Polis wa songea wameamua kuonyesha uma wa watz kuwa serikal ya tz sio legelege kama wengi wanavyoisema. Askar wanaonyesha ukakamavu na uimara wa serikali iliyopo madarakan. Nguvu wanayo, uwezo wanao vitendea kazi wanavyo na kizuri zaidi amri wanayo. Semeni tena serikali legelege muone uimara wake.
Hii post inanikumbusha mpuuzi mmoja alikuwa akijisivu kuwa yeye ni mwanaume wa shoka ana nguvu na sababu kubwa ni kuwa na uwezo wa kumpiga mkewe. Ila likija suala la kumhudumia kama chakula bora mavazi malazi na unyumba alikuwa hana uwezo huo.
Watu husema uimara si kupiga bali kuwa na uwezo wa kumridhisha mkeo. Tukija kwenye serikali, uimara wake si kuua au kuonesha kuwa una nguvu, hilo tunalijua kuwa lipo kwenye katiba, ulegelege unaoongelewa ni wa kuendeleza nchi na kukomboa na kukabiliana na changamoto zinazorudisha nyuma uchumi.