Somesha mtoto mmoja yaendelea- update. Asante waliojitokeza mpaka sasa

Mar 5, 2012
92
23
SOMESHA MTOTO MMOJA –KINACHOENDELEA.
Waliotoa fedha mpakasasa,
1. Mr.J.A .M........60,000
2. Mr. J.L. M....60,000
3. Mr. C. S. M-wa UK................50,000
4.Mr. A. K.............................60,000
5.Mr. T. M.....................50,000

Mategemeo:
6. Mdau toka Arusha anatuma muda wowote.

Napenda kutoa shukrani kwa waliokweishatoa na wale walioahidi kuchangia/kuingia ktk mpango huu waSOMESHA MTOTO MMOJA.
Kwa mapenzi ya Mungutunakusudia kusaidia wengi. JIULIZE JE NI WANGAPI WANAKWAMA KWA KUSHINDWA KULIPA ADA AMBAYO KWA MWAKA HAIZIDI 150,000, na JE NI WANGAPI MUNGU AMEWABARIKI WANAWEZA KUSAIDIA MPANGO HUU., KWA KUSOMESHA MTOTO MMOJA TU.

‘BADILI MAISHA YAMWANAFUNZI MMOJA, BADILI FAMILIA YAKE, BADILI TAIFA LAKO, BADILI DUNIA HII.


USHUHUDA MWINGINE, NAOMBAUSHAURI PIA.

Kuna mwanafunzi mwingineambaye toka January mpaka sasa ameshindwa kuendelea na masomo.
Jpili, nilikuwa sehemu nawa-TZ wenzangu tukijadili mambo ya taifa letu. Nikagusia na suala hili lakusaidiana sisi kwa sisi, mbali na kutegemea misaada toka nje. Baada ya kuzungumza,mzee mmoja akanifuata. Akaniambia binti yake ana matatizo ya shule. Nikamuahidi kuwa tukutane tuongee, nijueundani wa suala lake. Leo jioni nimewasiliana, tumekutana na kilio chake nihiki.
Mtoto wake alimaliza shule mwaka 2011, alipata alama 192 kati ya 250( Wastani wa 38 ya 50 kwa somo).Akapangwa shule ya Zawadi iliyopo Ilala, eneo la Tabata. Lakini baba yake mdogoakajitolea kumpeleka shule ya seminari ya Bigwa iliyopo Bigwa, ambako amesomamwaka mmoja, form one mwaka 2012, lakini bahati mbaya baba yake huyo mdogoanasema hana fedha za kuendelea kumsomesha tena, kwa hiyo binti yupo nyumbanitoka january mwaka 2013. Baba yake, ana uchungu sasa, binti muda wote analiaanaomba aende shule.


WAY FORWARD.
Mwenye wazo lolote lanini kifanyike, atusaidie wakati huo huo nasi unaendelea kutafuta namna yakumsaidia huyu binti, kwa kweli anajitahidi sana ktk masomo lakini, ndio hivyotena yupo nyumbani hajui hatma yake, na baba yake yupo lakini hana ajira yoyotewala kipato kingine, alikuwa anamsaidia mtu ktk biashara zake, yule mtu biasha imeporomoka kwa hiyo huyu mzazi kafukuzwa kazi.
MUNGU AWATANGULIE KTKKUTAFAKARI HILI.
MATEGEMEO.
Tunaomba walau kwa sasa wajitokeze watu 3 tu ili wale watoto 10 tuliowapataMorogoro tuweze kuwasaidia wote.

Mungu ni mwema, ndugu unaombwa kuingia ktk mpango huu, na utabarikiwa kwakubadili maisha ya mtanzania mwezako, familia yake, taifa, na dunia kwa ujumla
 
Back
Top Bottom