Soma Hapa Tafadhari,Nakutegemea!!

Hauko serious ndugu. Dollar 200!!! Kwani Tanzania umetoka lini?

mkuu hao watu wa ughaibuni wasikie tu, hapa utajiuliza maswali kibao yasiyo na majibu, kifupi ni kwamba wengi wao wanaenda tu kama kubahatisha, wanakuwa hawajui ugumu wa huko. Unaweza kuwashangaa mpaka basi, lakini ukweli ndo huo kwamba hali ni ngumu.

Muhimu mpe ushauri kama alivyoomba vinginevyo utaendelea kushangaa tu kwa sana!
 
Mkuu angalia ni bidhaa zipi unaweza kutoa huko uliko na kuleta Tanzania au nini unaweza kutoa Tanzania kupeleka huko uliko. Mara nyingi ukiwa nchi nyingine unaona vitu mbali mbali tofauti na nyumbani ambazo ni fursa tosha ya biashara ndogo. Utashangaa kuna biashara ndogo lakini ukivuka mpaka inakuwa na faida nzuri. Kuwa makini kuangalia na kuulizia bei za vitu mbali mbali na kulinganisha na bei za nyumbani. Nazungumzia vitu unaweza kusafirisha kwenye mabasi. Njia nyingine ya kujua nafasi zilizopo za biashara ndogo ndogo ni kwenda kwenye kituo cha basi zinazo enda au kutoka Tanzania na kuangalia ni bidhaa gani tayari watu wanasafirisha na ufanye utafiti wa faida yake. Unaweza pia kuongea na ma konda wakakujulisha ni kitu gani wanaona watu wakisafirisha kwa wingi.

Shukrani Sana ..nimekusoma Mkuu!
Nahitaji Kujipanga Kwani Biashara Ya Mipakani Ina Vikwazo Vingi Hvyo Mtaji Angalau Milioni Ndio Wa Kuanzia!
 
Watu Tunatofautiana Katika Utafutaji,hii Kazi Yangu Si Rasmi Na ndio Maana Nataka Kurudi Nyumbani Na Kujiajiri Mkuu!

Sawa kiongozi, kama umeweza kuchanga laki 3 kwa mwaka rudi home tu, njoo tutaabike pamoja.

Laki 3 si ndogo kuamua kuzizalisha mkuu, inatakiwa tu ujibane sana na usichague sana biashara ya kufanya (za halali lakini!), kama ni mitaa ya vijijini fikiria kupigisha simu na kuuza vocha au kama ulivyosema mwenyewe kununua nguo mijini na kuzipeleka vijijini hasa hasa wakati wa mavuno
 
kila Mtu Na Alivyojaaliwa Mkuu,sizani Kama Naweza Fanana Nawe Katika Mipango Ya Maisha!
Tafadhari Ushauri Wako my Dear!

Aisee kutokana na mtaji wako nimekosa cha kukushauri mkuu
 
Sawa kiongozi, kama umeweza kuchanga laki 3 kwa mwaka rudi home tu, njoo tutaabike pamoja.

Laki 3 si ndogo kuamua kuzizalisha mkuu, inatakiwa tu ujibane sana na usichague sana biashara ya kufanya (za halali lakini!), kama ni mitaa ya vijijini fikiria kupigisha simu na kuuza vocha au kama ulivyosema mwenyewe kununua nguo mijini na kuzipeleka vijijini hasa hasa wakati wa mavuno

Nitafanyia Kazi Ushauri Wako Makini My Dear!
 
Aisee kutokana na mtaji wako nimekosa cha kukushauri mkuu

Vipi Mkuu?Unaweza Kutoa Ushauri Wako Hata Kwa Kiasi Unachokifiria Kwani Itanisaidia Katika Mipango Ya Baadae!
 
Katika Hekaheka Za Utafutaji Niko Nje Ya Nchi
Nimeajiriwa Na sasa Nina Laki 3 Tsh...Ila Nahitaji Kurudi Tz Ili Nijiajiri.
Kwa Uwezo Wangu Mdogo Wa Kufikiri,ninampango Wa
Kujumua Viatu Mbeya Mjini
Na Kuanza Kuviuza Eneo
Nitokalo(kyela).

Ndugu Zangu Nishaurini Mbali Na Wazo Langu,Je Kuna Biashara Nyingine Naweza Fanya Na Ikatoa Faida ya Ziada?

NB:Haijarishi Mkoa Gani
ilimradi Biashara Hiyo Ina Manufaa!
Natanguliza Shukrani!
kama kweli unatoka Kyela, nakushauri tafuta eneo la kulima, nadhani kwa kilimo utapoata fedha nyingi kuliko hizo ulizo nazo
 
kama kweli unatoka Kyela, nakushauri tafuta eneo la kulima, nadhani kwa kilimo utapoata fedha nyingi kuliko hizo ulizo nazo

sawa Mkuu Ila Msimu Wa Mvua Ushapita Na Huku Hakuna Kilimo Cha Umwagiliaji!
 
una tshs laki tatu, uko nje ya nchi uantaka kurudi bongo je nauli unayo? ukifika bongo unafikia wapi ? kama huna nauli laki 3 zitaishia njiani itaishia njiani
 
una tshs laki tatu, uko nje ya nchi uantaka kurudi bongo je nauli unayo? ukifika bongo unafikia wapi ? kama huna nauli laki 3 zitaishia njiani itaishia njiani

Mkuu Hyo Ni Nje Na Nauli Yaani Hyo Ni Kwa Ajili Ya Biashara Tu...kula,Nauli,kulala Vinajitegemea!
 
sawa Mkuu Ila Msimu Wa Mvua Ushapita Na Huku Hakuna Kilimo Cha Umwagiliaji!
Unatoka kyela sehemu gani? Mbona kule Rugwa, kama vile maeneo ya Msoko, kuna mabonde mengi tu ambayo watu wanaendesha kilimo wakati wote!
 
Whats amazing ni jinsi thread kama hizi zinavyopata wachangiaji wengi kuliko thread serious!!! yes, and i am one of them...hahhahahahahahahahahaha
 
wabeba boksi bora mrudi tu bongo kama hali yenyewe ndio hivyo, loh.
 
Whats amazing ni jinsi thread kama hizi zinavyopata wachangiaji wengi kuliko thread serious!!! yes, and i am one of them...hahhahahahahahahahahaha

Hayo ni Mawazo Yako Na Kama Huna Ushauri Ni Bora Ukawa Kimya,Kwani Naamini Wako Watakao Nishauri Na Lengo Langu Kutimia!
Kwani Wewe Ulitaka Iwe Vipi...Ili Ujue Namaanisha?
Ulitaka Niombe Ushauri Wa Mbinu Za Kuwa Mkabaji Au Ulitaka Nitumie Kiswanglishi Katika Uandishi?

Tukikaa Vijiweni Bila Kujishughurisha Maneno,tukiomba Ushauri Kama Hivi... Mnakuja Na Kejeli...Hujanivunja Moyo Kwani Najua Kile Nafanya!
 
Huwezi kuwa ughaibuni halafu unarudi na sh. laki tatu ambayo ndiyo unayoitegemea kuanzisha biashara. Hauko serious. Hili jukwaa siyo la fictional stories. Watu kama nyie mtasababisha jukwaa hili lipoteze maana yake. Habari kama hizi peleka kwenye hoja mchanganyiko au jokes, sio hapa.
 
samahani Mkuu!!
Inaonekana Kiasi Changu Kimekughadhabisha...Nasema Tena Unisamehe Sikujua Kama Eneo Hili Ni Kwa Walio Staaribika Tu!
 
Ndiyo Hivyo...Nahitaji Kurudi Nyumbani Ndugu Yangu!
pole sana mkuu, ukifika nyumbani hebu ni-PM tuongeze huo mtaji tuungane tufanye biashara.
nimeona mtu kama wewe UNAEJIAMINI sio bure, kuna kitu cha zaidi ndani yako, ni zaidi ya binadamu wa kawaida!.
 
Fanya namna hii, tumia hizo laki 3 kama nauli ya kurudia huku na ukifika cha kufanya hakikosi!!!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom