Sophia Simba: Sijawahi shutumu CHADEMA kupata misaada kutoka nje

Kama Kiongozi wa Chadema namsikitikia zaidi kikwete aliyemchagua kuliko Sofia Simba mwenyewe ambaye kwa historia ya uropokaji wake wala simshangai kabisa. Ndiyvo alivyo.
 
Kama umemsikia wewe ni witness, sio evidence. Tunataka evidence.

Na iwe video clip, maana mmesema kasemea mbele ya camera.

Na mmesema amesema mara tatu, kwa hiyo mtakuwa na video clip tatu, weka evidence ya video clip moja tu!

Wewe komaa na hizo videoclips zako sisi tunaendelea........
 
Kama umemsikia wewe ni witness, sio evidence. Tunataka evidence.

Na iwe video clip, maana mmesema kasemea mbele ya camera.

Na mmesema amesema mara tatu, kwa hiyo mtakuwa na video clip tatu, weka evidence ya video clip moja tu!

She just used this philosophy wrongly: If you have any news, do not say it. If you have to say it do not say it in public. If you have to say it in public, do not write it. If you have to write it, do not sign it. If you have to sign it, then be ready for the consequences.
U know she said it in public without writing it knowing she can just deny it; but she forgot that electronic media is retrievable.

As I said, electronic media is retrievable. The only hope Sophia and his people (who are following up this discussion) have is that the video clip won't be there. And you can see how they are pushing, they want to be sure of what to do next. Whoever has it, I suggest you keep it and send it to CDM straight. Do not post it here!
 
hivi hicho chama kina viongozi?

aibu aibu aibu au wameshafuta ushahidi/video clips kule TBC?
 
Mi nshasema watu ni waoga sana, wanaogopa kusema ukweli wakidhani misaada itasimamishwa. Lakini mimi nilishaweka wazi. Baadhi ya watu na vyombo vya habari vinapotosha umma kuhusu hili swala. Swala hapa si nani anamfadhili nani bali ufadhili kwaajili ya kufanya nchi ionekane haitawaliki. Ukweli ni huu Balozi wa Denmark hapa nchini alianza harakati zake kule Zanzibar kupitia CUF akashindwa ingawa alileta chuki na kusababisha maafa makubwa tu sasa anataka kuleta hilo bara kwa kupitia CHADEMA. na hapa wanazunguka kama ilivyo marekani inavyotumia USAIDS kufanya kazi za CIA Denmark wanatumia shirika la actionaid na Global Platform Tanzania. Kuna kipindi nilisema nadhani hata Jamii Forum wanajua, sasa wameandaa makongamano ambayo ni mazuri na ninayakubali kama yalivyo maandamano yanayofanywa na CHADEMA ingawa tu maazimio ndiyo ninamashaka nayo. Tarehe 31/03/2011 kutakua na discussion on social media as a political tool Islam na Maxence wa jamii forum watasilisha mada on two biggest corruption scandals nitahudhuria ili kuona mdenish anatoa mwonngozo gani kupitia mawakala wao.

Mabulangati
Can you substantiate madai yako kuwa Action Aid na Global Platform zinatumika kama ilivyo kwa USAID inavyotumia CIA?
 
She just used this philosophy wrongly: If you have any news, do not say it. If you have to say it do not say it in public. If you have to say it in public, do not write it. If you have to write it, do not sign it. If you have to sign it, then be ready for the consequences.
U know she said it in public without writing it knowing she can just deny it; but she forgot that electronic media is retrievable.
She just used this philosophy wrongly: If you have any news, do not say it. If you have to say it do not say it in public. If you have to say it in public, do not write it. If you have to write it, do not sign it. If you have to sign it, then be ready for the consequences.
U know she said it in public without writing it knowing she can just deny it; but she forgot that electronic media is retrievable
 
For the very reason you are looking for
"For the very reason you are looking for it for."

Kifupi, evidence kwamba alisema hakuna!

Ndio maana sayansi inafundishwa shule kwa lazima toka darasa la tatu. Kwamba usiamini amini vitu bila ushahidi. Kizazi cha Babu wa Liliondo!
 
"For the very reason you are looking for it for."

Kifupi, evidence kwamba alisema hakuna!

Ndio maana sayansi inafundishwa shule kwa lazima toka darasa la tatu. Kwamba usiamini amini vitu bila ushahidi. Kizazi cha Babu wa Liliondo!

Likifika mahakamani; uliza evidence utapewa. Hao EU waliomjia juu unafikiri hawana. Wewe na Sophia wako mtalinywa hilo.
Hoja nyingine: Kama hakusema mbona jasho linawatoka?
 
Is that how you 'operate' huh? evidence kwani tuko mahakamani?
Absolutely, that's how I operate. That's what I benefited from my standard III science teacher, who said not to believe in any allegations without incontrovertible evidence.

National news involving foreign envoys, cabinet minister accuses external enablers for funding the opposition and stoking chaos, CHADEMA alleges, claiming she said it on TV, she denies it, he said, she said. Well, show the damn video! Simple as that.
 
Sijui kwa nini namuona huyu mama kama amekaa zaidi kijaluba kuliko mwana siasa. Anakana nini wakati mkanda upo TBC1?
 
hee we vp? Mbona undng'ang'ania mkanda uwekwe hpa. Subr akpndshw kzmban ndo udai mkanda. Hakn ambae hakmckia Sophia. Alyatamka tbc1, kwnye kpnd cha Jambo Tanzania tn cku hyo alkuw na Japhar! Aliambiwa unawaambia nn wanawake kuhusiana na cku ya wnawake dunian? Akaanza kuropoka huo ujnga wke bdla ya kujb alchoulzw. Mi mwnyewe nlbak namshangaa cz aljb k2 acchoulzwa. Lbda tbc1 waufche huo mkanda vngnevyo kaz anayo!
Ulete basi huo mkanda!

Mkanda si upo wa TBC? Weka tuone!
 
Absolutely, that's how I operate. That's what I benefited from my standard III science teacher, who said not to believe in any allegations without incontrovertible evidence.

National news involving foreign envoys, cabinet minister accuses external enablers for funding the opposition and stoking chaos, CHADEMA alleges, claiming she said it on TV, she denies it, he said, she said. Well, show the damn video! Simple as that.

Even Makamba taught science for STD III...no wonder you are the end result...keep on brooding
 
Hajakanusha hili.............mpaka leo:lol::lol::lol:
Saturday, November 7, 2009

Malecela ashauri Waziri Sophia Simba apimwe akili Mirembe





WAZIRI mkuu wa zamani, John Malecela jana alimshukia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba akisema kuwa tuhuma alizozitoa dhidi yake zinatokana na waziri huyo kuwa mgonjwa wa akili, huku mkewe ana Kilango, akimshangaa kwa kukalia tuhuma hizo kwa kipindi kirefu.Mbali na wanandoa hao, mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi naye alipuuza tuhuma alizorushiwa na Waziri Simba akisema kuwa hawezi kubishana na mjinga.


Malecela, Kilango na Mengi ni miongoni mwa watu kadhaa walioshambuliwa na Waziri Simba Jumatano, akiwatuhumu wanandoa hao kuwa walichukua fedha za kifisadi wakati walipofanya harusi yao mjini Dodoma na katika kampeni za urais za mwaka 2005, huku akimtuhumu Mengi kuwa anatumia vyombo vyake vya habari kuichafua CCM na serikali yake kwa maslahi binafsi.

Wote watatu hawakuingia ndani kukanusha madai hayo ya Simba wala kutoa ufafanuzi, na badala yake Mengi na Malecela walimrushia maneno makali wakimwita kuwa ni mgonjwa wa akili, asiye na maadili, mropokaji na ambaye si msafi huku Kilango akisema kuwa bado anatafakari.

Malecela, ambaye alikuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais (1990 hadi 1994), alidai kuwa Simba ni mgonjwa wa kichwa na akili hivyo anapaswa kupelekwa Hospitali ya Mirembe kabla ya kurudi Dar es Salaam baada ya bunge kuisha.

Hospitali ya Mirembe iliyo mjini Dodoma hujishughulisha zaidi na tiba ya watu wenye matatizo ya akili.

Kama ilivyokuwa kwa Kilango ambaye alidai juzi kuwa mashambulizi dhidi yake yanatokana na mumewe, Malecela naye jana alidai kushambuliwa kwake ni kutokana na mkewe Kilango kwamba ameona azungumze kwa kifupi kuhusu hali halisi ya akili ya Simba.

"Najua chanzo kikubwa ni mama (Kilango), yeye leo ametoa taarifa yake, lakini na mimi ninalo moja dogo la kusema kijana ambalo ni ushauri kwa Waziri Simba," alisema Malecela.

"Simba ni mgonjwa, ana matatizo ya akili kichwani, namshauri apelekwe au aende Mirembe akapimwe akili na kupata matibabu kabla hajarudi Dares Salaam."


Mzee Malecela ambaye ni mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, alisema Simba atafanya kosa kama atarudi Dar es Salaam bila kwenda Mirembe kupima akili na kupata matibabu.

"Asirudi Dar es Salaam bila kupita Mirembe kupima akili, kwa maana atakuwa amepoteza fursa ya kujua matatizo aliyonayo kichwani kwake," alisisitiza.


Kwa sasa Waziri Simba yuko Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge na alitoa kauli za kumshambulia Malecela, Kilango, Mengi na Mwakyembe kwenye mikutano inayoendelea baina ya wabunge wa CCM na Kamati ya Mwinyi ya kutafuta chanzo cha kutoelewana ndani ya chama hicho.

Malecela, ambaye aliwahi kuteuliwa kuwa mmoja wa watu sita wenye busara katika nchi za Umoja wa Madola mwaka 1985, hakueleza kama ana ushahidi wa madai yake.


Hata hivyo, Simba aliwahi kuugua akiwa Afrika Kusini na baadaye Hindul Mandal akiwa anasumbuliwa na kizunguzungu na kutapika, ugonjwa ambao waziri huyo aliwakariri madaktari wakisema utapona taratibu.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo tuhuma za yeye kufadhiliwa na Patel katika harusi yake na kupewa kiasi hicho cha fedha Sh200 milioni za kampeni za Urais mwaka 2005, Malecela alisema tuhuma hizo zimetolewa na mgonjwa.

Naye mbunge wa Same Mashariki, Kilango alionyesha kushangazwa na tuhuma hizo na kumshangaa waziri huyo kukalia tuhuma nzito alizozitoa kwa muda mrefu bila kuzifikisha kwenye vyombo vya sheria.


Kilango na Malecela walituhumiwa na Simba Jumatano kuwa nao walichukua fedha za ufisadi, akidai kuwa harusi yao ilifadhiliwa na Jeetu Patel, ambaye ni mtuhumiwa wa ufisadi na hali kadhalika kampeni za urais za Malecela za mwaka 2005.

Katika tuhuma zake, Waziri Simba alidai kuwa Kilango ni mnafiki na si msafi kiasi cha kuwanyooshea wenzake vidole na kwamba kelele zake zote zimetokana na kukosa kuwa mke wa rais baada ya Malecela kuenguliwa mapema na CCM kwenye mchakato wa kumpaya mgombea wake.

Lakini jana, Kilango alisema hatakatishwa tamaa na tuhuma hizo nzito, ambazo alisema bado anazitafakari, ili kubaini kiini chake na sababu za kutolewa sasa katika kipindi ambacho vita dhidi ya ufisadi imepamba moto.


Kilango, ambaye mwaka huu alitunukiwa Tuzo ya Mwanamke Jasiri na serikali ya Marekani, alimshangaa Simba kukaa kimya na tuhuma hizo tangu 2005 wakati vyombo vya dola vipo.


"Kama Mheshimiwa Simba alikuwa na ushahidi wa tuhuma nzito kama hizo tangu mwaka 2005 kama ambavyo anataka Watanzania waamini, bado haiingii akilini ni kitu gani kilichomfanya asitoe taarifa hizo katika vyombo vya dola,? alihoji Kilango.

Kilango alifafanua kwamba Simba ni waziri mwenye dhamana ya utawala bora ambaye ana vyombo vya uchunguzi chini yake kama Takukuru, lakini akashangaa kutovitumia.?Ni imani yangu kwamba, mheshimiwa Simba ambaye ni waziri katika Ofisi ya Rais atapimwa na wananchi kama malumbano anayoyaanzisha sasa yana chembe ya ukweli kiasi gani au ni kujaribu kuwahamisha Watanzania katika vita nzito dhidi ya ufisadi,? alisema.


Katika taarifa yake ya maandishi, Kilango alisema asingependa kuingia katika malumbano na waziri huyo kwa kuwa itawapa taabu Watanzania kutofautisha pumba na mchele.Kauli ya Simba inaonekana kuibua mjadala mpya katika vita dhidi ya ufisadi katika kipindi hiki ambacho kimetawaliwa na malumbano makali baina ya wabunge wanaojinadi kuwa ni makamanda wa vita ya ufisadi na wale wanaodai kuchukulia vita hiyo kuwa ni ya kukichafua chama na serikali.


Malumbano hayo yamefikia kipindi ambacho wabunge wenyewe wameanza kuhoji maamuzi yao ya kukubaliana na ripoti ya kamati teule iliyochunguza kashfa ya mchakato wa utoaji wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development na kutaka uchunguzi mpya ufanyike ukihusisha tume huru.


Tayari mawaziri wawili, Dk Makongoro Mahanga na Simba wamejitokeza kumtetea Edward Lowassa ambaye aliachia wadhifa wake wa waziri mkuu kutokana na kutakiwa na ripoti hiyo kufanya maamuzi kwa kutumia busara yake kutokana na kashfa hiyo.Hata mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge, ambaye alijiuzulu uwaziri baada ya kutajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada, naye amejikuta akipata watetezi, akiwemo Waziri Simba ambaye alielezea kuwa uchunguzi umeonyesha kuwa mwanasheria huyo mkuu wa zamani wa serikali hana hatia.
 
Back
Top Bottom