Soma tena kisha mtumie na mwenzio

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke, mkewe akakataa, akamwambia baba yake akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa zina mengi!

Akawa kila siku analalamika kwa babaake, mwisho babaake akamwambia basi ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!

Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha kikao cha ndugu wote pande mbili. Mzee akaanza kueleza jamani kijana wetu anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospitali zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga wa jadi amenipa dawa na ina masharti.

Inatakiwa atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu alipoolewa ndo kijana wetu atapona! Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote!

Je kina mama nani ataandaa? Walitoka nje wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana, mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia wanaume peke yao!

Mzee akamwambia mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo? Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani umejionea hali halisi. Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!

Kijana akazimia!

SOMA TENA KISHA MTUMIE NA MWENZIO
 
Siku hizi hatuna vifua vipana vya kuweza kutunza figisu figisu za ndoa hasa hilo la kutoka nje ya ndoa.
 
Hii inawafaa zaidi walio ndani ya ndoa maana vijana watachukua hii kama sababu za kutooa mapema
 
Hakuna taasisi watu wana rukiana sana kama hii enzi zetu tunapata fahamu timu ya taifa ya Uruguay ilikuwa inasifika kwa kutembeza kiatu(kupiga buti)yaani timu pinzani watatembezewa kiatu mpaka wanaogopa kisha Uruguay wanaanza kucheza mpira ilikuwa sio jambo la ajabu kuambiana yule jamaa tumchezee Uruguay.Sasa taasisi hii ya ndoa na mahusiano ina Uruguay nyingiiii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom