Somo kutoka kwenye mgomo wa madaktari na posho na posho za wabunge

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Serikali imeridhia Posho za Wabunge ziongezwe, lakini imegoma kusikiliza (sio kuongeza)
maslahi ya Madaktari hata baada ya wananchi kutaabika kwa kukosa huduma za afya
kutokana na Mgomo wa Madaktari unaoendelea ili kuishinikiza serikali ikae nao na kuzungumza
namna ya kuboresha maslahi yao. Tunajifunza nini kutokana na Matukio haya, hasa kwa kuoanisha
umuhimu wa makundi yafuatayo katika Jamii yetu.

SERIKALI --- WANASIASA---WANANCHI--WAFANYAKAZI.

Moja ya somo ni kwamba, Si kweli kwamba serikali yetu ni serikali ya watu, iliyochaguliwa na watu,
kwa manufaaa ya watu (Government of the people, by the people for the people).
Bali hii ni serikali iliyopo kwa Mujibu wa Katiba na sheria zake. Hivyo, haioni, na wala haitatokea ikawajibika
kwa wananchi.

Watanzania wanatakiwa wafumbuke macho sasa na kuangalia mambo haya kwa mapana zaidi,
serikali hii iko radhi kushirikiana na wanasiasa bila kujali matakwa ya wananchi na makundi yao
yote, kama wafanyakazi, wanafunzi, wakulima n.k

Na kwamba, hata wanasiasa wenyewe sio watu wa kuaminika kwamba wana dhamira ya dhati ya
kutetea masilahi ya wananchi huku wakijua wanaweza kujiingiza kwenye migogoro na serekali,
Vyombo hivi viwili (Bunge na Serikali) viko karibu zaidi ya ukaribu wowote uliopo kati yao na wananchi.

Wananchi tufunguke macho, tatizo sio serikali pekee, ni vyote, serikali na bunge. Na tusipofisha mahusiano
yao, basi tutaendelea kuona bunge linaloendeshwa kwa hisia zisizo na tija yoyote kwa wananchi mpaka
siku Yesu atakaporudi.
 
du mpaka YESU atakaporudi ngoja nipite sijakuelewa ntarudi baadaeutakapoamua WaTZ wafanyeje juu ya posho hizo na mgomo wa madaktari
 
Back
Top Bottom