Sophia Simba: Richmond haikulipwa hata senti tano

Hivi taifa liliingia hasara ya mabilioni mangapi kwa kukosa umeme kwa wakati kama tulivyoahidiwa na Richmond. Pamoja na hayo nauliza katika kipindi hicho:-
1. Watanzania wangapi walikufa.
2. Viwanda vingapi vilishindwa kufanya kazi ama kufungwa.
3. Kampuni ngapi zilipata hasara za mabilioni.
4. Ofisi ngapi za serikali hazikuweza kufanya kazi.
5. Watalii wangapi walivunja safari zao za kuitembelea Tanzania.
6. Wafanyakazi wangapi walipoteza ajira.
7. Familia ngapi ziliathirika kwa njia moja ama nyingine.

Duh, Sophia Simba - Waziri wa Utawala bora, Mbunge wa kuteuliwa na JK na Mwenyekiti wa Wake wa CCM.
images

Haya yawezekana tu Tanzania - nchi ya upendo, amani na utulivu.
kwingineko hilo domo lingetiwa kufuli.
Sasa hapa inabidi pia tuangalie jee walio mpigia kura kuwa mwenyekiti wa UWT nao wana akili au ndio Bendra hufuata upepo
 
..wakati mwingine, labda tumshauri Rais atambue kuwa wachumba waendelee kuwa wachumba, mashemeji, waendelee kuwa mashemeji, na viongozi wateuliwe kuwa viongozi. Mizigo ya Simba na Ghasia ni matokeo ya mkanganyiko wa kuteua bila kutambua iwapo wanaoteuliwa ni wachmba, viongozi au mashemeji.
'Bagambila balinsi'...... zibueni masikio msikie!

Hii kali sana , lakini inanikumbusha ile santuri ya manungayembe!
 
Uongo mwingine ni wa kijinga kweli! Richmondi haikulipwa? Hii sasa ni TOO MUCH! Sofia dadangu ACHIA NGAZI, umechemsha!
 
Back
Top Bottom