Soma hii ya uamsho ucheke mwenyewe, hawa jamaa wamechanganyikiwa

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Jana tulisikia kauli zenu na mukasema Uamsho wapo Serikali. Sisi tunayakubali maneno yenu na tunakiri kuwa ni kweli Uamsho wapo Serikalini. Ila nyinyi mumeshindwa kuwataja kwa majina sisi tutawataja kwa majina na vyeo vyao.

Muamsho wa kwanza ni Rais Jakaya Kikwete. Yeye ametuamsha kwa kutwambia wazi Wazanzibari kuwa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba haitoratibu Muungano. Hivyo ametuamsha na kutuwekea bayana Wazanzibari kuwa Tume hiyo haituhusu, sisi Wazanzibar kinachotuhusu kwenye Katiba ni Muungano. Katuamsha kuwa Tume hii ya Katiba si ya Muungano.


Kikwete huyo huyo ametwambia kuwa Muungano ushavunjwa na CCM NEC, na alisema NEC imeshaamuwa kuwa Rais wa Zanzibar asiwe Makamu wa Rais wa Muungano. Hivyo ametuamsha kuwa NEC imeenda kivyume na Hati ya Muungano na kwenda kivyume na makubaliano ni kuyavunja makubaliano, hivyo NEC imeuvunja Muungano.


Muamsho mkubwa zaidi ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Yeye alituamsha pakubwa tena akatutowa kwenye usingizi mzito pale alipotwambia kuwa Zanzibar si Nchi. Hata alipoambiwa ni nchi amekosea, akasema: “Sijakosea wala sijalewa. Zanzibar si nchi.” Kwa hakika, Pinda ametuamsha pakubwa.


Muamsho mwengine ni Mwalimu Julius Nyerere alipotwambia amechoka na sisi Wazanzibari; na hapa namnukuu: “Tumechoshwa na Wazanzibar i na Uislaam.” Kama si Muamsho, huyu ni nani?


Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Marehemu Mzee wetu Abeid Amani Karume, alituachia uswiya kwamba “Muungano ni kama koti, likitubana tutalivuwa!” Naye pia ni Muamsho.


Muamsho mwengine ni Mansour Yussuf Himid. Naye katuamsha si haba pale aliposema ndani ya Baraza la Wawakilishi kuwa serikali moja hataki kuisikia, mbili ni butu, anataka serikali tatu au vyenginevyo.


Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita, Shujaa Amani Karume ndiye aliyezidi sio tu kutuamsha, bali pia akatuletea Umoja wa Kitaifa na Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya mwaka 2010 tena akaifanya iwe shoka la kuvunja Muungano. Isomeni vizuri Katiba ya Zanzibar na hapo mutajuwa kuwa Karume ni Muamsho au si Muamsho.


Kwa hiyo, Stephen Wassira na UVCCM hamjakosea kusema Muamsho wapo Serikalini. Ni kweli. Tena wapo serikali ya Chama chenu. Wala msimtafute mchawi. Wachawi wenyenu.
 
Rais wa Kwanza
wa Jamhuri ya
Watu wa Zanzibar,
Marehemu Mzee
wetu Abeid Amani
Karume, alituachia
USWIYA-Sijakuelewa hapa shekhe. . .
 
dawa yao ni kuwapiga chini, waende wakalane wao kwa wao, kwani mafuta wanayongángania kuwa ni ya zanzibar, si yapo pemba? sasa muungano ukivunjika wakachimba mafuta, wa unguja watajua wapi watatoa mafuta, kwasababu yale ni ya wapemba, si wazanzibari....ni kitu gani kinatufanya tuwan'ga'ngánie hawa watu? si tuwachane nao tu?
 
Mbona Muamsho mwengine umemsahau weye! Tena Muamsho mkubwa. Maalim Seif na ndevu zake ni Muamsho anayetufadhili akipokea pesa kutoka kwa Sultani.
 
Nimerudi tena.

Msingi Mkuu wa kupunguza nguvu ya uamsho ni kukaa nao meza moja na kuandika madai yao yote.

Baadhi ya madai yao ndio yale yaliyomo kwenye kero za Muungano. Hawana jipya.

kupambana nao ni kuwapa nguvu.
 
Mbona Muamsho mwengine umemsahau weye! Tena Muamsho mkubwa. Maalim Seif na ndevu zake ni Muamsho anayetufadhili akipokea pesa kutoka kwa Sultani.

Muamsho mwingine ni mimi ....MAMA POROJO.

nimeona sitajwi nimejitaja mwenyewe endapo itakubarika.
 
Hii busara leo umeitoa wapi?

Eneo linalohusu dini wakati wote nina busara jaribu kunifuatilia.

Ibrahim ndiye baba wa waislamu na wakristo.

kumbuka: ibrahim akazaa na Sarah mtoto Isaka ndio wakristo na Ibrahim akazaa na hajra mtoto Ismael (ishmael) ndio waislamu..... sisi ni watoto wa baba mmoja mama mbalimbali.

Ni mitala tu inatusumbua. tukitaka kubaki salama tujitambue kama watoto wa baba mmoja kuliko kujinasibu na upande wa mama zetu (sarah na Hajra).
 
Mkijitenga nyie ndio mtapata hasara kuliko sisi, mimi najua nyumba zaidi ya 20 za wazanzibar mkiondoka tu nachukua kadhaa...
 
Nimerudi tena.

Msingi Mkuu wa kupunguza nguvu ya uamsho ni kukaa nao meza moja na kuandika madai yao yote.

Baadhi ya madai yao ndio yale yaliyomo kwenye kero za Muungano. Hawana jipya.

kupambana nao ni kuwapa nguvu.

Ulipigwa ban Mama Porojo..? Naona umerudi na busara kidogo..
 
Muamsho ni wewe mtooa mada mana umeniamsha niende chooni nikaamsha na haja zote kubwa na ndogo nikaamsha na mfuniko wa choo,alafu nikaamsha mainzi na mende nao wakaamsha buibui ili wawaamshe inzi wawadake hahaha uamsho ni noma
 
Eneo linalohusu dini wakati wote nina busara jaribu kunifuatilia.

Ibrahim ndiye baba wa waislamu na wakristo.

kumbuka: ibrahim akazaa na Sarah mtoto Isaka ndio wakristo na Ibrahim akazaa na hajra mtoto Ismael (ishmael) ndio waislamu..... sisi ni watoto wa baba mmoja mama mbalimbali.

Ni mitala tu inatusumbua. tukitaka kubaki salama tujitambue kama watoto wa baba mmoja kuliko kujinasibu na upande wa mama zetu (sarah na Hajra).

Nimekupata, ila hapo kwenye red unaleta utata zaidi, maeneo mengine je?
 
Yesu kristo na mtume Mohammed (SWA) walitumwa na Mungu kuifanya dunia iwe ya dini moja ama ukristo au uislamu hata walipokufa hawakuweza kukamisha mission hiyo...... je binadamu wa kawaida ambaye hata utume huna leo hii baada ya miaka 2000 baada ya kifo cha Yesu na miaka 1478 baada ya kifo cha Mtume Mohammad kazi hiyo haijaisha.

Je tunaopteza muda kuchukia dini nyingine tutafanikiwa???????

Tunapojadili suala hili dini zetu tuweke pembeni ndipo suluhu ya kweli itapatikana.
 
wagalatia jamani chonde chonde udini acheni mjadala hauhusu uislamu wala ukristo wala upagani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom