapo pima tairi ya gari ndogo kama ukilinganisha utakuta tairi kubwa ikizunguka mara moja ndogo itazunguka mara mbili.

120kph ya gari kubwa =140kph kwa gari ndogo

hahahah hahahhah ndugu yangu kweli uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana.....speed ni distance covered per time
na sio ukubwa wa matairi.km gari kubwa litatembea km 100 kwa muda wa saa 1 basi speed yake ni 100km/h
na gari ndogo ikiweza kutembea km 100 kwa lisaa liomoja na speed yake itakuwa pia ni 100km/h
msiwe mnakimbia science mapema sana.....
 
Nyie mnaleta utani, hebu chukulia speed ya basi 140 km/hr, likitambaa na hizo speed, hata land kruz yenye spd 220, kuliona ni ishu nyingine. Kwahiyo spd 120 ya gali iko juu ukilinganisha na ya pikipiki, pikipiki ikifika 120 inakuwa nyepesi na haikanyagi chini ipasavyo, gali ni tofauti.na ndo maana wanafizics wanasema ACCEleration due to GRAVITY.

Mkuu tena hii ya accelation due to gravity inakujaje HAPA! Kwani gari linashuka au kwenda hanga za juu kama space SHUTTLES za Kimerikani?
 
vina affect speed lakini havifanyi 120kph ya lori iwe kubwa 120kph ya vitz......rpm ni engine revolution per minute kwa gari yenye engine ndogo ita-rev higher kuattain 120kph,gari ya engine kubwa itarev-lower kuattain 120kph but once they both do 120kph the will arrive at a distance of 120km at the same 1hr time....

mfano rahisi l/cruiser v8 ikiwa at 2500rpm inapata 120kph but vitz has to be at 4000rpm to attain 120kph(at correct gear,if it is manual)

And a common motor bike with 5 gear shift has to go 12000 rpm for a speedometer to read 120km/hr provided it is at the right gear (5th gear). Gari yenye engine kubwa ina tairi kubwa!!
 
Back
Top Bottom