Special Schools za Bongo

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Habari wanajamvi,

Napenda kutanguliza definition ya special school kabla ya kuingia kwenye mada. Kwa 'special schools' nina maana shule za serikali zinachochukua wanafunzi waliofaulu vizuri au kwa maana nyingine wale wenye vipaji, kama ilivyokuwa Ilboru Secondary, nk.

Ningependa kujua Tanzania kuna/kulikuwa na special schools ngapi? Ivi bado zinahesabika kuwa special schools mpaka leo? Ningefurahi kujua pia miaka zilipoanzishwa hizi shule mbalimbali.

Na mwisho kabisa kama kuna any famous alumni wa hizo shule aliyeweza kufika mbali na kutoa mchango mzuri nchini mwetu.
 
Kwamba ni ngapi siwezi jua, ila naweza kutaja baadhi ambazo ni Tbr girls na Boys, Kibaha, Ilboru. \nyingine umri umekwenda siwezi zikumbuka. Sidhani kama leo bado zipo kama zamani. au ndo kuchakachuliwa zimefanyiwa,. Kwa alumni, kutoa mchango mkubwa wapom wemgi ila wemgi wao wamekimbilia nje ya nchi kutafuta maisha bora. Nawafahamu vijana nilosoma nao primary na naada ya o level walienda Ilboru na sasa mmoja yuko bondeni ni dr bingwa na wawili wako kwa watswana ni madr bingwa. Nchini humu sijui kimsingi!
 
kila waziri wa elimu ana sera zake mara zipo mara zimefutwa!zilikua msalato,kilakala,tabora girls,ilboru,kibaha,mzumbe,tabora boys!kwa ujumla tanzania haina system ya elimu inayoeleweka!
 
Enzi zetu Technical Schools zilikuwa special school vilevile kama Ifunda, Tanga, Moshi n.k Wamezaliwa Wahandisi mabingwa kutoka Tanga Technical Schools na wengine Ifunda..... Tanga School kuna alumini ila siku hizi imekosa mvuto baada ya kuona mwaka huu ina division 4 na zero kibao tofauti na miaka ya Mzee Teti tulipokuwa tunacheza na division one za point 7 hadi 17 nusu ya darasa.
 
Na alumni waliotusaidia?
Ina maana wamegoma kutusaidia au sisi hatutaki msaada wao?
 
Kwa hiyo mpaka sasa nilizozipata ni:
1. Ilboru
2. Kibaha
3. Tabora Girls
4. Tabora Boys
5. Mzumbe
6. Kilakala
7. Msalato
 
Back
Top Bottom