Somo la Physics, Chemistry Mazengo Secondary

Hahahaaaaa mkuu mimi nilikutana na Chitinde kwenye Physics full siasa, na Makunja kwenye # Kwa sasa ni DEO Serengeti aka best wa Mwiguru
 
Siku ya kwanza Mwalimu wa Physics advance anaingia darasani (Mazengo secondary), anajitambulisha kwa jina anaitwa MKOMA. Anaongea mambo mengi ya kujenga na kuongeza ufaulu, anazungumzia Timed test dah napata shauku kubwa sana nagundua kuwa ndoto zangu za kupiga div 1 ya point tatu na kutia heshima TZ nikiwa TO kutoka PCB zinakamilika.

Khaaa Imani inaniisha napatwa na mashaka siku iliyofuata siku ambayo mwalimu Mkoma anakuja kufundisha rasmi, aysee mwalimu wa Physics ana chaki tano kila moja na rangi yake, ana rula ndefu sana na nyingine fupi, ana duster la kufutia ubao.

Ooooh My God,anapiga mstari wa pambizo na chaki nyekundu. anaandika juu MECHANICS na chaki ya rangi ya njano anapigia mistari miwili na chaki ya blue.Anaandika Tarehe na chaki nyeupe,anakosea kidogo mwaka anarudi kuchukua duster.

Lahaula anachukua notes zake anakopi pale ubaoni kwa chaki nyeupe, ana mwaandiko mzuri sijapata kuona.Hata mwalimu wa Kiswahili na historia walionifundisha O level hawajawahi kuandika hivyo.

Ana maliza dakika zake 45, anasema kesho tutaendeleza sehemu inayofuata kwa leo nimemaliza mwenye swali tafadhali. Darasa zima linaangua kicheko, yeyee anasema mnafurahi haya bwana huyo anakusanya vitu vyake anasepa.

Mara anaingia Mwalimu wa Chemistry anasema yeye anaitwa Mutta au Anold Shwaziniga, amevaa miwani kama kwenye Terminator. Yeye ni beat mwanzo mwisho anasema kuna wenzetu waliotangulia walimuiba notes sasa amegoma hagawi tena notes hivyo tujitafutie.

Dahh wingu naliona katika haya masomo mawili nagundua sasa ni msuli binafsi na kukomaa na tution.. Ama kweli Physics na Chemistry Mazengo Secondary siwezi kuisahau kabisaa..
Mkuu mazengo Noma Sana, ndio maana jamaa zetu wengi waliamia tambaza , tosa , mkwawa etc , mgalula kwenye physics alikuwa anajitahidi
 
Back
Top Bottom