Somo la kitunguu saumu: Nguvu yake, tiba na maajabu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,751
4433ec83c0c29b46fd775e22e1defa9c.jpg

Kwanza nipende kumshukuru sana Lavan Island yeye ndio chachu ya mada hii...nilikuwa sina ufahamu wa kutosha kuhusu kitunguu saumu japo nilikuwa najua kuwa ni kinga nzuri kwa mtoto anayetaka usiku na kulialia, lakini kumbe kitunguu saumu ni kinga hatari kwa mambo ya kishirikina na viumbe roho wabaya

83805480c0069b5dac86d76530537f6b.jpg

Kitunguu saumu kwa jina la kitaalam Allium sativum sio kiboko ya wachawi tu bali pia ni kinga ya magonjwa mengi na hata wadudu waharibifu.

Hiki kiungo kimacholeta Ladha kwenye vyakula vingi kilianza kutumika zamani sana kwenye nchi nyingi duniani

Wamisri waliamini katika majini yanayonyonya damu watoto wakitumia kichane cha vitunguu saumu kuwa kinga watoto wao..sehemu za China Malaysia nk wazazi hutumia kuwapaka watoto kitunguu saumu kwenye paji la uso kama kinga ya nguvu za giza.

Kule Romania wao husaga na kupakaza kwenye milango na madirisha ya nyumba zao , mageti na hata kwenye pembe za ng'ombe wakiamini nguvu ya kitunguu saumu kwenye Kufukuza wachawi na viumbe roho wabaya.

Lakini pia ili kumlinda marehemu aliyekuwa na dalili za kugeuka jini au kuzuia asichukuliwe kishirikina walimlisha/walimwekea vipande kadhaa vya kitunguu saumu mdomoni...na hii pia ni kinga hata ya kuzuia roho yake isiweze kurudi mwilini

Huo ulikuwa ni upande wa giza lakini unapokuja kwenye afya ya kawaida ya mwili kitunguu saumu huongeza kinga mwilini, huku kikipunguza cholesterol kwa kiwango kikubwa mno huku kikisaidia kutanua mishipa ilisinyaa, zaidi hii kitu ni kinga bora sana ya cancer na hata mgonjwa mwenye dalili za cancer . BP kisukari nk nk...ukiweza kabla ya kulala tafuna kipande kimoja cha kitunguu saumu kile kisicho na harufu kali

Maajabu ya kitunguu saumu ni kwamba inakuwaje kitu kidogo namna hii kinakuwa na nguvu ya ajabu hata kuwa kinga kwenye nguvu nyingi za giza? Kimoja kinachosemwa saana ni ile harufu yake . . . majini mashetani na hata wachawi na washirikina wakiwemo wanga wana mzio mkali na harufu ya kitunguu saumu na vitu vichachu..hii ndio sababu pekee iliyoweza kutolewa mpaka sasa.

Lakini pia maajabu mengine ni ile nguvu ya Kufukuza hata wadudu waharibifu majumbani na mashambani kiasi cha kuvutia watengeneza madawa ya wadudu kukitumi.

Kuna watu baadhi si wachawi wala si washirikina lakini hupenda kutumia mchanganyiko wa Biblia takatifu kitunguu saumu na mafuta ya mzeituni kuwasaidia watu wenye magonjwa ya ajabu yanayohusishwa na nguvu za giza kwahiyo jamani pamoja na kuwa kiungo kimacholeta Ladha kwenye vyakula vingi lakini pia ni kinga ya magonjwa mengi na hata nguvu za giza

ef08580701efcecb9f1b952283712432.jpg
 
Katika nchi za wenzetu wazungu wengi walikuwa hawakijui kitunguu saumu. Miaka ya karibuni baadhi wameanza kufahamu umuhimu wa kitunguu saumu kwa kinga mbali mbali za magonjwa yanayowaathiri wanadamu. Na kwa kuwa wengi hawajui namna ya kukitumia kwenye chakula wameamua kukitafuna ili kujipatia hiyo kinga inayopatikana kupitia kitunguu saumu.
 
Somo zuri. Kwa kuongezea kwa wenzang kwenye tendo la ndoa ni shida kidogo kitunguu swaum ni moja kati ya dawa kurekebisha tatizo hilo. Chukua vipande 10-15 then katakata vipande vidogo vidogo kisha kunywa na maji kwa kila asubuh na jion. Ahsanteni ni dawa nzuri sana ndg zangu
 
Ahsante kwa somo mkuu, tatizo LA nguvu za kiume siku hizi limekua kubwa kuliko nguvu za Giza, sasa vinabust mambo yetu?
Si unaonainatanua mishipa iliyosinyaa?
Unachifanya unachukua asali maji ya moto na kitunguu saumu robo lita ya maji moto kitunguu saumu vipande viwili asali vijiko vitatu daily kwa mwezi mzima
 
yaani ndo hivihivi tu mkuu..hapana kwakweli jazia nyama hapo..mchango wako unahitajika
Mkuu Mshana ameeleza vema, katika falme za kiganga haswa ukanda wa pwani kitunguu hiki hutumika katika mazindiko mazito mazito na hapo mchawi akasome.

Pia kinatumika katika kufukuza majini wabaya, pia ni miongoni mwa tiba kwa mtu aliyedhuriwa na jini, huondoa upepo mbaya wa mtu aliyekumbwa na shetani na pia husaidia kwa maradhi mbali mbali ya husda kwa watoto.

Katika tiba ya kawaida kinasaidia mambo mengi sana na bado kila siku kinagundulika kuwa ni dawa ya maradhi mengine zaidi, hutibu tatizo la kupata choo, wenye maradhi ya ubaridi/kupooza na hata wenye presha.

Karibu kila mtihani kwetu binadamu jibu lipo kwenye mimea tatizo ni kujua kipi kina kazi ipi......Mungu ameweka maradhi na tiba zake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom