Jay Milionea
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 1,185
- 154
WAZIRI WILLIAM LUKUVI ABAINISHA MASUALA MUHIMU SEKTA YA ARDHI KATIKA "TUNATEKELEZA" TBC1 27/08/2016
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Serikali ya Awamu ya Tano imeanza kutekeleza program kabambe ya kupima ardhi yote ya Tanzania;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Utekelezaji umeanza mkoani Morogoro kwa kushirikiana na kampuni binafsi zilizosajiliwa ili kila mwananchi awe mkulima, mfugaji, mwenye kiwanda, shamba na kila aina ya shughuli atapimiwa eneo lake kuliongezea thamani;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Nakuhakikishia katika miaka 10 kila kipande cha ardhi Tanzania kitakuwa kimepangwa na kupimwa;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Serikali imeanza kudhibiti bei ya kupima ardhi kwa kushirikiana na wapimaji binafsi;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Serikali itaweka ukomo wa kumiliki ardhi.Haiwezekani mtu anamiliki ardhi kubwa ambayo hata haitumii;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Ni marufuku wageni na wawekezaji kwenda vijijini moja kwa moja kununua ardhi.Waje kwangu au wapitie TIC tutawapa ardhi haraka wawekeze;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Mtu anayetaka kujenga kiwanda popote aje kwangu nitampatia ardhi ndani ya siku 7;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Wizara imeshatenga viwanja 240 kwa ajili ya Viwanda Kigamboni.Anayetaka aje hakutakuwa na rushwa wala ubabaishaji;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Wawekezaji wanaohodhi tu ardhi bila kuitumia muda wao umekwisha.Rais kashaagiza na tunafanyiakazi.Wasiotumia ardhi tutawapatia wengine;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Wananchi wote waliodhulumiwa viwanja Dar es Salaam kwa makosa ya watendaji wa Serikali tumeanza kuwapa fursa na heshima ya kuwapa viwanja vingine mbadala;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Naagiza Halmashauri zote ziwapatie viwanja mbadala wananchi ambao walidhulimiwa viwanja vyao kwa makosa ya watendaji;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Wananchi wote walioko kwenye makazi holela tutawapa heshima ya kushirikiana nao na kuwapimia ili wafaidike na makazi yao na kulipa kodi;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Mji mpya wa Kigamboni...nimeona wamekuja wadau wana mawazo mapya baads ya kuwa Manispaa.Tutazungumza nao zaidi. Hatutashindwana.
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: NHC inajiendesha kibiashara lakini nimezuia kupandisha kodi mpya hadi niridhie;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Ni ndoto yangu kuifanya sekta ya ardhi ichangie zaidi katika pato la Taifa
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Nataka pia kutimiza ndoto ya Rais Magufuli ya kuondokana na migogoro isiyo na tija ya ardhi;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Muda wa watendaji kusababisha migogoro umekwisha...muda wa watu kuhodhi ardhi kubwa bila kuitumia nao umekwisha;
[HASHTAG]#LUKUVI[/HASHTAG]: Wapo wananchi wameanza kunisifu na wapo wanaonilaumu wakitamani nifike kila mahali kuwasaidia lakini nashindwa. Lakini bado ninasafari ndefu kuwafikia; Nitafurahi kuona siku moja nchi hii haina migogoro ya ardhi.