Someni taarifa ya Bernard Kamilius Membe

Zanzibar siyo nchi. Haitambuliki kimataifa.
Kama sio nchi mbona hazijasajiliwa morogoro ?Mpaka kieleweke, jamuhuri ya watu wa Zanzibar kwanza. JMT dhaifu na omba omba, lazima wafuate amri ya bwana Mzungu. Sasa bado ndoa za jinsia moja. Wahenga walisema ''Bure ghali'' na hakuna msada usio malengo........
 
Ngoma mbichi kabisa jamani,kama naona vile matokeo ya utafiti wa Membe,kuwa kweli wamesajili na kweli zinapeperusha bendera,atasemaje?maana Serikali ya Muungano ikikataa na Kufuta usajili,hapo ndipo utamu utanogeshwa,Zanzibar wakiamua kusajili kwa bendera yao je?au Umoja wa Mataifa utawakoromea?au wataambiwa hawana haki na uwezo sababu wako kwenye Muungano(labda ili kuwabana) najua nao Zanzibar watafyatuka kurudi kwenye kero za Muungano upya na kwa nguvu zaidi!!!!napenda kuona itaishaje!
 
Zanzibar siyo nchi. Haitambuliki kimataifa.
Jasusi, hawaelewi kuwa pale UN New York ipo bendera ya Tanzania na hakuna ya Zanzibar. Ni kwa muktadha huo Marekani waliona meli zenye bendera ya Tanzania na wametoa malalamiko kwa Tanzania.

Wale wanaosema kuna sheria gani imevunjwa nadhani wanapaswa kuelewa kitu kinachoitwa diplomasia.
Kuna sheria, kanuni, mikataba na maazimio. Kwahiyo kushikilia sheria gani imevunjwa ni kuangalia jambo katika mtizamo finyu sana.

Kidiplomasia waziri wa Zanzibar kulitolea kauli jambo hili ni utaratibu wa kawaida wa Wazanzibar kukurupuka bila kufahamu wanasema au wanatetea nini. Kuna waziri mmoja wa mambo ya nje wa Tanzania na hayo ya baraza la wawakilishi yanabaki kuwa mambo ya barazani kama vile tunavyojadili Simba na Yanga. Hata hivyo timu hizo pia zina bendera lakini hazina kiti wala waziri wa mambo ya nje.

Kama kuna ujinga ni pale nitakaposikia kuwa suala hili ni sehemu ya kero za muungano. Ni ujinga kwasababu kwa kutumia Tanzania Zanzibar inachangia 0% na inapata 7%. Hiyo ni pamoja na misaada na madeni.
Kwa deni la nje la nchi Zanzibar inalipa ''0'' na wala haijawahi kulalamika kuwa inakosa fursa za muungano za kulipa deni la nchi.

Lakini pia kama ni kero za muungano mbona Zanzibar haijawahi kujitokeza na kudai kuwa Gaidi la kimataifa M. Ghailani ni raia wa nchi yao? Iweje leo wasimame na kusema meli za mafuta ni za nchi yao! Kwanini Ghailan asiwe kero kwa Tanzania kama kero za meli kwa upande wao!

Na mwisho, wanaposafiri wanabeba passport za Tanzania, kwanini hilo lisiwe kero kama basi bendera na nembo ya Tanzania hawazitambui?
 


  • Bernard Kamilius Membe



    Serikali imepokea taarifa kuhusu tuhuma za meli za Iran kupeperusha bendera za Tanzania ili kukwepa vikwazo. Serikali ya Jamhuri ya Muungano na SMZ hazitaki kupuuza taarifa hizi. Serikali zote mbili zimeamua kufanya uchunguzi ili kuthibitisha. Tanzania imewaarifu nchi zilizolalamika marafiki kuwaomba kusaidiana nasi kufanya uchunguzi na kushirikiana kuthibitisha taarifa hii. Tumefanya hivyo kwa kuzingatia uwezo wetu wa kiutafiti na kutaka utafiti huu kuwa huru kwa kuwashirikisha wao wenye ujuzi mkubwa. Tunafanya hivyo kwa kuwa wakala wa ZMA anayefanya kazi za kusajili amekana kusajili meli za Iran, Balozi wa Iran nchini aliitwa akakanusha. Tutakapopata matokeo ya utafiti na ikithibitika kuwepo na ukweli hatua zitachukuliwa mara moja. Tukithibitisha tuhuma hizi tutafutilia mbali usajili wa meli hizo. Tunafanya hivyo kutimiza wajibu wetu kimataifa hususan Azimio 1920 la UN Security Council.Tanzani sio adui wa nchi yoyote duniani. Tunafurahia mahusiano yetu na nchi zote duniani. Hili ni jambo linalogusa maslahi ya Tanzania nje na maslahi ya Tanzania ya ndani (Muungano), tujihadhari na namna tunavyolizungumzia. Tusimame pamoja kama taifa. Nchi kwanza!


Huu undumilakuwili unatugharimu sana, we utakuwaje rafiki wa marekani na wakati huohuo rafiki wa palestina (wale waliokuwa wanamhifadhi osama)? Raki wa Israel na wakati huohuo rafiki wa ahmadinejad, mwenye ndoto za kuifuta israel kwenye ramani ya dunia?

''Tujihadhari namna tunavyolizunguamzia suala hili'', hii tabia nyingine siipendi sana kutoka viongozi wa ccm, kila wakati kujazana uoga tu, kuna kipi cha ajabu kwenye hili, tujihadhari na nini hapa? kwa hili is either white or black hakuna cha kujihadhari wala hakuna siasa, amueni nini mnataka yaishe!

UDHAIFU:
Mnyika alisema kuna mtu dhaifu, watu wakapiga keleleeeee utafikiri katukana, sasa mtu kutoka marekani anajua meli za iran zinapeperusha bendera ya TZ, watu wetu wenye dhamana wanaishia tu kuuliza SMZ na balozi wa iran, eti kwa sababu smz wamekataa sasa wanaomba marekani isaidie kwenye uchunguzi, kama huu sio udhaifu basi tuuiteje, upuuzi au?

1. serikali yetu inataka marekani ishiriki kwenye huo uchunguzi kwa sababu inataka kujikomba kwa marekani, ili ionekane haina dhambi yeyote ndio maana iko tayari kuruhusu uchunguzi huru, huku ni kujikomba, kujipendekeza, na ni ujinga, kama serikali inao uwajibikaji huo, basi tuunde kwanza tume ya kuchunguza kutekwa kwa ulimboka

2. Udhaifu mwingine kwenye hili ni kwamba serikali haiwezi kufanya uchunguzi yenyewe, serikali imelala tu, watu wanapeperusha bendera ya nchi yenu nyie hamjui? mnapewa taarifa mnashindwa kuchunguza, kitu kikubwa mnachoweza kusema. . . "tumewauliza SMZ na balozi wa Irani wamekataa" kweli? hii ni aibu na ni UDHAIFU!

Kama machinery yote ya serikali haiwezi kwenda extra mile, inaishia tu kuuliza kitu ambacho hata mie ningeweza kufanya, hii serikali iko na kazi gani sasa? . . . DHAIFU!
 
History repeats itself.

Then: OIC ,wallahi imebidi tujitoe.

Now: Wallahi imebidi tufute usajili wa meli za Iran.
 
Kwa assumption kwamba Membe ni mahakama!

Kama mamlaka imesajili na kui"visha" meli ya nje BENDERA ya TAIFA...pasipo mamlaka ya juu (Diplomatic-Balozi & mambo ya nje) kujua, bado unasubili mahakama kutambua hili ni kosa?? mahakama ikapigilie muhuri tu wa hukumu...
 
Hapa tumeshikwa pabaya!!
Tukipiga biti juu ya hii issue nao wataondoa madaktari wao.
 
Sasa mtu anayetuhumiwa apewe nafasi kubwa ya kuchunguza kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kuchunguza?

Membe hapa anatia mashaka.ikitokea ikawa kweli sidhani jambo la kufuta usajili tu litakuwa limetosha.Kama Tanzania inawajibika kweli kweli bila unafiki kwenye majukumu yake kimataifa ni lazima hili suala lifikishwe UN security Council.Huku kutakuwa ni kuichafua Tanzania na ni uchokozi hasa ukizingatia meli yenyewe ni ya Serikali.Tanzania itakuwa imewasaidia iran kukwepa vikwazo.Pia Tanzania itaingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia kwa kushindwa kwajibika kimataifa.Nakumbuka cyprus na Malta(siyo malta kinywaji kama wengine mnavyotamani) wako katika shinikizo kubwa kutoka EU waache kutoa msaada wa kuruhusu bendera zao zitumike kusafirisha cargo za Iran

Pia,Membe anaposema anazingatia wajibu kwa kutumia azimio namba 1920 la baraza la Usalama sioni uhusiano wowote uliopo hapo labda atumie kipengele dhaifu cha 'political will' katika kutatua mgogoro.Azimio namba 1920 lilikuwa mahsusi kwa migogoro western sahara na wakimbizi

Kwa nini usimshauri wenje alisimamie bungeni hili?uchochezi tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom