LE GAGNANT
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 1,241
- 251
Edward Moringe Sokoine ansifika kuwa alikuwa mmoja wa viongozi wapenda haki na uwajibikaji. Lakini alikuwa pia na silka ya utawala wa ki-imla, nakumbuka jinsi alivyolishughulikia suala la wahujumu uchumi, kipindi kile badala ya kutatua tatizo la uhaba wa bidhaa ndiyo ikawa bidhaa zinafichwa na kuuzwa kwa bei za kuruka. Kwa maoni yangu ni kiongozi wa kutumia mamlaka zaidi kuliko kutafuta suluhisho la matatizo ya nchi. Kwa kizazi cha siasa za sasa sidhani kama angefika mbali.