Yataje tuendelee na mjadala!
Hivi kuna dili gani jamani huko hadi kujenga airport kubwa kama hiyo?
Huenda siko updated na habari zingine. Naomba mwenye taarifa sahihi anihabarishe.
Point of correction, runway ndo ndefu kuliko Nyerere airport, lakini ukubwa wa hangar na surrounding buildings haiwezi ikawa kama Nyerere airport.
Hivi lengo kubwa la kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa mbeya nini hasa? na uwanja uko katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi, au ni kwa kuwa zimegundulika dhahabu na madini mengine mengi pale mbeya? au kuna biashara gani nyingine inayoifanya mbeya iwe busy na nchi nyingine direct?
1. Mbeya ndio hub ya mikoa ya kusin kibiashara ie iringa,ruvuma na RukwaMobile
2. Mbeya ndo inalink na Burundi,DRC,Malawi na Zambia kibiashara so kukiwa na flight itarahishisha hawa watu kuja dsm au kwenda maeneo mengine ya Tz.Ndo maana daily basi si chini ya Nne hutoka Tunduma kwenda dsm same from Kyela kwenda Dsm
3.Northern malawi na northern Zambia mahitaji yao mengi hutegemea mbeya kwa kuwa commercial hub zao ie Lusaka na Blantyre ziko umbali wa zaidi ya 1000km toka miji kama ya kasama,Karonga,Mzuzu,Mpulungu
4.Mbeya as a city deserve to have an international airport
5.Hii itarahisisha export ya bidhaa kama maparachichi na maua to mention but a few
6.Wawekezaji itakuwa raisi kuja kuvinjari na kutafuta vitu vya kuwekeza kuanzia kwenye kilimo mpaka madini
Kwani hawastahili kuwa na uwanja huu? Wapi inatakiwa kuwe na International Airport?
Sawa ila inanima sana kuona tunaibiwa mali zetu, kiukweli inauma kuona mapato ya madini ni kidogo sana ukilinganisha na uhalisia, na hawa jamaa huwa wanafanya vitu kwa malengo binafsi,palipo na interest zao ndo wanaweka vitega uchumi ili wajinufaishe, kuwepo uwanja mbeya nafurahi ila uwe na manufaa ya kweli ya jiji la mbeya.Erick madini pia ni contributing factor but with Songwe International Airport uchumi wa Mbeya utakua haraka pamoja na neighbouring regions
Hivi lengo kubwa la kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa mbeya nini hasa? na uwanja uko katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi, au ni kwa kuwa zimegundulika dhahabu na madini mengine mengi pale mbeya? au kuna biashara gani nyingine inayoifanya mbeya iwe busy na nchi nyingine direct?
Hizo zote zinaweza kuwa ni sababu, na cha muhimu zaidi ni kuwa mbeya kuna "potential" kubwa ya kuweza kuzalisha mazao mapya yanayoharibika kwa muda mfupi ambayo yanahitaji kusafirishwa haraka yatokapo mashambani kama mauwa, matunda na mboga mboga. Kwa kuwa na uwanja wa ndege na ndege za uhakika za kwenda nje unaongeza uwezo wa kuuza hayo mazao nje kwa unafuu zaidi kwani huhitaji miundombinu ya kuyahifadhi kwa muda mrefu, hiyo inabaki kuwa kazi ya mnunuzi wako wa nje. Uwanja wa ndege wa Kimataifa kwa Mbeya ni muhimu sana na nnashangaa mpaka Kikwete ndiyo amekumbuka hilo na analitimiza, sijui wakuu wa kabla yake walikuwa wamelala?
Hapo nimekuelewa. Mbeya walistahili kuwa na uwanja wa ndege wa kimataifa kitambo sana. Kukosekana kwa uwanja huu kumeathiri kwa kiasi kikubwa mkoa huu na jiji hili kwa ujumla. Nasikia siasa za chuki na visasi zinazidi kudumaza mkoa na jiji la Mbeya. Watu wanashindwa kwenda kufanya kazi au kufungua biashara kwa kuwa Mbeya iko isolated sana katika suala la usafiri wa anga ila usafiri wa barabara ni wa uhakika.Wanastahili na walitakiwa wawe nao tangu zamani ila kwanini hata ule mdogo wa kawaida haukuwa na umaarufu????? leo wanaibuka na wa kimataifa....nini kipo nyuma yake? jiulize hapo.*
Ni kweli kabisa, jiji la Mbeya kwa siku kuna magari makubwa zaidi ya kumi na sita (16) yanayotoka hapo kwenda Dar es Salaam (SUMRY Matatu, Mbeya Express Moja, Green Star Moja, Hekima Moja, Lutweledi Moja, Budget Moja, Upendo Moja, Prince Muro Moja, Nganga Moja/Mbili, Al Saed Moja, Abood Moja/Mbili, Hood Moja/Mbili, Jenjela Moja, na mwengine taja mwenyewe). Hapo hujataja yanayotoka Kyela, Tunduma, na yale ya Wamalawi yanayotoka Malawi, na pia yale yatokayo Zambia. Pia hujaongelea magari yatokayo Mbeya kwenda Iringa, Songea, Dodoma, na Arusha. Mbeya ni eneo potential sana kwa watu kupata wateja wa usafiri wa ndege. Ajabu mpaka sasa bado kuna vindege vidogo ambavyp vinatoza wastani wa dola 350 kwenda Dar es Salaam tena sio go and return.Ndo maana daily basi si chini ya Nne hutoka Tunduma kwenda dsm same from Kyela kwenda Dsm
Kuna mzungua alikuwa nakuja Mbeya akaambiwa ni 850km toka dsm akauliza ni nchi ingine au bado ni Tz?Swali la pili akauliza is it necessary twende kwa gari?hamna fast moving trains au ndege maana ni umbali mrefu!
Dreva wake akamjibu this is Africa ivyo unavyovisema uku havipatikani