SONGEA: Maandamano yameanza upyaaa, mabomu yanarindima!

Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,289
781
Niko songea muda huu, polisi wanarusha mabomu ya machozi ovyo.

Kuna taarifa ambazoo sijazithibitisha kuwa mtu mwingine ameuwawa mchana huu, na nyingine zinasema wananchi wamekamata wauwaji wawili, nachoweza kuthibitisha ni maandamano na mabomu ya machozi. Nikipata za ndani kutoka kwa wenyeji nitazileta hapa.

Kamanda ni heri ajiuzuru!
 
Aisee saa hizi inaelekea usiku, madhara yanaweza kuwa mabaya, hivi kwanini polisi hawawachukulii hatua hao wauaji na badala yake inawalipua tena Raia...watu wa haki za binadamu pliiz, Mama bisimba ingilia kati
 
Niko songea muda huu, polisi wanarusha mabomu ya machozi ovyo. Kuna taarifa ambazoo sijazithibitisha kuwa mtu mwingine ameuwawa mchana huu, na nyingine zinasema wananchi wamekamata wauwaji wawili, nachoweza kuthibitisha ni maandamano na mabomu ya machozi. Nikipata za ndani kutoka kwa wenyeji nitazileta hapa. Kamhanda ni heri ajiuzuru!

Asante kwa taarifa sasa kweli tz na ccm imefika mwisho
 
haki haipatikani sokoni lazima kupambana viva wanasongea.hizi sio enzi za ndio mzee.!
 
hivi Baba MwanaAsha akiwa kama Amiri Jeshi mkuu, anatoa maagizo gani kwa hawa askari ambao wanakua wanaua na kunyanyasa raia ambao wapo katika harakati za kudai haki zao???
 
Mpaka mchana huu mji wa Songea umekuwa na utulivu ukilinganisha na siku ya jana. Watu wameonekana wakiendelea na shughuli zao kama kawaida huku wengine wakiwa katika vikundi wakijaribu kutafakari yale yaliyojiri jana na mustakabari wake.

Mchana wa leo kunatarajiwa kuwe na kikao cha mkuu wa mkoa na wananchi, hivyo wananchi wanajiandaa kwenda katika kikao hicho na kutoa dukuduku walilonalo kuhusu mambo yaliyojiri siku zilizopita.

Polisi nao wameonekana wapo katika doria katika gari lao wakizunguka mitaani.

Tutaendelea kupashana habari kadri matukio yanatokea.

Mchana mwema.

Chanzo: Songea Yetu: Songea shwari!

Ina maana mambo yamebadilika jioni hii?
 
Moja ya status kwenye Group ya Wanasongea Facebook dakikia 26 zilizopita: "Jaman ya jana yale POlisi na wananchi Ruvuma mabomu yameanza kutumika tena mungu tunusuru jaman sahizi tunarudije nyumbani jaman jaman Songea tunakwisha!"

Alipoulizwa kama yameanza tena anadai: "Sahizi jaman ni ghafla tu kazi zimeanza mabomu yanarushwa huko nje nipo hapa ofisin kwetu tumejifungia ndani hakutokeki kabisa."

Log In | Facebook
 
...naamini muda si mrefu yataanza mauaji ya visasi kati ya raia na polisi.
 
hivi Baba MwanaAsha akiwa kama Amiri Jeshi mkuu, anatoa maagizo gani kwa hawa askari ambao wanakua wanaua na kunyanyasa raia ambao wapo katika harakati za kudai haki zao???[/
QUOTE]

Polisi wa Tanzania 95% matokeo yao ya form four ni sawa na ya Mwanaasha Jakaya Kikwete...so what do you expect toka kwa mkuu wa kaya!!!!?
 
Akihojiwa na radio moja inayorusha matangazo yake hapa Songea kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika jeshi la polisi hapa mkoani alisema maandamano yaliyofanyika jana hapa mjini yameshinikizwa na vyama vya siasa na wanaharakati. Huku akishindwa kusema ni chama gani kilichoshinikiza maandamano hayo ambayo yeye anayaita vurugu.

Aliongeza kusema kuwa wanasiasa na wanaharakati hao waliwahonga watu pesa ili waandamane. Alipoulizwa anauhakika gani na hilo akasema hizo ni taarifa za kiinterejensi. Alipoulizwa kuhusu polisi kutumia nguvu zaidi katika kupambana na waandamanaji yeye alisema inapobidi nguvu lazima zitumike, lakini itaundwa tume ya kuchunguza mauaji hayo.

Chanzo: Songea Yetu: "Siasa chanzo cha maandamano Songea"

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa wananchi wakiwa kwenye maandamano hayo walivamia Ofisi za Chama cha Mapinduzi Manispaa ya Songea na Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Vijijini walipiga mawe milango na kisha kuchoma bendera na kuleta hasara za mali nyingine za chama hicho, walivamia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,walivamia Ikulu ndogo walipiga mawe, walivamia Kituo cha Polisi na kupiga mawe na kuharibu baadhi ya magari ya wananchi.

Chanzo: Songea Yetu: Vurugu Songea askari polisi mbaroni‏

Wakati huo huo, kupitia mtandao wa facebook mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anasema: "Napenda kutoa pole zangu za dhati na masikitiko kwa ndugu zetu wana Songea kwa kile kilichojiri leo, kwa Jeshi la polisi kuendelea kufupisha maisha na idadi ya Watanzania wenzetu wasio na hatia pia kuwapa wengine vilema vya maisha kwa risasi utafikiri walikuwa ni majambazi, waharamia, nk! Je na tutaendelea kutoa pole zetu mpaka lini kwa makusudi ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi na Jeshi la Polisi nchini?. Si wakati wa kumuogopa mtu sasa bali ni wakati wa Mapinduzi mwananchi amka."

Chanzo: Log In | Facebook
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom