Soya inasababisha cancer?

mamakunda

JF-Expert Member
Jul 4, 2010
370
16
Leo tukiwa katika mazungumzo ya hapa na pale katika kituo changu cha kazi nimestuka kusikia kuwa lile ganda la Soya linaweza kusababisha kansa! Kwa kweli nimestuka sana manake watoto wangu nimekuwa nikiwatengenezea lishe iliyochanganywa na Soya!

Nilichokuwa nafanya ni kukaanga tu ile soya ili kuua protein inhibitor iliyoko kwenye ganda (kwa mujibu wa kitabu cha turejee edeni/mwandishi nimesahau) ila kina list ya vyakula na jinsi ya kuviandaa na faida zake mwilini!

Je ndugu zangu ni kweli?
 
..sina uhakika na hili lakini nami nimewahi kusikia hivyo na kutokana na niliyoyasikia nacheza nayo mbali kabisa.
 
Soya unatakiwa uipike kwanza na kuichubua maganda kama kahawa ndo uianike ukaange uisage for lishe na hutegemea na mahitaji kama kwa uju ama chai
 
Loweka soya siku 2 toa maganda yote, osha mara 8 kuhakikisha maganda yote yameondoka then anika na usage unga wako.
 
Angella, nafaka zote kama maharage, mahindi, karanga, korosho nk zote zinasababisha kansa. Sina nia ya kuwatisha watu ila ukweli ni kwamba kama nafaka itakuwa attached na aspergillus hii ni aina ya fungus ambayo huwa inatoa sumu iitwayo aflatoxin. Sumu hii inasababisha kansa.

Kinachoweza kufanya nafaka kupata hawa fungus ni kutokukauka vizuri wakati wa kuvunwa na ndio maana unashauriwa uchague vizuri kabla ya kuitumia. pia unapotaka kuzisaga hakikisha ni kavu kabisa kabla ya kusaga na baada anika unga sehem kavu na hakikisha unga huo hautumiki kwa muda mrefu. Iwe ni kwa kipindi kisichozidi wiki 2, tena ukiwa eneo kavu.
 
angella nafaka zote kama maharage, mahindi, karanga, korosho nk zote zinasababisha kansa. sina nia ya kuwatisha watu ila ukweli ni kwamba kama nafaka itakuwa attached na aspergillus hii ni aina ya fungus ambayo huwa inatoa sumu iitwayo aflatoxin. sumu hii inasababisha kansa.

kinachoweza kufanya nafaka kupata hawa fungus ni kutokukauka vizuri wakati wa kuvunwa na ndio maana unashauriwa uchague vizuri kabla ya kuitumia. pia unapotaka kuzisaga hakikisha ni kavu kabisa kabla ya kusaga na baada anika unga sehem kavu na hakikisha unga huo hautumiki kwa muda mrefu. iwe ni kwakipindi kisichozidi wiki 2, tena ukiwa eneo kavu.

Kwa hiyo mkuu,sie tunaosaga dona na kukaa nalo miezi mitatu twala sumu?
OTIS
 
Kwa hiyo mkuu,sie tunaosaga dona na kukaa nalo miezi mitatu twala sumu?
OTIS
Kha!ni kweli maana mimi nikisaga unga hata huo wa lishe hata miezi sita nautumia tu hata ukiweka wadudu nachekecha kisha nakoroga uji wangu naendelea kuutumia. hata kama nikikaa nao mwaka maadamu haujaharibika nautumia so nala sumu! Haaataarii!

Nilichokuwa nafahamu kuwa hayo maganda pia yana sumu inayoua macho ndio maana unashauriwa Maharage au jamii yake uroweke usiku kabla ya kupika ili kuondoa ile sumu iliyokwenye ganda.

Wataalamu mtufafanulie zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom