Sorry madam (Destination of my enemies)

Mkuu mbona ilipoishia ile sehemu ya mwisho na ilipoanzia leo kama hamna uhusiano.
kuna matatizo yametokea kidogo.. sehemu ya 71 mpaka 80.. zimecollapse.. na hiyo sehem ya 71 nimepost kimakosa ni ya part1 ya hadithi hii.. endelea tu kusoma utaelewa.
 
SORRY MADAM (90)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
INGHIA GOOFLE PLAYSTORE NA DOWNLOAD
APPLICATION(APP) YA STREAM NATION UWEZA
KUSOMA STORI ZA WAANSHI MAHIRI EDDAZARIA
G.MSULWA NA GIFT KIPAPA KWA VIFURUSHI VYA
MWEZI KWA SH 5000 NA KIFURUSHI CHA WIKI
MBILI KWA SH 3000.
ILIPOISHIA
“Na tambua Eddy nimesha mfahamu, na Eddy huyo
huyo ndio atakaye kuja kuja kukuangamiza, na
kuanzia hivi sasa usinihusishe na mipango yako ya
kikatili”
Manka alizungumza kwa hasira huku akijikongoja
kutoka mlangoni ila kabla hajafika mlangoni huku
nyuma akasikia bastola ikikokiwa, taratibu
akageuka na kumkuta Mzee Godwin akiwa
amemnyooshea bastola ya uso, huku macho yam
zee Godwin yakiwa yametawaliwa na ukungu
mwekundu wa hasira hadi mkono wake ulio shika
bastola ukawa unatetemeka.
ENDELEA
“Na mimi unahitaji kuniua, kama unavyo hitaji
kumuua Eddy?”
Manka alizungumza huku machozi yakimwagika,
Mzee Godwin akaendelea kumshikilia Manka
bastola huku akizidi kutetemeka kwa hasira.
“Kwa nini hukumuua Mery nilipo kuagiza pale
Arusha?”
“Damu ni nzito kuliko maji baba, na Mungu aliweza
kunipa roho ya ujasiri ya kumuacha akiwa hai,
kumbe ni mama yangu mdogo. Nimekua bila ya
kuwa na mama, ila wewe hulioni hilo hadi unahitaji
nimuue mama yangu mdogo si ndio?”
Hasira ya Manka na kulia kwake kukamfanya
aishiwe nguvu, za miguu na kujikuta akianguka
chini. Kwa haraka mzee Godwin akairudisha
bastola yake mkononi na kumnyanyua Manka na
kumuweka kitandani kisha akatoka chumbani
humo akiwa na hasira kali.
“Hakikisheni Manka hatoki humu ndani”
“Sawa mkuu”
Mzee Godwin akaondoka huku akiwa na mlinzi
wake anaye muamini, moja kwa moja wakarudi
ikulu kuendelea na majukumu yao.
***
Rahab, Phidaya na Agnes walikesha wakipiga
hadithi mbalimbali, kila mmoja akijaribu kusimulia
maisha yake ya utotoni na usichana.. Hadi inafika
alfajiri hapakuwa na aliye pata hata lepe la
usingizi, kila mmoja wao aliweza kufikiria mambo
yanayo muhusu kwenye maisha yake hususani
kwa wakati huu.
“Yaani Erickson ninampenda sana, na endapo
nitakuja kujua ana mwanamke mwengine
nitahakikisha nina muua huyo mwanake”
Agnes alizungumza kwa kujiamini na kuwafanya
Phidaya na Rahab kutazama, kabla ya Phidaya
ajazungumza kitu Rahab akamuwahi.
“Shoga wewe nawe kwa wivu, unamuua
mwanamke mwenzako kisa mwanaume?”
“Ahaaa weee Erickson wangu mtamu sana, yaani ni
mwanaume shababi, anaye jua kucheza na
mwanake sita kwa sita”
“Cha kufanya inabidi ikitimu saa mbili uende
ukamuangalie hospitalini”
“Hapo Rahab umezungumza poit huwa
ninakupendea hapo tu”
“Ndio hivyo usijikalie hapa kumbe kama ulivyo
tuambia mpenzi wako ni mgonjwa”
“Sawa”
Muda wote huo Phidaya alikaa kimya akiyafikiria
maneno ya Agnes jinsi yalivyo utibua moyo wake,
hata urafiki ambao ulikuwa kwa masaa machache
tayari umesha ingia shubiri. Wakaandaa kifungua
kinywa, kila mtu akanywa kwa jinsi alivyo weza
kunywa chai hiyo yenye itafunwa vingi.
Phidaya akarudi sebleni alipo iacha bahasha yake,
akaichukua pamoja na karatasi iliyopo pembeni
ambayo hakuiweka kwenye bahasha hiyo. Kabla
hajaiingiza karatasi hiyo ndani ya bahasha
akaipitishia macho taratibu ili kufahamu ni karatasi
za nini. Phidaya hakuamini kitu alicho kiona
kimeandikwa kwenye karatasi hiyo, maelezo
yanaonyesha uhusiano alio kuwa nao Erickson
ambaye ni Eddy pamoja na Manka ambaye ni wifi
yake.
‘Imekuwaje hadi ukweli umejulikana?’
Phidaya alijiuliza huku akiketi kwenye sofa, macho
yake yakawa na kazi ya kuirudia rudia karatasi hiyo
mara kadha.
‘Ila dokta aliye fanya hivi alisha kufa’
Phidaya alizidi kuzungumza mwenyewe huku
akiitazama karatasi hiyo, hadi Rahab anafika
sebleni hapo, ndipo alipo iingiza karatasi hiyo
kwenye bahasha.
“Karatasi za nini?”
Rahab aliuliza huku akijirusha kwenye sofa.
Phidaya hakujibu kity chochote zaidi ya kukaa
kimya.
“Vipi mbona kimya?”
“Agnes yupo wapi?”
“Nimemuacha akielekea chumbani kwake kuoga”
“Kuna kitu nahisi hakipo sawa”
“Ahaaa kama ni mada hizo tutazizungumza
tukiondoka hapa”
Rahab alizunguzma kwa sauti ya chini huku
akimtazama Phidaya kwa macho makali. Haukupita
muda sana Agnes akatoka akiwa amevalia suti
nyeusi. Akamrushia Rahab funguo ya gari moja
huku yeye akiwa na funguo ya gari la serikali.
“Mutatumia gari hiyo”
“Una magari mangapi shosti?”
“Mmmm huko uwani yamejazana mengi, sikumbuki
kwa haraka nina magari mangapi, si unajua
kwamba starehe yangu kubwa ni magari”
“Wewe kiboko”
Wakatoka kwa pamoja na kuelekea eneo la nyuma
la nyumba ya Agnes ambapo kuna banda kubwa
alilo lijenga lenye magari mengi yaliyo funikwa.
Rahab akayahesabu kwa haraka haraka akapata
idadi ya magari ishirini na tano.
”Wee mtoto wa kike magari yote haya ni ya nini?”
“Wee acha tu sina mtoto sina ndugu, pesa yangu
yote ninayo ipata ni kununua magari. Hapo kuna
magari ambayo tangu niyanunue, nimeyaendesha
kutoka bandarini hadi hapa”
“Wee kiboko sasa hii funguo uliyo nipa nitafungulia
gari lipi?”
“Minya rimoti, litakalo piga alamu ndio hilo hilo”
Rahab akafanya kama alivyo ambia, gari la
pembeni lake likaanza kupiga alamu, wakalifunua
turubai lililo lifunika gari hilo.
“Hiyo ni Alteza new modern zimetoka mwaka huu”
Agnes alizungumza huku akilitazama gari yake
hiyo mpya kabisa. Rahab akaingia na kuliwasha
gari hilo.
‘Mamaeee huyu msenge ana hela’
Rahab alijisemea kimoyo moyo, baada ya gari hiyo
kumuonyesha tanki lake limejaa mafuta. Rahab
akafungua kioo cha upande wake ili kuzungumza
na Agnes.
“Wee mtoto sikuwezi”
“Kwa nini?”
“Gari ipo full tank, nilidhani itakuwa na mafuta ya
kulisukumia hadi sheli”
“Nyoo, gari zote hapa unapo ziona zipo full tank.
Sasa utawasiliana na mimi ukiwa na simu, au hadi
simu nikupe”
“Acha ujinga, nitanunua”
“Haya mwaya, Phidaya karibuni tena jamani”
“Asante”
Phidaya akaingia ndani ya gari, wakaondoka na
kumuacha Agnes akiingia kwenye gari lake lenye
namba za usajili za wizara yake. Moja kwa moja
Agnes akaanzia hospitali ya Agakhan, ambapo
akaelekea kwa daktari mkuu wa hospitali hiyo.
Akamuuliza kuhusiana na mgonjwa wake ambaye
ni Erickson Ford, majibu aliyo kutana nayo
yakamshosha sana.
“Ameibiwaje ibibiwaje?”
“Kusmea kweli mimi jana sikuwepo usiku, ila
nasikia hata walinzi wa raisi walishindwa kuwazuia
hao walio muiba”
“Mungu wangu sasa itakuwaje?”
“Ndio hapo naona muheshimiwa ana lishuhulikia
huli, naamini atapatikana tu”
“Sawa nashukuru dokta”
Agnes akaondoka hospitalini hapo huku akiwa
amejawa na mawazo chungu nzima, hakujua ni
nini anacho weza kukifanya ili kumpata Erickson
wake.
***
“Tunaelekea wapi?”
“Tunaelekea Bagamoyo”
“Hivi unatambua kwamba hatujampata Eddy na kitu
kilichopo kwenye hizi karatasi zinaonyesha
kwamba Eddy na Manka ni ndugu na inavyo
onyesha kuna kamchezo ambacho kamechezeka
hapa”
Ikambidi Rahab kusimamisha gari lake pembeni na
kuchukua karatasi anazo pewa na Phidaya,
akazitoa kwenye bahasha na kuzitazama kwa
umakini. Macho yakamtoka alipo weza kuona
majibu hayo ya DNA
“Umezipatia wapi hizi karatasi?”
“Kwa daktari mmoja ambaye alijirusha dirishani
baada ya kuniona anaoneka alisha wahi kufanya
mpango wa kuniua akiwa na Ranjiti aliye kuwa
mume wangu”
Rahab akazipitia karatasi hizo zenye maelezo ya
kina hadi jina la Eddy liliandikwa humo ndani,
anaye tajwa kwamba ndio Erickson Forrd.
“Na ninavyo hisi huyo rafiki yako Agnes atakuwa
amezisoma karatasi hizi”
“Mungu wangu”
“Yaani hapa tunatakiwa kuhakikisha kwamba
tunampata Eddy na kama ni vipi ni lazima tuweze
kurudi Agakhan, tukamtafute”
Rahab akafikiria kwa sekunde kadhaa, hapo hapo
akageuza gari kwa kasi na safari ya kuelekea
hospitali ya Agakgan ikaanza huku mawazo yao
yote yakimuwaza Eddy.
Wakafika hospitali ya Agakhan, wakalikuta gari
ambalo alikuwa akilitumia Eddy likiwa katika eneo
la maegesho. Wakiwa hapo wakamuona raisi
Godwin akiingia kwenye gari lake pamoja na
walinzi wake, wakawasubiria waondoke hapo kisha
Rahab akashuka na kuelekea lilipo gari ambalo ni
mali yake.
“Sijui ametoroshwa toroshwa vipi”
“Nasikia walio mtorosha ni wanawake mmoja ni
kama mchina machina hivi”
Rahab aliweza kuyasikia mazungumzo ya wauguzi
hao wawili wanao fanya usafi katika eneo hilo la
maegesho.
“Lakini nasikia yule ni mke wa raisi ndio maana
mwenyewe akaja hapa”
“Yaani hao walio mtorosha watakiona cha
mtemakuni, si unaona mzee alivyo toka hapa jicho
jekundu kama ndimu”
Rahab aliendelea kuwasikiliza wauguzi hao wa kike
wanao onekana kuutumia mdua wao mwingi katika
kupiga stori pasipo kufanya kazi. Rahab akajaribu
kuufungua mlango wa gari lake, kwa bahati nzuri
haukufungwa.
“Hivi huyo aliye toroshwa si ndio yule aliye pigwa
na polisi”
“Ndio huyo, anaitwa Erickson”
“Samahani dada zangu”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wauguzi
hao walio katisha mazungumzo yao haraka
iwezekanavyo, wauguzi hao wakaonekana
kumkazia macho Rahab, wakijaribu kumfananisha
na mke wa raisi aliye pita, ila mavazi aliyo yavaa,
wakaamini kwamba mke wa raisi hawezi kuvaa
mavazi ya aina hiyo wakiamini watakuwa
wamemfananisha.
“Eti Erickson ametoroshwa?”
Wauguzi hao wakatazamana kisha wakamtazama
Rahab anaye wauliza swali hilo.
“Ahaa naamini mutakuwa munanishangaa kuweza
kuwauliza swali kama hilo, ila Erickson ni kaka
yangu”
“Waooo kumbe ni mkwe wa raisi?”
Rahab akatabasamu huku akitingisha kichwa
akikubaliana na wauguzi hao ambao wanaonekana
kufurahishwa na kauli hiyo.
“Sasa basi, ila hizi ni fununu fununu tu. Tunasikia
eti jana, Erickson alivyo letwa na mchumba wake
Manka kuna wanawake walikuja wakamteka, huyo
mmoja wanasema ni mswahili ila mwengine ni
Mchina. Tena wamepigaje huyo Manka nasikia
kwamba eti ni bwana wao”
“Bwana wa nani hapo?”
Rahab aliuliza kama vile hawajui Madam Mery
pamoja na Sa Yoo.
“Huyo mwanamke nasikia ndio mpenzi wake na
huyo mchina amekuja naye kupiga kug fu,
wamemtandika Manka hadi kalazwa huko ndani”
“Asanteni jamani”
“Ila umbea nao dili dada. Yaani umefanana na mke
wa raisi Godwin aliye pita”
Kauli ya muuguzi huyo mmoja ikamstua Rahab, ila
akajikata kuutoa mstuko huo ili wauguzi hao
wasimstukie.
“Ahaa si unajua kwamba duniani watu ni wawili
wawili”
“Kweli aisee mumefanana, hadi kucheka”
“Kweli jamani asanteni”
Rahab akaingia kwenye gari hilo, na kuikuta funguo
ya gari ikiwa eneo la funguo na inavyo onekana
jana Manka alivyo fika nalo hapo hospitalini
hakuichomoa. Akawasha na kuliweka sawa gari
hilo, akaliendesha hadi sehemu alipo muacha
Phidaya ndani ya gari la Agnes.
“Endesha hilo tuondoke”
“Imekuwaje?”
“Sa Yoo na Madam Mery wamemchukua”
“Sasa watakuwa wamekwenda wapi?”
“Bagamoyo nahisi?”
“Mmmm kwa bagamoyo itakuwa ngumu si unaona
pale njiani kuna kizuizi cha Polisi”
“Sasa watakuwa wamekwenda wapi?”
“Nimepata wazo hembu tukawatazame nyumbani
kwangu, tukiwakosa hapo basi tutajua ni wapi kwa
kwenda”
“Sawa”
***
Kwa haraka Madam Mery akamuwahi Shamsa na
kuanza kusugua sugua kifuani mwake ila kutapika
kupungue. Sa Yoo naye aliye kuwa amelala
akakurupuka baada ya kusikia sauti ya Shamsa,
akiugulia ugulia.
“Ehee vipi tena?”
Sa Yoo aliuliza kwa mshangao huku akisimama.
“Kamletee maji jikoni”
Sa Yoo akauondoka hospitalini hapo, baada ya
dakika mbili akarudi akiwa ameshika kombe
kubbwa lililo jaa maji pamoja na kidishi kidogo.
Akamnywesha Shamsa maji, akasukutua na
kuyatemea maji hayo kwenye kidishi hicho.
“Unajisikiaje?”
“Maumivu mgongoni?”
“Ni risasi uliyo pigwa sijui na nani?”
“Kwanza nimefikaje fikaje hapa?”
Shamsa alizungumza huku akihema.
“Ulikuja jana na gari sisi tukasikia honi getini
kutoka tukakukuta ni wewe”
Gafla kitu kizito kilicho rushwa dirishani na kuvunja
dirisha hilo la kioo lililopo hapo hospitalini,
kikaanza kutambaa huku kikitoa moshi mwangi
mweupe na wenye hewa nzito inayo chefua
kuanzia koo hadi macho ya kila mmoja aliye
kuwepo katika sebule hiyo, alijikuta akikohoa huku
machozi yakimtoka. Kabla hawajajua ni nini cha
kufanya milio ya risasi ikaanza kusikaka nje
ikivunja vunja vioo vya madirisha ya sebule nzima
na kuwafanya Sa Yoo na wezake kuchanganyikiwa.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 91 YA SIMULI HII.
 
ile imehamishiwa jukwaa la wakubwa omba access ya jukwaa hilo kwa invisible
Doh, invisible mwenyewe ha respond, una namba Yake??? Au na Mimi nianzishe topic yangu ya kitandani anihamishie Kule automatic??
 
SORRY MADAM (91)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
JIUNGE NA MAGROUP YANGU YA WHATSAPP NA
FACEBOOK, YANAYO HUSIANA NA HADITHI TU KWA
KIIINGILIAO CHA SH 2000 KWA MWENZI.
0657072588.
ILIPOISHIA
Gafla kitu kizito kilicho rushwa dirishani na kuvunja
dirisha hilo la kioo lililopo hapo hospitalini,
kikaanza kutambaa huku kikitoa moshi mwangi
mweupe na wenye hewa nzito inayo chefua
kuanzia koo hadi macho ya kila mmoja aliye
kuwepo katika sebule hiyo, alijikuta akikohoa huku
machozi yakimtoka. Kabla hawajajua ni nini cha
kufanya milio ya risasi ikaanza kusikaka nje
ikivunja vunja vioo vya madirisha ya sebule nzima
na kuwafanya Sa Yoo na wezake kuchanganyikiwa.
ENDELEA
“Nini hicho jamani?”
Sa Yoo aliuliza huku akikohoa sana, japo
anaelekewa kabisa ni kitu gani kinacho tokea, ila
alijikuta akiuliza swali ambalo hapakuwa namtu
hata mmoja aliye weza kulijibu kwa haraka zaidi ya
wote kukohoa kohoa.
“Sa Yoo msukumeni Eddy munifwate”
Shamsa alizungumza huku akijikaza kunyanyuka
kwenye kochi, Sa Yoo na Madam Mery nao
wakajikaza kusukuma kitanda hicho alicho lalia
Eddy, ambaye naye muda wote ana kohoa.
Wakamfwata Shamsa aliye ingia kwenye moja ya
chumba ambacho hakina kitu chochote zaidi ya
picha picha nyingi zilizo bandikwa ukutani, Sa Yoo
akafunga mlango wa chumba hicho na kumtazama
Shamsa akitoa picha kubwa iliyopo ukutani.
Shamsa aalipo fanikiwa kusogeza picha hiyo iliyo
ficha batani nyingi zilizopo kwenye ukuta. Shamsa
kwa haraka kwa kutumia mkono ambao hauna
jeraha, akaminya batani hizo akionekana zina
namba ya siri, Sa Yoo na madam Mery wakajikuta
wakishangaa, kipande cha ukuta mwengine ndani
ya chumba hicho ambacho kikifunguka.
“Nendeni”
Shamsa alizungumza, Madam Mery na Sa Yoo
wakamsukuma Eddy hadi ndani ya chumba hicho
ambacho ni cha siri, kisha yeye akaingia na ukuta
huo kujifunga. Shamsa akawasha taa zilizomo
ndani humo. Ukubwa wa chumba hicho kilicho jaa
mitambo mingi, kikawashangaza Madam Mery na
Sa Yoo.
“Waoooo”
Sa Yoo alizungumza huku akisogelea moja ya
mtambo mkubwa uliopo ndani ya chumba hicho,
akiushangaa jinsi ulivyo.
“Hii ni nini?”
“Anaye fahamu ni Eddy mwenyewe, mimi huwa
nina iona tu hiyo mitambo”
“Eti Eddy hii ni mitambo ya nini?”
“Nitawaambia pale muda utakapo fika”
***
Kitu cha kwanza baada ya kufika ikulu, Mzee
Godwin akaitisha kikao cha dharura. Wataalamu
wake maalumu wanao husika na maswala ya
teknologia, akakutana nao kwenye ukumbi huo wa
mkutano huku akiwa na kartasi mbili zenye sura ya
Sa Yoo pamoja na madam Mery.
“Nahitaji hizi sura muzitafute sasa hivi kwa
kutumia satelait”
“Sawa mku”
Kazi ikaanza ya kuzitafuta sura za Madam Mery na
Sa Yoo. Wataalamu hao wakazichukua picha hizo
na kuzi scan na kuziingiza kwenye mtandao
maalumu ambao wameuunganisha na satelaiti
zenye rekodi ya kila kiumbe aliyepo juu ya ardhi.
Sura za watu kadhaa ndani ya Tanzania zikaanza
kupita kwa kasi kwenye kioo kikubwa cha Tv
iliyopo humo ndani ya ofisi ya raisi, iliyo
unganishwa na kompyuta inayo fanya kazi hiyo ya
kutafuta sura hizo za watu.
Alama nyeukundu ikalia na kuonyesha sura ya
madam Mery na sehemu ilipo, haikuchukua muda
sana ikaonyesha na sura ya Sa Yoo na wote
wanaonekana wapo sehemu moja.
“Andaeni kikiso ninakwenda kuwatafuta watu hawa
hakikisheni kwamba wanapatikana wakiwa hai”
“Sawa mkuu”
Mzee Godwin akingia ndani kwake, akabadilisha
mavazi yake, akavaa kombati za jeshi ambazo
alikuwa anazitumia akiwa mkuu wa majeshi kabla
ya kuliasi. Akachukua bastola zake mbili zenye
silaha za kutosha. Akatoka nje na kukuta kikosi
cha vijana wake wapatao ishirini wakiwa wamesha
jiandaa kwenye magari maalimu yenye uwezo wa
kubebe silaha nzito.
“Mkuu nakuomba usiende”
Mlinzi wa mzee Godwin alizungumza huku
akimzuia, ila kwa jicho kali alilo katwa na mzee
Godwin akajikuta akitulia kimya, na kumfwata mzee
huyo anaye onekana kushikwa na hasira kali sana.
Wakaingia kwenye magari, mlinzi wa mzee Godwin
akatoa simu yake na kuandika ujumbe mfupi wa
mesiji na kuutuma kwenye simu ya mmoja wa
walinzi wanao mlinda Manka hospitalini.
“Lazima huyu malaye leo nimuue kwa mkono
wangu mimi mwenyewe”
Alizungumza Mzee Godwin huku magari yakizidi
kusonga mbele kuelekea sehemu ambapo ndipo
anaamini alipo Madam Mery pamoja na Sa Yoo
walio muiba mkwe wake, aliye pelekea hadi Manka
kuwa na gadhabu sana.
***
“Madam kuna ujumbe ambao nimepewa nikupatie”
Mlinzi huyo alizungumza huku akimkabidhi Manka
simu yenye ujumbe ulio tumwa, unao someka
‘MUHESHIMIWA ANA GADHABU SANA, ANA
KWENDA KUMVAMIA MADAM MERY NA
INAONEKANA SEHEMU TUNAPO ELEKEA NI
NYUMBA YA ZAMANI YA KAKA YAKO EDDY’
Ujumbe huo ukamkurupusha Manka kitandani na
kujikuta akishuka na kusimama, akamtazama
mlinzi huyo aliye simama pembeni yake.
“Kuna gari?”
“Ndio muheshimiwa”
“Nahitaji kuondoka hapa sasa hivi”
“Ila muheshimiwa alisema kwamba usiondoke”
“Unataka kumuona muheshimiwa wako anaingia
kwenye matatizo mengine ambayo yataigharimu
serikali eheeee”
Manka alizungumza kwa hasira hadi mlinzi huyo
akawa ana tetemeka. Hapakuwa na jinsi zaidi ya
kukubali kuondoka hospitalini hapo. Mlimzi mmoja
akawa na jukumu la kuiendesha gari hilo la ikulu
huku mwengine akiwa ameketi siti ya nyuma, na
Manka akawa na kazi ya kumuelekeza mlinzi huyo
ni wapi kwa kwenda. Kwa njia za mikato mikato
wakafanikiwa kukuta msafara wa Mzee Godwin
ukiwa unakaribia kabisa kufika nyumbani kwa
Eddy.
“Uzuie kwa mbele”
“Sawa madam”
Mlinzi huyo akaongeza mwendo ulio zipita gari
zote hizo, akafunga breki kwa mbele, na kuiziba
barabara nzima ya lami na kusababisha gari zote
zilizopo kwenye msafara kusimama gafla. Manka
akaitazama saa iliyomo ndani ya hilo gari
inaonyesha ni saa moja kasoro. Akashuka kwenye
gari na kusimama mbele ya msafara wa magri
hayo.
“Huyu mtoto mwendawazimu amekuja kufanya
nini?”
Mzee Godwin alizungumza huku akishuka kwenye
gari hilo macho yake yakiwa na hasira kali sana,
akamtazama Manka aliye simama mbele ya
msafara huo huku mikono yake akiwa
ameinyoosha kama yesu alivyo sulubishwa.
Akaachia msunyo mkali na kuanza kutembea kwa
mwendo wa haraka hadi sehemu alipo simama
Manka.
“Baba kwa nini unaf…….”
Kofi zito lililo tua shavuni mwa Manka likamfanya
akatishe ile kauli ambayo alianza kuizungumza.
Kila mlinzi aliyopo eneo hilo akawa kimya
akitazama vita kati ya baba na mwana.
“Ondoka mbele ya uso wangu”
Manka huku machozi yakimwagika, akanyoosha
tena mikono yake kama alivyo kuwa ameinyoosha
hapo awali.
“Baba kwa nini unataka kumuua mama mdogo
amekufanyia nini wewe?”
Kofi jengine zito likatua shavuni mwa Manka, hili
likamfanya kuyumba mara kadhaa, kisha akaka
sawa na kurudia mtindo wa kunyoosha mikono
yake na kumzuia mzee Godwin asifanye chochote
juu ya madam Mery.
“Huwa nikiwa katika hali kama hii sinto jail kama
wewe ni mwanangu au laa, nitakuchangua ubongo
wako. Toka mbele ya uso wangu”
“Baba siwezi kufanya hivyo”
Mzee Godwin kwa hasira akachomoa bastola yake
na kumnyoshea Manka aliyo isogelea karibu kabisa
na kuigusa bastola hiyo kwa paji lake la uso.
“Kama utakubali kuona damu ya mwanao
mpendwa wa kike ikimwagika mbele yako nipige
risasi”
Mzee Godwin akamtazama jinsi Manka alivyo
simama mbele hapo, bila ya Manka kujua ni kitu
gani kinaweza kufwata akastukia akipigwa na
kitako cha bastola hiyo kwenye shingo yake na
kuanguka chini na kupoteza fahamu.
Mzee Godiwin akawaamuru walinzi hao hao ambao
walikuja na Manka wamchukue na kumpekea ikulu,
huku safari ikaendelea. Wakafika kwenye geti
kubwa, mzee Godwin akashanga kuona ni
nyumbani kwa Eddy na anapafahamu vizuri sana.
“Pumbavu huyu mshenzi ndio aliye watuma hawa
malaya zake kumteka mkwe wangu, pumbavu
sana”
Mzee Godwin alizungumza huku akishuka kwenye
gari, akawaamuru askari wake alio kuja nao
kuvamia ndani ya nyumba hiyo na kuhakikisha kila
aliye kuwemo ndani ya nyumba hiyo anatiwa
mikononi akiwa hai.
Askari wenye mabomo ya machozi wakingia ndani
ya geti kwa umakini huku wakiwa wamavalia vifaa
maalumu vya kujikinga na moshi mkali wa
mabomu hayo. Wakakuta gari mbili zikiwa nje
hapo huku moja likiwa ni gari la wagonjwa, lililo
ibiwa jana hospitalini.
“Wamo humu humu ndani”
Mmoja wa askari alizungumza huku akinyata hadi
dirishani, akasikia sauti za kike bila ya kuuliza
mara mbili mbili akarusha bomu moja la machozi
mwenzake akarusha bomu la pili la machozi, kisha
wakarudi nyuma. Askari wengine walio kuwepo
nyuma yao wakanza kushambulia kwa risasi.
Kwenye vioo pamoja na milangoni.
“Acheni kushambulia”
Mzee Godwin alipaza sauti na kuwafanya askari
wote kuacha kushambulia kwa risasi ndani humo
“Nimesema ninahitaji wakiwa hai sitaki hata mmoja
nimkute amekufa”
“Sawa mkuu”
Ikawabidi askari hao kuvamia ndani, na kukuta
sebleni hakuna mtu ila kuna vitu vina ashiria
kwamba watu wapo humu humu ndani ya hii
nyumba.
***
Rahab akajikuta akipunguza mwendo kasi wa gari
lake, baada ya kuona gari mbili za ikulu ambazo
hutumika kwenye mashambulizi hususani pale
ikulu inapo vamiwa zikiwa zimesimama nje ya geti
la nyumba ya Eddy.
“Kuna nini pale?”
Phidaya aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka.
Tayari wasiwasi mwingi ulisha anza kumvaa
“Pale kuna uvamizi”
“Uvamizi wa nini tena”
“Walinzi wa mzee Godwin ndio wamevamia eneo
hili”
“Mungu wangu wamesha jua ni wapi Eddy alipo”
“Usishuke kwenye gari”
Rahab alizungumza huku akishuka ndani ya gari,
baada ya kulisimamisha gari lake mbali kidogo na
ilipo nyumba ya Eddy. Akaanza kutembea kwa
mwendo wa tahadhari. Milio ya risasi, ilimuashiria
kabisa, ajiweke tayari kwa lolote. Akazidi kupiga
hatua hadi karibu kabisa na lilipo simama gari
moja, akachungulia ndani ya gari hilo akakuta
hakuna mtu wa aina yoyote.
Akanyata hadi kwenye gari la pili akakuta kuna
askari mmoja amesimama nje hapo huku akiwa
ameshika bunduki yake. Bila ya kupoteza muda
Rahab akamrukia askri huyo, akampiga ngumi
kadhaa na kumuzimisha hapo hapo.
Akaichukua bunduki hiyo na kusimama getini,
akachungulia na kuona jinsi Mzee Godwin anavyo
pandisha ngazi za kuelekea ndani ya jumba la
Eddy. Nje ya kuna askari wanne wamesimama
wakiwa na bunduki zao.
Rahab akatoa magazine ya bunduki hiyo aina ya
AK-47 na kukuta ina risasi za kutosha, akashusha
pumzi kidogo huku akifumba macho yake,
kumbukumbu za bomu lililo muua mume wake
aliye kuwa raisi, zikamjia kichwani mwake na
kujikuta akifumbua macho huku ameyeng’ata
meno, akaanza kuzimimina risasi hizo kwa askari
hao walio simama akili na macho yao zikiwa
kwenye tukio hilo.
Rahab alipo hakikisha kwamba askari hao wote
wamekufa, akaingia ndani huku bunduki yake ikiwa
mkononi mwake, akajibanza kwenye gari la
wagonjwa na kusikilizia ni nini kinacho endelea
huko ndani.
“Nenda kaangalie ni nini kilicho tokea nje huko”
Mzee Godwin akamuagiza mlinzi wake akatazame
nje baada ya kusikia milio ya risasi. Milio mlio wa
risasi ukwastua Mzee Godwin na askari wake na
kuwafanya akili zao zote kuzipeleka nje na
kuachana na swala la kuwaska Madam Mery na Sa
Yoo.
“Mlindeni raisi”
Mmoja wa askari hao alizungumza huku wakiwa
wanatoka nje, wakiwa wamemzunguka raisi
Godwin na kumuweka katikati.
“Yes nafasi nzuri sana”
Rahab alizungumza huku akinyanyuka kutoka
katika sehemu aliyo jibanza. Kila risasi moja anayo
ipiga inaondoka na askri mmoja. Mzee Godwin
akajikuta akichanganyikiwa baada ya kuzidi
kuwaona askari wake wanaanguka mmoja baada
ya mwengine hadi akabaki yeye mwenyewe.
“Mikono juu”
Rahab alizungumza huku akimuamuru Mzee
Godwin aliye inyoosha mikono yake juu pasipo
kupenda. Bastola zake zote mbili akazitupa
pembeni akiashiria kushindwa.
“Rahab…….?”
“Ndio mimi, una shangaa sana kuniona eheee?”
Rahab alizungumza huku akiwa ameushikilia mtutu
wa bunduki akipiga hatua za taratibu akimfwata
mzee Godwin katika eneo alilo simama.
“Wewe na mumeo si niliwaambia muondoke nchini
kwangu?”
“Nchi hii wala sio ya kwako. Huna maamlaka ya
kunifukuza mpumbavu wewe”
“Mshezi wewe nitaku…….”
Rahab akamtandika mzee Godwin risasi ya mguu
na kumfanya aanguke chini na kutoa ukelele mkali
wa maumivu. Ukimya ulio tawala kwa dakika
kadhaa ukamfanya Phidaya kushuka ndani ya gari
na kuanza kutembea kwa umakini huku akielekea
getini, alipo fika, akachungulia, akamuona Rahab
alivyo mshikia bundiki Mzee Godwin. Phidaya
akaingia kwa kujiamini hadi sehemu alipo simama
Rahab
“Phidaya!!”
“Mshenzi mpumbavu huyu mzee muue”
Phidaya alizungumza kwa hasira huku akiwa
amemkodolea macho mzee Godwin.
“Phidaya nenda ndani ukawatazame kina Sa Yoo”
“Sawa”
Phidaya akapandisha ngazi hizo kwa haraka hadi
sebleni, hakukuta mtu kwa haraka akili yake
ikamtuma kupandisha gorofani ambapo pia
hakukuta mtu wa aina yoyote. Kwa haraka
akashuka na kukumbuka kuna chumba ambacho
siku za nyuma mume wake alisha mueleza kukiwa
na tatizo anaweza kukimbilia kwneye chumba
hicho na kujificha.
Akaingia kwenye chumba hicho na kukuta sehemu
ambayo kuna batani nyingi, picha yake ikiwa
imeondolewa. Akaingiza namba za siri za
kuufungua mlango huo ulio kaa mithili ya ukuta,
ukafunguka na kukutana na mwanga wa taa
ukionyesha kwamba watu wamo humo ndani.
Phidaya akaingia ndani humo, hakuamini macho
yake baada ya kuwakuta Shamsa, Eddy, Sa Yoo na
Madam Mery wakiwa wanatizama ni nani anaye
ingia. Sa Yoo akamkimbilia Phidaya na
kumkumbatia kwa nguvu.
“Tumeshinda jamani”
Phidaya alizungumza kwa furaha huku akimuachia
Sa Yoo na kumfwata mume wake sehemu alipo
lala. Cha kwanza kukifanya akampiga busu la
mdomo Eddy aliye achia tabasamu pana baada ya
kumuona mke wake huyo.
“Honey tumemtia Godwin mikononi mwetu”
“What……?”
Madam Mery alizungumza huku akimtazama
Phidaya usoni, kwa maana jambo alilo lizungumza
hakuna mtu ambaye anaweza kuliamini kwa haraka
kiasi hicho.
“Rahab yupo hapo nje kwenye ngazi amemshikia
bunduki”
Sa Yoo akajikuta akishangilia kwa furaha, ila sura
ya Madam Mery ikapoteza furaha, na kumfanya
Eddy naye kupoteza furaha yake.
“Ina maana hamuniamini au?”
“Phidaya nina mjua Godwin hawezi kukamatika
kiholela kiasi hicho”
Madam Mery alizungumza kwa msisitizo, huku
akiwa amemkazia macho madam Mery
“Jamani nimemkuta akiwa amelala chini mguuni
amepigwa risasi”
“Kwa nini tubishane twendeni tukamuone”
Sa Yoo akaanza kukisukuma kitanda cha Eddy
huku Phidaya na Madam Mery wakiwa
wametangulia mbele, huku Shamsa akifwata kwa
nyuma. Wakatoka kwenye vyumba hivyo na
kwenda nje. Walipo fika kila mmoja akabaki
ameduwaa hususani Phidaya kwa maana Raisi
Godwin na Rahab wametoweka eneo hilo.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 92 YA SIMULI HII.
 
SORRY MADAM (92)
(Destination of my enemies)

WRITER………………………………………………………………….………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..…… www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT………………………………………………………………………….0657072588/0768516188
JIUNGE NA MAGROUP YANGU YA WHATSAPP NA FACEBOOK, YANAYO HUSIANA NA HADITHI TU KWA KIIINGILIAO CHA SH 2000 KWA MWENZI. 0657072588.

ILIPOISHIA
Sa Yoo akajikuta akishangilia kwa furaha, ila sura ya Madam Mery ikapoteza furaha, na kumfanya Eddy naye kupoteza furaha yake.
“Ina maana hamuniamini au?”
“Phidaya nina mjua Godwin hawezi kukamatika kiholela kiasi hicho”
Madam Mery alizungumza kwa msisitizo, huku akiwa amemkazia macho madam Mery
“Jamani nimemkuta akiwa amelala chini mguuni amepigwa risasi”
“Kwa nini tubishane twendeni tukamuone”
Sa Yoo akaanza kukisukuma kitanda cha Eddy huku Phidaya na Madam Mery wakiwa wametangulia mbele, huku Shamsa akifwata kwa nyuma. Wakatoka kwenye vyumba hivyo na kwenda nje. Walipo fika kila mmoja akabaki ameduwaa hususani Phidaya kwa maana Raisi Godwin na Rahab wametoweka eneo hilo
ENDELEA
“Wamekwenda wapi?”
Phidaya aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka. Madma Mery akajikuta akikaa chini, huku nguvu za mwili zikiwa zimemuishia.
“Tuondokeni eneo hili si salama”
Eddy alizungumza huku akijaribu kukaa kwenye kitanda, maumivu makali aliyo yapata kwenye mbavu zake hayakumzuia kabisa kuweza kunyanyuka na kukaa kitako.
“Utataka kwenda wapi Eddy?”
“Ni bora nyinyi kuondoka kuliko kuingia mikononi mwa askari”
“Unataka kusema kwamba…….”
Phidaya aliuliza huku macho yake akiwa amemtolea Eddy aliye lala kwenye kitanda hicho.
“Ondokeni eneo hili sio salamaa”
Eddy alizungumza kwa msisitizo na kuwafanya Shamsa kuelewa maana yake ni nini. Shamsa kwa haraka akaingia ndani, moja kwa moja akaelekea katika chumba ambacho walikuwepo. Akachukua mbastola nne zenye magazine zilizo jaa risasi kisha akatoka nje kwa haraka.
“Inabidi kuondoka eneo hili sasa hivi”
“Na Eddy?”
“Mimi mutaniacha hapa, ondokeni”
Taarifa hiyo, ikauingiza moyo wa Phidaya simanzi kubwa sana, kwa maana hakujua ni kwanini mume wake amechukua maamuzi kama hayo. Kwa haraka akamfwata Eddy kitandani na kukumbatiana huku Phidaya machozi yakimwagika, na Eddy machozi yakimlenga lenga.
“Nitakuwa salama”
Phidaya hakujibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuzidi kumwagikwa na machozi, tayari Shamsa alisha ingia kwenye moja ya gari, ambalo ni mali ya ikulu. Madam Mery na Sa Yoo nao wote wakaingia ndani ya gari hilo na kumsubiria Phidaya anaye endelea kumng’ang’ania mume wake.
“Nenda mke wangu nitakuwa salama”
“Niahidi hauto kufa?”
“Nakuahidi, kimbia kabla askari hawajafika hapa”
Phidaya akamuachia Eddy na kumpiga busu la mdomo, kisha akashuka kwenye ngazi hizo kwa haraka na kuingia ndani ya gari, Shamsa ambaye tayari alisha lifungua geti hilo muda alipo kuwa anashuka chini, akakanyaga mafuta ya gari hilo ambalo ni aina ya Aud 5q lenye sifa ya kuto kuingia risasi na ndio gari ambalo hutembelea raisi Godwin.
Kipindi gari hiyo inamalizikia kutoka nje, machozi yakatiririka usoni mwa Eddy ambaye hakuweza kujumuika katika safari hiyo, kwanza kutokana na mshono wa oparesheni aliyo fanyiwa jana tu, pili ni kutokana hajulikani kama yeye ndio Eddy, ila anajulikana kwa jina la Erickson Forrd hii ni kutokana na sura yake.
Hazikupita hata dakika tano, ving’ora vya gari za polisi pamoja na usalama wa taifa vikasikika nje ya nyumba ya Eddy. Alicho kifanya Eddy ni kujilaza kitandani hapo huku machozi yakiendelea kumwagika.
Askari wengi wenye bunduki mikononi mwao wakaingia ndani humo kwa umakini, wakaanza kukagua maiti moja baada ya nyingine.
“Erickson”
Eddy akamuona Manka akimfwata sehemu alipo lala. Taratibu Manka akapiga magoti chini, na kumbusu Eddy mdomoni.
“Nashukuru Mungu nimekupata”
Eddy hakujibu kitu zaidi ya kumwagikwa na machozi usoni mwake. Madaktari wa jeshi walio fika eneo hilo la tukio, wakamchukua Eddy na kumuingiza kwenye gari ya wagonjwa, huku akiambatana na Manka ambaye hakuhitaji kumpoteza tena.
Askari walio baki huku nyuma kazi yao ikwa ni miili ya askari walio pigwa risasi, kati ya askari ishirini walio fika katika eneo hilo, ni mmoja tu ambaye ni mlinzi wa raisi Godwin aliye weza kuwa hai japo hali yake ni mbaya
“Muheshimiwa raisi…..a…me..ch…..u”
Hakumalizia kitu alicho kuwa anakizungumza akapoteza fahamu.
“Muwahisheni hospitalini, huyu atatufaa”
Mkuu wa kitengo cha polisi kanda maalimu bwana Erinest Komba aliwaeleza vijana wake, ambao wakafwata amri kama alivyo zungumza mkuu wao. Habari ya raisi Godwin kutoweka ikaanza kusambaa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii, huku vituo vya televishion na maredio vikiwa vinatafuta ukweli juu ya jambo hilo. Hapakuwa na mkuu yoyote wa jeshi aliye weza kudhibitihs habari hizo kwa maana hapakuwa na mtu mwenye ushahidi katika hilo.
***
“Jikaze usilie, unavyo lia unadhani mimi nitafanyaje?”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Phidaya anaye lia njia mzima
“Ila mume wangu atakuwa kwenye matatizo”
“Sio rahisi kwa Eddy kuingia kwenye matatizo ndio maana akatuambia tuondoke”
Muda wote madam Mery akawa kimya akilichunguza gari hilo, kwa bahati nzuri akaona kifaa maalumu ambacho kipo siti ya nyuma ya dereva eneo alilo kaa yeye kinacho weza kuonyesha ni sehemu gani raisi yupo, hata walinzi wake wanapo kaa ikulu.
“Shamsa simamisha gari?”
“Kuna nini?”
“Simamisha gari kwanza”
Shamsa ikambidi kutii kile kitu ambacho madam Mery amemueleza, kwa haraka madam Mery akashaka kwenye gari, akamuomba Shamsa kufungua buti ya gari, Shamsa akaminya batani iliyo ruhusu buti ya gari hilo kufunguka, madam Mery akalinyanyua, akakuta kifaa kidogo kinacho ongoza kifaa alicho kiona ndani ya gari hilo.
“Ohoo ni GPRs system”
Sa Yoo alizungumza mara baada ya kuona kifaa hicho.
“Ndio nini?”
Shamsa aliuliza mara baada ya kushuka kwenye gari na kuzunguka nyuma kwenye buti ya gari hilo.
“Sehemu yoyote tunapo kwenda nah ii gari lazima tuonekane”
“Sasa inakuwaje?”
Hata kabla Sa Yoo hajajibu swali hilo, wakaziona gari nne nyeusi, aina ya GVC zinazo piga ving’ora zikiwafwata kwa kasi katika eneo hilo.
“Ohooo rudini kwenye gari wote”
Shamsa alizungumza kwa haraka akafunga buti ya gari hilo, wote wakaingia ndani gari, bila ya kupoteza muda, Shamsa akakanyaga mafuta ya gari na kuondoka eneo hilo kwa kasi kubwa.
“Fungeni mikanda”
Shamsa alizungumza huku akifunga mkanda wa siti aliyo kalia. Gari hizo nne za makachero wa usalama wa taifa, zikazidi kuifukuza gari hiyo ya raisi huku mkuu wao aliye panda gari la mbele akiwa na simu maalumu inayo onyesha gari hilo la raisi kila sehemu anapo kwenda.
“Ongeza mwendo, hawa watu ndio walio mteka raisi”
“Sawa mkuu”
Dereva huyo, ambaye naye ni kachero anaye sifika katika maswala ya uendeshaji wa gari kwa kasi, akawa ndio kama amechochewa, akazidi kukanyaga mafuta kwa kasi, hadi madereva wezake wanao endesha magri matatu yaliyo nyuma yao akawaacha kwa umbali kidogo.
“Wanazidi kutufwata”
Sa Yoo alizungumza huku mara kwa mara akigeuza kichwa chake nyuma. Katika uendeshaji wa gari, Shamsa anajimudu sana, ila kitu kinacho mfelisha kwa wakati huu, ni bega lake lililo pigwa risasi, na ndio kwanza kidonda hakijapona na maumivu anayo yaoata hapo ni makali kupindukia sema tu anajikaza kuwaokoa wezake kwa maana wakiingia mikononi mwa Makachero hao, hakuna mtu mwenye jawabu la kujua ni nini atakacho fanywa.
“Sa Yoo”
“Mmmmm”
“Nasikia kizunguzungu”
Shamsa alizungumza na kuwafanya wezake wote kumkodolea mamcho, kwani mwendo anao tembea nao Shamsa unaelekea kwenye spidi mita mia mbili isitoshe barabara waliyopo Sa Yoo haifahamu, na madam Mery naye hawezi kuendesha gari kwa mwendo huo, wala Phidaya ambaye anaonekena kichwa kujawa na mawazo mwengi. Kadri jinsi Shamsa anavyo zidi kuendesha gari hilo ndivyo jinsi maumivu ya bega yalivyo pelekea kizunguzungu zidi kumtawala na kusababisha macho yake kutoa anza kuona mbele vizuri.
***
Breki ya kwanza ikawa ni ikulu, madaktari walio andaliwa kumpokea Erickson waka tayari wamesha andaa kitanda maalumu cha kumpakiza Erickson. Gari la wagonjwa linalo milikiwa na jeshi lilipo simama tu, mlango wa nyuma ukafunguliwa, wakaingia madaktari wawili, wakakishusha kitanda cha Erickson huku Manka naye akifwatia kwa nyuma. Moja kwa moja wakamkimbiza katika chumba maalumu anacho tibiwa raisi.
“Dokta vipi hali yake itakuwaje?”
“Tunamchoma sindano ya usingizi kidogo maumivu anayo yapata yapungue na baada ya hapo tunauchunguza mshono wake kama utakuwa na mapungufu basi tutaufanyia marekebisho”
“Sawa nakuamini daktari hakikisha hali ya Erickson inakuwa sawa, na endepo ataamka hakikisheni munanijulisha mimi kwanza kabla ya mtu mwengine”
“Sawa madam”
Baada ya Manka kutoa maagizo hayo, moja kwa moja akaelekea kwenye chumba cha mawasiliano na kukuta wakuu wa majeshi na viongozi baadhi wa serikalini, akiwemo makamu wa raisi pamoja na waziri mkuu wakiwa wanafwatalia mashindano ya gari hilo la raisi na makachero wa usalama wa ataifa, yanayo chukuliwa muda huo moja kwa moja na helcoptar ya jeshi inayo tumia katika maswala ya habari.
“Mumefanikiwa kujua ndani ya gari kuna raisi?”
Manka aliwauliza viongozi hao huku macho yake yakitazama tv kubwa iliyopo ndani ya ofisi hiyo kubwa ya mawasiliano.
“Hapana ila tuna imani kwamba wamemshikilia”
“Wanaelekea wapi kwa sasa?”
“Wapo katika barabara ya Morogoro, sasa kuna baria Chalinze nina imanigari hiyo itasimamishwa”
Manka akakaa kwneye moja ya kiti, huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio. Japo baba yake ni mkosaji na amewakosea watu wengi sana ila moyo wake umejaa mapenzi tele kwa baba yake, hakuwa tayari kuweza kusikia kwamba baba yake amepata tatizo baya.
***
“Muheshimiwa tuombe ruhusa ikulu kuweza kuishambulia hii gari?”
Mmoja wa makachero alizungumza huku akimtazama bosi wake aliye kaa siti ya nyuma.
“Hatuwezi kufanya hivyo raisi yupo ndani ya gari hilo”
“Wanakwenda kasi sana”
“Ni lazima tuwapate, nimeambiwa hapa Chalinze kuna kizuizi cha jeshi, naamini tukifika hapo watasimama”
Mkuu huyo alizungumza huku akilitupia macho gari hilo la raisi linavyo zidi kwenda kasi, gafla gari hiyo ikaanza kuyumba yumba na kuwafanya makachero wote kushangazwa.
Sa Yoo akagundua asipo fanya kitu basi wanapo elekea wanakwenda kufa, akayatupia macho yake kwenye helcopta iliyopo juu kidogo pembeni yao inayo wafwata.
“Sa Yoo, nisaidie”
Shamsa alilalama huku nguvu za mikono zikimuishia na kulifanya gari hilo kuyumba yumba. Kwa haraka Sa Yoo akafungua mkanda wa siti yake, kisha akaufungua mkanda wa siti ya Shamsa kisha kwa umakini mkubwa huku akiwa ameushikilia mskani wa gari hilo akijitahidi kuliweka sawa. Shamsa akahamia kwenye siti aliyo kuwa amekaa Sa Yoo kisha Sa Yoo akakaa kwenye siti hiyo.
Kitu cha kwanza kufanya Sa Yoo, akafunga breki za gari hilo na kuifanya isimame, gari zinazo wafukuzia kwa nyuma nazo zikajikuta zikipunguza mwendo.
“Wee Sa Yoo umefanyaje, wanakuja hao”
Phidaya alilalama huku akitazama nyuma. Sa Yoo hakujibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kutema mate kidogo kwenye kiganja chake cha mkono wa kulia, kisha akayapekecha kwenye kiganja cha kushoto. Akatazama kwenye kioo chake cha pembeni na kuona jinsi gari hizo nne zinavyo zidi kuwasogelea.
“Shamsa funga mkanda”
Sa Yoo alipo maliza kuzungumza maneno hayo, akakanyaga breki pamoja na mafuta kwa kwa wakati mmoja na kuzifanya tairi za nyuma ya gari hilo kuserereka kwenye lami hiyo na kusasabisha moshi mwingi ambao uliwafanya madereva wa gari hizo za makachero, kuzidi kupunguza mwendo kwa maana mbele hawaoni. Sa Yoo alipo hakikisha kwamba moshi umekuwa mwingi akaachia breki na kuyaruhusu matairi yote kuanza kuzunguka kwa kasi ambayo alisha itafuta kwa dakika kadhaa.
“Anaondoka huyo munapunguza mwendo nini?”
Ilisikika sauti ya makamu wa raisi kwenye kinasa sauti cha mkuu wa makachero.
“Nenda nenda wanaondoka hao”
Mkuu huyo alizungumza na kumfanya dereva wa gari lake kuongeza mwendo. Hadi wanaupita moshi huo, gari ya raisi ilisha waacha kw umbali mkubwa na kuwafanya madereva wa magari hayo kuchanganyikiwa na kuzidi kuendesha mwendo kasi.
“Shamsa unajisikiaje?”
“Ongeza AC kidogo”
Sa Yoo akafanya kama Shamsa alivyo muagiza, huku akizidi kuendesha gari hiyo kwa mwendo kasi, kwa wingi wa magari yanayo kwenda nje ya Dar es Salaam, na kuingia ndani ya Dar es Salaam, yakamfanya Sa Yoo mara kwa mara kupunguza mwendo na kuyapita pale anapo pata nafasi ya kufanya hivyo. Hata kwa upande wa magari hayo ya makachero hali ikawa ni hiyo ila kwao kidogo ikawa kina unafuu, hii ni kutokana na gari zoa kuwa na ving’ora na ni sheria kwa madereva pale wanapo sikia ving’ora vya polisi au vya gari za wagonjwa ni lazima kuzipisha gari hizo.
“Ongeza mwendo tunakaribia kuwafikia”
Mkuu huyo alizidi kulaalama na kumfanya dereva wake kuongeza mwendo.
“Shamsa unataka kufanya nini?”
Sa Yoo aliuliza baada ya kumuona Shamsa akishusha kioo cha gari kwa upande alio kaa yeye. Shamsa akatoa bastola mbili akazichunguza vizuri, alipo pata uhakika zina risasi za kutosha. Akashusha pumzi kidogo na kuwatazama Phidaya na madam Mery alio keti siti za nyuma.
“Lipite hilo lori la mafuta”
“Mbele kuna basi linakuja?”
“Wewe lipite tu”
Sa Yoo akawasha taa zote za mbele, japo ni mchana, ila sababu ya kuwasha taa hizo ni kumushiria dereva wa basi hilo kupunguza mwendo, kisha akaanza kulipita lori hilo lenye matela, mawili ya mafuta. Dereva wa basi alipo ona ishara ya gari hiyo ndogo, yenye alama gari analo tumia raisi, akapunguza mwendo kasi wake. Sa Yoo akafanikiwa kulipita lori hilo, Shamsa bila hata ya kuhofia chochote, akajichomoza kwenye kioo, akapiga risasi tairi za mbele ya lori hilo na kulifanya kuanzakuyumba, akapata upenyo mwengine wa kufyatua risasi kwenye tanki hizo za mafuta na kusababisha mlipuko mkubwa katika barabara hiyo. Gari zote za makachero zikajikuta zikifunga breki baada ya lori walilo litarajia kulipita, kulipuka na kuanguka na kusababisha kuifunga barabara.
“Fuc*”
Mkuu wao huyo alijikuta akiachia matusi mengi kwani, huo ndio mwisho wa kulikimbiza gari hilo la raisi. Taratibu Shamsa akakaa kwenye siti yake na kufunga kioo cha gari.
“Kazi nzuri mwanangu”
Phidaya alijikuta akimsifia Shamsa huku akitabasamu kwa maana hakuamini kitu alicho kifanya, japo bado anaumwa.
“Asante mama”
“Shamsa angalia kule mbele”
Sa Yoo alizungumza huku taratibu akipunguza mwendo kasi wa gari, wote wakajikuta wakitazama mbele, kila mmoja akahisi kuchanganyikiwa kwa maana barabara nzima imefungwa na vifaru vya jeshi, huku mikonga yao ikiwa wameielekezea gari yao, ikiashiria kwamba wakifanya ubishi basi mizinga hiyo ya mabomo itakuwa ni alaki kwao.
“Jesus Christ”
Madam Mery alijikuta akitokwa na maneno hayo huku akibaki ameduwaa, na Sa Yoo akajikuta akisimamisha gari asijue nini cha kufanya.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 92 YA SIMULI HII.
 
SORRY MADAM (93)
(Destination of my enemies)

WRITER………………………………………………………………….………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..…… www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT………………………………………………………………………….0657072588/0768516188
JIUNGE NA MAGROUP YANGU YA WHATSAPP NA FACEBOOK, YANAYO HUSIANA NA HADITHI TU KWA KIIINGILIAO CHA SH 2000 KWA MWENZI. 0657072588.

ILIPOISHIA
“Kazi nzuri mwanangu”
Phidaya alijikuta akimsifia Shamsa huku akitabasamu kwa maana hakuamini kitu alicho kifanya, japo bado anaumwa.
“Asante mama”
“Shamsa angalia kule mbele”
Sa Yoo alizungumza huku taratibu akipunguza mwendo kasi wa gari, wote wakajikuta wakitazama mbele, kila mmoja akahisi kuchanganyikiwa kwa maana barabara nzima imefungwa na vifaru vya jeshi, huku mikonga yao ikiwa wameielekezea gari yao, ikiashiria kwamba wakifanya ubishi basi mizinga hiyo ya mabomo itakuwa ni alaki kwao.
“Jesus Christ”
Madam Mery alijikuta akitokwa na maneno hayo huku akibaki ameduwaa, na Sa Yoo akajikuta akisimamisha gari asijue nini cha kufanya.

ENDELEA
Ukimya ukatawala ndani ndani ya gari. Kila mtu hakujua ni kitu gani ambacho anaweza kukifanya kwa muda huo kwa maana wanajeshi wenye silaha walisha anza kujitokeza na wengine kadhaa wakaanza kulisogelea gari lao.
“Ngoja nishuke”
Madam Mery alizungumza huku akiwatazama wezake.
“Unataka kwenda wapi, si unaona hao wanajeshi wana silaha watakukamata”
“Nalitambua hilo, kushuka kwangu kwenu itakuwa ni rahisi nyinyi kuokoka”
“Hembu acha upuuzi madam Mery, baki kwenye gario”
Phidaya alizungumza kwa kufoka, ila akawa amesha chelewa kwani Madam Mery alitoka kwenye gari huku mikono akiwa ameinyoosha juu.
***
“Najua munamtaka raisi Godwin, ila sisi hatunaye”
Sauti ya Madam Mery ilitoka kwenye vipaza sauti vilivyomo katika chumba hicho cha mawasiliano na kumfanya Manka kunyanyuka na kuzidi kupiga hatua kutazama Tv kubwa iliyopo katika chumba hicho.
“Wasifanye kitu chochote”
Manka alizungumza na kuwafanya watu wote waliomo ndani ya chumba hicho kumtazama mara mbili mbili.
“Kwa nini muheshimiwa?”
“Hawa hawana raisi, ila wawakamate kupitia wao tutajua ni wapi alipo raisi”
“Sawa mkuu”
Iikatolewa amri ya kuwakamata Madam Mery na wezake wote waliopo kwenye gari hilo.
***
Jinsi wanajeshi wanavyo zidi kulisogelea gari lao ndivyo jinsi madam Shamsa, Sa Yoo na Phidawa walivyo zidi kuchanganyikiwa.
“Phidaya funga mlango”
Sa Yoo alizungumza na kumfanya Phidaya kuufunga mlango wa upande alio kuwa amekaa madam Mery.
“Gari hii haiingia risasi, kwa hiyo hata wakitushambulia hatuwezi kuudhurika”
Sa Yoo alizungumza huku taratibu akianza kuirudisha gari hili nyuma. Wanajeshi wote walipokea amri ya kuto kushambulia gari hilo, na hilo ndilo lililo kuwa kosa kubwa sana kwao kwani Sa Yoo baada ya kuona hakuna kitendho chochote kinacho weza kuchukuliwa na wanajeshi hao. Kwa haraka akaigeuza gari na kurudi walipo toka kwa mwendo wa kasi sana.
“Tunarudi tena Dar?”
Phisaya aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka, Sa Yoo hakujibu chochote zaidi ya kuzidi kuendesha gari hilo kwa mwendo kasi sana. Akilini mwa Sa Yoo akawa anaifikiria njia ambayo aliiona imekatika kipindi wakiwa wanaelekea Chalinze. Kilomita mbili mbeleni, akakunja kushoto mwa barabara na kuingia katika njia ya vumbi iliyo jaa vibonde bonde vingi, ikiashiria kwamba haitumiki kwa magari.
“Helkopta hiyo bado inatufwatilia”
Shamsa alizungumza huku akiitazama kupitia kioo cha mbele.
“Haina shida hiyo helkopta ni ya kurusha matangazo, kwa hiyo hapo wanatuchukua video”
“Sasa ni lazima kuishusha kwa maana hatuwezi kujua tunapo elekea, kwa maana kwaa sasa ni lazima kuweza kujificha”
“Basi fanya kazi yako mama”
Sa Yoo alizungumza na kwa mara nyingine tena Shamsa akafungua kioo cha gari hilo, akachomoza mikono yake yote miwili na kuanza kuishambulia Helkopta hiyo kwa risasi mfululizo hadi ikafikia kipindi helkopta hiyo ikaanza kutoa moshi mwingi ulio ipelekea kuyumba sana na mwisho wa siku kuanguka na kulipuka ikiwa na rubani wake pamoja na fundi mitambo.
Kwa umbali fulani kutoka eneo ilipo anguka helkopta Sa Yoo akalisimamisha gari na kushuka moja kwa moja akazunguka nyuma ya gari, akafungua buti na kuanza kukitazama kifaa ambacho kila gari ya riasi inapo elekea ni lazimwa waweze kuiona.
“Ina bidi kukitoa kwa maana bila ya kufanya hivyo, bado hatujawa salama”
Sa Yoo alizingumza huku Shamsa na Phidaya wakikitazama kifaa hicho, Shamsa akatoa bastola yake na kukitandika pasipo kujali chochote. Na kweli kifaa hicho kikasambaratika na kupoteza mawasiliano na Ikulu ya raisi.
“Sasa tunaelekea wapi?”
Hata mimi sifahamu, tujaribu jaribu kuelekea mbele labda tunaweza kupata makazi ya watu”
“Kweli?”
“Ndio”
Wakaingia kwenye gari, ikiwa ni majira ya jioni. Wakazidi kuchanja mbuga kuelekea wapipo pajua. Hadi inatimu saa moja usiku, wakawa wamfika kwenye moja ya kijiji cha Wamasai.
“Jamani tuombeni hata maji”
Phiday alizungumza, Shamsa akayachunguza mazingira ya eneo hilo wakiwa ndani ya gari hilo huku akijaribu kuwatazama watoto wa kimasai wanao lisogelea gari hilo na kulishangaa.
“Hii sehemu ni salama”
“Umejuaje Shamsa”
“Hawa ni watu jamii ya wafugaji, wanaitwa Wamasaidi. Ni watu wanao penda sana kutoa misaada kwa wale wenye shida ya uhitaji”
“Isije ikawa ni mtego tukashuka kwenye gari wakatushambulia?”
“Kila mmoja achukue bastola kwa ajili ya kujilinda yeye mwenyewe”
Shamsa akawapa kila mmtu bastola yake moja, Sa Yoo akatafuta sehemu yenye muembe mkubwa na kulisimamisha gari huku watoto wa kabila hilo la kimasai wakizidi kuwashangaa. Wa kwanza kufungua mlango na kushuka kwenye gari akawa ni Shamsa akawatazama watoto hao walio valia lubega kisha akaanza kuwapa mikono kwa ajili ya kuwasalimia.
Asili yao ya kiarabu, ikawafanya watoto hao kuzishangaa sana ngozi zao. Kwani kwa miaka yao yote tangu wazaliwe hawajawahi kuwaona watu weupe, na niwachache sana tena wakubwa wao, ndio walisha wahi kupewa siku misaada ya mambo mbalimbali na shirika moja la Wajerumani walio watembelea mwaka ya 2002.
“Sogea sogea”
Sauti ya kijana mmoja mwenye cheo cha morani alizungumza huku akiwasogeza watoto hao wambao walimzunguka Shamsa.
“Habari yako muzungu”
Moran huyo alizungumza huku akimpa mkono Shamsa aliye utazama, kisha akaukutanisha na mkono wake huku akiachia tabasamu usoni mwake.
“Salama habari yako”
“Salama, nyinyi kuja tena tupa sisi musaada?”
“Ahaa tumekuja kuwatembelea”
“Basi njooni muone kina laiboni”
Kwa kuwakonjeza Shamsa akawaamuru Sa Yoo na Phidaya kushuka kwenye gari. Kila mmoja akashuka kwenye gari huku bastola yake akiwa ameichomeka kiunoni mwake na kuifunika na stati alilo livaa na si rahisi kwa wamasai hao kugundua kwamba wana silaha.
Watoto hao wa kimasai wakawazunguka huku kila mtoto akitaka kuwagusa Phidaya na Sa Yoo. Sa Yoo kwa kupenda watoto hakujali kushikwa na watoto hao muda wote akawa ameachia tabasamu huku na yeye akiwashika mkino watoto wawili.
Wakapelekwa hadi kwenye moja ya kijumba kilicho ezekwa na na nyasi. Wakakaribishwa ndani na kukuta wazee wanne wakiwa wamekaa kwenye viti vidogo vinavyo itwa vigoda. Kijana huyo akatoa salamu kwa luga ya kimasai na kuwaanza kuwaeleza wazee hao kwamba wanawake hao wamekuja kutoa msaada kwenye kijiji chao ila alitumia lugha hiyo ya kimasai kuwaelezea wazee hao.
“Wanasema munatokea wapi?”
Kijana huyo alizungumza huku akiwatazama Phidaya na wezake. Sa Yoo akadakia kulijibu swali hilo.
“Tunatokea Japani”
Kijana huyo akazungumza kwa kimasai na kuwafanya wazee hao kutingisha vichwa vyao huku sura zao zikiashiria zina furaha kusikia hilo.
“Wanasema mumetuletea nini?”
Sa Yoo akatazamana na wezake huku akiwa hana kitu cha kujibu. Shamsa akameza fumba la mate kidogo na kulijibu swali hilo.
“Tumekuja kuwatembelea na kujua ni jinsi gani munavyo ishi na mazingira ya hapa na tukirudi kwetu Japan basi tutawaletea mahitaji yote ambayo mutakuwa munayahitaji”
Shamsa alizungumza kwa kujiamini, kijana huyo akawatasfiria wazee hao wakuu wa kijiji hicho kwa lugha ya kimasai.
“Wanawauliza munahitaji chakula?”
“Ndio”
Phidaya akawa wa kwanza kulijibu swali hilo huku akiwa ametabasama kwa maana ni njaa kali inausumbua utumbo wake. Wakapelekwa kwenye moja ya nyumba, na kukuta wasichana wawili wa kimasai. Wakawandalia chakula ambacho kila mmoja ndio mara yake ya kwanza kukila kwani ni madonge donge ya damu ya ng’ombe iliyo chemswa pamoja na maziwa yalio sindikwa.
“Mmmmm”
Phidaya aliguna, hata hamu ya kula chakula hicho, ikaanza kumakatika taratibu
***
Kitendo cha helkopta ya kijeshi inayo husiana na maswala ya habari, kutunguliwa. Ikamuudhi kila mtu aliye kuwepo katika chumba cha mawasiliano hususani makamu wa raisi.
“Muheshimiwa kwa hili unatakiwa kutoa amri”
Mmoja wa kiongozi wa jeshi alizungumza huku akimtazama makamu wa riais aliye ikinja sura yake akionekana dhairi kwamba ameshikwa na hasira kali sana katika hilo.
Daktari wa ikulu akaingia katika chumba hicho(control room), moja kwa moja akamfwata Manka sehemu alipo kaa na kumnong’oneza sikioni. Kwa haraka Manka akaanza kutoka kwenye chumba hicho huku akifwatana na daktari hiyo.
Wakaelekea kwenye chumba alicho lazwa Erickson na kumkuta akiwa amefumbua macho yake akiwatazama wanavyo ingia kwenye chumba hicho. Moja kwa moja Manka akaelekea kwenye kitanda alicho lala Erickson.
“Unajisikiaje?”
Manka aliuliza kwa sauti ya unyonge.
“Safi tu”
“Dokta kidonda chake kinaweza kuwa vizuri hadi lini?”
“Ahaa kitachukua kama wiki mbili hadi tatu kukauka kabisa”
“Erickson usijali, upo katika mikono salama na wala hakuna mtu ambaye anaweza kukuteka tena”
Eddy kwa haraka haraka akafikiria kitu cha kuzungumza. Akameza mate kidogo kisha akamtazama Manka usoni mwake.
“Agnes yupo wapi?”
Manka akabaki kimya huku akimtazama Erickson asijua ni nini atakijibu.
“Ahaaa.a..ahaa kwa sasa sio vizuri kumuulizia kikubwa ni kuangalia afya yako”
Mlango ukafunguliwa na akaingia mwanajeshi mmoja aliye piga saluti kwa Manka na kutoa maelekezo aliyo kuja nayo.
“Muheshimiwa makamu wa raisi amaruhusu jeshi kuwatafuta wale wasichana na kuhakikisha kwamba wanakamata ama kuuwa”
“Kwa nini ametoa ruhusa hiyo!?”
Manka aliuliza huku akisimama akionekana kushangazwa sana na ruhusa hiyo.
“Sijatambua muheshimiwa”
Manka akataka kutoka ila Erickson akamuuliza swali lililo mfanya kugeuka na kumtazama.
“Ni wasichana gani hao wanao taka kuuliwa?”
“Ni wale ambao walikuteka”
Eddy akaonekana kushushwa ila hakuhitaji kuzungumza chochote kuepuka kujulikana kwamba yupo pamoja na wasichana hao.
“Ngoja nikalizui hili swala”
Manka akaondoka katila chumba hicho huku akiongozana na mwanajeshi huyo na kumuacha Erickson na daktari. Eddy akatamani kuzungumza kitu ila akajizuia.
Manka akaingia kwenye chumba cha mawasiliano. Moja kwa moja akamfwata makamu wa raisi.
“Ni amri gani umetoa?”
“Nimeagiza vijana wakawakamate au kuwaua”
“Sihitaji kuona damu zinamwagika”
“Ila kumbuka mimi ndio mwenye mamlaka ya kuiongoza nchi, kama makamu wa raisi”
“Haijalishi na mimi ni waziri wa ulinzi, sihihitaji vijana wangu waende kufa”
Manka akachukua simu inayo tumika katika kuwasiliana na vikosi vya jeshi vilivyo anza kueleka katika njia ambayo wamepita kina Shamsa.
“Nimesema vikosi vyote virudishwe nyuma”
“Ila madam…..”
Ilisikika sauti ya kamanda wa vikosi hivyo.
“Sihitaji vya ila, nasema vikosi vyote v….”
Makamu wa raisi akampokonya mkonga wa simu Manka na kuuweka sikioni mwake.
“Endesha majeshi hakikisheni munaleta maiti za hao mawanawake”
Manakamu wa raisi alizungumza na kuurudisha kwa nguvu mkonga huo wa simu kwenye sehemu yake maalu. Manka akamtazama mzee huyo kwa macho makali na kuachia msunyo mkali ulio wafanya watu wote ndani ya chumba hicho kikubwa kumgeukia na kumtazama kwa mshangao.
***
Vikosi vya majeshi vyenye silaha vipatavyo nane, vyenye watu zaidi ya kumi na mbili vikazidi kusonga mbele kama amri ya makamu wa raisi ilivyo tolewa. Wakiwa kwenye magri yao ya kijeshi kila mmoja kati yao akawa na uchu mkali wa kihitaji kuwakamata wasichana hao wanao sadikika kumteka raisi wa nchi mbaya zaidi mwanamke waliye mkamata hajafungua kinywa chake kusema ni wapi raisi alipo japo wamempatia kipigo kikali ila hajazungumza neno la aina yoyote
“Jamani mimi nimeshindwa kula hiki chakula”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya kunong’oneza, japo ana njaa ila akashindwa kabisa kula chakula hicho. Sa Yoo hakujali chakula hicho kimepikwaje, akazidi kukila na kuonekana kukifurahia sana.
“Kula hata kidogo”
Shamsa alizungumza, ila Phidaya akasimama, na kumnyooshea Shamsa mkono.
“Nini?”
“Naomba funguo ya gari nikalale kwenye gari mimi?”
Shamsa akamkabidhi Phidaya funguo ya gari, akatoka chumbani hapo. Binti mmoja wa kimasai akaliona jeraha la Shamsa kwenye bega lake. Taratibu akamsogelea na kulitazama vizuri na kumfanya Shamsa kuacha kula na kumtazama binti huyo aliye nyanyuka na kuchukua kibuyu kimoja kilicho fungwa kwa juu na mfuko mweusi.
“Hii ni dawa ya vidonda”
Binti huyo alizungumza Kiswahili fasaha hadi Shamsa akashangaa kwa maana walidhani kwamba mabinti hao walio waandalia chakula hawajui lugha ya Kiswahili zaidi ya kimasai. Binti huyo akamimina unga unga huo kwenye kiganja chake cha mkononi na kuumpaka Shamsa kwenye kidonda chake na kumfanya asikie maumivu makali yaliyo dumu kwa dakika tano mfululizo na kupotea.
“Unajisikiaje?”
“Ahaaa kidogo afadhali”
Shamsa alizungumza huku jasho likimwagika.
“Ndani ya siku mbili kitakauka na kupona”
Phidaya alipo toka ndani humo hakwenda moja kwa moja kwenye gari, akaanza kuzunguka zunguka kutazama mazingira ya kijiji hicho kilichopo katikati ya eneo lenye majani mengi. Akapanda kwenye moja ya kichuguu kilihopo katika eneo hilo. Kwa mbali akaona taa za mianga ya magari zikikaribia kufika kwenye kijiji hicho.
‘Mungu wangu’
Phidaya akashuka kwa haraka kwenye kichuguu hicho na kukimbilia hadi kwenye nyumba alipo waacha Shamsa na Sa Yoo.
“Kuna nini mbona mbio mbio?”
Phidaya akawatazama wasichana hao kisha akachuchumaa na kumnong’oneza Shamsa
“Nahisi kuna askari wanakuja maeneo haya kututafuta”
Shamsa akawa kama mtu aliye lipiliwa na jambo fulani kwa haraka akanyanyuka na kutoka katika chumba hicho, ikawabidi wezake wote kumfwata hata binti huyo wa kimasai anaye fahamu Kiswahili akawafwata kwa nyuma.
“Wapo wapi?”
Shamsa aliuliza, Phidaya akakimbilia kwenye kichuguu hicho wote wakapanda wakaziona gari hizo zinavyo zidi kuja kwa kasi katika kijiji hicho. Binti huyo wa kimasai akaanza kupiga vigelegele vya kuashiria kuna jambo limejitokeza. Vijana wa kimasaid wakiwa na mikuki pamoja na ngao zao wakatoka kwenye boma zao na kukimbilia kwenye kichuguu hicho.
“Tunavamiwa”
Binti huyo alizungumza kwa lugha ya kimasai. Kiongozi wa vijana hao wa kimasai akawaamuru wezake wote kutawanyika, na kujificha na endapo watu hao wanao kuja watakuwa na jambo lolote baya basi wawavamie.
“Tnafanyaje sasa?”
Phidaya aliuliza huku mwili mzima ukimtetemeka.
“Nifwateni mimi”
Binti huyo wa kimasai alizungumza na kushuka kwenye kichuguu hicho. Wote wakamfwata kwa nyuma akwapeleka kwenye moja ya handaki wanalo jificha pale kunapo tokea uvamizi. Wakakuta wamama na watoto pamoja na wazee wakiwa wamasha ingia kwenye handaki hilo wamejificha baada ya kupigwa kwa vigelegele hivyo.
“Munaweza kujificha humu na maadui wasijue ni wapi nyinyi mulipo”
Hata kabla hawajazungumza chochote, milio ya risasi ikaanza kusikika ikirindima nje ikiashiria kwamba watu hao walio kuja kwenye kijiji hicho si wema kabisa.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 94 YA SIMULI HII
 
SORRY MADAM (94)
(Destination of my enemies)

WRITER………………………………………………………………….………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..…… www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT………………………………………………………………………….0657072588/0768516188
JIUNGE NA MAGROUP YANGU YA WHATSAPP NA FACEBOOK, YANAYO HUSIANA NA HADITHI TU KWA KIIINGILIAO CHA SH 2000 KWA MWENZI. 0657072588.

ILIPOISHIA
“Nifwateni mimi”
Binti huyo wa kimasai alizungumza na kushuka kwenye kichuguu hicho. Wote wakamfwata kwa nyuma akwapeleka kwenye moja ya handaki wanalo jificha pale kunapo tokea uvamizi. Wakakuta wamama na watoto pamoja na wazee wakiwa wamasha ingia kwenye handaki hilo wamejificha baada ya kupigwa kwa vigelegele hivyo.
“Munaweza kujificha humu na maadui wasijue ni wapi nyinyi mulipo”
Hata kabla hawajazungumza chochote, milio ya risasi ikaanza kusikika ikirindima nje ikiashiria kwamba watu hao walio kuja kwenye kijiji hicho si wema kabisa.

ENDELEA
Karibia watu wote ndani ya handaki miili yao ilipatwa na woga. Wamama walio kuwa na watoto wadogo waliwakumbatia watoto wao huku wakiachia vilio vilivyo wafanya Sa Yoo na Shamsa kushangaa.
“Hatuwezi kukaa humu ndani na kuona watu wasio wenye hatia wakiwa wanakufa pasipo sababu ya msingi”
Phidaya alizungumza huku akiwatazama Shamsa na Sa Yoo ambao muda mwingi waliwatazama wanamama hao na watoto wanavyo angua vilio.
“Una maana gani?”
Binti huyoo wa kimasai aliuliza huku mwili ukimtetemaka. Shamsa akataka kuchomoa bastola yake, ila Sa Yoo akamuwahi mkono huo na kumzuia.
“Sio sehemu yake hii”
Sa Yoo alizungumza huku akiondoka kwenye handaki hili, akapandisha ngazi huku nyuma yake akifwatia Phidaya na Shamsa.
“Tafadhali usitoke baki humu ndani”
Shamsa alimueleza binti wa kimasai ambaye aliwafwata kwa nyuma walipo kuwa wakitaka kutoka. Bimti huyo akawa muelewa na kurudi ndani ya handaki.
Milio ya risasi iliendelea kurindima, huku vijana wa kimasai wanao tumia silaha za jadi wakiendelea kuteketea kwa maana uweozo wao wa kupambana ni mdogo kuliko uwezo wa wanajeshi hao.
Hapakuwa na mazungumzo zaidi ya kuhakikisha kwamba wanatetea kijiji hicho kinacho poteza watu wake kwa sababu yao. Kila mmoja akakimbilia katika sehemu ambayo anaweza kuhakikisha kwamba haonekani na kuanza kujibu mashambulizi ya wanajeshi hao
***
“ARGAAAAAAAAAAAAAAAAAAA…………..”
Ukelele mkali ulisikia katika moja ya chumba kilichopo chini ya ardhi kwenye handaki ambalo, mikaka kadhaa ya nyuma iliyo pita, lilikuwa likitumika kama maficho ya majambazi wa kike walio tokea kuitingisha serikali ya Tanzania.
Sura ya Rahab iliyo jaa hasira na uchungu mwingi ikaendelea kuonekana mbele ya uso wa raisi Godwin ambaye amening’inizwa hewani kwa mikono yake kufungwa na kamba ngumu ya manila, kila mkono umefungwa upande wake, na miguu yake nayo imefungwa kila mmoja upande wake. Huku mwili wake ukiwa hauna nguo hata moja.
Kitu ambacho Rahab anakifanya ni kila mara kupiga teke kwa chini kwenye sehemu za siri za Mzee Godwin na kumfanya atoe ukelele mkali.
“Niue tu lakini sio kunifanyia unyama wa aina hii”
Mzee Godwin aliye jaa damu kwneye sura yake iliyo chakaa kwa kipigo kilali alicho patiwa na Rahab, alizungumza huku akimtazama Rahab, aliye mjibu kwa kumtandika ngumi moja kali ya uso, na kuzifanya damu kuzidi kumtoka raisi Godwin kwenye sura yake.
“Mume wangu Praygod, alikufa kifo kikali cha kikatili na wewe ndio msababishaji wa hili”
“Mimi sifahamu hilo”
“Ahaaa ufahamu si ndio?”
“Ndio sifahamu”
“Basi kwa kipigo hichi utafahamu tu”
Rahab akachukua mashine maalumu ya shoti, akachukua nyaya mbili za hasi na chanya moja akaifunga katika uume wa mzee Godwin na mwengine akaufunga kwenye gololi za mzee huyo, kisha akarudi mezani ilipo mashine hiyo yenye swichi ya kuongezea mtetemesho wa shoti.
Bila hata ya huruma, Rahab akaiwasha mashine hiyo na kumfanya mzee Godwin kutetemeshwa karibia mwili mzima. Mzee Godwin alizidi kulia kwa maumivu makali sana anayo yapata. Tangu kwenye maisha yake yote hakuwahi kuweza kukutana na maumivu makali ya namna hiyo japo alikuwa ni mwanajeshi na aliweza kukutana na waalifu wengi alio weza kuwabana na mashine hiyo ya shoti ila kwa sehemu alipo wekewa nyanya hio ndivyo jinsi alivyo zidi kuona maisha yake yanakwenda ukingoni hata kabla ya kufanikisha malengo yake ya kuifanya nchi ya Tanzania kuwa na utawala wa kifalme na si wa uraisi tena.
Maumivu makali aliyo yapata yakapelekea mzee Godwin kupoteza fahamu hapo hapo. Hilo wala halikumuogopesha Rahab alicho kifanya ni kuzima mashine hiyo. Akachukua ndoo kubwa, akaingia bafuni akakinga maji kwenye bomba hadi, ndoo hiyo ikajaa. Akarudi nayo kwenye chumba cha mateso, akamwagia maji hayo mzee Godwin na kumfanya kustuka kutoka katika hali ya kupoteza fahamu.
“Zoezi letu linaendelea pale pale”
**(MASAA KUMI NYUMA)
Baada ya Phidaya kuingia ndani, kwa haraka Rahab akapiga hatua hadi pale alipo lala raisi Godwin, akapiga na kitako cha bunduki kichwani na kumfanya raisi Godwin kuzimia hapo hapo. Kutokana na uwezo wake wa ziada wa nguvu zake ambazo siku nyingi hazitumii, kutokana na watu walio mzunguka. Akambeba mzee Godwin begani mwake na kutoka naye hadi nje, akamuingiza kwneye moja ya gari la askari wake alio kuja nao hapo.
Akaingia upande wa dereva na kuondoka eneo hilo, kwa mwendo wa kasi huku miyoni mwake akiwaomba msamaha weze kwa kitendo hicho cha kuondoka na Mzee Godwin ambaye wanamuwinda wote.
Rahab akazidi kuendesha gari hiyo kuelekea katika barabara ya Tegeta, inayo pitia mkoa wa Pwani, njia nzima Rahab akawa anaomba kutoweza kukutana na kizuia ambacho jana yake waliweza kukutana nacho.
Maombi ya Rahab hayakuweza kufanya kazi kwani kizuizi hiyo kilikuwepo tena kwa muda huo ulinzi ulizidi kuongezwa kutokana na taarifa iliyo tolewa kwamba raisi wa nchi ametekwa na wanawake ambapo picha zao ziliswambwazwa kwa haraka kupitia vyombo vya habari. Ukaguzi wa gari zote zinazo pita katika kizuizi hicho ulifwanywa kwa umakini mwingi.
Taratibu Rahab akalisimamisha gari lake pembeni. Akashuka na kufungua kwenye butiya gari hilo. Kwa bahati nzuri akakutan silaha moja inayo tumika katika kufyatulia mabomu yanayo itwa ‘Rocate Ranger’. Bila hata ya kujiuliza maswali mara mbili mbili. Akalifunga bomo moja, kisha akasimama katikati ya barabara. Akavuta pumzi nyingi huku mzinga huo akiwa ameuweka begani mwake. Akalifyatua bomu hilo lililo kwenda kwa kasi na kulipua magari ya polisi yaliyo kuwa karibu na kizui hicho. Mlipuko mkubwa wa gari mbili za pilisi ukawafanya askari na wanajeshi walipo katika eneo hilo kuchanganyikiwa.
Akarudu kwenye buti na kuurudisha mzinga huo, kisha akachukua bunduki aina ya MK 47, iliyo chomekwa magazine zenye risasi za kutosha. Akachukua magazine sita na kuzichomeka kwenye mfuko wa surulai yake. Alipo hakikisha kwamba yupo sawa, akafunga buti ya gari hilo na kuanza kufyatua risasi kuelekea walipo wanajeshi na polisi huku akiwafwata.
Shambulizi hilo lilizidi kuwaangusha wanajeshi na askari ambao wala hawakutarajia kama kuna ambushi ya namna hiyo inaweza kuokea eneo hilo kwa wakati huo.
Askari walijaribu kurudisha mashambulizi lakini hawakuweza kwani adui yao hawakumuona kwa haraka ila walicho kumbana nacho ni risasi tu. Watu walio kuwa kwenye magari yao walichanganyikiwa, wengine walishaka na kukimbia kuyaokoa maisha yao, ila wengine walibaki kwneye magari yao wakiamini kwamba hiyo ndio sehemu watakayo okoa maisha yao.
Jinsi watu walivyo tawanyika ndivyo jinsi ilivyo wachanganya wanajeshi wachache walio bakia, kwa maana hawaruhusiwi kushambulia raia ambao hawana hatia. Rahab ambaye kwa mara kadhaa alijibanza kwenye magari, aliendelea kuwashambulia na kuwaa wanajeshi na askari wote.
Akaanza kuwakagua askari na wanajeshi mmoja hadi mwengine kuangalia aliye hai, alimshindilia risasi, aliye kufa alimuacha.
“Pumbavu”
Rahab alizungumza baada ya kuona shambulizi lake limekamilka. Akarudi kwenye gari na kumkuta mzee Godwin ndio anastuka, huku akijitingisha kichwa chake akijaribu kufikiria ni eneo gani ambalo yupo. Akampiga kisukusuku cha shingo na kumfanya azimie tena.
Akawasha gari na kuanza kuipitisha pembeni ya barabara hadi kwenye kizuizi kilicho wekwa. Akashuka akamvua mwanajeshi mmoja nguo zake akaziweka begani na kurudi kwenye gari, akamtoa mzee Godwin naye akamuweka begani. Akavuka kizuizi hicho cha geti na kumuingiza mzee Godwin kwenye moja ya gari la jeshi. Akaliwasha na kuondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi. Kila aliye badi katika neo hilo hakuamini kujiona amesalimika na wanajeshi na askari walio kuwa wakiwakagua magari wamesalimika.
Rahab akaanza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine. Huku akiliendesha gari hilo la jeshi kwa mwendo wa kawaida. Akazivaa nguo za mwanajeshi aliye mvaa na kuendelea na safari yake. Moja kwa moja akaelekea kwenye msitu ambao kuna handaki lao ambalo ni miaka mingi imepita hajafika.
Akafanikiwa kufika katika handaki hilo, akashuka huku bunduki yake ikiwa mkononi, akayachunguza mazingira hayo yaliyo yaa nyasi nyingi. Akafungua mfuniko wa handaki, na kuanza kushuka taratibu kwenye ngazi za kueleka chini. Japo kuna giza nene sana, ila hakuweza kuogopa. Akafika sehemu anayo fahamu kuna swichi ya kuwashia taa ndani ya handaki hilo. Akaiwasha mwanga mkali ukatwala ndani ya handaki hilo. Akaendelea kukagua chumba kimoja hadi kingine. Ila vitu akavikuta vikiwa vimechanguka changuka kwneye baadhi ya vyumba, alipo ridhishwa na chumba hicho, akatoka kwenye handaki. Akaelekea kwenye gari, ila kitu kilicho mstua ni mlango mmoja wa gari hilo la jeshi kuukuta wazi. Kwa haraka akakimbilia hadi kwenye gari, akamkuta mzee Godwin akiwa hayupo. Ila kwa bahati nzuri, michiziri ya damu na alamaza za miguu, iliyo jichora kwenye ardhi kutokana na ardhi hiyo kulowana na mvua iliyo nyesha usiku katika eneo hilo. Akaanza kuifwatilia miguu hiyo kwa mwendo wa kasi na kwa tahadhari kubwa. Hakufika mbali akamuona mzee Godwin akijikongoja akijaribu kukimbia.
Akamuwahi na kumuangusha chini. Mzee Godwin akajaribu kuonyesha ubavu kwa Rahab, ila alicho kutana nacho ni aibu tupu kwake, kwani kipigo kikali aliambulia kutoka kwa binti huyo anaye onekana kuwa na nguvu ambazo hata mzee Godwin zilimuogopesha kwa maana hata ngumi anayo mshushia ina ujazo mkubwa hata zaidi ya mwanaume.
Uso wa mzee Godwin ulichanwa maeneo ya jicho la kushoto kwa ngumi nzito iliyo tua eneo hilo sekunde chache zilizo pita na kusababisha damu nyingi kumwagika. Rahba alipo hakikisha raisi Godwin amelegea twepele tepwele. Akaanza kumburuza hadi lilipo gari, akafungua nyuma ya gari hilo aina ya ‘Pick Upp’ kulipo funikwa na turubai. Akakutana na mashine moja kubwa ya shoti pamoja na baboksi aliyo yafungua akakuta yana chokleti, biskuti pamoja na juisi, vyakula ambavyo wanavitumia wanajeshi pale wanapo kuwa wameweka kambi sehemu.
Kabla hajalifunika bosky hilo akaona kamba kubwa ya manila iliyo pembeni ya boski pamoja na kisu kidogo cha kukunja na kukunjua.
Akaichukua kamba hiyo na kumfunga Mzee Godwin kwenye miguu na kuanza kumburuza kuelekea ndani ya handaki hilo. Mzee Godwin akajikuta akishangaa handaki hilo kwa maana hata yeye kuna kipindi alisha wahi kujificha humo. Rahab akafungua chumba kimoja akatoa kitanda kilicho kuwa katika chumba hicho na kuvihamishia sehemu nyingine. Alipo maliza ndani ya chumba hicho kuna vyuma vilivyo chomekwa kwenye ukuta.
Akachukua kamba hiyo ya manila, akazikata katika kamba nne na kumfunga mzee Godwin ambaye hajiwezi kufanya chochote, kwenye mikono pamoja na miguu. Alipo hakikisha amemaliza zoezi hilo dogo. Akamvua nguo zake zote na kubakiwa mtupu. Kisha akampandisha kwenye vyuma hivyo na kumchanua kama vile watu wanao wamba ngozi ya ng’ombe au mbuzi.
Akarudi kwenye gari, akaihamishia mizigo yote iliyopo kwenye gari hilo ndani ya handaki, alipo hakikisha kila kitu kimekwisha akafunga handaki kwa ndani na kuingia kwenye chumba alipo mzee Godwin na kuanza kumuhoji maswali ambayo mzee Godwin hapo mwanzo hakushirikiana naye katika kumjibu ila kipigo kilipo anza akajikuta akijibu kwa kusua sua. Ila alipo anza kupigwa sehemu zake za siri, hapo ndipo alipo mjua Rahab ni mkatili sana
***
Milio ya risasi ilisikika kupitia simu ya upepo iliyopo kwenye moja ya meza katika chumba cha mawasiliano ndani ya ikulu.
“Unaisikia hiyo milio”
Manka alizungumza kwa kufoka huku akimtazama makamu wa raisi, aliye mkazia jicho. Manka akaichukua simu hiyo ya upepo na kuisogeza karibu na mdomo wake.
“Waziri wa ulinzi ninazungumza hapa, tupeni ripoti ni kitu gani kinacho endelea?”
“Muheshimiwa, tunashambuliwa huku na wanakijiji”
Sauti ilisikika kwa kila mtu katika chumba hicho na kiwafanya wote kuwa kimya.
“Wanakijiji gani?”
“Ni wamasaidi wana silaha za jadi muheshimiwa. Vijana wangu wanazidi kupungua muheshimiwa”
“Nimesema rudisheni majeshi nyuma”
Gafla makamu wa raisi akampokonya Manka hiyo redio ya upepo na kuisogeza mdomobi mwake na kumfanya Manka kukasirika.
“Nimesema yoyote atakaye ingilia opareshini hii, muueni sawa”
“Sawa mkuu”
Manka, akakunja ngumi huku akiyang’ata meno yake. Kitendi cha makamu wa raisi kumgeukia huku akiishusha simu hiyo ya upepo kutoka katika usawa wake wa mdomo, akakutana na ngumi moja ya shavu iliyo muangusha chini hadi miwani yake kubwa kiasi ikaangukia pembeni. Makamu wa raisi akajaribu kurudisha kombora hilo, alilo patiwa na Manka ila akajikuta akikutana na ngumi nzito mbili zilizo tua kifuani mwake, zikamnyumbiasha na kumuangusha chini.
Viongozi na wafanyakazi walio kuwa katika chumba hicho wote wakajikuta wakishangaa, kwani wengi wao ndani ya chumba hicho wapo kinyume na makamu wa raisi kwa maana ana tumia mamlaka yake vibaya.
Manka akapiga hatua hadi alipo anguki makamu wa raisi anaye jizoa zoa kunyanyuka. Akaiokota simu ya upepo huku akimtazama mzee huyo, aliye itibua hasira yake.
“NIMESEMA KAMA WAZIRI WA ULINZI, RUDISHENI MAJESHI NYUMA NA MURUDI KAMBINI”
“Sawa madam”
Manka akaiweka simu yake pembeni. Kabla hajafanya kitu chochote simu yake ikaita, akaitoa mfukoni na kuipokea pasipo kupokea.
“Manka ninakuomba unirudishie Erickson wangu”
Sauti ya Agnes ilisikika masikioni mwa Manka na kujikuta akiwatzama watu waliomo ndani ya chumba hicho cha mawasiliano. Akatoka katika chumba hicho ili azungumze vizuri na Agnes.
“Una uhakika na unacho kizungumza?”
“Ndio nina uhakika wa asilimia mia moja wewe ndio uliye mchukua Erickson”
“Hembu nisikilize wewe malaya. Urafiki wangu mimi na wewe usiwe ni chanzo cha kuzungumza upumbavu kama huo, na kama ungekuwa na uchungu na huyo Erickson ungemtafuta tangu jana sawa”
“Ahaaa mimi leo Malaya si ndio?”
“Ndio, si ndio kazi uliyo kuwa unaifanya udogo wako, tena iwe mwisho kunitafuta”
Manka akakata simu, alipo geuka nyuma akamkuta John akiwa na mlinzi wake, akawatazama kwa macho makali na kusubiria wanacho taka kukizungumza.
“Ninasikia kwamba mkuu ametekwa?”
“Sio swali hilo ni jibu”
“Hadi sasa hivi mumefikia wapi?”
“Unauliza hivyo kama nani?”
“Kumbuka kwamba mimi ndio msaidizi wake kwenye chama cha D.F.E”
“So nikusaidieje ikiwa wewe ndio msaidizi wake?”
Majibu ya Manka yakamkatisha hata tama John ya kitu ambacho alipanga kukizungumza kwa wakati huo. Manka akaondoka, na kurudi katika chumba cha mawasiliano ambapo humo kwa watu ambao sio wahusika wa ngazi za juu au si mfanyakazi wa kitengo hicho cha mawasiliano haruhusiwi kuingia.
‘Anajiona jeuri, nitamuangusha’
John alijisema kimoyo moyo huku akiwa amekasirika. Akakumbuaka maneno aliyo yasikia akiwa wanamkaribia Manka sehemu alipo kuwa amesimama
‘…….Ungekuwa na uchungu na huyo ERICKSON ungemtafuta tangu jana sawa’
“Nirudishe kwenye gari sasa hivi”
John alizungumza huku akiendela kuyafikiria maneno hayo. Wakapifaka kwenye maegesho kabla hajaingizwa kwneye gari, akawa amepata picha kamili ya kitu alicho kuwa akifikiria.
“Erickson yupo humu ikulu”
“Umejuaje bosi?”
“Huyu Manka nahisi alikuwa anazungumza na Agnes ambaye anahangaika kumtafuta huyo Erickson”
“Sasa mkuu unahitaji mimi nifanye nini?”
“Hakikisha unajua ukweli na kama yupo humu ndani yah ii ikulu, hakikisha kwamba unamuua”
“Sawa mkuu”
***
Agnes akakata simu aliyo kuwa ameiweka loudspeaker na wezake watatu alio kuwa nao ambao ni Anna, Fetty na Halima walisikia mazungumzo yote na wote wakajikuta wakiwa wamechukizwa na maneno ya Manka.
“Ina maana anatumia mabavu kukuchukulia mpenzi wako si ndio?”
Fetty alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka.
“Ndio maana yake.”
“Ni lazima tumuonyeshe sisi ni nani kwa maana naona hatujui vizuri”
“Kitu kingine kama nilivyo waambia ni lazima kumrudisha Rahab kwenye timu na kitakacho fwata hapa ni lazima kumuangusha Manka na baba yake”
“Umoja”
Halima alizungumza huku akinyoosha mkono wake wa kushoto alio kunja ngumi, wote wanne wakaikutanisha mikono yao ya kushoto walio kunja ngumi.
“Umoja ni nguvu, utengango ni udhaifu”
Walizungumza kwa pamoja huku wakikumbatia kwa pamoja, wapanga kuuangusha utawala wa mzee Godwin na mwanaye Manka
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 95 YA SIMULI HII
 
SORRY MADAM (99)
(Destination of my enemies)

WRITER………………………………………………………………….………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..…… www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT………………………………………………………………………….0657072588/0768516188
JIUNGE NA MAGROUP YANGU YA WHATSAPP NA FACEBOOK, YANAYO HUSIANA NA HADITHI TU KWA KIIINGILIAO CHA SH 2000 KWA MWENZI. 0657072588.

ILIPOISHIA
“Tumeweza kuchukua vipimo kwa mgonjwa, kiujumla afya yake ipo vizuri, ila ana vimelea vya ugonjwa wa saratani, ambao imetulazimu kwamba kuanza kufanya matibabu leo hii hii, ila ninaamini kwamba kila kitu kinaweza kuwa vizuri”
Manka akajikuta akishusha pumzi nyingi huku akiwa amemtazama daktari huyo. Mlio wa simu ukawastua wote walio kaa eneo hilo, Manka akajipapasa mfukoni mwa koti lake akatoa simu yake na kufungua ujumbe huo wa meseji na kuisoma meseji hiyo iliyo mstua na kumfanya anyanyuke kwenye kiti alicho kalia huku macho yakiwa yamemtoka na kuwafanya Madam Mery na Madam Mery kumtolea macho wakitaka kufahamu ni kitu gani kilicho andikwa kwenye meseji hiyo.

ENDELEA
Manka akahisi mwili mzima ukitaka kumuishia nguvu, taratibu akaka kwenye kiti huku akiwa ameishia simu yake. Ikambidi Madam Mery kuichukua kwa haraka simu hiyo na kuusoma ujumbe ambao umeandikwa.
(TUNAHITAJI KUFANYA MABADILIKO, MUACHIE ERICKSON, TUKUPATIE GODWIN. NA SWALA HILI LIFANYIKE NDANI YA MASAA 24 LEO)
Madam Mery akashusha pumzi nyingi, ukimya ukatawala ofisini humo, daktari asifahamu kinacho endelea. Ubaya wa meseji hiyo iliyo tumwa, nambaya yake ni Private, ikimaashisha kwamba haijaweza kuonekana na kufahamika mtumaji ni nani. Manka akaichukua simu yake na kupiga baadhi ya namba na kuiweka sikioni.
“Ndio muheshimiwa”
“Niandalieni kikao cha wakuu wote wa majeshi, ninakuja sasa hivi ikulu”
“Sawa muhehsimiwa”
Manka akakata simu, akanyanyuka kwenye kiti na kupiga hatua hadi mlangoni kisha akageuka na kumtazama dokta na Madam Mery aliyepo nyuma yake.
“Dokta nahitaji mgonjwa wangu mumpatie matibabu ya kutosha. Na hitaacha walinzi waweze kumlinda, yoyote ambaye hausiki na kuingia kwenye chumba hicho ninakuomba asiingie”
“Mimi nitabaki kukaa na mgonjwa”
Madam Mery alizungumza huku akimtazama Manka, ambaye naye akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akaitingisha kichwa cha kukubali mama yake mdogo huyo kuweza kubaki hapo hospitalini na kumlinda Erickson.
“Sawa muheshimiwa”
“Tafadhali daktari ninakuomba sana mgonjwa wangu mumtazame kwa maana yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu”
“Usijali hilo muheshimiwa, tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kwa maana kazi yetu ni kuokoa maisha ya wa watu”
“Nitalishukuru daktari”
Manka na madam Mery wakatoka katika ofisi hiyo na kuanza kuelekea katika chumba alicho lazwa Erickson, ila ukweli wa kila kitu ni madam Mery pekee ndio anafahamu kwamba Erickson ndio Eddy, ambaye amefahamu kwamba pia ni mwanaye, japo amezaliwa na mwanamke mwengine ambaye si dada yake.
“Mama mdogo nakuomba uwe makini na Erickson, kwa maana sijui ni kitu gani nifanye juu ya hii meseji”
“Usiwe na shaka katika hilo, ninakuomba uende ukafanye kikao hicho, na aikiwezekana tutawageuka wote hao, watamkosa Erickson na pia tutamuokoa muhueshimiwa”
“Asante mama mdogo kwa ushauri wako”
Manka akamkumbatia madam Mery kwa nguvu, kisha wakaingia kwenye chumba alicho lazwa Erickson ambaye kwa sasa anahemea mashine yahewa safi.
“Erickson wangu ni mzuri eheee?”
Manka aliuliza huku machozi yakimlenga lenga. Madam Mery akatingisha kichwa akionekana kukubaliana na lile ambalo amelizungumza Manka.
“Mama mdogo, tafahdali mlinde sana Erickson”
“Usijali wewe niachie walinzi tu wakusaidiana nao”
“Unahitaji wangapi?”
“Wanne”
“Sawa sasa hivi ninawaacha hapo nje”
Wakatoka wote kwa pamoja ili Manka amuonyeshe madam Mery walinzi atako waacha hapo nje. Walipo maliza zoezi hilo la kutambulishana. Manka akaondoka eneo la hospitali na kuelekea ikulu na kumuacha madam Mery akiwa amekaa chumba kimoja na Erickson ambaye hadi sasa hivi hajazinduka katika usingizi mzito ulio tokana na kuchomwa sindano ya usingizi.
***
Shamsa moja kwa moja akaelekea hadi nyumbani kwa Eddy mara tu ya kutoka kwenye korongo. Kitu cha kwanza kukifanya baada ya kufika karibu kabisa na nyumba hiyo akasimamisha gari lake, kisha akashuka na kuanza kutembea kwa miguu hadi getini. Ukimya ulio tawala ndani ya nyumba hiyo dhairi kunaonyesha hakuna mtu wa aina yoyote ndani ya nyumba hiyo, ukizingatia akili ya viongozi wengi sasa hivi walipo serikalini pamoja na askari akili zao zipo katika kumtafuta raisi Godwin.
Akaingia kwenye geti, kwa umakini mkubwa, alipo hakikisha kwamba eneo la nje hapo lipo salama, moja kwa moja kwa mwendo wa kasi akaingia ndani, hali ya sebleni hapo haikuwa tofauti sana na siku ambayo waliondoka. Akalelekea kwenye chumba cha ardhini ambapo, ndipo pesa za Eddy alipo ziweka. Akaingiza namba za siri kwenye mlango wa chumba cha kwanza kisha akaitoa picha kubwa iliyopo ukutani na kukuta sehemu nyingine ya kuingiza namba za siri ili mlango wa chumba cha pili uweze kufunguka.
Akatuliza akili yake kisha akaanza kuingiza namba ambazo anakumbuka jinsi siku alivyo kuja eneo hilo na Eddy, vidole vyake vilivyo kuwa vikiminya minya hizo batani.
Haikuwa kazi ngumu kwake, mlango huo ambao ni kipande cha ukuta ukafunguka taratibu. Shamsa akaingia ndani ya chumba hicho na kukuta pesa zote walizo ziacha zikiwa humo humo. Kwa haraka akaanza kubeba vibunda vingia na kuviweka katika chumba cha kwanza, alipo hakikisha pesa ambayo ameichukua hapo inamtosha, akaufunga mlango huo, akatoka na kuelekea katika chumba chake cha kulala. Akafungua kabati lake na kutoa begi lake kubwa la mgongoni, akashuka nalo kutoka gorofani hadi kwenye chumba hicho kilichopo chini ya ardhi.
Akaanza kuziingiza pesa hizo ambazo kwa haraka haraka hakujua ni kiasi gani kwa maana zimefungwa nyingi kwenye vibunda. Alipo malinza kulijaza begi hilo akarudi nalo chumbani kwake. Akaingia bafuni na kuoga, akabadilisha nguo na kuvaa nguo nyingine ambazo zilikuwa kwenye kabati lake hilo.
‘Niende bank gani nikabadilishe hii pesa?’
Shamsa alizungumza huku akijitazama kwenye kioo, jinsi alivyo pendeza. Suruali yeusi, buti nyeusi, tisheti jeupe pamoja na kikoti cheusi, alikiri mwenyewe kwamba amependeza. Akafungua tena kabati lake na kutoa kofia nyeusi na kuivaa.
‘Hapa sio rahisi kwa mtu kuweza kunifahamu’
Shamsa alizungumza huku akiendelea kuzungumza mwenyewe. Akachukua parfum yake moja ambayo kipindi cha nyuma alikuwa anaipenda sana kujipulizia kwenye mwili wake. Akaitingisha kidogo, akafungua mfuniko wake na kuanza kujipulizia mwilini mwake, ila gafla kichefuchefu kikamkamata na kujikuta akiuziba mdomo wake an kukimbilia bafunini, akainama kwenye sink la kunawia na kuanza kutapicha.
“Ohoo Mungu wangu nini tena?”
Shamsa alijiuliza huku akijitazama kwenye kioo kilichopo kwenye sink hilo. Akafungu maji na kuanza kusukutua na kuyatema kwenye sinki huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio.
“Nina nini tena”
Alijiuliza huku akianza kutoka bafuni huko, akaka kitandani akizidi kufikiria ni kitu gani ambacho kinamsumbua kwa wakati huo. Kidogo nguvu zikamrudia na hali ya mapigo ya moyo kumuenda kasi ikampungua. Akanyanyuka kitandani akanyanyua begi lake lililo jaa pesa, akalibeba mgongoni na kuanza kutoka ndani homo. Akajikaza na kuanza kutembea moja kwa moja hadi kwneye gari lake alipo liacha.
Akashusha pumzi nyingi, mara baada ya kukaa kwenye siti ya dereva, akafunga mlango huku begi hilo la pesa akiwa wameliweka siti ya pembeni.
Safari ikaanza kuelekea benki yoyote ambayo alihisi kwamba anaweza kupata huduma ya kubadili pesa hiyo ya kimarekani na kupewa shilingi. Akafika baki ya Bacrayse maeneo ya Posta, akasimamisha gari lake eneo la maegesho kisha akashuka na kuelekea ndani.
“Nahitaji kubadili pesa”
Alimueleza muhudumu wa mapokezi, ambaye alimuonyesha mlango wa kuingia kwenye moja ya ofisi ya wahudumu wanao shuhulika na ubadilishaji wa fedha za kigeni. Akaingia kwenye ofisi hiyo na kumkuta dada mmoja mwembamba kiasi aliye valia vizuri sara zake na kupendeza. Akalivua begi lake na kukaa kwenye kiti alicho karibishwa kukaa
“Nahitaji kubadili pesa”
“Ni kiasi gani?”
Shamsa akafungua begi lake hilo na kuanza kutoa vibunda hivyo vya pesa na kuanza kuvipanga hapo mezani. Kadri jinsi anavyo vitoa ndivyo jinsi dada huyo alivyo baki ameshangaa kwa maana katika utendaji wake wa kazi hakuwahi kukutana na mtu anabadilisha pesa kiasi hicho kikubwa.
“Inabidi tuzihesabu”
“Sawa hakuna shida”
Dada huyo akaanza kufungua rababend ya kibunda kimoja moja na kuweka noti hizi kwenye mashine maalumu ya kuhesabia pesa. Kazi ya kuzihesabu pesa hizi ikachukua dakika kumi na tano hadi wanamaliza na kiasi cha pesa ambacho kimepatikana hapo ni dola milioni mbili na laki nne, ambazo ni sawa na shilingi bilioni tano na milioni arobaini za kitanzania.
“Unaweza kubibadilishia hiyo dola laki nne?”
“Na hizi mbili”
“Nahitaji kufungua akaunti na niziweke”
“Sawa”
Wakaanza kufanya harakati za Shamsa kufungua akaunti kwa kuwahonga wahudumu wanao mshuhulikia swala la kumfungulia akaunti, haikuchukua muda kitu alicho wapatia ni picha za passport size alizo piga nje ya benk hiyo kwenye moja ya studio. Hadi lisaa moja linakatika kila kitu Shamsa akawa amemaliza hadi kadi ya benki akawa amepatiwa. Akazibeba milioni mia nane arobaini kwenye begi lake huku pesa nyingine akiziweka kwneye maboksi aliyo patiwa hapo benki, akaziingiza kwenye gari lake na kuondoka.
Kizungu zungu na kustuka mapigo ya moyo kwa mara kadhaa, kukamfanya Shamsa kuamua kupitia kwenye hospitali moyo iitwayo Bochi, maeno ya Mbezi kwa msuguri. Akachukua noti kadhaa na kushuka kwenye gari lake, akalifunga vizuri na kuingia hospitalini hapo. Akamuhonga nesi wa mapokezi ili aweze kuonana na daktari kwa haraka haraka. Kweli nesi huyo akampatia nafasi ya kipekee ya kumuingiza kwenye chumba cha daktari japo kuna foleni ya kina mama wamejipanga wakisubiri huduma.
“Unajisikiaje”
Shamsa akaelezea tatizo linalo msumbua, daktair moja kwa moja akatambua kwamba binti huyu ni mjamzito, japo hakutaka kukisia akaamua kumfanyia vipipo vya kupima mimba. Shamsa akayasubiria majibu ndani ya chumba hicho hicho cha daktari.
“Dokta nina sumbuliwa na nini?”
Daktai akatabasamu huku akiwa ameshika karatasi aliyo andika majibu hayo. Akaiweka miwani yake vizuri na kuyapitia majibu kwa mara ya pili kisha akamtazama Shamsa.
“Hongera sana binti, unaonekana una ujauzito wa mwezi moja sasa”
“Dokta What……?”(Daktari nini?)
“Vipimo vinaonyesha wewe ni mjamzito wa mwezi mmoja sana”
Shamsa akajikuta akifumba mdomo wake kwa kiganja cha mkono wa kulia, hakuamini kwamba ipo siku anaweza kupata ujauzito tena wa mwanaume anaye muheshimu kama baba yake, ambaye ni Eddy. Akaikwapua karatasi ya daktari hiuyo na kuisoma vizuri, hapakuwa na kitu kilicho badilika zaidi ya majibu konyesha yeye ni mjamzito.
“Dokta asante”
Shamsa akanyanyuka na kuondoka ofisini humo akiwa katika hali ya mshangao. Hakujua hata aanze vipi kumueleza Eddy. Akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo, safari ya kueleka alipo waacha Phidaya na Sa Yoo ikaanza huku njia nzima kichwa chake kikiwa na mawazo mengi sana. Shamsa akafanikiwa kufika salama salami kwenye kijiji cha Wamasai hao, akakuta wakiwa kwenye mkutano huku Phidaya na Sa Yoo wakiwa wamesimama pembeni.
“Umechelewa hadi tukapatwa na wasiwasi”
Phidaya alikuwa wa kwanza kuzungumza mara baada ya Shamsa kushuka kwenye gari. Wakasalimia kwa kukumbatiana.
“Mbona umechelewa”
Shamsa akawaadisia mambo aliyo kutana nayo huko alipo toka, huku swala la yeye kuwa mjamzito akawaficha wezake.
“Wanajadili nini hao?”
“Wanajadili juu ya vifo vya vijana wao”
“Nimekuja na pesa za kutosha tunaweza kuwapatia wao, kama rambirambi yetu”
“Basi ngoja nifanye kumuita mmoja wao ili nimueleze hili swala”
Sa Yoo akamuita binti ambaye walikuwa naye akamueleza kitu wanacho taka kukifanya, binti huyo akapeleka ombi hilo kwa mwenyekiti wa mkutano huo ambaye naye aliweza kuwaeleza wanakijiji wote walio kubaliana kwa pamoja kupokea rambirambi hiyo.
“Tuwape tu sisi tuondoke zetu, nimesha choka kukaa hapa kijijini”
“Hapana mama, tuwasimamie wanaweza kudhulumiana si unafahamu hii ni pesa”
“Kweli unacho sema Shamsa”
Wakakubaliana kwa pamoja na kila familia ambayo ilipoteza kijana mmoja iliweza kupatiwa milioni kumi. Zoezi hilo likachukua masaa matatu na kumalizika pasipo kutokea vurugu ya aina yoyote. Shamsa, Sa Yoo na Phidaya wakawaaga wanakijiji hao walio ingiwa na furaha ya pesa, na kuondoka zao kijiji hapo.
***
“Hii meseji niliyo mtumia Manka ninaamini kwamba ni lazima itamchanganya”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake walio kaa kwenye sofa za hapo sebleni mwa Agnes.
“Sasa itakuwaje, akikataa kumleta Erickson?”
Agnes aliuliza huku akimtazama Rahab usoni anaye onyesha kudhamiria kufanya kile ambacho amekifikiria.
“Nitamuua Godwin kwa mkono wangu”
“Ila Rahab tufanye kwanza mabadilishano ya Erickson na Godwin”
“Kisha, hata kabla hawajamchukua Godwin tunamuua”
Fetty alizungumza na kuwafanya wezake wote kulifikiria swala hilo.
“Natambua kwa sasa atakuwa amekwenda kujadiliana na viongozi juu ya meseji uliyo mtumia”
“Alafu Anna wewe si waziri wa mambo ya ndani, fanya basi uende ikulu ukajue mpango wao ni nini”
“Alafu?”
“Ukisha fahamu mimi huku nyuma nitamtumia Manka meseji nyingine ya kumambia ni wapi tuje kufanya mabadilishano”
“Sawa nitaifanya hiyo kazi”
Anna akakubaliana na wezake, akatoka nje na kuingia kwenye moja ya gari alilo kabidhiwa na Agnes, akaondoka na kuianza safari ya kwenda ikulu.
“Jamani alafu nina namba ya meja Paul Msuya”
“Wa nini tena huyo?”
“Huyu siku alisha wai kunigusia juu ya jeshi kupanga kufanya mapinduzi ya serikali ya sasa hivi, na kama tukiwahi kuungana nao basi tunaweza kuichukua hii nchi”
Wazo la Halima likawafanya wote kukubaliana nao. Halima akatoa simu yake mfukoni na kumpigia meja Paul Msuya na kuiweka loud speaker
“Ndio Meja”
“Nahitaji tuonane kwa mazungumzo yake uliyo wahi kunishirikisha”
“Ohooo safi sana waziri kwa sasa upo wapi?”
“Nipo nyumbani kwangu, sasa sijui tuonane wapi?”
Wakapanga sehemu ya kuonana, ndani ya nusu saa lijalo, Wote wanne walio salia wakaondoka huku wakiwa kwenye magari tofauti tofauti kila mmoja. Wakafika sehemu waliyo kubaliana kuweza kufika na kumkuta meja huyo akiwa na vijana wake wanao mlinda.
“Naona umekuja na timu yako”
“Ndio kwa maana tunataka kufanya kitu cha uhakika katika hili”
“Na huyo si alikuwa ni mke wa muheshimiwa Preygod”
“Ndio meja”
Meja Paul Msuya akasimama kwa haraka na kupiga saluti akiwa pamoja na vijana wake jambo lililo mshangaza sana Rahab.
“Heshima yako mkuu”
“Nashukuru”
“Ni vyema sana tumekupata kwa maana karibia asilimia sabini ya jeshi la Tanzania tulikuwa tunamuunga mkono raisi Praygod, ni wachache sana walio kuwa juu yetu wanao muunga mkono raisi Godwin”
“Sasa huyo unaye sema ni raisi Godwin mimi kwa sasa ninaye”
“Unaye sijakuelewa”
“Baada ya kifo cha mume wangu, na mimi nimeamua kulipiza kisasi kwa Godwin kwa maana yeye ndio amehusika na kifo cha raisi Praygod”
“Ina maana raisi Praygod amefariki?”
“Ndio amefariki, katika mlipuko ulio tokea pale Mlimani City mwezi ulio pita”
“Mungu wangu”
“Nahitaji unikutanishe nia viongozi wote wa jeshi, nataka kufanya mapinduzi na kuhakikisha tunaitoa mizizi yam zee Godwin yote”
“Sawa mkuu”
“Na hili sihitaji liweze kuchukua muda mrefu, leo au kesho kazi iwe imesha kamilika, sinto weza kuona nchi yangu inaendeshwa katika hali isiyo zinga haki na katiba iliyo wekwa”
Rahab alizugumza kwa machungu sana na kuwafanya wote kutulia na kumsikiliza kwa umakini na hapo ndipo ikaonyesha kwamba kuna nguvu ya utawala ambayo Rahab anayo.
“Sasa mkuu unatuhitaji sisi jeshi kuweza kufanya nini?”
“Nahitaji ikulu nzima muweze kuiweka chini ya jeshi, huku wanajeshi wote wanao onekana kuwa ndio wasaliti wa hii nchi muweze kuwatia nguvuni na mkono wa sheria unakuwa juu yao. Na kingine, kwa wale ambao watakuwa ni wakaidi, basi damu haina budi kumwagika”
“Sawa madam”
“Andaa vikosi vyote na uwajulishe juu ya ujumbe wangu na ujumbe alio nipatia mume wangu, nchi hii ni nchi ya kila mwananchi na si nchi ya familia moja wala ukoo mmoja, hatuwezi kufwata maamuzi ya kichwa kimoja ni laziama kufwata maamuzi ya pamoja. Mimi na wezangu hapa tunahitaji makombati ya kijeshi pamoja na silaha”
“Ina maana hawa mawaziri nao watavaa, mavazi hayo?”
“Ndio meja, hawa ni mahodari zaidi ya unavyo wafikiria”
Rahab alizungumza kwa kujiamini. Akatoa simu yake mfukoni na kuisoma meseji iliyo ingia kutoka kwa Anna ambaye yupo ikulu.
(NIMEFIKA NA NIPO KWENYE KIKAO TUMA UJUMBE)
Rahab kwa haraka akaandika meseji nyingine na kumtumia Manka. Alipo malinza hapo, kikao hicho cha dharura walicho kutana na meja kikavujwa rasmi huku Fetty na Anna wakiondoka na meja huyo kwenda kambini huku Agnes na Rahab wakirudi nyumbani kuendelea na mpango wao wa mapinduzi.
***
Wakiwa wanafikiria ni nini cha kufanya juu ya meseji ambayo kiongozi wao ametumiwa na mtu ambaye anaonekana ndio mtekaji, ujumbe mwengine wa meseji ukaingi kwenye simu ya Manka na kwa haraka akaufungua na kuusoma.
(LEO SAA SITA KAMILI USIKU, TUKUTANE DARAJA LA KIGAMBONI KUFANYA MABADILISHANO YA ERICKSON WETU NA RAISI GODWIN, OLE WAKO UJE NA ASKRI TUTAKUONYESHA)
Meseji hiyo ya kitisho ikamfanya Manka kushusha pumzi huku akiwatazama watu waliomo humo ndani ya kikao. Akawasha maiki yake kwa kuminya batani ya kuwashia na kuwaomba watu wote wamsikilize. Akaisoma meseji hiyo kila mtu akaonekana kuogopa kwa maana hapo ni lazima kufanywe maamuzi magumu.
“Madam miimi ninakushauri kwamba ni vyema tukamtoa huyo Erickson anaye mtaka na tena kwenye daraja la baharini, vijana wetu wanaweza hata kujificha ndani ya maji na muda ukimfika tunawaokoa wote wawili”
“Kweli muheshimiwa, ninaungana kabisa na mkuu wa jeshi la maji, mimi nipo tayari kutoa vijana wakaweza kupambana katika hili”
“Nimewaelewa je ikishindikana inakuwaje?”
“Sidhani kama hao magaidi wana uwezo wa kuweza kupambana na serikali na kuiangusha chnini. Serikali yetu ina nguvu ndio maana tukakuteua wewe kutuongoza. Muheshimiwa fanya maamuzi magumu katika hilo”
“Ila kana nilivyo waeleza hapo awali, Erickson ni mgonjwa, itakuwaje katika hili?”
“Madam kama atakuwa amezinduka, anaweza hata kukalishwa kwenye kiti cha magurudumu, na kabla hajafika kwa magaidi hao tunaweza kumchukua”
Manka akanyamaza kimya akiwaza mawazo hayo yanayo tolewa na wakuu hao wa vikosi mbali mbali vya majeshi. Hapakuwa na njia yoyote zaidi ya kuwaamini, na kufanya maamuzi hayo ambayo kwa upande wake kusema kweli ni magumu. Ujumbe ukatumwa hospitalini kwa walinzi, wakaoambiwa waweze kuwaleta ikulu Erickosn na madam Mery. Huku hekaheka za kuanza kufanya maandalizi ya tukio la saa sita usiku yakaanza, vikosi maalumu, vikaanza kuwekwa tayari kwa kazi hiyo. Hata Manka mwenyewe akajiandaa kijeshi kuhakikisha kwamba baba yake na Erickson wanarudi mikoni mwake.
Haukupita muda mrefu Erickson na madam Mery wakafikishwa Ikulu huku Erickson akiwa amesha zinduka. Wakamueleza Erickson mpango mzima ambao upo mbele yao.
“Erickson mpenzi wangu ninakuomba sana uweze kunisaidi katika hili”
Manka alizungumza kwa shauku, Eddy akamtazama Manka jinsi anavyo muomba, akaona akikataa inaweza kuleta picha mbaya, ikambidi kukubali. Madkatari wa hapo ikulu wakitwa na kuanza kumuandaa Erickson kwa kumchoma sindano ambazo walidai zinaweza kumpatia nguvu na kuondoa mamumivu yote ya kidonda anacho kisikia. Walipo maliza kufanya hicho, Erickson akavalishwa jaketi la kuzuia risasi na nguo za kawaida.
“Nitaweza kutembea mwenyewe”
“Kwa hiyo hauta kaa kwenye kiti cha matairi”
“Ndio dokta”
Vikosi vyote vilipo hakikisha vimekaa sawa, wakaanza kusubiria muda na masaa yasonge ili waweze kwenda kwenye sehemu ya tukio kwenye daraja la Kigamboni lililo jengwa juu ya bahari.
***
Mipango yote waliyo panga Manka na viongozi wengine wa kijeshi, Anna akavifikisha kwa Rahab na wezake, hawakupoteza muda wakawasiliana na meja Paul Msuya, na kumueleza kila kitu. Naye hakuta kupoteza muda akaanza kupanga vikosi vyake vya uvamizi Ikulu kwa ajili ya kuipindua nchi.
“Sisi tutadili na hao wote ambao watakuwa chini ya maji wamejificha”
Anna alizungumza huku akiwatazama wezake.
“Anna na Halina nyinyi mutakuwa chini ya daraja, Agnes utakuwa na bunduki ya kudungua kisha mimi na Fetty tutakuwa na huyu fala”
“Sawa”
“Kingine tukumbuke kwamba yote haya tunayafanya kwa ajili ya macho ya mamilioni ya watanzania wanao tarajia nchi yetu kurudi katika mfumo ambao walisha uzoea. Hili tunalo kwenda kulifanya si kwa faida ya nchi na si kwa faida ya matakwa yetu binafsi”
Maneno ya Rahab yakamgusa kila mmoja na wote wakajikuta wakikumbatiana kwa pamoja huku kila mtu akiwa amepania kazi ambayo anakwenda kuifanya kwa siku ya leo. Hawakujua kama kuna kupona au kufa, ila walicho kusudia ni kuhakikisha kwamba wanatimiza kile walicho kihitaji kukifanya. Wakavalia mavazi ya kijeshi, kial mmoja silaha yake akaiweka katika sehemu ambayo amekusudia kuiweka. Anna na Halima, wakabeba na nguo pamoja na mitungi ya kuwasidi kukaa chini ya maji kwa muda mrefu, baada ya kila mmoja kuhakiksha maandalizi yake binafsi yamekamilika, wakatoka nje na kumchukua raisi Godwin wakaumuingia kwenye gari aina ya Range rover ambayo ni nyeusi, wakapanda Rahab na Fetty ambaye ni dereva. Anna Halima na Agnes wakaingia kwenye gari jengine ambalo ni BMW X6. Kila mmoja wao akawa na kifaa cha mawasiliano ambacho kiliweza kiwawezesha wote watano kuweza kuwasiliana kwa wakati mmoja.
“Hivi sasa ni saa mbili usiku, safari yetu moja kwa moja itakuwa hadi Kigamboni mwanzo wa daraja, na baada ya hapo tunaweza kusubiri hadi pele saa sita itakapo timu”
“Sawa”
Wakatoka kwenye jumba hilo la Agnes, aliye mpa maelezo mlinzi wake kufunga geti na kukaa ndani na asitoke. Safari ikaanza huku gari waliyo panda Agnes ikitangulia mbele na gari waliyomo Rahab ikifwatia nyuma. Hawakwenda kwa mwendo wa kasi kuhofia kustukiwa, uzuri wa gari zote zina vioo vyeusi ambavyo sio rahisi kwa mtu wa nje kuweza kuona ndani.
Wakafanikiwa kufika Kigamboni saa tatu na nusu usiku na kuwawahi hata makachero wa serikali walio fika saa nne kamili usiku.
Anna na Halima wakavaa mavazi yao ya kuzamia ndani ya maji pamoja na gesi zao kisha wakatoka na kuzama baharini pasipo mtu yoyote kuweza kuwaona zaidi ya Agnes, ambaye yeye alisalia ndani ya gari peke yake. Masaa yakazidi kwenda taratibu, kila mmoja akatamani kuweza kuona saa sita inafika kwa haraka.
Makachero kutoka ikulu pasipo kufahamu kwamba wanacho kifanya wanaonwa na maadui zao, wakaanza kuzuia magri yaliyo kuwa yanahitaji kupita katika daraja hilo na hadi inatimu saa sita kasoro tano, gari la Manka akiwa na Erikckson aliye mpakiza siti ya nyuma likafika mwanzo wa daraja kuelekea Kigamboni.
“Naona wamesha fika”
Fetty alizungumza huku akiwa analitazama gari la Manka kwakutumia darubini.
“Liweke gari barabarni”
“Poa”
Fetty akaliwasha gari na taratibu akaanza kojongea kwenye daraja hilo. Manka naye alipo weza kuiona gari hiyo akawasiliana na makachero wake walio zagaa kila mahali, na kuwaeleza kwamba wahusika wamesha fika.
”Kuweni makini na musifanye chochote pasipo mimi kuweza kuwapatia amri ya kufanya”
“Sawa mkuu”
Manka naye akalisogeza gari lake taratibu. Kisha akalisimamisha umbali mkubwa kutoka lilipo simama gari Rahab. Saa sita kamili ilipo fika, simu ya Manka ikaita, akaitoa mfukoni mwake na kukuta namba inayo piga hapo ni hiyo private namba. Kwa haraka akaipokea na kuiweka simu yake sikioni.
“Habari Manka, naamini umekuja na mtu tunaye muhitaji”
“Ndio na mimi ninaimani umekuja na baba yangu”
“Yupo, mshushe Erickson nasi tumshushe baba yako mzee Godwin”
“Sawa”
Manka akakata simu na kumgeukia Erickson aliye mpakiza siti ya nyuma.
“Honey wakati ndio huu, nakuomba ushuke, vijana wapo chini ya daraja watafanya yao”
“Sawa”
Erickson, taratibu akafungua mlango wa gari hilo, kabla hajashuka Manka akamshika mkono, wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha akamuachia. Eddy akapiga hatua hadi mbele ya gari la Manka linalo washa taa zenye mwanga mkali, na kwa upande wa mbele ya daraja akamuona Rahab akimshusha raisi Godwin, japo Rahab amejificha sura yake kwa kujichora na rangi nyeusi wanazo tumia wanajeshi wakiwa vitani ila aliweza kumfahamu kutokana na tembea yake. Erickson akageuka na kutazama nyuma, Manka kwa ishara akamuomba atembee. Erickson taratibu akaanza kutembea akilifwata gari la Rahab lilipo, huku Mzee Godwin naye akianza kutembea kwa kuchechemea akionekana ni mtu mwenye majeraha makubwa sana. Wakazidi kutembea huku pande zote mbili wakiwatazama jinsi wanavyo tembea. Agnes aliye jificha sehemu akiwa na bunduki yanye lensi ya kuona mbali, akawa analifwatilia tukio hilo kwa umakini.
Ila Agnes akiwa eneo hilo akaona kuna sehemu moja ya pemeni ya bahari kukiwa na mtu ambaye ana bunduki kama yake, na ameielekeza kwa Eddy kwa haraka Agnes akanza kuimvuta mtu huyo karibu na kumkumbuka kwamba mtu huyu ni mlinzi wa John.
“Shitiii”
Agnes akaikoki bunduki yake na kumuelekezea mtu huyo na kumpima maeneo ya kichwa. Mzee Godwin hadi anakaribiana na Erickson akaweza kuona alama nyekundu ya buduki ikiwa imemlenga Erickson kifuani. Kwa haraka Mzee Godwin kwa akamuwahi Erickson ambaye anatambua ni mkwe kwa mwanaye Manka, akamsukuma na risasi ambayo ilipangwa kumpiga Erickson ikapiga mzee Godwin mgongoni na kumuangusha chini na kumfanya Eddy kushangaa na kwaharaka akaipiga magoti chini na kumgeuza Mzee Godwin na kumkuta akimwagikwa na damu mdomoni.
“BABABAAAAAAAAAA”
Eddy alipiga kelele humu machozi yakianza kumwagika usoni mwake na kumfanya Mzee Godwin kutabasamu na kumshika mkono wa kulia Eddy na kuuweka kifuani mwake.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 100 NA YA MWISHO YA SIMULI HII YA KUSISIMUA
 
SORRY MADAM (100) final episode
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
JIUNGE NA MAGROUP YANGU YA WHATSAPP NA
FACEBOOK, YANAYO HUSIANA NA HADITHI TU KWA
KIIINGILIAO CHA SH 2000 KWA MWENZI.
0657072588.
ILIPOISHIA
“Shitiii”
Agnes akaikoki bunduki yake na kumuelekezea
mtu huyo na kumpima maeneo ya kichwa. Mzee
Godwin hadi anakaribiana na Erickson akaweza
kuona alama nyekundu ya buduki ikiwa imemlenga
Erickson kifuani. Kwa haraka Mzee Godwin
akamuwahi Erickson ambaye anatambua ni mkwe
kwa mwanaye Manka, akamsukuma na risasi
ambayo ilipangwa kumpiga Erickson ikapiga mzee
Godwin mgongoni na kumuangusha chini na
kumfanya Eddy kushangaa na kwaharaka akaipiga
magoti chini na kumgeuza Mzee Godwin na
kumkuta akimwagikwa na damu mdomoni.
“BABABAAAAAAAAAA”
Eddy alipiga kelele humu machozi yakianza
kumwagika usoni mwake na kumfanya Mzee
Godwin kutabasamu na kumshika mkono wa kulia
Eddy na kuuweka kifuani mwake.
ENDELEA
“Eddy”
Mzee Godwin aliweza kuitambua sauti ya Eddy na
kulia kwake. Eddy kwa hasira akaanza kuivua sura
yake ya bandia, japo imeshikana sana na ngozi ya
uso wake, ila hakujali hayo maumivu. Mzee
Godwin akaendelea kumuangalia Eddy kitu anacho
kifanya hafi ikafikia hatua akamaliza kabisa kuivua
sura yake na kubaki na sura alisi.
“Baba fungua macho please”
Eddy alizungumza huku machozi yakimwagika
usoni mwake. Japo baba yake huyo ameweza
kumfanyia mambo mengi mauvu katika maisha
yake yote ila damu ni nzito kuliko maji.
“Ku….uu…wa…..jasiri D.F.E1993”
Mzee Godwin alizungumza maneno hayo kwa
shida kidogo na hapo hapo akakata roho. Kitendo
cha mzee Godwin kuanguka chini na kunyanyuliwa
na Erickson, kiliweza kumstua Manka aliye anza
kushuka kwenye gari kwa garaka, na kuanza
kukimbilia eneo alipo kaa Mzee Godwin na
Erickson. Agnes hakutaka kumpa nafasi nyingine
mlinzi wa John ambaye alikuwa akihangaika
kuikoki bunduki yake. Akamtandika riasi moja ya
kicha na kumchangua hapo hapo. Makachero
wengine walipo ona makubaliano yameingia dosari
wakaanza kufaya mashambulizi kwa kina Rahab na
Fetty, ambao nao waliweza kuyajibu mashambulizi
hayo huku wakiwa amejificha pembeni ya gari lao.
Agnes akashusha pumzi huku akimtazama Manka
kwa kutumia lenzi ya bunduki yake, akikimbilia
eneo alipo Erickso.
“Mpumbavu wewe”
Agnes alizungumza huku akiikoki bunduki, yake.
Alipo hakikisha Manka amekaribia kufika karibu
kabisa na walipo Eddy na mzee Erickson, akaivuta
traiga ya bunduki hiyo na kuiruhusu risasi moja
kutoka kwa kasi. Kitendo cha Manka kumtazama
Erickson na kukuta akiwa ni Eddy, alistukia
akianguka chini na hapo hapo akakata roho, risasi
aliyo ifyatua Agnes iliweza kutua kichwani mwa
Manka ndio iliyo yakatisha maisha ya msichana
huyo.
Eddy alihisi kuchanganyikiwa, baada ya kumuona
Manka akiwa amelala chini, damu nyingi zikiwa
zimesambaa kwenye lami. Halima na Anna wakiwa
chini ya maji, waliweza kupambana na makachero
wengine ambao walitumwa kuimarisha ulinzi chini
ya daraja hilo. Mapambano yao yakawa ni kufa na
kupona. Halima akajitahidi kupambana kadri ya
uwezo wake, ila kwa leo bahati haikuwa kwake
kwani kachero aliye kutana naye aliweza kumzidi
kwa kila kitu na kujikuta akifia kwenye mikono ya
kachero hiyo kwa kuchomwa kisu cha shingoni.
Kifo cha Halima, kilimshangaza sana Anna, aliye
jikuta akiivunja shingo ya kachero aliye kuwa
akipambana naye na kuimtoa mtungi wa gesi alio
jifunga nao mgongoni. Akamfwata kachero aliye
muua Halima, akaanza kuparanganaye, mapigano
kati yao yaliweza kumpa ushindi Anna japo naye
aliweza kujeruhiwa na kisu cha kachero hiyo ila
akafanikiwa kummaliza maisha yake. Taratibu Anna
akaanza kuufwata mwili wa Halima sehemu unapo
elea elea. Akaushika, na kujikuta akianza kulia kwa
uchungu, kwa maana hakutarajia kama rafiki yake
huyo anaweza kukutwa na mauti. Agnes kazi yake
ikawa ni kuwaua makachero wote ambao
wanapambana na kina Fetty na Halima. Haikuwa
kazi ngumu kwake kwa maana sehemu alipo jificha
ni si rahisi kwa mtu kuweza kumuona ila yeye
aliweza kuona eneo zima.
***
Wanajeshi na walinzi walio weza kubaki ikulu kwa
ajili ya kuimarisha ulinzi kwa siku hiyo hawakuwa
na bahati, kwa maana waliweza kushambuliwa na
wanajeshi ambao wamevalia kombati za jeshi la
taifa, ila utoafuti ni kwamba karibia wote
wamejifunga vitambaa vyekundu katika mikono yao
ya kushoto. Walijitahidi kuilinda Ikulu ila
hawakuweza kwa maana shambulizi hilo ni kubwa
na la kustukiza. Meja Paul Msuya aliweza
kuwaongoza vijana wake katika kufanya mapinduzi
hayo ya kuing’oa serikali yam zee Godwin
madarakani.
Zoezi lao halikuchukua muda mrefu sana, wakawa
wamesha maliza kazi yao na kuiwek aikulu chini
ya ulinzi wao. Meja Msuya akatuma wanajeshi
wengine kwenda katika daraja la kigamboni
kumsaidia mkuu wao ambaye ni Rahab. Milio ya
risasi, iliwafanya wakazi wa maeno ya Posta na
Kigamboni kuingiwa na hofu kubwa sana, kwa
maana sio hali ya kawaida na hawakujua ni kitu
gani kinacho endelea. Wananchi wengi walio
ingiwa na woga, kila mmoja aliweza kujificha
sehemu ambayo alihisi anaweza kuokoa maisha
yao. Wapo ambao waliweza kujificha chini ya
vungu za vitanda vyao, wengine walijificha kwenye
makabati, wengine waliamua kujifuanika mashuka
gubigubi na kujinyoosha vitandani mwao na
kuigiza kama wamekufa. Ukawa ni usiku mgumu
sana kwao. Wanajeshi wanao muunga mkono
Rahab, wakafika katika dareja la Kigamboni na
kukuta mambo ndio yanamalizikia malizikia, huku
walinzi wengi wa raisi Godwin wakiwa wamesha
potea maisha yao. Wakaweza kuuona mwili wa
mzee Godwin na mwanaye Manka wakiwa tayari
wamesha teketea kwa kupigwa risasi.
Ushindi huo uliweza kumfurahisha kila mmoja aliye
husika katika oparesheni hiyo ya kuipindua serikali
yam zee Godwin, mtu ambaye walimuona ni kama
diktekta katika kuiongoza nchi.
“Kwa nini mumuue na Manka ana kosa gani?”
Eddy alizungumza huku akimgandamiza Rahab
kwenye gari huku akiwa amemkuja kombati la jeshi
alilo kivaa maeneo ya kifuani.
“Eddy please reduce your anger”(Edd tafadhali
punguza hasira yako)
“Nipunguze vipi hasira, wakai mumemuua mtu
ambaye hata hatia eheee”
Eddy aliendelea kufoka, huku akiendelea
kumkandamiza Rahab kwenye gari hilo. Fetty na
Agnes ambao wapo pembeni, walikaa kimya huku
Agnes akiwa haamini macho yake kwamba
Erickson ambaye alikuwa anampenda siku zote
kumbe ni Eddy ambaye tayari alisha weza kuiona
sura yake kwenye picha na kuelezwa na Manka
kwamba waweze kumuangamiza.
“Eddy am sorry”
Agnes alizungumza huku akipiga magoti chini,
Agnes akatoa bastola yake na kumkabidhi Eddy.
“Niue kwa sababu mimi ndio niliye muua Manka”
“Umemua Manka kwa wivu wako wa kijinga, Manka
mimi ni dada yangu”
Eddy alizidi kuzungumza kwa hasira, akaitazama
bastola aliyo ipokea kutoka kwa Agnes, kwa hasira
akachomoa magazine yake na kuigawanya vipande
viapnde na kuitupia ndani ya bahari. Eddy
akaondoka eneo hilo huku akiwa analia kwa
uchungu. Akaeleka hadi kwenye mwili wa Manka
ulio zungukwa na wanajeshi wa mapinduzi.
Taratibu Eddy akapiga magoti chini, kisha taratibu
akamnyanyua Manka kwa mikono yake miwili na
kuanza kutembea naye kuelekea kwenye gari walilo
kuja nalo. Wanajeshi wote wakasimama kwaenye
mstari mmoja na kumpigia saluti Eddy anaye
elekea kwenye gari. Akauingiza mwili wa Manka na
kuulaza katika siti ya nyuma ya gari hilo kisha
akapanda mbele, taratibu akalirudisha nyuma,
akakunja kona na kuondoka na kuwaacha
wanajeshi pamoja na Rahab wakimshangaa.
Rahab akawagiza wanajeshi wengine kuingia ndani
ya maji na kuanza kumtafuta Halima na Anna. Kwa
bahati nzuri akawaona wakiwa wapo eneo moja.
Wakamsaidia Anna kutoka kwenye bahari, huku
wengine wakiubeba mwili wa Halima na kutoka
naye kwenye bahari. Rahab, Fetty na Agnes
walivyo muona Anna ametoka ndani ya maji hayo
akiwa anamwagikwa na machozi, wakatambua kwa
haraka kwamba kuna jambo baya limeweza
kutokea.
Walipo uona mwili wa Halima ulio bebwa na
wanajeshi hao, machozi yakaanza kumlenga lenga
kila mmoja wao. Fetty na uhodari wake wote
akajikuta akiangua kilio huku akiumtazama Halima
kuhakikisha kama kweli amekufa au wanatania.
“Halipa tafadhali huwezi kufa kirahisi kiasi hichi”
Fetty alizungumza kwa uchungu na kuwafanya
wezake wengine nao kuangua kilio, japo Rahab
alijikaza na kulia taratibu taratibu. Wanajeshi hao,
wakauchukua mwili wa Halima na kuupakiza
kwenye gari, na kuondoka nao kueleka katika
hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuihifadhi.
Wanajeshi wengine walio salia wakauchukua mwili
wa Mzee Godwin ambao hakuna mtu aliye
uthamini, sana. Wakautupia ndani ya gari na
kuondoka nao.
“Muheshimiwa Ikulu ipo tayari kwa ajili yako”
Mwanajeshi mmoja alizungumza na Rahab.
Wakaingia nanye kwenye gari moja ya ikulu walio
kuja nayo eneo hilo na kuondoka naye. Fetty na
wezake wakapanda katika magari mawili waliyo
kuja nayo na kuongozana na gari hiyo kueleekea
Ikulu.
***
“Hii Laptop ni ya nani?”
Sa Yoo aliuliza huku akiitazama Laptop aliyo
ipakata kwenye mapaja yake wakiwa ndani ya gari
kurudi Dar es Salaam.
“Nimeikuta humu humu, nahisi itakuwa ni laptop
ya Eddy”
Shamsa alijibu huku akeindelea kuongeza mwendo
kasi wa gari hiyo.
“Sasa tunakwenda wapi Shamsa?”
“Mama tunakwenda nyumbani kwako”
“Huoni kama kuna harari?”
Hakuna mtu, kupo salama kabisa”
Waliendelea kuzungumza huku wakizidi kusonga
mbele. Safari yao haikuchukua masaa mengi hii ni
kutokana hakuna magri usiku huo. Wakafanikiwa
kufika nyumbani kwa Eddy, Shamsa akashuka na
kufungua geti kisha akarudi kwenye gari akaingia
ndani, na kulisimamisha gari hilo mbele ya ngazi
za kupandia kueleka kwenye mlango wa kuingilia
ndani ya jumba hilo.
Wote wakashuka na Shamsa akaeleka getini na
kulifunga geti. Wote kwa pamoja wakaingia ndani.
Moja kwa moja wakaelekea chumbani kwa Shamsa,
ambapo Phidaya na Sa Yoo wakaanza kuoga kwa
kupokezana kwani ni kwa muda sasa miili yao
haijagusa maji kabisa.
“Shamsa hivi hii tv inafanya kazi kweli?”
Sa Yoo aliuliza huku akiitizama tv uliyopo ukutani
yenye ukubwa wa nch 41.
“Ahaa wala sifahamu ni muda sana sijaiwasha”
“Waya wake upo wapi?”
“Huo hapo chini una ning’inia”
Sa Yoo akauchukua waya huo na kuuchomeka
kwenye soketi. Akawasha Tv hiyo, kwa bahati
nzuri ikawaka na haikuwa na tatizo la aina yoyote.
“Ina king’amuzi chake ndani kwa ndani, unaweza
kupata local chanel”
“Ahhha sawa”
Sa Yoo akaanza kutafuta chaneli zinazo patikana
kwenye tv hiyo, kwa bahati nzuri akapata chaneli
ya TBC1. Miziki inayo onekana kwenye Tv hiyo,
ikawafanya waburudike japo wote sio wapenzi wa
muziki ila wanaburudika kiaina. Phidaya akatoka
bafuni akiwa amejifunga taulo.
“Jamani nimeimisi nyumba yangu”
Phidaya alizungumza huku akijitupa kitandani.
Akalala chali huku akisikilizia ubaridi mkali wa AC
(Air condition) unavyo ipuliza ngozi yake.
“Breking News?”
Sa Yoo alizungumza huku akiongeza sauti ya Tv
hiyo. Wote macho wakayatolea kwenye Tv hiyo.
Wakamuona muandishi wa kike aliye jitambulisha
jina lake na kuzungumza alicho kizungumza.
“UTAWALA WA RAISI GODWIN UMEPINDULIWA, NA
SASA UTAWALA HUO UNAONGOZWA NA MKE WA
ZAMANI WA RAISI PRAYGOD MAKUYA ALIYEKUWA
RAISI ALIYE SHINDWA KWENYE UCHAGUZI MKUU
BI RAHAB PRAYGOD. TUUNGANE NA MUANDHISHI
WETU ALIYOPO IKULU KWA TAARIFA ZAIDI”
Wote ndani ya chumba wakabaki kimya huku
wakishangaa, hakuna aliye fahamu kitu kinacho
endelea kwa wakati huo. Swali walilo jiuliza ni
kwamba yupo wapi raisi Godwin. Wakamuona
Rahab aliye kaa kwenye meza iliyo jaa maiki za
waandhisha wa habari, huku yeye akiwa amevalia
mavazi ya kijeshi huku usoni mwake akiwa na
tabasamu pana.
“Ndugu zangu Watanzania. Nimatumaini yangu
mupo salama, japo wengi wenu muliweza kupatwa
na wasiwasi mkubwa juu ya mapinduzi haya yaliyo
weza kutokea. Ninamshukuru Mungu mapinduzi ya
serikali hii yamekwenda salama. Huku nikiwa ndio
kiongozi wa mapinduzi haya. Ninawahakikishia
wananchi wote wapenda amani na wapenda nchi
yetu kwamba, kuanzia sasa nchi hii ni nchi ya
amani na utulivu”
“Nipo tayari kuweza kusikiliza maoni ya wananchi
juu ya nani aweze kuongoza nchi hii. Mimi sio
mroho wa madaraka. Ninawatangazia rasmi
kwamba nchi kuanzia leo itaongozwa na jeshi hadi
pale atakapo patikana raisi ambaye mumemchagua
nyinyi kwa kura zetu”
“Pia ninawatangazia kwamba aliye kuwa ni mtawala
wa hi inchi, akatumia madaraka yake vibaya kwa
manufaa yake na familia yake hususasi mwanaye
wa kike, basi hadi ninapo zungumza sasa hatunao
kwenye huu ulimwengu. Nitaandaa utaratibu
ambao kila mwananchi atashiriki kupiga kura yake
kwa haraka iwezekanavyo ili kuweza kuhakikisha
kwamba nchi inapata kiongozi mahiri na hodari.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika,
asanteni waandishi wa habari”
Rahab alimaliza kuzungumza, na habari hiyo
ikaisha na miziki ikandelea. Kila mtu ndani ya
chumba hicho akawa kimya, hakuna aliye weza
uzungumza kitu chochote. Sa Yoo akashusha
pumzi huku akitabasamu.
“Sasa imekwisha”
Hata kabla hawajajibu chochote, wakastukia
kishindo kizito getini. Wote wakakurupuka, na
kushuka gorofani huko na kupita sebleni kwa kasi
na kutoka nje. Wakakuta gari moja nyeusi ikiwa
imesimama nyuma ya gari lao wlilo kuja nalo,
huku geti kubwa likiwa lienguka chini, inaonyesha
limegongwa na gari hiyo. Wote wakabaki kimya
huu wakilitazama gari hilo, hawakuweza kumuona
mtu aliyopo ndani ya gari hilo kutokana na vioo
vyote vya gari hilo nivyeusi.
Mlango wa dereva ukafunguliwa, ukatangulizwa
mguu wa kulia, kisha mtu huyo akatoka. Wote
hawakuamini walipo muona ni Eddy, akishuka
kwenye gari hilo akiwa katika sura yake ya asili.
Kwa haraka Phidaya akaanza kushuka kwenye
ngazi hizo, akamkimbili Eddy aliye simama
pembeni ya gari hilo akimtazama. Wakakumbatiana
kwa pamoja, huku wakipigana mabufu mfululizo.
Hakuna kati yao aliye weza kuzungumza zaidi ya
kumwagikwa na machozi tu. Sa Yoo na Shamsa
wakabaki wakitabasamu.
“Upo salama mke wangu?”
“Ndio honey”
“Matatizo yamekwisha mke wangu”
“Asante honeny”
Wakaachiana, Eddy akanyoosha mikono yake huku
kwa ishara akiwaita Sa Yoo na Shamsa ambao nao
walishuka kwenye gari hizo kwa kasi, na wote
wawili kwa pamoja wakamkumbatia Eddy kwa
nguvu. Furaha ikatawala kati yao, kila mmoja
alipatwa na furaha ambayo tangu azaliwe hajawahi
kuipata furaha hiyo. Phidaya naye akamalizia kwa
kuwakumbatia wote watatu kwa pamoja.
“Nawapenda sana, bila ninyi mimi sio kitu”
Eddy alizungumza. Wakaachiana kisha Eddy
akafungua mlango wa nyuma ya gari hilo.Wote
watatu wakastuka baada ya kuukuta mwili wa
Manka akiwa amelala kwenye siti hizo.
“Mungu wangu!!”
Phidaya alizungumza huku akijiziba mdomo kwa
kiganja, hakuamini, msichana mzuri kama Manka
anaweza kupoteza maisha kwa wakati kama huo.
Wakiwa wanaendelea kuutazama, simu iliyo
mfukoni mwa Manka ikaanza kuita, wote wakasita
kuitoa, ila Eddy akajikaza na kuingiza mkono wake
kwenye mfuko wa suruali ya Manka, akatoa simu
hiyo na kukuta namba mpya. Wakatazamana na
Eddy akaipokea na kuiweka sikioni.
“Manka ni kweli eti umekufa?”
Ilikuwa ni sauti ya madam Mery ambayo Eddy
aliweza kuitambua kwa haraka. Akashusha pumzi
kisha akazungumza.
“Manka amekufa”
“Ed…..d….e….d..y unach……o zaungu…..mza ni
kweli?”
Madam Mery alizungumza kwa kubabaika
akionyesha dhairi kwamba amesha patw na hisia
za kulia.
“Ndio mdam Mery na hapa nina mwili wake na
nipo nyumbani kwangu”
“Na…na….akuja”
Simu ikakatwa, Eddy akairudisha simu hiyo
mfukoni mwake, akiwa ana mawazo mengi,
hakujua ni nini anacho weza kufanya kwa wakati
huo juu ya mwili wa dada yake. Taratibu Eddy
akautoa mwili huo na kuubeba, akapandisha nao
ngazi na kuingia nao sebleni, akaulaza kwenye
kochi taratibu. Kwa haraka haraka ukiingia sebelni
hapo na ukiwa haujui ni kitu gani ambacho
kinaendelea unaweza kusema kwamba Manka
amelala tu na yupo hai. Haukupita muda mrefu
wakasikia mngurumo wa gari nje. Wakasikia hatua
za miguu zikianza kupanda kwenye ngazi hizo,
mlango ukafunguliwa kwa nguvu, akaingia madam
Mery ambaye nywele za kichwani mwake
zimechanguka changuka kwa kuchanganyikiwa.
Akaangaza macho yake huku na kule, yakatua
kwenye sofa alilo lazwa Manka huku pembeni ya
sofa hilo akiwa amekaa Eddy aliye jiinamia.
“Manka mwanangu vipi mama, mbona unalala
hivyo jamani”
Madam Mery alizungumza huku akiangua kilio
kizito. Akamkumbatia Manka huku akiendelea kulia
kwa uchungu. Hakuna ambaye aliweza
kuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kukaa
kimya, ila Eddy machozi yalizidi kumtiririka,
hakuona sababu ya Manka kuweza kupoteza
maisha kwenye siku kama ya leo. Alianza
kujilaumu moyoni mwake kwa kuona kwamba
kuvaa sura yake ya bandia kulipekea Manka
kuweza kumpenda pasipo kufahamu kwamba wao
ni ndugu.
“Ohooo Manka, tazama sasa mdogo wako amebaki
peke yake, unahisi haya maisha yatakuwa vipi
sasa?”
Madam Mery alizidi kulalamika huku akiwa analia
na mikono yake akiwa imemkumbatia Manka.
Masaa yakazidi kwenda na kukatika hadi ikafika
majira ya asubuhi. Sa Yoo akatoa wazo la Manka
kupelekwa katika chumba cha maiti ili kuhifadhiwa
na wao wafanye harakati za mazishi.
Hakuna ambaye aliweza kupinga wazo lake kwa
maana, endapo watazidi kukaa na mwili huo humo
ndani, utaharibika. Eddy na Shamsa wakaupeleka
mwili huo hospitali ya Muimbili na kuwaacha Sa
Yoo, Phidaya na madam Mery wakimfariji.
Wakafanikisha kuuhifadhi mwili huo. Wakaanza
kutafuta sehemu za majeneza, ambapo
wakamchongeshea jeneza zuri lenye rangu nyeupe
pamoja na gauni moja zuri jeupe. Wakalipeleka
hospitalini hapo, ambapo mwili wa Manka
ukaoshwa kwa mara nyingine na wahudumu wa
chumba hicho cha kuifadhia maiti, walipo maliza
wakamvisha Manka gauni hilo, kisha wakamuweka
kwenye jeneza. Ukimtazama kwa haraka unaweza
kusema Manka ataamka pale utakapo muita, ila
sivyo tayari amesha ondoka duniani.
Wakatafuta gari maalumu la kubebea amiti
wakaongozana nalo hadi nyumbani kwa Eddy
ambapo wakakuta watu ambao Sa Yoo aliweza
kuwatafuta, wakawa wamesha maliza kuchimba
kaburi na kulijengea, karibu kabisa na kaburi la
mama Eddy.
“Samahani tunaweza kupata mchungaji?”
Sa Yoo alimuuliza mmoja wa watu hao, walio
chimba kaburi hilo na kulijengea. Mtu huyo
akamjibu anaweza kupata mchungaji, akatoa simu
yake na kumpigia mchungaji wa kanisa lake analo
sali. Akamueleza kila kitu mchungaji huyo
hakuchukua muda mwingi sana, akafika katika
eneo hilo. Japo Manka ni mtu aliye kuwa
akiheshimika katika serikali ya baba yake, ila
mazishi yake yalihudhuria watu wachache sana,
kama mazishi ya raisi Praygod. Mchungaji
akafanya taratibu zote za mazishi na wakamzika
Manka, na watu hao wambao ni wataalamu sana
kwa kujengea makaburi, siku hiyo hiyo wakajengea
makaburi hayo na wakalipwa ujira wao na
kuondoka.
***
Viongozi na vijana wote wa kikosi cha D.F.E,
walipata pigo ambalo kila mmoja lilimgusa sana
kwenye maisha yake. Kufa kwa kiongozi na mmiliki
wa kikosi hicho chenye viongozi wengi kutoka nchi
mbalimbali duniani, kuliashiria hali ya kikosi hicho
kwenda kuanguka. John naye alihisi
kuchanganyikiwa baada ya kutuma vijana wake
wengien kwenda kumfwatilia kijana wake na kukuta
amekufa kwa kupigwa risasi na kazi ambayo
alimtuma iliwezza kushindwa.
Mikakati na mipango ya kuuiba mwili wa mzee
Godwin ndani ya mochwari ya hospitali ya
Muimbili ikaanza, hadi inatimu saa sita mchana
tayari mwili wa mzee Godwin ukawa umesha ibwa
ndani ya hospitali hiyo na moja kwa moja
ukasafirishwa kwa ndege hadi katika makao makuu
ya kikosi hicho. Kisiwa kizima ambacho ndio kina
kambi ya D.F.E kikagubikwa na majonzi.
Wakaandaa mpango mzima wa mazishi wa
kiongozi wao. Mazishi hayo yakaudhuriwa na
viongozi wengi kwa siri, sana pasipo wengine nchi
zao kuweza kutambua.
Mazishi ya mzee Godwin yakafanyika kwa mfumo
wa kijeshi. Mwili wa mzee Godwin ukachomwa
sindano ya kukaushwa ambayo inaweza kufanya
kazi katika mwili huo zaidi ya hata miaka kumi.
Wakautengenezea jeneza la vioo na kuihifadhi
mwili huo kwenye moja chunba maalumu,
ambacho kinalindwa kwa masaa ishirini na nne.
“Ni lazima tulipize kisasi juu ya kifo cha mkuu
wetu”
John alizungumza kwenye kikao hicho na
kuwafanya viongozi wezake ndani ya ukumbi huo
kukubaliana na wazo lake.
***
Rahab, Anna, Agnes na Fetty nao wakajumuika na
vionozi wengine serikalini kufanya mazishi ya
kiongozi wao Halima, ambayo yalifanyika katika
makaburi ya Sinza. Mazishi hayo pia yaliudhuriwa
na wananchi wengi ambao wamebeba mabango
yaliyo andikwa meseji tofauti tofauti. Huku wengine
wakisemea Halima, umekufwa kwa ajili ya
watanzania wote. Wengine waliandika na kusema
kwamba Halima ni mama wa taifa. Kila mmoja
aliweza kuguswa na kifo chake.
Mazishi yakamalizika, siku hiyo ikapita, siku iliyo
fuata kwa kupitia vyombo vya habari Rahab
akawatangazia wananchi jinsi ya kufanya maamzi
ya kumchagua ni nani wanaye ona anaweza
kuchukua kiti cha mzee Godiwn.
Japo Rahab hakujiweka kwenye kinyang’anyiro
hicho zaidi ya kuwataja viongozi ambao walikuwa
madarakani, ila wananchi karibia aslimia tisini na
sita wakamchagua Rahab na kumuhitaji awe raisi
wa kwanza mwanamke nchini Tanzania.
“Hii ni nafasi ya pekee watanzani walio kupatia,
waonyeshe kwamba wanawake tunaweza na sisi ni
zaidi ya wanaume wao”
Fetty alimuabia Rahab, ambaye hakuwa na
kipingamizi. Hapakuwa na mwananchi ambaye
alimkataa Rahab, kwa kura hizo za mauoni Rahab
akachukua kiti cha uraisi. Siku ya kuapishwa
ikapangwa, katika uwanja wa taifa wa mpira
wananchi wengi wa kila rika waliweza kuhudhuria
eneo hilo, ambapo waliweza kushuhudia jaji mkuu
akimuapisha Rahab Praygod kuwa ndio raisi mpya
wa Tanzania. Shangwe nderemo zilirindima nchi
nzima, natumaini ya mabadiliko kwa Watanzania,
yakaanza kufufuka tena.
***
“Jamani mimi ninaomba niondoke na kurudi kwetu
Japani”
Sa Yoo alizungumza huku akitazama jinsi Rahab
akiapishwa kupitia tv kubwa iliyopo hapo sebleni.
Eddy na Phidaya wote wakamgeukia na
kumtazama.
“Sa Yoo kwa nini usibaki hapa?”
“Nimepakumbuka nyumbani nahitaji kwenda
kuwaona ndugu zangu, jamaa zangu na watu
wengine”
“Kusema kweli kwa mimi kama mimi siwezi
kukuzuia, ila kikubwa nakushukuru kwa msaada
wako wote ulio weza kunipatia”
“Na mimi nitamsindikiza”
Shamsa alizungumza, huku akishuka kwenye ngazi
za gorofa
“Ehee na wewe unataka kutukimbia?”
“Nitarudi, ila ninamsindikiza rafiki yangu
nitakwenda kukaa naye huko siku mbili tatu kisha
ninarudi”
“Mimi sina maneno”
Eddy alizungumza huku akitabasamu, kutokana
baba amekubali basi Phidaya hakuwa na namna
yoyote ya kuwazuia mabinti hao walio ishi nao
kwenye shida na raha. Siku iliyo fuata Shamsa na
Sa Yoo wakaanza mikakati ya kutafuta hati za
kusafiria, kwa kutumia pesa ya kuwahongo watu
wanao shuhulika na utengenezaji wa hati za
kusafiria, kazi kwao ikawa ni rahisi. Siku hiyo hiyo
wakapata hati za kusafiria na kurudi nyumbani.
Walishangazwa sana kukuta gari nyingi nyumbani
kwa Eddy huku kukiwa na walinzi wengi wanao
onekana kumlinda raisi.
“Ina maana Rahab yupo hapa?”
“Nahisi”
Walinzi baada ya kuwahoji maswali wakawaruhusu
kuingia ndani. Wakamkuta Rahab akiwa amekaa
sebleni pamoja na Eddy. Wakamsalimia, kisha wao
wakamuulizia ni wapi Phiday alipo, wakaelezwa
yupo jikoni na wao wakaenda eneo hilo na
kuwaacha waendelee na mazungumzo yao.
“Eddy bila ya wewe mimi siwezi kuiongoza hii nchi
peke yangu”
“Sasa Rahab unataka mimi nifanye nini?”
“Nataka uwe msaidizi wangu, nataka nikuteue kuwa
makamu wa raisi”
Eddy akaka kimya na kushusha pumzi. Akafikiria
ombi hilo kwa sekunde kadhaa kisha akanyanyua
sura yake na kumtazama Rahab.
“Nimekubaliana na ombi lako muheshimiwa raisi”
Eddy alizungumza huku akitabasamu.
Wakanyanyuka kwa pamoja na kupeana mikono,
Rahab akaonekana kuwa na furaha sana kwa Eddy
kukubali.
“Ila vipi kidonda chako?”
“Kina endelea kukauka taratibu”
“Basi jiandae kesho uweze kufika ikulu nianze
kukutangaza”
“Sawa”
Wakapata chakula cha mchana kwa pamoja kisha
Rahab akaondoka na kumuacha Eddy akiwa na
furaha sana, pamoja na familia yake kwa ujumla.
Eddy akawaelezea Rahab, Sa Yoo na Shamsa ombi
alilo elezwa na Rahab, wote wakafurahi na
kumuomba aweze kuhakikisha kwamba anafanya
kazi yake kwa juhudi na kwa manufaa ya
watanzania wote kwa maana nafasi hiyo waliitafuta
kwa muda mrefu.
“Madam Mery yupo wapi?”
Sa Yoo aliuliza huku akimtazama Phidaya usoni.
“Amesha ondoka na kuelekea Mwanza nyumbani
kwake”
“Hata kutuaga?”
“Nyinyi si muliondoka na kumuacha amelala”
“Sisi tutaondoka kesho mchana saa saba kuelekea
Japani, tumesha weka booking ya ndege”
“Ahaa basi, kila mmoja nitampatia kiasi cha dola
milioni tano tano”
“Kweli Eddy?”
“Ndio”
“Wee Sa Yoo sasa hivi usimuite Eddy, muite
makamu wa raisi Eddy”
Phiday alizungumza kwa utani na wote wakacheka.
Eddy akaingia kwenye chumba chake cha siri,
akatoa kiasi kikubwa cha pesa ambacho ni sawa
na milioni kumi. Sa Yoo na Shamsa akawapatia
kila mtu kiasi sawa, kisha wakazipakiza pesa hizo
kwenye magari lao na kwenda nazo benki. Shamsa
akaziingiza kwenye akaunti yake na Sa Yoo
akaiziingiza kwenye akaunti yake ya benki ya
Japani yenye tawi lake nchini Tanzania. Wakarudi
nyumbani na kufanya maandalizi ya kila kitu.
Siku iliyo fwata alfajiri na mapema gari kutoka
ikuku zipatazo nne zikafika nyumani kwa Eddy.
Kiongozi wa msafara huo akamtaarifu Eddy juu ya
ujio wao hapo ni kuwachukua na kuwapeleka Ikulu,
ambapo shamra shamra za kumuapisha makamu
wa raisi zimeanza.
Eddy na Phidaya wakajiandaa vizuri sana, Eddy
akavalia suti nyeusi na shati jeupe pamoja na tai
ndogo nyeusi, huku Phidaya akivalia gauni refu
jeupe lenye mstari mmoja mkubwa kiunoni wenye
rangi nyeusi. Huku miguuni akiwa amevalia viatu
vyeusi ambavyo ni virefu kiasi. Wakaagana Sa Yoo
na Shamsa, kwa maana hawato weza kuhudhuria
sherehe hizo za kuapishwa kwa Eddy kutokana na
ndege yao kuondoka saa saba mchana.
Eddy na Phidaya wakaingia kwenye gari hizo na
kuondoka. Sa Yoo na Shamsa nao wakaingiza
mabegi yao kwenye gari lao.
“Hiyo laptop si uingize chumbani kwa Eddy?”
“Yaa ndio nataka niipeleke”
Shamsa akaipeleka laptop ya Eddy ndani kwake,
kisha akatoka, wakaondoka na Sa Yoo. Wakapitia
kwenye maduka ya simu wakanunua simu nzuri,
na kuelekea uwanja wa ndege. Kutokana muda wa
kuripoti kwa abiria uwanjani hapo ni saa moja
kabla ya ndege kuondoka, ikawalazimu kuti sheria
hiyo.
“Hapa si kuna wifi?”
Sa Yoo alimuuliza Shamsa, ambaye alimjibu kwa
kutingisha kichwa. Sa Yoo akaanza kuperuzi
kwenye mtandano kwa kutumia Internet iliyopo
hapo uwanja wa ndege. Muda wa andege yao
kuondoka, ukawadia. Wao nao waka ni miongoni
mwa abiria wlio ingia kwenye ndege hiyo ya
shirika la ndege la Air Ways. Wakaka kwenye siti
moja, huku Shamsa akiwa ameweka earphone zake
masikioni.
Abiria wakatangaziwa kufunga mikanda yao, ndege
inaondoka. Shamsa na Sa Yoo wakafanya hivyo,
taratibu ndege hiyo ikaanza kuondoka eneo hilo la
uwanje wa Mwalimu J. K Nyerere. Ndani ya dakika
kadhaa tayari ikawa imesha iacha ardhi ya
Tanzania.
“Shamsa muone Eddy”
Sa Yoo alizungumza na kuonyesha video inayo
onekana kwenye simu yake, mbayo hayo ni
matangazo ya moja kwa moja yanayo ruka kutoka
katika viwanja vya Ikulu. Shamsa akamtazama
Eddy aliye shika biblia akiapa juu ya kulitumikia
taifa la Tanzania kwa haki na uadilifu.
“Ohooo mwangu, tazama ulivyo pata baba mzuri
na anaye jituma. Mungu akubariki nikuzae kwa
amani?”
Shamsa alizungumza huku akilishika shika tumbo
lake kwa kiganja cha kulia.
“I….iii ina maana Shamsa una mimba ya Eddy?”
Sa Yoo alizungumza huku macho yakimtoa
“Ndio, nina mimba yake. Na wewe ndio mtu wa
kwanza kukuambia hili. Na ninapo kwenda sinto
rudi tena nchini Tanzania”
“Kwa nini sasa?”
“Endapo Phidaya atagundua kwamba nimebeba
mimba ya Eddy, basi visa na mikasa mipya
inaweza kuibuka, jambo ambalo silitaki kuliona
linatokea katika maisha ya mwangu wala katika
maisha ya mwanangu. Nitamlea mwangu kwa
kadtr ya uwezo wangu na atapata malezi bora.
Ninakuomba Sa Yoo unitunzie siri hii”
“Usijali rafiki yangu siwezi kuitoa siri hii na sinto
fungua kinywa changu kuweza kumueleza yoyote
juu ya hii siri”
Sa Yoo alizungumza na wote wakashikana mikono,
na safari ikazidi kusonga wakielekea nchini Japani,
wote wakiwa na furaha na amani katika maisha
yao kwani kila kitu cha ubaya kimesha fika tamati.
MWISHO
 
Back
Top Bottom