Somo la Kujitambua

Mapinduzi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
2,422
94
Watu wamekuwa wakitatizwa na matatizo ya kimaisha kama vile (kijamii i.e mapenzi, kikazi, kifamilia, kiuchumi na kisiasa). Almost kila mmoja wetu ameshapitia dhahma moja au nyingi kutokana na mambo ya mapenzi. Kwa wengine imepelekea kukata tamaa ya kuishi na wengine kufikia hata kutaka kujiua na wengine kujiua kabisa.

Kuutambua mwili na baiologia yake (hususan viungo, milango ya fahamu na hormones husika) kunaweza kusaidia katika kukabiliana na matatizo yanayohusiana na maisha kwa ujumla (matatizo ya matatizo binafsi kama vile ugonjwa, kijamii, kisiasa na kiuchumi). Ingawa kila mwanadamu responded differently kwenye matatizo, nini kinasababisha kupata hisia husika i.e kulia, kucheka, kuumia tu moyoni, kupata msongo wa mawazo, kujiua, kudharau na kuendelea na maisha etc.

Je, kwa ujumla, ni nini kinatokea mwilini pale unapokumbana na moja au zaidi ya matatizo yaliyotajwa hapo juu. Tusaidiane kujitambua ili kuweza kuchagua njia muafaka ya kutatua matatizo/ au jinsi ya kubeba hisia zhusika pale matatizo yanapojitokeza.
 
Back
Top Bottom