SOMO LA JIOGRAFIA, NECTA, TAASISI YA UKUZAJI MITAALA NA UPUMBAVU WA WALIMU (O level)!

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Ni jambo la kusikitisha sana kuona somo la Jiografia linazidi kufanya vibaya pamoja na umuhimu wake. Kuna mambo mengi yanayochangia kufanya vibaya kwa somo hili na wadau wamekaa kimya katika taifa hili lililokosa mwelekeo. limekosa mwelekeo wakati ni tegemeo na kiungo muhimu kwa michepuo mingi kuliko somo lolote Tanzania.

Binafsi ni mdau na mwalimu wa somo husika na leo naanzisha thready hii wenzangu mchangie kwani najua nyie ni miongoni mwa waathirika hawa. Zifuatazo nisababu za kufanya vibaya kwa somo hili kwenye mitihani ya taifa.

Kwanza ni NECTA na Taasisi ya ukuzaji mitaala kwa kukaliwa na watu ambo binafsi ama hawajui walifanyalo au wamejaa ujuaji unaozidi kipimo na usioendana na wakati wa sasa.

Hawa jamaa wamekuwa wakitoa syllabus ambazo hazieleweki na mfano mzuri ni hii ya sasa ambayo ni ya 2005. Haileweki katika maeneo mengi ila mija ni kutokuwa na maelekezo ya moja kwa moja ya mambo gani yafundishwe.

Wamekuwa wakitoa maswali nje ya muktasari uliopo hasa kwa olevel

Pili,Walimu pia wan aochaguliwa ni walewale katika kutunga na kuhakiki na au kusahihisha mitihani kwa njia ya upendeleo kwamba ni somo rahisi na kila mtu anaweza kufundisha au kufanya chocho. Ni waalimu hawa hawa wanao pewa ulaji kilaini hutunga maswali magumu ili wakubalike kwa wateuzi wao bila kujali janga la kitaifa. Huu sasa ndo upumbavu.

Tatu, wizara imekuwa haina vitabu vya somo ata kwa kuviagiza nje na wachakachuajiwamekuwa wakijiamulia kutunga watakayo na ambayo hayaidhinishwa na wizara, wako wachapishaji wengi mtaani na hii huongezea mkanyiko kwa wanafunzi. Kwa mfano hakuna kitabu cha Research cha Secondary!!!! Pia chain survey imapitwa na wakati na hakuna ata shule moja yenye vifaa vyake.

Kuna jambo la nne la tuition na waalimu feki ambao wengi wao ni wale wenye dvs o na 4 ya kidato cha nne au sita. na kwa kawaida hawa ndo wamekuwa naTuitiion centre kubwa hapa TZ.

kuna Upuuzi mwingi, wadau changieni ili ata vyombo vya habari vitusaidie kutatua tatizo hili. Ni mengi ila naomba kuwasilisha.
 
Mkuu karibu umemaliza kila kitu kiasi kwamba tunashindwa hata kuchangia. Ila kitu kingine ni kwamba walimu wazuzri wa jiografia wanaomaliza vyuoni wanakwenda kufanya kazi inje ya ualimu hivyo kufanya shule nyingi zikose walimu wazuri.
 
Tatizo lingine ni walimu wa kigeni ambao hawaijui geography ya Tanzania kwa ufasaha,utakuta wanachanganya maeneo kwa sababu hawajui mokoa yalipo.Watanzania wanafurahia watoto wao wafundishwe na wakenya au waganda wakiamini kuwa wako juu kuliko wazawa.Nilishuhudia Mkenya mmoja akiwaambia kwamba mlima kilimanjaro uko Kenya,japo alikuwa akiwatania lakn wanafunzi wengine waliamini.Huu ndio upumbavu ambao aliyeanziaha thread hii ameusema kwenye jamvi hili.Sikatai walimu toka nje lakn si kila somo
 
hongera sana mtoa mada kwa kuanalyse matatizo sugu. Mimi pia ni mdau yaani mwalimu wa somo la jiografia secondary, tatizo la vitabu ni kubwa vitabu viko vya aina nyingi na vyote havikidhi, kuna topics ambazo ni irrelevant na hazieleweki kwa watoto, mitihani mingine maswali yake hayaendani na vitu vilivyoko ktk muhtasari, na tatzo kubwa lingine ni waalimu wamejitokeza walimu feki wengi hasa ktk matuition ambao hawajui somo vizuri ambao wamekuwa wakiwamislead watoto na inakua vigumu kuwaelekeza tofauti kwa kuwambia hicho sicho sahihi ni hiki ni wachache tu watarespond. Jamani tukumbuke na serikali insist yafuatayo:-
1) Jiogrofia ni miongoni mwa masomo ya sayansi linahitaji umakini ktk vitabu, muhtasari, na ufundishwaji pia lazima liendane na elimu kwa vitendo (practical) ili lieweke vizuri we needs geography labs
2) Jiographia ni somo muhimu kwa sababu linahusika na maisha ya kila siku, pamoja na mazingira yetu na ni muhimu kueleweka kwa kila mtu regardless field zao
3)Jiografia ni kiungo ktk combination za masomo mengi kuliko masomo yote ya a level kwa walioko ktk mchepuo wa sayansi, sanaa,na biashara kwa hiyo lipewe uzito unaostahili na sio kuchukuliwa ka somo la kawaida ambalo unaweza kufaulu hata pasipo kufundishwa
 
Ni kweli mdau, pia vitabu vya jiografia havieleweki ni vipi hasa vinatakiwa vitumike, walimu wanachanganya wanafunzi, wanasema msitumie kitabu fulani na wakati huohuo mwalimu huyohuyo anatumia kitabu hicho hicho kutungia maswali na mitihan ya shuleni. Na zaidi ya hayo serikali inatoa syllabus wakati haina mpango wa kutoa vitabu vinavyoendana na hiyo syllabus, it's so rediculous!
 
Maswali ya mitihani yote yanatungwa na walimu wenyewe na wanayapeleka NECTA. NECTA inafanya kutoa versions kadhaa za mtihani wa mwisho na unajadiliwa na jopo la wataalamu wa somo ambao ni waalimu na wanasema iwapo mitihani hiyo iko nje ya mitaala au labda haipimi yale yaliyokusudia . Baada ya mapitio hayo NECTA inachagua maswali toka katika maswali yaliyojadiliwa halafu inatunga mtihani.

Sasa walaumu walimu walioenda NECTA au ujiangalie wewe mwenyewe upya yawezekana hufuati mitaala unabaki kuingia darasani na kutumia muda mwingi kuzungumza yaliyo nje ya mada ya siku.
Je ualimu ulisomea wapi?
 
hongera sana mtoa mada kwa kuanalyse matatizo sugu. Mimi pia ni mdau yaani mwalimu wa somo la jiografia secondary, tatizo la vitabu ni kubwa vitabu viko vya aina nyingi na vyote havikidhi, kuna topics ambazo ni irrelevant na hazieleweki kwa watoto, mitihani mingine maswali yake hayaendani na vitu vilivyoko ktk muhtasari, na tatzo kubwa lingine ni waalimu wamejitokeza walimu feki wengi hasa ktk matuition ambao hawajui somo vizuri ambao wamekuwa wakiwamislead watoto na inakua vigumu kuwaelekeza tofauti kwa kuwambia hicho sicho sahihi ni hiki ni wachache tu watarespond. Jamani tukumbuke na serikali insist yafuatayo:-
1) Jiogrofia ni miongoni mwa masomo ya sayansi linahitaji umakini ktk vitabu, muhtasari, na ufundishwaji pia lazima liendane na elimu kwa vitendo (practical) ili lieweke vizuri we needs geography labs
2) Jiographia ni somo muhimu kwa sababu linahusika na maisha ya kila siku, pamoja na mazingira yetu na ni muhimu kueleweka kwa kila mtu regardless field zao
3)Jiografia ni kiungo ktk combination za masomo mengi kuliko masomo yote ya a level kwa walioko ktk mchepuo wa sayansi, sanaa,na biashara kwa hiyo lipewe uzito unaostahili na sio kuchukuliwa ka somo la kawaida ambalo unaweza kufaulu hata pasipo kufundishwa

Mkuu unakijua kitabu cha physical Geog. cha Said Ayub? Kikoje?
 
Ni kweli mdau, pia vitabu vya jiografia havieleweki ni vipi hasa vinatakiwa vitumike, walimu wanachanganya wanafunzi, wanasema msitumie kitabu fulani na wakati huohuo mwalimu huyohuyo anatumia kitabu hicho hicho kutungia maswali na mitihan ya shuleni. Na zaidi ya hayo serikali inatoa syllabus wakati haina mpango wa kutoa vitabu vinavyoendana na hiyo syllabus, it's so rediculous!

Kuna mfano topic ya Survey kwa A na O level naamini kuwa hakuna shule ata moja pengine yenye vifaa hivi. Mwenye data atujuze
 
Back
Top Bottom