Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
kuna mambo mengi sana yanatokea huko vijijini na vyombo vya habari hawaviripoti hata waandishi wa habari hawaripoti mambo haya
NB:hii post nimeiquote hapa hapa jamvini . dk. Slaa alikuwa anajibu swali la mtu . tujadili yaliyomo
Ni dakika chache tu nimeingia kutoka Kaliua na Urambo. Tumekuwa na mikutano mitatu ya hadhara, tumefungua ofisi na matawi ya Chama. Hivyo si kweli kuwa Chadema inalipiza kisasi kwa CCM.
1)Kwanza inaelekea wengi hawafahamu malengo ya mikutano ya vijijini, na hasa kwa kuwa wanapata magazeti, wanatazama TV wanaamini Watanzania wote wanafanana. Lengo la Chadema katika hatua hii siyo kuwaambia CCM mbinu ya kuleta maendeleo wala kuwapa mikakati ya maendeleo. Ikumbukwe kuwa Chadema haikusanyi kodi yeyote ya wananchi na hivyo katika kipindi katika ya Uchaguzi kazi ya Chama cha siasa ni kujijenga kwa uchaguzi ujao,kukosoa Serikali iliyoko madarakani katika sera,Ilani na utekelezaji wa sera na ilani hiyo,kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuelewa udhaifu wa Chama hicho Tawala ili katika uchaguzi ujao tuiondoe. Hii ndiyo kazi yetu ya kikatiba. Chama cha siasa chenye kujua wajibu wake hakiwezi kuwa wasindikizaji tu. Sisi si washauri wa Serikali kwa kuipatia mbinu za kuongoza au mikakati ya kuongza na kuleta maendeleo. Kama yuko anayefikiri hivyo ni vema arejea vizuri majukumu ya vyama vya siasa.
2)Sisi tunaofika vizuri ndio tuko kwenye mazingira ya kutafsiri nini kizungumzwe katika kijiji fulani tofauti na kingine. Hii inatokana na uelewa unaotofautiana. Katika kijiji kingine hata ajenda iliyokwisha kuzoeleka kwa watu wa vijijini kama Listi of Shame iliyotolewa 2007 inabidi itolewe upya kwa kuwa wananchi hawajawahi kujua ni kwanini nchi yeny utajiri mkubwa kama TZ inaweza kuwa maskini, au inakuwaje wako wanaoogelea katika utajiri mkubwa wakati wao hawana zahanati, maji, wanakula mlo mmoja bila kujua kuwa inatokana na rasilimali nyingi kutafunwa na mafisadi. Najua wako ambao wanaumia kwa sababu zao kila tunapowataja mafisadi, lakini katika mazingira kama hayo Mwanasiasa makini ni yule anayejua mahitaji ya wananchi wake. Hivyo, Msishangae wana JF kuona tunayarudia yale yale. Mtakuwa wabinafsi iwapo hamtapenda watanzania wenzenu wayajue mnayoyajua nyie.
3) WanaJF wako katika jamvihili wanaoishi dunia yao wenyewe, au kwa kutaka au kwa bahati mbaya. Mathalan, nimestuka sana, kama niliyoelezwa Kaliua ni ya kweli Tanzania kuna ndugu zetu wanaishi bado Tanganyika ni si mwaka 47. Kaliua mtu mmoja aliyetajwa kama Baraka,mtoto wa Kapuya amekuwa tishio kwa wana Kaliua wote.Wanakaliua wanapigwa,wanachomewa nyumba, wanauawa na wakilalamika polisi nao inafyata kutokana baba Baraka kuwa tishio. Katika mazingira kama hayo usifikirie utazungumzia maendeleo zaidi ya kuwajengea ujasiri,mbinu za ukombozi na hata kuwafafanulia ufisadi mkubwa katika Jimbo kama hilo. Haiingii akilini mwa yeyote, kwa umaskini mkubwa tulioona Kaliua, na bado 72 Millioni zimetafunwa kwa jina la au kupitia kasma ya Mishahara (mishahara hewa, mishahara kulipwa kwa watumishi waliofariki, waliofukuzewa watoro n.k.) Kwa bahati mbaya hata tunapokuwa na Waandishi wa habari katika ziara mazingira na hotuba kama hizo hazipati nafasi kwa sababu yeyote ile, au hata kwa vile tu mwandishi anachagua anayotaka yeye.
Hali inatisha, ndiyo maana Chadema tumedhamiria kutoa elimu katika vijiji mbalimbali kati ya sasa na 2015. Wanaoumia na hiyo waumie tu. Wananchi wengi vijijini ndicho wanachohitaji kwa CCM siku mmoja haitawapa elimu hiyo. Wilaya/Jimbo Maskini kama Kaliua haingii akilini inapotokea Halmashauri inashindwa kutumia Tshs 659,697 Millioni katika mwaka wa Fedha, na hatimaye isionekane katika B/F kwa kuwa mfumo wa uhasibu wa almashauri hauna utaratibu huo. Matokeo yake hakuna anayejua fedha hizo zimeenda wapi. Kama Madfiwani wa Kamati ya Fedha hawajapangia matumizi ni nani anapangia matumizi. Kama Chadema hatutakemea ufisadi wa namna hiyo nani akemee. Ikumbukwe hii ni wilaya iliyokuwa hadi mwaka wa ukaguzi yaani Juni 30, 2010, mawaziri wawili na Spika wa Bunge.
Ndugu zangu wengine kwenye jamvi hili wanazungumza tu nadharia bila kujua hali halisi ya nchi yetu, au kwa makusudi tu wanataka kutuondoa kwenye ajenda zetu. Hatoki mtu hapa "ngo"(kwa lugha ya kina Kombani. Atakuwa mwanasiasa wa ajabu ambaye anahutubia mbele ya Ofisi ya "Spika" iliyojengwa Urambo, wakati Urambo haina Bunge na hivyo haina Spika. Hii ni ofisi iliyojengwa kwa milioni zaidi ya 300 na kuwekewa fenicha ya zaidi ya 170 Millioni, katika jimbo ambalo hakuna zahanati, vituo vya afya n.k. Mwanasiasa atakayeacha kutaja Ufisadi huu kwa kuwa wanaJamvi wachache wadhani wamechoka kusikia habari ya ufisadi atakuwa siyo mwanasiasa Makini. Kafiribigiri,naamini nimeeleweka.
Tushuke chini, tusidhani maisha ndani ya jamvi hili ndivyo yalivyo vijijini. Hata kama sisi tuna maisha mazuri, tuwafikirie wazazi wetu,shangazi zetu,wajomba zetu ambao bado wanaishi nyumba za tembe na majani, ambao mlo wa siku ni shida, ambao wameacha kula nyama kwa kuwa bei haishikiki nakadhalika. Hizi ni ajenda za kudumu na ndiyo namna ya kuondoa umaskini wa wananchi wetu kwa kuikaba serikali ngazio zote iache ufisadi na ielekeze rasilimali zote kuwahudumia wananchi badala ya kujijengea mahekalu, kutembelea mashangingi ya millioni 500. Hii ndiyo ajenda,inaewzerkana wewe huipendi lakini vijijini ndiyo mambo yenye "mshiko"
NB:hii post nimeiquote hapa hapa jamvini . dk. Slaa alikuwa anajibu swali la mtu . tujadili yaliyomo