Songwe International Airport

Ni kweli kabisa, Mbeya nzima kwa siku kuna magari makubwa zaidi ya kumi na sita (16) yanayotoka hapo kwenda Dar es Salaam (SUMRY Matatu, Mbeya Express Moja, Green Star Moja, Hekima Moja, Lutweledi Moja, Budget Moja, Upendo Moja, Prince Muro Moja, Nganga Moja/Mbili, Al Saed Moja, Abood Moja/Mbili, Hood Moja/Mbili, Jenjela Moja, na mwengine taja mwenyewe).*
Duh uko juu ila na shabiby wameanza safari ya dar mbeya. Hope we ni Mwa-Ozzie*
 
Kuna mzungua alikuwa nakuja Mbeya akaambiwa ni 850km toka dsm akauliza ni nchi ingine au bado ni Tz?Swali la pili akauliza is it necessary twende kwa gari?hamna fast moving trains au ndege maana ni umbali mrefu!
Dreva wake akamjibu this is Africa ivyo unavyovisema uku havipatikani
Achana na mawazo ya kufikiria fikiria wazungu wanasemaje kuhusu matatizo yako. Ikiwa ni muhimu kujengwa ni muhimu tu.Kwani huko kwao uzunguni hakuna masafa kama hayo.Na mbona siku nyengine wanakwama viwanjani wakajilalia juu ya mabench.
 
Hizo zote zinaweza kuwa ni sababu, na cha muhimu zaidi ni kuwa mbeya kuna "potential" kubwa ya kuweza kuzalisha mazao mapya yanayoharibika kwa muda mfupi ambayo yanahitaji kusafirishwa haraka yatokapo mashambani kama mauwa, matunda na mboga mboga. Kwa kuwa na uwanja wa ndege na ndege za uhakika za kwenda nje unaongeza uwezo wa kuuza hayo mazao nje kwa unafuu zaidi kwani huhitaji miundombinu ya kuyahifadhi kwa muda mrefu, hiyo inabaki kuwa kazi ya mnunuzi wako wa nje. Uwanja wa ndege wa Kimataifa kwa Mbeya ni muhimu sana na nnashangaa mpaka Kikwete ndiyo amekumbuka hilo na analitimiza, sijui wakuu wa kabla yake walikuwa wamelala?
Haijalishi uwanja umejengwa na Kikwete au Mkapa, ila Mbeya wanahitaji Uwanja wa ndege wa kimataifa. Ila inaonesha ulianza kujengwa mwaka 2001.

government has finally affirmed that the fourth international airport currently being built in Mbeya Region will be opened this December. The confirmation comes as the project has lasted for a decade since it kicked off in 2001.
Source: TanzaniaNews24
 
Ni kweli kabisa, Mbeya nzima kwa siku kuna magari makubwa zaidi ya kumi na sita (16) yanayotoka hapo kwenda Dar es Salaam (SUMRY Matatu, Mbeya Express Moja, Green Star Moja, Hekima Moja, Lutweledi Moja, Budget Moja, Upendo Moja, Prince Muro Moja, Nganga Moja/Mbili, Al Saed Moja, Abood Moja/Mbili, Hood Moja/Mbili, Jenjela Moja, na mwengine taja mwenyewe).*
Duh uko juu ila na shabiby wameanza safari ya dar mbeya. Hope we ni Mwa-Ozzie*
Mimi Mmalawi, watu wa huko ni ndugu zangu na majirani zangu. Nilishaishi huko miaka ya nyuma. Ninajitahidi kufuatilia maendeleo yao kama majirani zangu na pia nina assets zangu huko.
 
Achana na mawazo ya kufikiria fikiria wazungu wanasemaje kuhusu matatizo yako. Ikiwa ni muhimu kujengwa ni muhimu tu.Kwani huko kwao uzunguni hakuna masafa kama hayo.Na mbona siku nyengine wanakwama viwanjani wakajilalia juu ya mabench.
Lakini si ndio wawekezaji mnaowataka kila siku?
 
Mimi Mmalawi, watu wa huko ni ndugu zangu na majirani zangu. Nilishaishi huko miaka ya nyuma. Ninajitahidi kufuatilia maendeleo yao kama majirani zangu na pia nina assets zangu huko.

Ok sawa, karibu sana tz ingawa tunasonga mbele taratiiiiiibu kimaendeleo
 
Faidhafoxy nakukatisha uwanja wa Mbeya alianza kujenga Mkapa tena kwa kasi kubwa. Ila alipoingia Kikwete kasi hiyo imepungua sana. Jaribu kufuatilia sina maana ya kumpinga Kikwete la hasha, ila tu naweka kumbukumbu sawa hapa.

kuna tetesi kuwa kutokamilika kwa uwanja kunatokana na mivutano ya kisiasa eti watu wa Kas hawapendi maendeleo ya Kusini
 
Wana JF,
Hili jamvi kweli ni la ma great thinkers, nimependa michango yenu.
Ila kwa Fazafoxy kidogo sijamuelewa anakoelekea ktk thread hii, maana inajulikana kabisa uwanja huu wa mbeya hadi sasa tangu uanze kujengwa imepita miaka kumi lakini, labda kwa bahati mbaya au makusudi tu, anaeleza kuwa ni juhudi za JK.
Wakati kwa hakika JK ndio analaumiwa kwa kuchelewesha kumalizika uwanja huu kutokana na kisirani chake.
Wakati uwanja huu unaanza kujengwa JK hakuwa Rais, hivyo ni juhudi za Mkapa labda na Mzee Mwinyi,
Ni kituko kwa kiwanja cha aina hii kujengwa kwa zaidi ya miaka kumi ........
 
Faidhafoxy nakukatisha uwanja wa Mbeya alianza kujenga Mkapa tena kwa kasi kubwa. Ila alipoingia Kikwete kasi hiyo imepungua sana. Jaribu kufuatilia sina maana ya kumpinga Kikwete la hasha, ila tu naweka kumbukumbu sawa hapa.

Uwanja wa ndege unauongea wewe ulikuwa si wa kiwango cha Kimataifa, nno uongea mimi ni wa Kimataifa "International Airport".
 
Wana JF,
Hili jamvi kweli ni la ma great thinkers, nimependa michango yenu.
Ila kwa Fazafoxy kidogo sijamuelewa anakoelekea ktk thread hii, maana inajulikana kabisa uwanja huu wa mbeya hadi sasa tangu uanze kujengwa imepita miaka kumi lakini, labda kwa bahati mbaya au makusudi tu, anaeleza kuwa ni juhudi za JK.
Wakati kwa hakika JK ndio analaumiwa kwa kuchelewesha kumalizika uwanja huu kutokana na kisirani chake.
Wakati uwanja huu unaanza kujengwa JK hakuwa Rais, hivyo ni juhudi za Mkapa labda na Mzee Mwinyi,
Ni kituko kwa kiwanja cha aina hii kujengwa kwa zaidi ya miaka kumi ........

Mkapa ilikuwa ni kiwanja cha hadhi ya kitaifa (Domestic Airport) na kama kawaida yake alimpa mkandarasi "bomu" kama ilivyokuwa kwa Rada na Ndege na huyo Mkandarasi kashindwa na watu washagawana chao kama kawaida.

Kikwete ndio kachoresha upya ramani za uwanja wa Kimataifa na tayari mambo yameshaanza, moto moto.
 
Go east, go west Kikwete ni mtu wa fitna sana...kachelewesha huo uwanja kisa anaona mwandosya atapata umaarufu... Tangu nikiwa primary early 90s tulikua tunajua kiwanja kikubwa kitajengwa songwe na chuo kikuu kikubwa kujengwa Iyunga... Guess what happened when Kikwete came!! A very big university for mbeya is still a dream, songwe airport still U/C. Northeners naturally hawapendi mbeya iendelee kwa sababu resources ziko chache hivyo wanazipeleka kwao bt JK yeye ni fitna tu za kisiasa... Oh poor Mbeya!!!!
 
Hizo zote zinaweza kuwa ni sababu, na cha muhimu zaidi ni kuwa mbeya kuna "potential" kubwa ya kuweza kuzalisha mazao mapya yanayoharibika kwa muda mfupi ambayo yanahitaji kusafirishwa haraka yatokapo mashambani kama mauwa, matunda na mboga mboga. Kwa kuwa na uwanja wa ndege na ndege za uhakika za kwenda nje unaongeza uwezo wa kuuza hayo mazao nje kwa unafuu zaidi kwani huhitaji miundombinu ya kuyahifadhi kwa muda mrefu, hiyo inabaki kuwa kazi ya mnunuzi wako wa nje. Uwanja wa ndege wa Kimataifa kwa Mbeya ni muhimu sana na nnashangaa mpaka Kikwete ndiyo amekumbuka hilo na analitimiza, sijui wakuu wa kabla yake walikuwa wamelala?

Faidhafoxy nakukatisha uwanja wa Mbeya alianza kujenga Mkapa tena kwa kasi kubwa. Ila alipoingia Kikwete kasi hiyo imepungua sana. Jaribu kufuatilia sina maana ya kumpinga Kikwete la hasha, ila tu naweka kumbukumbu sawa hapa.

Mkuu huyi Muache tu yeye kazi yake kusifia nzi mwenzake jk hawachelewi kukuruka
 
Mkapa ilikuwa ni kiwanja cha hadhi ya kitaifa (Domestic Airport) na kama kawaida yake alimpa mkandarasi "bomu" kama ilivyokuwa kwa Rada na Ndege na huyo Mkandarasi kashindwa na watu washagawana chao kama kawaida.

Kikwete ndio kachoresha upya ramani za uwanja wa Kimataifa na tayari mambo yameshaanza, moto moto.
Jk ataweka na zimamoto za bajaj pia?

Leo umesema kweli wakandarasi bomu mkapa ni CCM so na jk ni CCM samaki mmoja akioza wote ni uozo tu
 
PCCB, National Audit, NSSF, etc (Government offices) zinajenga very big buildings mikoa mingine bt guess what they build for mbeya... Despite all the tireless efforts by Mr. Mwakipesile to convince NSSF invest in mbeya, they ended up building a single floor house in the CBD!!
 
Mkapa ilikuwa ni kiwanja cha hadhi ya kitaifa (Domestic Airport) na kama kawaida yake alimpa mkandarasi "bomu" kama ilivyokuwa kwa Rada na Ndege na huyo Mkandarasi kashindwa na watu washagawana chao kama kawaida.

Kikwete ndio kachoresha upya ramani za uwanja wa Kimataifa na tayari mambo yameshaanza, moto moto.

Are you or just a quote from the so-called Q......???? "Show forgiveness, speak for justice and avoid the ignorant." (Qur'an 7:199)

If you are, Please re-call when did Mr. Mkapa speak of constructing a "DOMESTIC AIRPORT", Can you produce the international airport re-designing or drawings other than the initial design?

Anyway, always your short minded and thinking foxy views are known even before uttered.

Look at her!!!
 
Mbeya ni bread basket ya Tanzania Angalia indicator za uchumi zifuatazo ambazo zikipata uongozi wenye vision basi nchi ya Tanzania inaweza kuondokana na hali ya kuwa nchi ombaomba wa dunia kwa 'potential iliyopo Mbeya tu':-
1.Kilimo cha nafaka zote kuanzia mahindi, ngano, shayiri, ulezi, na ndizi za aina zote
2. Ardhi inayokubali kulima mazao ya mboga kama maharage, njegere, mbaazi. kunde. viazi mviringo na alizeti
3. Kahawa yenye ubora wa viwango vya dunia inalimwa kwa wingi wilaya za Mbozi, Mbeya na Ileje
4. Chai inapatikana wilaya ya Rungwe ambako pia viwanda vya kusindika vipo
5. Zao la pamba na tumbaku linalimwa wilaya ya Chunya
6. Wilaya ya Kyela ni maarufu kwa zao la Cacao na ufuta
7. Wilaya ya Mbaralli ni maarufu kwa uzalishaji wa Mpunga bora na kama lingeendelezwa kitaalamu lingeweza kukidhi mahitaji yote ya mchele kwa bara la Africa
8. Dhahabu inachimbwa na wajisiriamali wadogo wadogo huko wilayani Chunya
9. Makaaa ya mawe yanapatikina Kiwira wilaya ya Rungwe na Msangano wilaya ya Mbozi
10. Marble kwa ajili ya kutengeneza marumaru inapatikana Mbaralli na Mbozi
11. Madini ya graphite na chokaa yanapatikana wilaya ya Mbeya ambayo ndicho chanzo cha mali ghafi ya Tembo Cement pLe Songwe.
12.Kuna vivutio vya utalii kama vifuatavyo:
(a) Ziwa Nyasa kwa mpaka wa Kyela na Ileje
(b) Ziwa Rukwa kwa upande wa Chunya
(c) Meteorite (kimondo) cha Mbozi
(d) Ziwa la ajabu la Ngozi lililopo milima ya Mporoto
(e) Daraja la 'Mungu'
(f) Mto Songwe unaohama hama kati ya mpaka wa Ileje na Malawi

13. Chanzo cha maji ya mto Ruaha ambao baadaye unaungana na mito midogo midogo ya Kilombero na kuingia kwenye mto Ruvu chanzo chake ni Mbeya
14. Ufugaji wa Ng'ombe, mbuzi, kondoo unafanyika kwa kiwango kikubwa kwenye bonde la Usangu na bonde la Songwe

15.Shughuli za uzalishaji mazao ya misitu zinafanyika kwe ye misitu mikubwa ya kitaifa pale Kawetere na Kiwira
16. Uvuvi katika ziwa Nyasa na ziwa Rukwa bila kusahau mto Songwe ni moja ya shughuli kuu ya uchumi.
17. Kuna viwanda vinavyofanya kazi kama kiwanda cha Tembo cement, TBL, Pepsi, Cocacola, na cha nguzo za Tanesco.
18. Aidha kuna viwanda ambavyo havifanyi kazi kama ZZK, Hi-Soap, Mbeya textile na wajasiriamali wadogo waxogo kwenye mfumo wa SIDO
19. Kuna vyuo kama TEKU, MIST, Mzumbe Univesity
20. Mwishowe ni raslimali ya wananchi wa Mbeya ambao wote kwa asili yao ni wachapakazi. Kwa mila za watu wa Mbeya mtu mvivu hakubaliki katika jamii. Anaweza hata kukosa mke au mume kama ikijukikana kuwa ni mvivu

Kwa kweli unaweza ukasema kuwa Mungu amewapendelea wananchi wa Mbeya. Wanacho hitaji ni Serikali ya Tanzania tu kuwapa support kidogo tu kwa ku imarisha miundo mbinu ya usafirishaji kama reli, barabara na kiwanja cha ndege cha Songwe.

Jingie ni kufufua viwanda vilivyokufa kama kile cha Mbeya Textile ili kupromote kilimo cha pamba kule wilayani Chunya.
 
FaizaFoxy ni tatizo.Miongoni mwa watu wanaojulikana Lakini langu la msingi ni serikali kutokuona inapoteza mapato mengi sana kwa kutokua na uwanja huko,wakidhani wanaikomoa mby kumbe ni ujinga tu.Ndio maana msimamo wangu ni CCM kuondoka madarakani ili watu tuanze na mawazo mapya.Tuache mawazo mgando yaliyopo sasa.
 
1. Mbeya ndio hub ya mikoa ya kusin kibiashara ie iringa,ruvuma na RukwaMobile
2. Mbeya ndo inalink na Burundi,DRC,Malawi na Zambia kibiashara so kukiwa na flight itarahishisha hawa watu kuja dsm au kwenda maeneo mengine ya Tz.Ndo maana daily basi si chini ya Nne hutoka Tunduma kwenda dsm same from Kyela kwenda Dsm
3.Northern malawi na northern Zambia mahitaji yao mengi hutegemea mbeya kwa kuwa commercial hub zao ie Lusaka na Blantyre ziko umbali wa zaidi ya 1000km toka miji kama ya kasama,Karonga,Mzuzu,Mpulungu
4.Mbeya as a city deserve to have an international airport
5.Hii itarahisisha export ya bidhaa kama maparachichi na maua to mention but a few
6.Wawekezaji itakuwa raisi kuja kuvinjari na kutafuta vitu vya kuwekeza kuanzia kwenye kilimo mpaka madini

Dah,yaani ulivo elezea kwa ufupi na ufasaha ina nitamanisha kuja
mbeya maana naona ndo mji mpya wa kibiashara sasa.

Tatizo baridi,ilinitesa sana enzi niko Iyunga secondary.
 
FaizaFoxy ni tatizo.Miongoni mwa watu wanaojulikana Lakini langu la msingi ni serikali kutokuona inapoteza mapato mengi sana kwa kutokua na uwanja huko,wakidhani wanaikomoa mby kumbe ni ujinga tu.Ndio maana msimamo wangu ni CCM kuondoka madarakani ili watu tuanze na mawazo mapya.Tuache mawazo mgando yaliyopo sasa.

Faiza si tatizo, mimi naunga mkono hoja ila naisherehesha kwa kukumbusha yaliyojiri. Kikwete kisha tangaza Mbeya lazima International Airport.
 
Back
Top Bottom