Sophia Simba: Siasa na tendo la ndoa

sikuona sababu ya kutumia maneno ya kumvunjia heshima mama sofia simba . Mwandishi angeweza kutumia njia nyingine kufikisha ujumbe kuliko kumzalilisha mama wawatu . sijui kama wenzangu mmefurahishwa na hiyo habari lakini kwangu umeniuzunisha saana kwa sababu naona hatua iliyofikiwa na baadhi ya waandishi ni mbaya yakukosa maadili na kutotumia au kukiuka taaluma. am so disappointed
 
Simba kama Waziri wa serikali ni mteule na mwakilishi wa rais; hakuomba kazi ile. Kama ana mapungufu, basi hayo ni mapungufu ya rais pia, ambaye alimwona Simba kuwa ni bora sana kufanya kazi nyeti hiyo kati ya watanzania takribani millioni arobain.
 
Mwandishi kaandika vizuri kwenye kolamu zote nne, ila nadhani ile paragraph ya mwisho ameimaliza vibaya na inaweza kumletea matatizo:

(a) Kwa ku-generalize kuwa nafasi zote za uwaziri zimekwisha rahisishwa, anakuwa anahusiha mawaziri wote wa serikali. Itategemea jinsi atakavyotetea statement hiyo ila mawaziri wote wanaweza kudai kawatukana. Rais hawezi kulalamika hapa kwa sababu ni wazi ameshindwa kumwajibisha Sofia kutokana na statement aliyotoa kuhusu ngono. Kitakachomsaidia mwandishi hapa ni endapo tu inajulikana kuwa mawaziri wana wawajibu wa kumkemea waziri mwenzo kwenye vikao vya kabineti anapokosea mbele ya jamii , lakini hawakufanya hivyo kwa Sofia.

(b) Kwa ku-conclude kuwa ngono ndiyo iliyompa Sofia uwaziri ni jambo zito ambalo anaweza kutakiwa kutoa proof. Kwa hilo anawachanganya Rais, Sofia, na waziri Mkuu, kwa hiyo wote wakilalaminka na kumtaka atoe proof kama kweli Sofia alipewa uwaziri kutokana na ngono, mwandishi anaweza kujikuta katika wakati mgumu.
 
Mkuu hii kali,haya magazeti sasa hivi yatakuwa kama ya ulaya,hawaogopi kulipa mijihela?
Hapa miye NO COMENTS
 
sikuona sababu ya kutumia maneno ya kumvunjia heshima mama sofia simba . Mwandishi angeweza kutumia njia nyingine kufikisha ujumbe kuliko kumzalilisha mama wawatu . sijui kama wenzangu mmefurahishwa na hiyo habari lakini kwangu umeniuzunisha saana kwa sababu naona hatua iliyofikiwa na baadhi ya waandishi ni mbaya yakukosa maadili na kutotumia au kukiuka taaluma. am so disappointed
Ndugu... Maadili ni nini? Sofia ana maadili? Mwandishi hajamdhalilisha (na sio kumzalilisha!!!!!) bali amempa ukweli. Kama umekuwa-disappointed wewe na roho yako.... hayo hayatuhusu.....
 
Katika system inayojali collective responsibility, maneno haya yamesemwa na chama si mtu, na kama chama hakikubaliani nayo kitamchukulia hatua ofisa wake na kumtaka ayakane hadharani.

Kwa kuwa hatujasikia kukanwa kwa maneno haya, watu tunaoelewa "collective responsibility" tunayachukulia maneno haya yasiyo ustaarabu kwamba ni maneno rasmi ya CCM, si ya Sophia Simba tu.

Vipi na wakinababa wa CCM wenye wake wasio CCM, nao wawabyime unyumba? Katika vitu vyoote ambavyo mtu anaweza kuvitumia ili kutoa a political statement huyu mama kaona unyumba ndiyo cha kwanza? Kinababa wenye ukame wakija kumvamia yeye kwa sababu kawaambia wake zao wasiwape unyumba atasemaje?

Hivi Sophia Simba anaona kinamama ni watu wa kutakiwa unyumba tu? Hajaona kwamba kinamama wanataka unyumba nao?

Halafu kinamama wanalalamikia mfumodume, wakati wanawake kama hawa wanaendeleza mfumodume kuliko mwanamme yeyote.

Vikaragosi vichwapanzi kama hawa walitakiwa waende viwanja vya Ilala pale kuna bars za kuimba taarabu, uongozi wa nchi shughuli pevu.
 
Tatizo la hii nchi yetu ni kupeana madaraka kama shukurani na watu hawaangalii ufanisi na uelewa wa mtu, sophia simba hakufaa hata kupewa uwenyekiti wa mtaa, ni mtu mlopokaji, asiyeweza ku-reason mambo, ni mkurupukaji, angalia anapewa wizara ya utawala bora, kuwashauri wanawake wawanyime unyumba waume zao kisa si wanachama wa CCM hilo ni jambo la kuongea mbele ya jamii? unafungua domo na kuongea upuuzi kama huo? mimi naamini huyu SOPHIA SIMBA, akili zake ziko kwenye uti wa mgongo tu, kichwa hakina kitu, empty box, mtu makini hawezi ongea utumbo huo.
 
Makala hiyo nimeisoma na ni makala safi sana. Mwandishi kayaeleza yote yale kulingana na kauli za Sophia mwenyewe. Wa kuhukumiwa ni Sophia mwenyewe na si mwandishi kwa kumpa ukweli wake. Tatizo viongozi wetu wanaropoka hovyo na bahati mbaya hakuna anayewawajibisha, acha magazeti yawarudishe kwenye mstari
 
Sophia Simbaaaa................................

Waziri huyo..... no wonder! Wakuu hatuna haja ya kupoteza nguvu zetu kwa shangingi!
 
Huyu SS anafaa kuwa mgombea mwenza wa JK kwenye uchaguzi ujao. Bravo SS!!!!!
 
Hii mbinu ya kunyima wanaume unyumba ilibuniwa India miaka mingi sana. Kuna wanawake wa kihindi waligoma kuwapa waume zao unyumba ili kuwashinikiza waache kupigana vita. Walifanikiwa.

Wanawake wa Kenya nadhani ndo walikua wakwanza kuitumia hii mbinu kama silaha ya kisiasa miaka michache tu iliyopita ili kushinikiza waume wao waache siasa za majitaka. Hawakufanikiwa.

Nadhani Waziri Simba anawaiga tu hawa waliomtangulia. Hii mbinu inafanikiwa 100% kama wanawake wote katika jamii/nchi watashiriki kikamilifu na sii baadhi tu. Ndio maana hii mbinu ilishindwa Kenya na hapa pia itashindwa.
 
Hii mbinu ya kunyima wanaume unyumba ilibuniwa India miaka mingi sana. Hii mbinu inafanikiwa 100% kama wanawake wote katika jamii/nchi watashiriki kikamilifu na sii baadhi tu. Ndio maana hii mbinu ilishindwa Kenya na hapa pia itashindwa.
Machngudoa watashangilia. Hebu wajaribu
 
Akili za kuambiwa changanya na za kwako, sasa nyie wanawke wa ccm mlio na waume zenu walioo upinzani muendekezeni huyo pashkuna muone moto utakavyo awakia, yeye hana mume ndiyo maana anataka wote mufanane, muogopeni kama ukoma changono huyo.
 
hii hoja ya sofia simba ni made in kenya
kweli safari hii kila kitu kitatoka kenya
 
Hivi katika hili anayeumia ni mwanaume peke yake? Mbona mara nyingi nimesikia wanawake wakiomba talaka kutokana na kunyimwa unyumba na wame zao? Na je wanaume wenye wake ambo si ccm? Au umuhimu ni kwa wanaume tu, wanawake hawana maana?

Amandla......
 
KUNA dhana iliyojengwa kwamba watu wenye fikra nyepesi hujadili watu; wenye fikra za kati hujadili matukio na wale wenye fikra pevu hujadili dhana au tuseme mawazo.

simba_195.jpg
Ingawa ni ukweli kwamba nadharia hii hutoa changamoto katika jamii ili watu wajielekeze kujadili mambo ya maana na si kubobea katika umbeya, ni vigumu pia kufungwa katika misimamo hii hasa tunapotazama ofisi za umma na waliozikalia.

Hakuna ubishi kuhusu nafasi ya waziri katika serikali kwamba ni kubwa, nzito na nyeti katika kuendesha si nchi tu, bali pia katika kushughulikia matatizo ya wananchi.

Kwa kawaida mtu anayebebeshwa jukumu la uwaziri katika jamii kama yetu, anatarajiwa awe ni mtu ambaye ana upeo, anayetambua dhamana aliyopewa ina maana gani kwa taifa lake?

Ndiyo maana hata “wanaposaga” fedha za walipa kodi, inakuwa si shida sana kwa sababu wanatarajiwa kusaidia kutatua kero za jamii.

Nafasi za uwaziri katika nchi zote duniani ni chache lakini nyeti, ndiyo maana wenye wajibu wa kuteua watu wa kushika nafasi hizo hutakiwa kujaa hekima na busara ili uteuzi utakaofanywa kwa kweli uonekane ukijielekeza kuisadia jamii kukabiliana na changamoto za maisha.

Unapozungumzia uwaziri kwa taifa kama hili, kinadharia unazungumzia mtu aliyepewa dhamana ya ofisi ya umma akiwa na mlolongo wa changamoto.

Kwanza, kuwa mstari wa mbele katika kusaka mwarobaini wa umasikini wa watu wetu; kuwa mbunifu wa kutumia rasilimali za taifa ili kuleta mabadiliko ya maana katika maisha ya wananchi kwa ujumla wake.

Uwaziri kwa maneno mengine unatakiwa uelekezwe kwa mtu ambaye atatambua kwamba cheo alichopewa ni mzigo; ni kutumika, ni kutumwa na kukosa usingizi.

Kama hiyo ni sehemu ya sifa ya mtu anayestahili kukabidhiwa nafasi ya uwaziri; basi hapana shaka kwamba wengi wa mawaziri wetu hawastahili katu kukalia nafasi walizopewa.

Hawastahili kwa sababu wamekosa sifa hizo kutokana na matendo yao kila uchao; ni watu wasiosumbuliwa na umasikini wa watu wetu.

Lakini zaidi sana ni watu wasiokuwa na fahamu kama wao ni mawaziri na kwamba wanatarajiwa walau waonyeshe mfano wa nini kifanyike ili kutokomeza umasikini wetu.
Bahati mbaya wengi wamebakia kuwa watazamaji. Hawana mbinu wala mikakati.

Kwa kawaida uwaziri ni dhamana, na kwa maana hiyo ni vigumu kuutengenisha uwaziri na utu wake, vimeshikamana kwa kuwa ni kwa muunganisho wa utu na uwaziri (cheo) ndipo maana ya nafasi hiyo inaonekana kwa jamii.

Yupo Waziri wa Ofisi ya Rais Utawala Bora, Sofia Simba, huyu pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT-CCM), ni waziri ambaye amepewa dhamana nzito, ‘utawala bora’.

Katika malengo makuu ya Mpango wa serikali wa Kupunguza Umasikini nchini (Mkukuta) suala la utawala bora ni miongoni mwa malengo makuu matatu yaliyoanishwa.

Mengine ni kuwaongezea watu kipato na kuwapatia maisha bora. Kwa maana hiyo, suala la utawala bora ni jambo linalopewa umuhimu wa kipekee ili kung’oa umasikini nchini.

Kwa hiyo, Sofia si waziri mwepesi kwa maana ya majukumu ya utawala bora; ni waziri ambaye katika hali yoyote ile kuzungumzia habari ya mapambano dhidi ya rushwa nchini angepaswa aonekane akiwa mstari wa mbele kwa sababu hilo ni eneo lake la kujidai.

Ukizungumzia habari ya demokrasia; hapo kungekuwa ni nyumbani wake; lakini pia ukizungumzia habari ya kudhibiti watumishi wanaojihusisha na vitendo vya ukiukaji wa maadili na sheria za utumishi, hapo pia ungemwona. Lakini wapi!

Pamoja na majukumu yote haya, Sofia ni mweupe kama ubongo wa kichanga cha leo. Hana lolote katika fikra zake kinachokaribia kumfanyakutambua majukumu yake.

Ni waziri ambaye kwa utumishi wake wa miaka takribani mitano sasa kwanza kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na sasa Utawala Bora, ni vigumu kusema kwa yakini anafanya nini serikalini kama si kusubiri mshahara na marupurupu mengine ya uwaziri tu.

Hivi karibuni kwa kuthibitisha kiwango cha ufinyu wa fikra zake, aliwaambia wanawake wa CCM kwamba kama waume wao wanasaidia vyama vya upinzani, basi njia ya kuwakomesha ni kuwanyima tendo la ndoa.

Eti tendo la ndoa kwake ndicho kitu anachokiona cha maana na muhimu kutumika kama silaha! Sofia! Sofia!

Naogopa kumtaja Mama huyu kama ni mkware au vipi, yaani pamoja na nafasi zake zote alizoshikilia – waziri, mwenyekiti wa UWT, mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama chake, uwezo wake wa kifikiri hauvuki hisia na matamanio ya ngono!

Huyu ni kiongozi anayejinasibu kuwa anaweza kuwaunganisha wanawake na kuwaelekeza kwenye ukombozi wa kweli.

Ni mwanamke ambaye alitarajiwa kuwa nguzo ya wanawake wa CCM katika kuwaunganisha na kuwaelekeza kwenye njia inayofaa katika mapambano dhidi ya umaskini.

Ni mwanamke ambaye kwa macho ya wengi, angejua vilivyo njia bora zaidi za kupita ili wanawake wa taifa hili wajikomboe dhidi ya madhila ya umasikini wa kipato.

Alitakiwa kufahamu kwamba madhira haya yanachangiwa pamoja na mambo mengine, mfumo dume unaokataa kutambua nafasi za wanawake katika milki ya mali katika jamii.
Sofia kila anapomwaangalia wanawake wenzake anamwangalia kama mashine ya kumtuliza mwanaume; fikra zake kuhusu wanawake ni ngono.

Kwake, haoni nguvu nyingine yoyote ya wanawake ambayo inaweza kutumiwa kuleta mabadiliko katika jamii yetu; kwake mwanamke ni kiungo chake cha uzazi basi.

Katika dunia ya watu wanaowaza sawasawa siku Sofia alipotoa kauli ya kuwataka wanawake wawanyime waume zao unyumba, tungeona taharuki kubwa serikalini na hata bosi wake angemkemea kama si kumweka pembeni.

Lakini kwa kuwa nafasi za uwaziri zilikwisha kurahisishwa siku nyingi, bado ataendelea kutesa na kutesa, kwani ana shida gani wakati akili yake imeganda kwenye ngono na hicho ndicho kilichompa uwaziri?


Gazeti MwanaHalisi

http://www.mwanahalisi.co.tz/akili_ya_sofia_haiwezi_kuwaza_zaidi_ya_ngono

 
Mawaziri kama hawa ndiyo wanaonyesha picha halisi ya udhaifu wa Kikwete ktk maamuzi ya kuteua viongozi (sijui kama aliponea hapo)
 
Back
Top Bottom