Hotuba za Rais Magufuli za kichwani zinakera, asome hotuba anayoandaliwa

Watanzania tumerogwa nani sijui? Lazima tukubali kwamba, hiki sio kipindi cha kurembesha speech na sura, HAPA KAZI Tu, nibora tukasupport mambo mazuri anayofanya Rais Magufuli, hiki sio kipindi cha kupeana ahadi na maneno mazuri yasiotekelezeka, Binafsi nafurahi nikisikia Magufuli ametumbua majipu kwa vitendo, kuliko Story tupu kama walivyokuwa viongozi waliopita. Watanzania tubadilike tuache ushabiki husiokuwa na tija kwa taifa.
 
Unajua hata mimi nilimpigia kura Lowassa ila haimaanishi kuwa sioni anachokifanya Mheshimiwa Raisi.

Honestly kama wewe sio mtu wa vyama uta-thamini na kuelewa vuguvugu lililopo moyoni mwa raisi.

Jana nilibahatika kuwepo kwenye hadhira ile. Niseme jana, kwa mara ya kwanza, wakati raisi akiongea nilitokwa na machozi ya furaha. Mimi sitaki raisi wa hotuba nzuri, zenye kiswahili kizuri, zenye maneno mazuri. Namtaka raisi kama Magufuli.

Jana kwa mara ya kwanza nilifurahia kukosea! Nilifurahia kuwa kura yangu haikufanikiwa. (najua kwa mtu wa upizani akisoma hapa atasema, 'unajuaje Lowassa angefanya zaidi?') najua! NI MIMI..nimefurahia kukosea!!!

Mh. Raisi alisema vitu vingine unatamani ufanye kidiplomasia lakini kama una uchungu na taifa lako unashindwa kujizuia. Mfano; kama mtu mmoja alipewa Tsh. bilioni 70 akatengeneza vitambulisho mil. 22 na mwingine akapewa Tsh. bilioni 176 akatengeneza vitambulisho mil. 2 (ingawa taarifa zao ni vitambulisho mil. 6) unahitaji uchunguzi gani tena kujua kuna mchezo mchafu unafanyika?

Well tungekuwa kama Marekani tungesema raisi haongei kama raisi ila jiulize, unadhani alichokisema Mh. raisi Mugabe kwenye mkutano wa AU ni uchizi au hana hulka za uraisi!?? Ni ukweli..na ukweli hauna urembo...haurembwi!!!!

 
Speech za Rais Magufuli zinashida kidogo, Rais akizungumza anazungumza kama mtu aliyejaa visasi na sifa nyingi, hana utaratibu mzuri katika kupangilia kile anachokisema.

Kama rais anapaswa kuzungumza kwa utaratibu na mpangilio hata kama ni sehemu anasisitiza jambo, vijembe kwa walio chini yake ni kutafuta tu kick kwa wananchi ambao mwenyewe keshatujua na amejawa na sifa tunazompa kila siku. Rais ni reflection ya watu alionao.

Ndugu yangu wewe utakuwa unamatatizo; ni vema ukafikiri tena walau mara tatu then ukatafakari. Na inaelekea wewe si Mtanzania kabisa na inaelekea hupendi kiongozi bora ambaye ni mzalendo mwenyekulinda maslahi ya wote wenye nacho na wasio nacho. Jitahidi kula chakula chakula bora ladba kitakusaidia. Nakusihi uwe na "jicho lenye radha" kama kweli unafahamu kiswahili sanifu.
 
Speech za Rais Magufuli zinashida kidogo, Rais akizungumza anazungumza kama mtu aliyejaa visasi na sifa nyingi, hana utaratibu mzuri katika kupangilia kile anachokisema.

Kama rais anapaswa kuzungumza kwa utaratibu na mpangilio hata kama ni sehemu anasisitiza jambo, vijembe kwa walio chini yake ni kutafuta tu kick kwa wananchi ambao mwenyewe keshatujua na amejawa na sifa tunazompa kila siku. Rais ni reflection ya watu alionao.

Mimi naona umekurupuka kuposti hichi ulichoposti hapa, au unaweza kuwa wewe ni mpinzani aliyejipanga kukosoa kila kitu as if wewe huna mapungufu..vingevyo unaweza kuwa ni miongoni mwa wenye majibu. Muache rais afanye kazi yake.
 
Hatuhitaji hotuba tamu tamu, tunataka uwajibikaji. Pole sana
Kama uwajibikaji wenyewe ndio huu, basi kazi ipo. Kama alikuwa anataka kutuonesha kwamba kweli ana uchungu, Rais angeanza kutuambia kwanza mshahara wake ni kiasi gani, na baada ya hapo atamke kwamba unashushwa na sasa utakuwa kiasi fulani. baada ya hapo itakuwa rahisi kushusha mishahara ya vigogo wengine. tatizo hapa ni kwamba sera za CCM zilikuwa ni kupandisha mishahara na marupurupu ya wakubwa kwa kiasi kikubwa sana. kwa hiyo asichague mmoja tu hapa na pale. sera hiyo yote iangaliwe upya, kwa viongozi wote, pamoja na wabunge ambao walikuwa wanadai na wao washirikishwe ili wapitishe miswada. Nyerere alifanya hivyo mwaka 1967. alikata mshahara wake mwenyewe, na wengine wakafuatia. na alipoona tatizo kubwa la ufisadi, uongozi ulikaa chini na kuibuka na Dira ya Azimio la Arusha. miiko ya viongozi iliwabana viongozi wenyewe. walianza na wao wenyewe. wengine akina Kambona wakakimbia nchi. Rais anatakiwa aje kwanza na Dira ambayo itaongoza maamuzi na utendaji wake, na kurahisisha utendaji wa wale walio chini yake. vinginevyo itakuwa ni vurugu tu. haiwezekani kuendesha nchi kwa decrees tu tena za kutolewa papo kwa papo.

Ni kutokana na kuugua muda mrefu mno tunadhani kwamba chochote kinachotoa nafuu ni dawa nzuri, hata kama ina secondary effects mbaya mno. hapa inatakiwa tafakuri ya ndani. kama unafikira karibu karibu tu wala huwezi kuelewa kinachoongelewa
 
Nimeipenda hii "Ule usemi wa Uchunguzi bado unaendelea wakati umemshika mtuhumiwa na meno ya Tembo..............''Polisi wajifunze amesema hataki tena kuusikia:confused::confused::confused:
 
Mimi naona umekurupuka kuposti hichi ulichoposti hapa, au unaweza kuwa wewe ni mpinzani aliyejipanga kukosoa kila kitu as if wewe huna mapungufu..vingevyo unaweza kuwa ni miongoni mwa wenye majibu. Muache rais afanye kazi yake.

Inawezekana hakumuelewa,maana kila binadamu na namna ya uelewa wake.Nilichokifikiria ni kwamba anataka MAHAKAMA zitende haki kwa kutumia muda mfupi.Kesi nyingi zinalala kwa kisingizio cha UCHUNGUZI haujakamilika.Ametaka Mahakimu walitendee haki TAIFA na kila kesi watende haki inavyowezekana,wasijali hata kama ni mbunge/waziri ana kosa la jinai ahukumiwe tu kuingana na kosa lake.

In short angependa kuuona mihimili huu ukiwa HURU.Ndivyo nilivyomuelewa.

Ila la TBC angemwita Mkurugenzi wa TBC kumuuliza kama hawezi kutumia njia nyingine hayo matangazo ya BUNGE yakapata MATANGAZO na ikawa kipata kwa shirika na Serikali.
 
Wacha azungumze hii nchi ilishaharibika viongozi waliachia watendaji wakwapue kwa wanavyotaka hivyo inahitaji ukichaa kidogo kufanya maamuzi Magumu kama haya. Wanaomkandia nahisi ni masalia ya walionufaika na ukwapuaji wa utawala wa awamu ya 4. Magufuli aluta continua
 
nchi imejaa wahujumu uchumi aongee kwa kutabasamu unajua uchungu alionao kwa taifa letu? muacheni aungurume kama simba na bado mtanyoooooka tu
 
Kazungushe mikono kule unazijua hata sifa za good speech ama unakurupuka tuu...!!! Unasema zinakukera speech za babu yenu za dakika3 zilikua zina nn tutolee upuuz wa Monduli hapa kanywe viroba kulee




Yawezekana hapo ulipo huna uhakika wapi utapata mlo wa siku,umejawa na kiburi na kinyongo na mwepesi wa kulipuka usikiapo yaliyo kinyume na hao unaowaabudu.

Kwako wewe kauli bora na za kukumbukwa ni zile za kuwataka watanzania wasio na uwezo wa kulipia nauli ya vivuko wapige mbizi,au ile iliyowaasa wakazi wa Buziku Jimbo la Chato kuwa kama wanataka barabara ya lami,wajisaidie haja Kubwa, kisha yeye ataleta buldoza lije lishindilie vinyesi vyao na kuwa lami.Hizo ndizo aina ya kauli unazopenda kuzisikia toka kwa huyo unayemsujudia.

Ni ujinga kuigeuza siasa kuwa uadui kiasi cha kuona kila anayetofautiana nawe kimtazamo,basi ni adui yako.Ndiyo Maana leo hii Taifa limepigwa upofu likisubiri yatakayotokea huko Zanzibar baada ya watawala"kung'ang'ania madaraka".

Hakuna anayethubutu kuukemea ujinga na upumbavu wa watawala,kwani kwao wao ujinga na upumbavu ni tunu ya Taifa na ndiyo maana wapo tayari kumnyamanzisha yoyote na kwa ghalama yoyote yule anayejaribu kuwakemea.

Kama wewe ndiye kielelezo cha wana CCM,basi huko CCM kuna tatizo Kubwa la nakisi ya fikra linalopaswa kushughulikiwa kwa nguvu zote kuliko tunavyoshughulika na utumbuaji vipele.
 
Asee hawa ndiyo wanaotapanya ela wakati watu wengine hawana uhakika wa mlo wa kesho. Rais kaza nati zaidi!
TUJITEGEMEE. Namshukuru Mungu kwa kufanya ndoto zangu kuwa za kweli. Kwani kwa rais huyu Tanzania tunaelekea kuwa Donor Country.
 
no problem as long as zinaleta tija kwa nchi....yule sio mwanasiasa kiviile...hata waliomteua kugombea wanalijua hilo lakini wakampa nafasi...hii inamanisha walijua watz tunahitaji maendeleo sio porojo.....all in all tayari ndo rais ...vumilia tu ndg usiempenda kaja...
 
Back
Top Bottom