South Korea: Angalia jinsi wenzetu walivyo serious na swala la rushwa

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
haya ni maneno ya balozi wa south korea alipokuwa akibadilishana mawazo na nd. Mengi.

Alikuwa akijibu swali na Mengi aliyetaka kujua ni namna gani nchi hiyo imeweza kufanikisha vita hiyo. Alisema uchunguzi na kuadhibu watuhumiwa ndio dawa ya mafanikio katika vita hiyo na kwamba mbinu hiyo imesaidia Korea Kusini kufanikiwa katika eneo la rushwa.
“Marais wetu wawili wastaafu walifunguliwa mashtaka na walifungwa, kisha wakalipa walichokuwa wameiba, nchini mwetu kila mmoja anajua rushwa hairuhusiwi kabisa,” alisema.
Alisema watu wenye mamlaka na wenye fedha nyingi nchini humo, wanafuatiliwa kwa karibu na jamii nzima ili kuhakikisha kwamba wanalitumikia taifa na sio vinginevyo.

chanzo. Nipashe.

i hope Bw Hosea anayecheka na wala rushwa kila kukicha atakuwa amejifunz kitu hapa.
 
Hajifunzi mutu hapa ni ruswa kwakwenda mbele
 
South Korea sio wasafi ki-hivyo. Wamepiga hatua lakini sio sahihi kwa huyo balozi kutuambia wamesafisha. Sumsung inawamaliza na hata Rais ana doa la Sumsung. Cha kuchekesha ni kwamba hii company imekuwa too big & too 'sensitive' kwa hiyo wanapiga chenga hata kwenye uchunguzi. Kwa kifupi rushwa bado ipo na hata hapa TZ hawa wakorea wanahonga (state corruption) kufanikisha miradi yao. tungebadilishana notes tu lakini usafi bado.
 
Hapa kwetu Tz nani atamkamata mwenzake angali wote wamechafuka kwa rushwa.
 
Dawa tunayo lakini wengi hatuijui, mpaka idadi ya watanzania itakapoijua hii dawa ndo tutasonga mbele. Dawa hiyo ni kuondoa chama kongwe, CCM No 1. Baada ya kuitoa, tunapiga demo la ukweli, funga funga na kufilisi watu malizao kutokana na makosa. Litakuwa somo tosha kwa wanaopenda kujineemesha kupitia jasho la wengine kwa ujanja ujanja.
 
Back
Top Bottom