Soma maamuzi ya hakimu huyu juu ya ndoa

Hakuna maamuzi ya aina hii ya kesi za ndoa
Kuna procedure zake na namna ya kufikia au kutoa hukumu kuwa mume na mke waachane
Hakuna sehem katika sheria ya ndoa waliposema kuwa mke arudi kwa baba yake mpaka maamuzi mengine yafikiwe
Ina maana hapo hakimu amewatenganisha hata kabla ya kusikiliza shauri lao
Kuna mabaraza ya kata na viongozi wa dini na washenga ambako kote huko wanatakiwa watoe maamuzi tena kwa maandishi kuwa wameshindwa kusuluihisha ndoa hiyo na ndipo shauri linapelekwa mahakamani.
Mahakama itasikiliza pande zote mbili pia na kuona kama kuna haja ya kuvunja ndoa husika
Na sababu za ndoa hiyo kuvunjika lazima zielezwe wazi kama adultery, vipigo, kushindwa kwa mwanaume kuconsume the marriage, kichaa may be mwanaume amekuwa kichaa au kifungo cha zaidi ya miaka mitano, na makosa mengine ambayo mahakama itaona kuwa hiyo ndoa imeshindikana beyond repair

hilo somo ni somo potoshi. barua imesema binti akae kwa wazazi wake haidi uamuzi wa mahakama utakapofikiwa juu ya hiyo ndoa. ndoa haijavunjwa hapo. tusiangalie mambo juu juu. hivi kama huyu mwanamke usalama wake u hatarini na mwanaume hajapatikana. huyu mwanamke anakwenda kukaa wapi? anasaidiwaje? au angekwenda mahabusu mpaka uamuzi wa ma hakama ufikiwe?.

barua hiyo ni hati ya utambulisho wa huyo binti kwa wazazi wake. sote hapa hatufahamu yaliyojiri kwa undani. si vema kuchukulia juu juu kuwa hakimu amepotoka. mathalani huyu binti ameiambia mahakama kuwa kwa mumewe sio salama na mahamama imejiridhisha kuwa si salama , na bado isichukue hatua zozote za kumlinda, angedhuliwa kwa namna yoyote bado tungelalamika kuwa mwanamke hakulindwa kwa uzembe.

aliyeiweka hii barua hapa ni mvivu sana. hiyo barua angeiweka akitoa na ufafanuzi juu ya nini kinajiri ktk hiyo kesi. lakini yeye ameipost na kurudia maandishi yaliyopo ktk waraka
 
Ndiyo maana sasa hivi wanatakiwa mahakimu wenye uelewa wa sheria sio hao wanaohukumu kwa "kuhisi na kudhani"
 
jamani tusitoe hukumu bila kujua 'facts' za hii kesi ili tujue vipi hakimu alifikia maamuzi haya.
 
Back
Top Bottom