Sore nipples

Aunty Lao

JF-Expert Member
Jul 7, 2008
214
17
Za leo ndugu wapendwa, jamani na shoga angu ametoka kujifungua j,pili hii iliyopita na ametokwa na michubuko kwenye chuchu zake mpaka anashindwa kunyonyesha mtoto kwa maumivu anayoyapata. Dr. mwenye kujua hili naomba anisaidie please.
 
anatakiwa anapomnyonyesha mtoto ahakikishe chuchu yote imeingia ndani ya mdomo, ma awe anamshikia nyonyo hii itapunguza maumivu na kuchubuka. Ila sifahamu kama kuna dawa ya kutumia kuondoa michubuko wakati ananyonyesha, labda wenye utaalam watakusaidia.
 
Siyo kwamba chuchu hizo zinakauka tu sana?!
(btw, mimi siyo daktari wa chuchu, ila nauliza tu kutokana na maelezo uliyotoa, ahsante)
 
Sio kwamba zimekauka, zina michubuko ya vidonda na zimeturn reddish.
 
Hadi zinakuwa nyekundu?...daaah, kwa kweli hilo tatizo laweza kuwa kubwa... ni bora tusubirie madaktari. Hata hivyo namtakia mgonjwa ahueni.
 
Siyo kwamba chuchu hizo zinakauka tu sana?!
(btw, mimi siyo daktari wa chuchu, ila nauliza tu kutokana na maelezo uliyotoa, ahsante)

Nimewahi kusikia Vaseline huwa inasaidia, lakini akiwa anataka kunyonyesha inabidi ayasafishe matiti ili kuondoa hiyo Vaseline kabla ya kumnyonyesha mtoto.
 
Kwanza nakupongeza kwa kumsapoti rafiki yako kwa hili, hii niliipata wanangu walipokuwa wachanga ,inasababisha maumivu makali wakati wa kunyonyesha kiasi kwamba watoto walikuwa wakianza wakitaka kunyonya mie mwili una anza kutetemeka nikifiria maumivu ntayopata

Mara nyingi tatizo ni kwamba mtoto anapopokea ziwa wakati wa kunyonya anashika chuchu tu…inatakiwa anyonye chuchu PAMOJA NA part kubwa ya sehemu nyeusi inayozunguka chuchu (areola). Ili kufanikisha hilo mtoto anapopokea breast inabidi afungue mdomo wake really wide. Baadhi ya watoto wanahitaji msaada ktk hilo..lactation consultant mmoja alinipa solution ambayo ilinisaidia sana kumaliza tatizo haraka…

mtoto anapotaka kunyonya asimpe ziwa mara moja ila amguse guse kwanza na chuchu kwenye mdomo wa juu…mtoto atafungua mdomo zaidi ili kupata chuchu…atakapo fungua mdomo wake really wide amshike nyuma ya shingo/kichwa na kumsogeza kwenye ziwa a bit fast but gently and firmly..yaani mtoto afuate ziwa sio mama ampelekee mtoto ziwa mdomoni…wakati huo huo mkono mwingine wa mama ushike ziwa yaani kama analikamua hivi (breast sandwich) to make the areola longer and narrower and easier for baby to take into his mouth

maziwa ya mama pia yanasaidia sana ku soothe sore nipples, akachukue kidogo na kupaka kwenye chuchu baada ya kunyonyesha. Tatizo likiendelea aende hospitali kucheck couses nyinginezo kama candida infections etc

pia nenda kwenye discussion furum ya www.lalechelegue.net pale kuna kina mama wanaonyonyesha na breastfeeding experts toka kila kona ya dunia, nina uhakika utapata mchango mwingi tu toka kwa wenye experience kama hii

mwisho mwambie rafiki yako asiache kunyonyesha, hili tatizo litaisha tu na mwanae atakuwa feeding expert..
 
Jamani asanteni sana kwa maoni yenu nimefurahi sana. Yamenipa mwanga mzuri na nitakwenda kumuelimisha na shoga pia.
 
Helloz wandugu wapendwa,

Naendelea na hihi mada yangu, huyu bibi kapona tayari ila yaliomkuta baada kujifungua ni bilaa. Alitoboka utumbo kwa kunywa dawa fulani alizopewa kama antibiotic ikiwemo diclofenac, Sasa ilibidi apate operation wazibe tundu kwenye utumbo. Ila mpaka sasa hivi anaonekana bado hana hamu ya kula ambayo imemfanya maziwa yake yakauke kwa lishe ndogo. Nini sasa anaweza kutumia ili maziwa yaweze kuwastimulated tena! Pili kitovu cha mtoto hukauka baada ya siku ngapi! maana cha mwanae chaonekana kinyevunyevu bado, Je kuna something wrong hapo nako? asanteni tena kwa msaada wenu.
 
Anywe uji mwepesi,maziwa,supu na mtori,km bado atafute maziwa ya kopo ingawa ya mama ni nora zai,kuhusu kitovu ni hadi siku 40 wengine na kidogo ila anapoenda clinic awaoneshe hicho kitovu watajua chakufanya wenyewe kwani watoto wengine vinachomwa nasikia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom