Soma mwenyewe uone aina ya viongozi tulionao

Nteko Vano

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
434
111
[h=1]Mukama, Mzindakaya matatani Mukama, Mzindakaya matatani[/h]

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 22 February 2012-MWANAHALISI

MRADI wa maji uliogharimu Sh. 1. bilioni ambao uliolenga kunufaisha vijiji vitatu sasa unanufaisha familia moja, imeelezwa.

Vijiji vinatajwa kulengwa ni Nkundi, Fyengereza na Kalundi, vilivyopo wilayani Nkasi, mkoani Rukwa.

Habari kutoka wizara ya Maji zinasema, matumizi ya fedha hizo yanadaiwa kuidhinishwa na Willson Mukama alipokuwa katibu mkuu wa wizara hiyo. Hivi sasa, Mukama ni katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aliyetajwa kuhusika na matumizi ya maji yaliyogharimu mabilioni ya shilingi ni Chrisant Mzindakaya aliyekuwa mbunge wa Kwela (CCM).

Mzindakaya hivi sasa, ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo la taifa (NDC). Taarifa kutoka katika vijiji hivyo vitatu zinasema wakati mamia ya wanavijiji wakikosa maji, mradi unaotokana na kodi za wananchi unahudumia mtu mmoja.

Wanasema tangu bwawa hilo lijengwe hawajawahi kuruhusiwa kutumia maji yake kwa kunywa wao wala mifugo yao.

Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini, Ali Keissy Mohamed, ambapo bwawa hilo limejengwa, amesema suala hilo lilishafikishwa hata bungeni, ambapo kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) imeamuru bwawa hilo wapewe wananchi.

Hata hivyo, Keissy amesema, Mzindakaya ametaka alipwe kwa ardhi yake ambamo bwawa limejengwa. “Tunamshangaa sana. Anadai fidia ya nini wakati yeye ndiye aliomba bwawa hilo lijengwe kwenye eneo lake, badala ya eneo la vijiji hivyo,” amehoji mbunge.

Amesema, “Hili ni tatizo kubwa kwa wananchi kwa sababu wamebaki hawana maji hata ya kunawa uso. ”Alipoulizwa Mukama kwa nini aliidhinisha ujenzi wa bwawa katika eneo binafsi la Mzindakaya alisema, “…Kama tatizo, liko wizarani, waulize wao…”

Alipoambiwa kwamba wananchi wanadai kuwa suala hilo linafuatiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa nchini (TAKUKURU), Mukama alisema, “Kumbe Takukuru wanapohoji watu wanaripoti kwako. Waulize hao Takukuru wakupe maelezo.”

Msemaji wa Takukuru, hakupatikana kueleza kuhusiana na madai kuwa wanafuatilia suala hili.

Taarifa zinasema wakulima hawakuwahi kushirikishwa kutoa uamuzi wapi bwawa hilo lijengwe. “Mbali na kuwa wananchi hawakushirikishwa, uongozi wa kampuni ya SAAFI Ltd., ambayo inamiliki bwawa hilo, wanawanyanyasa wananchi wangu,” ameeleza mbunge Keissy.

Amesema, “Wananchi wangu hawana hata maji ya kunawa uso, lakini Mzindakaya anatumia maji yalioletwa kwa fedha za umma kunyweshea mifugo yake. Hili jambo hatuwezi kuendelea kulivumilia...”

Kutokana na utata uliogubika ujenzi huo ambao unadaiwa kugharimu kiasi cha Sh. 1.092 bilioni, serikali imelazimika kutafuta fedha nyingine zitakazotumika kujenga miundombinu ya kusambaza maji kutoka kwenye bwawa la Mzindakaya.

Miundombinu hiyo itakayojengwa, tayari imetumia kiasi cha Sh. 130 milioni.
Kwa mujibu wa waraka wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali wa 11 Machi 2011, serikali iliagizwa kuweka miundombinu hiyo ili wananchi wanaozunguka bwawa la Kawa, wilayani Nkasi wapate maji.

Aidha, Bunge liliagiza eneo lililojengwa bwawa hilo lililopo kwenye shamba la Mzindakaya linachukuliwa na kumilikiwa na serikali.

Katika kutekeleza maagizo ya Bunge, serikali ilifanya kikao cha pamoja kilichowashirikisha viongozi mbalimbali akiwamo mkuu wa mkoa wa Rukwa. Wengine waliohudhuria mkutano huo, ni mkuu wa wilaya ya Nkasi, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri, mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya SAAFI na uongozi wa kijiji cha Nkundi.

Katika kikao hicho mambo kadhaa yalikubaliwa. Miongoni mwa yaliyokubaliwa ni kampuni ya SAAFI ambayo imejengewa bwawa hilo na serikali kwa fedha za umma baada ya Mukama kuidhinisha, ni kufungwa mkataba kati yake na wadau wa bwawa hilo kuhusu matumizi yake.

Waraka wa kamati ya Bunge unaonyesha kuwa kampuni ya SAAFI ilikubali kutobughudhi upatikanaji wa maji kwa wananchi husika na ulinzi wa eneo utatolewa.
Wakati Bunge liliagiza bwawa hilo lichukuliwe na serikali, wizara ya maji imejifunga kwenye makubaliano na kampuni ya SAAFI kujenga bwawa ambalo litakabidhiwa halmashauri ya Nkasi ambalo litasambaza maji kwenye vijiji hivyo.
Bwawa hilo litajengwa kwa fedha za wananchi.

Makubaliano mengine ni halmashauri ya wilaya ya Nkasi kukubali kuwa itakamilisha ujenzi wa bwawa na miundombinu ya kisha kuiendesha.

Kwa mujibu wa kifungu cha pili cha makubaliano ya mkataba, wanasheria wa serikali na kampuni ya SAAFI wamekubaliana kuandaa rasimu ya mkataba ambao utasainiwa na pande hizo mbili ili kuepuka mgogoro wa bwawa hilo.

Wachambuzi wa mambo wanasema, kutajwa kwa Mukama kwenye kuidhinisha matumizi haya ya mabilioni ya fedha za umma kunamuweka Rais Jakaya Kikwete katika wakati mgumu wa kusafisha chama chake. Kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji Na. 11 ya mwaka 2009, kifungu cha 10, maji yote ni mali ya umma na yanatumika kwa utaratibu uliowekwa na sheria.

Kwa maana hiyo, bila kujali bwawa ni la nani na liko wapi, mtu yeyote ana haki ya kutumia maji hayo ili mradi afuate taratibu zilizowekwa.

Hata hivyo, pamoja na kuwapo kwa sheria hiyo, wananchi wanaozunguka bwawa hilo wanadai kuwa mengi ya yale yaliyokubaliwa na yaliyomo kwenye sheria ya maji hayajatekelezwa.

Baadhi ya wananchi wamenukuliwa wakiwatuhumu wafanyakazi waliopo kwenye shamba hilo kwa kuwanyanyasa, kuwapiga na hata kuwajeruhi kutokana na kugombea maji hayo.

Mzindakaya alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kujibu madai ya kuzuia wananchi kutumia bwawa lililojengwa kwa kodi zao, hakupatikana.
 
Mukama, Mzindakaya matatani Mukama, Mzindakaya matatani

kumbe chanzo ni Mwanahalisi? liko kazini hizo mkuu, halina ukweli wowote hilo, usipoteze muda wako.
 
hii nchi sijui tunaishi kwa kunyenyekeana au kwa njia ya kishirikina . Lakini ipo siku haya yote yataisha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom