Soma ujirekebishe nafsi yako

Mahmood

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
7,909
2,477
Mwenyezi Mungu anawataka Waislamu wapende kheri kwa ajili ya ndugu zao kama wanavyopenda kheri kwa ajili ya nafsi zao. Na akafanya hayo ni mizani ya kujipima mtu imani yake. Basi ikiwa sivyo hivyo, basi kuna upungufu katika imani yake. Na haya katuhakikishia Mtume Muhammad S.A.W. katika Hadithi zifuatazo:

Mtume Muhammad S.A.W. Kasema,

1-Hataamini mmoja wenu mpaka apende (kheri) kwa ajili ya ndugu yake kama anavyopenda (kheri) kwa ajili ya nafsi yake.

2- Pia Kasema, Penda (kheri) kwa ajili ya watu kama unavyopenda (kheri) kwa ajili ya nafsi yako uwe Mu-umin.

3-Mu`adh bin Jabal R.A.A. alimuuliza Mtume Muhammad S.A.W. kuhusu bora ya imani. Akasema: "Bora ya imani ni kumpenda Mwenyezi Mungu na kuchukia kwa ajili ya Mungu, na ufanye ulimi wako kwa ajili ya kumtaja Mola. Akasema: Na kitu gani ewe Mtume wa Mungu? Akajibu: Penda (kheri) kwa ajili ya watu kama unavyopenda (kheri) kwa ajili ya nafsi yako. Na uchukie (shari) kwa ajili yao kama unavyochukia (shari) kwa ajili ya nafsi yako. Na sema yaliyo ya kheri au nyamaza (kimya).

4-Mtume Muhammad S.A.W. alimuuliza Yaziid, "Jee, unapenda Pepo? Akajibu, "Ndiyo." Akasema, "Basi penda (kheri) kwa ajili ya ndugu yako kama unavyopenda (kheri) kwa ajili ya nafsi yako."

5- Mtume Muhammad S.A.W. Kasema, Asiyeshughulikia jambo la Waislamu, basi huyo si miongoni mwao.

6- Pia Kasema, Mwislamu kwa Mwislamu ni kama majengo yaliyoshikamana moja baada ya moja.

7- Mtume Muhammad S.A.W. Kasema, Mwislamu ni kioo cha Mwislamu (mwenziwe) akiona aibu amtengeneze.

8- Pia Kasema, Mfano wa Waislamu katika kupendana kwao, na kuhurumiana kwao na upole wao, ni kama mfano wa mwili ukishtakia kiungo kimoja vitaitana mwili mzima kwa kuumwa na homa.

9- Mwislamu ni ndugu wa Mwislamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom