Sorry Mr. President.. Tanzania is NOT IN a "State of Emergency..."

Je analijuwa hilo? Iwapo tunaweza kuthibitisha juu ya uelewa wake katika hilo basi hata matendo yake yange tosha kutuonyesha anayofikiri na kuhitaji pasi na kujadili maneno yake ambayo siku zote yamedhiirika hayana uhusianao wowote na yeye mwenyewe binafsi.

Nadhani mara nyingine lawama na shutuma pia zinaunganisha washauri wake na waandishi wake wa hotuba kwa kuto kujuwa nini maana ya rais na uzito wa kauli za rais. Hapa bora tuandike sufuri tujipange upya 2015 kama kweli tunaipenda nchni yetu, maana namuona kama vile naye kisha staafu tayari ukimwangalia matendo yake kulinganisha na matatizo yanayoikabili taifa letu, tayari amekaa pembeni kaichia gari liende lenyewe kwa kasi ya mteremko, tuombe mungu lisidumbukie korongoni!
 
Hapa Rais kachapia Kiswahili na ndio confusion yenyewe........nadhani hakufikiria vizuri nini cha kuseam au gazeti lime misquote kauli yake:

“Tuko katika hali ya dharura. Sioni hisia za haraka za kuchukua uamuzi na hatua nyingine muhimu za kukabiliana na dharura ya upatikanaji wa umeme. Hatuwezi kuendeleza kuwa na kigugumizi katika kuchukua uamuzi wa kuitoa nchi katika changamoto kubwa hizi za upatikanaji wa nishati,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Ubwana mkubwa wa kila mmoja wetu utatambuliwa kutokana na mafanikio ambayo kila mmoja wetu ataonyesha katika kukabiliana na hali hii ya upatikanaji wa nishati.”

Wakuu tusidhani JK ametoa maneno haya kwa bahati mbaya!! Yeye mwenyewe anajua "yeye na serikali yake hawafanyi chochote kwa maslahi ya nchi" sentenso kama hizi anazitumia ili tusije mfunga baadaye!!

JK ni raisi mzembe sana, maana anajua hana uwezo wa kumuwajibisha mtendaji wake yeyote, kwenye issue yoyote ile. Huu mkutano kauita baada ya kuona hali ya umeme imepungua makali, nyie subirini tu katika siku chache zitakazokuja akiulizwa kuhusu umeme, ndo utamueleza majibu atakayotoa!!!

I am just seek and tired with Mr. Prezidaa's words...
 
So far I'm sure he doesn't even remember what he said yesterday!!!!!!!
 
mkuu
you are right. Mkuu wa kaya alikuwa ameiweka tz katika 'auto pilot' sasa aliporudi akijaribu kuingiza gear zinakataa. Haya yangekua na maana kubwa yangekuja wakati ule kila mtu anazungumzia hili janga sasa inatuchanganya kwani yeye anaonekana mgeni nyumbani kwake
 
Binafsi ningependa kujua kama Rais alitumia neno "hali ya dharura" which still falls under "state of emergency"...
Kama hujui Rais alitumia maneno gani kwa nini post ya kwanza ya thread umenukuu? Umemnukuu nani? Umetoa wapi hiyo quote, umeitunga? Halafu unasingizia magazeti.

Nadhani umefanya kusudi, intrigues zako nazielewa uzuri. Kwa sababu, kwanza, unajua fika kuwa sheria na Katiba ya nchi haina kitu kama "hali ya dharura." Ibara ya 32 imeanisha "hali ya hatari," period! There is no such thing as "hali ya dharura."

Second, umem quote mtu kwa lugha mbili, ikimaanisha fika kwamba nukuu moja ni tafsiri yako wewe! Lakini ulitaka kutuchanganya makusudi ili tusijue Rais katamka maneno yepi, emergency au dharura. Na unajua fika kwamba kisheria emergency sio dharura, ni hatari, na Rais hakutamka neno hatari wala emergency. Taarifa yako iliopoonekana ni uongo ukataka kusingizia magazeti.
 
Here I can see now there are two things involving the speech of Mr. present. One is the way he was addressing his subordinates, two is the way Mzee Mwanakijiji presented the issue.
You can agree with me that Mr. Present was not talking about a Country being in Emergency State he was addressing the issue of Power by lamenting his subordinates the way they are acting on the issue. I think Daily News made a mistake on selection of words sio kosa lako mzee mwanakijiji
 
Jamani 'State of Emergency' hutafsirika kuwa nchi iko katika hali ya hatari na sio hali ya dharura.......Rais kasema tuko katika dharura na sio hali ya dharura ndio maana nasema kachapia Kiswahili.......neno dharura lina mitego mingi kwenye mabasi wanaandika kimakosa mlango wa dharura kama tafsiri ya emergency door badala ya mlango wa kutumia kunapokuwa na hatari mfano mzuri wa matumizi ya neno hili ni huu:

Swahili Example: mpelekee Gloria ujumbe huu kwa dharura

English Example: take this message urgently to Gloria
 
Kwa nini kila mara tunakuwa katika udharura hasa kwenye suala muhimu kama la umeme. Tangu 2006 hadi leo Serikali ya kikwete ipo kwenye hali ya udharura na nadhani tutaendelea na udharura hadi 2015! Aibu kubwa kwa nchi. Inamaana viongozi wa CCM hawana mipango ya mudas mfupi, wa kati na muda mrefu?
A state of emergency is a governmental declaration that may suspend some normal functions of the executive, legislative and judicial powers, alert citizens to change their normal behaviours, or order government agencies to implement emergency preparedness plans. It can also be used as a rationale for suspending rights and freedoms, even if guaranteed under the constitution. Such declarations usually come during a time of natural or man made disaster, during periods of civil unrest, or following a declaration of war or situation of international or internal armed conflict. Justitium is its equivalent in Roman law.

In some countries, the state of emergency and its effects on human rights and freedoms and governmental procedure are regulated by the constitution and/or a law that limits the powers that may be invoked. Rights and freedoms may be suspended during an emergency, for instance, freedom of movement, but not non-derogable rights. In many countries it is illegal to modify the emergency law or the constitution during the emergency.
 
“Tuko katika hali ya dharura na mimi sioni hisia za uharaka wa kuchukua uamuzi na hatua nyingine muhimu za kukabiliana na udharura wa upatikanaji wa umeme na nyenzo nyingi za kuzalisha umeme.

“Hatuwezi kuendeleza kuwa na kigugumizi katika kuchukua maamuzi ya kuitoa nchi katika changamoto kubwa hizi za upatikanaji wa nishati,” Rais Kikwete aliwaambia watendaji hao wa Serikali yake wanaohusiana na sekta ya nishati"

Hayo ndio maneno ya mkuu wa kaya aliyoyatamka ikulu alipokutana na wadau wa umeme, mtu huyu huyu ndiye alimwambia mwandishi wa habari wa BBC huko South Africa baada ya kuulizwa mipango yake ya kumaliza tatizo akajibu kuwa serikali yake haina uwezo wa kutengeneza mvua leo hii ndio anadai haoni hisia za uharaka wa kuchukua uamuzi.

Namshangaa Kikwete anavyolalamika! Kama hawa watu amewapeleka Ngurdoto, hawakumwelewa, kawapeleka Hombolo hawajamwelewa, achilia mbali hizo semina zinazoitwa capacity building zisizotangazwa. Haya maneno mawili ndo watamwelewa?
 
kile kilikuwa kikao cha kupeana posho kutoka kodi za walalahoi wa tanzania kwani pale wengine hawahusiki na umeme
 
Jinsi ilivyoripotiwa ni kana kwamba alimaanisha anashangazwa kwanini watu hawaonekani kuonesha "a sense of urgency" na wanashindwa kufanya maamuzi magumu. Waandishi wetu wanatumia neno "hali ya dharura" au "state of emergency" kama walivyoripoti Daily News bila kujua kuwa maneno hayo ni maneno ya kisheria na yana maana yake yanapotumiwa na RAis. Binafsi ningependa kujua kama Rais alitumia neno "hali ya dharura" which still falls under "state of emergency"..

Kwa hiyo wewe ndio bingwa wa kutafsiri alichomaanisha?

Kwa ufupi tafsiri yako si sawa next!
 
Back
Top Bottom