Speaker Makinda akutana na Balozi wa Ujerumani nchini

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,885
6,885
IMG_7068+(1).JPG
Speaker makinda na Balozi wa Ujerumani nchini Hon. Clause Peter Blandes walipokutana kufanya mazungumzo ofisini kwa Speaker makinda.
Katika kikao kilichopita ambacho kilipitisha rasimu ya sheria ya kutunga katiba mpya, mbunge mmoja wa CCM Livingstone Lusinde, alishusha shutuma nzito dhidi ya ujerumani kwamba wanaifadhilia Chadema kupinga mswada wa sheria. Je, kikao hiki speaker Makinda amelenga kunusuru kueleweka vibaya tuhuma bungeni juu ya ujerumani na hivi kujaribu kujisafisha? Ujerumani ni moja ya mataifa ya ulaya yanayoifadhilia sana Tanzania.
 
Wanatapatapa

Tatizo ni elimu ya baadhi ya wabunge wa CCM kama Livingstone Lusinde, hana upembuzi wa anachoongelea bila kufanya utafiti ili kujiridhisha na asemacho. Anaongea kama yule Kalegesi niliyemsoma kwenye hadithi ya kitabu cha Oxford English East Africa nilipokuwa shule ya msingi. Anakuwa kama scrubu moja nati yake imelegea vile, na hivyo wrench ingali inatafutwa ili kuikaza nati ili iweze kustahimilivi vizuri.
 
Huyo Balozi waa Ujerumani Ki-Bena anauweza ndio wapate kuelewana?

Labda Mama kiroborobo licha ya kibena kuwa lugha yake ya kwanza, huenda alijifunza kidachi na hivyo anaweza kumwelewa na hata alimsalimia "guten morgen, vi gets innen Hon. Clause?
 
Kwa Lucinde kusema aliyosema hilo ni moja, lakini kitendo cha Spika kukaa kimya wakati mbunge anatoa tuhuma nzito kama hizo za nchi moja kufadhili machafuko kwenye nchi nyingine hilo ni jambo la kisikitisha. Spika alitakiwa amwambie Lucinde ama athibitishe kauli yake au aifute.

Lucinde anakuwa mtu wa tatu toka CCM kutuhumu nchi za nje kufandhili machafuko hapa Tanzania. Wengine ni Sophia Simba na Benard Membe. Diplomasia sifuri kabisa.
 
ccm kazi yao ni kuropoka tu,hukumsikia katibu wao mkuu akidai kuna magaidi yameingizwa na chama cha siasa nchini?
waziri mkuu analia,rais analalamika mawaziri wamechanganyikiwa, tumuombe mungu atunusuru miaka minne si mingi.
 
Kwa Lucinde kusema aliyosema hilo ni moja, lakini kitendo cha Spika kukaa kimya wakati mbunge anatoa tuhuma nzito kama hizo za nchi moja kufadhili machafuko kwenye nchi nyingine hilo ni jambo la kisikitisha. Spika alitakiwa amwambie Lucinde ama athibitishe kauli yake au aifute.

Lucinde anakuwa mtu wa tatu toka CCM kutuhumu nchi za nje kufandhili machafuko hapa Tanzania. Wengine ni Sophia Simba na Benard Membe. Diplomasia sifuri kabisa.
Hapa umenena, shutuma hizi ni nzito mno kwa mhimili mmojawapo wa serikali kushushia tuhuma nzito kwamba Ujerumani inafadhilia machafuko nchini, mmoja wapo akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje Membe bila kutoa uthibitisho.

Sasa Membe mambo yamemshinda kutetea nchi wahisani wakati wameanza kusitisha misaada, ameamua kumtumia speaker wa Bunge amnusuru.
 
Labda Mama kiroborobo licha ya kibena kuwa lugha yake ya kwanza, huenda alijifunza kidachi na hivyo anaweza kumwelewa na hata alimsalimia "guten morgen, vi gets innen Hon. Clause?
duh mkuu unaonyesha umahiri wako, icho ndo kijerumani????????? au ndo habari za asubuhi?? aya bana tutese mi sjaambua kitu
 
Hapa umenena, shutuma hizi ni nzito mno kwa mhimili mmojawapo wa serikali kushushia tuhuma nzito kwamba Ujerumani inafadhilia machafuko nchini, mmoja wapo akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje Membe bila kutoa uthibitisho. Sasa Membe mambo yamemshinda kutetea nchi wahisani wakati wameanza kusitisha misaada, ameamua kumtumia speaker wa Bunge amnusuru.
mko correct, hawa ccm ni mavuvuzela, stori za kwenye kahawa wanazipeleka bungeni, kama membe, sophia simba wamefikia kuongea upupu huu inshort wanajustify walivyo mambumbu wa kufikili, kwani wao si ndo wamepewa dhamana katika uongozi wa nchi hii basi wangekuja na ushahidi wa kweli na kuuweka bayana ikibidi wamfukuze balozi kama anausika au anafanya mipango ya kuvuruga utulivu tulionao Tanzania, zaidi hawana ndo baada ya kulopoka hapa anaonekana spika Bi Kiroboto akijipeleka kuomba msamaha kwa yote yaliyofanyika bungeni, haya maCCM ni mavuvuzela tu yanaaribu badae yanaomba radhi..
 
img_7068+(1).jpg
speaker makinda na balozi wa ujerumani nchini hon. Clause peter blandes walipokutana kufanya mazungumzo ofisini kwa speaker makinda.
katika kikao kilichopita ambacho kilipitisha rasimu ya sheria ya kutunga katiba mpya, mbunge mmoja wa ccm livingstone lusinde, alishusha shutuma nzito dhidi ya ujerumani kwamba wanaifadhilia chadema kupinga mswada wa sheria. Je, kikao hiki speaker makinda amelenga kunusuru kueleweka vibaya tuhuma bungeni juu ya ujerumani na hivi kujaribu kujisafisha? Ujerumani ni moja ya mataifa ya ulaya yanayoifadhilia sana tanzania.

arudishe hela zetu kwanza,,,zile 280000/
 
tatizo ni elimu ya baadhi ya wabunge wa ccm kama livingstone lusinde, hana upembuzi wa anachoongelea bila kufanya utafiti ili kujiridhisha na asemacho. Anaongea kama yule kalegesi niliyemsoma kwenye hadithi ya kitabu cha oxford english east africa nilipokuwa shule ya msingi. Anakuwa kama scrubu moja nati yake imelegea vile, na hivyo wrench ingali inatafutwa ili kuikaza nati ili iweze kustahimilivi vizuri.

in fact i hate that man, lusinde.
 
Back
Top Bottom