Kaka Mkubwa
Senior Member
- Oct 10, 2008
- 154
- 10
Hivi raisi huyu atashughulikia kila upuuzi? Amekuwa katibu kata?
Tatizo kubwa ni pale tulipojibana kwamba Serikali haiwezi kufanya biashara; hii kitu itatuumiza sana kama tusipoibadili maana ni wazi haina maana yoyote kama tutaweka misingi imara ya "accountability". Hata hao waliokuwa wanalazimisha tuamini kuwa Serikali haiwezi kufanya biashara wanaanza kujirudi kwa ku'nationalize' mali zilizopo nchini kwao baada ya kupata somo toka China (usiniambia ni sababu ya 'financial crisis' ilhali chanzo chake ni China kuzalisha mali zilizoua soko la bidhaa za Magharibi).... na kutokana na kutoa pesa zake itachukua muda wa miaka 8 kabla ya mkataba wake kuisha.
kama ni chafu, uza. uza hata masoko mengine yaliyobaki kama tandare,buguruni, magomeni, kimala na mengine. tunahitaji majengo mazuri, mapya, yenye usafi, vyoo vizuri, na wauzaji wazuri. sio unanunua kitu anayekuuzia ameenda ****** hajanawa mikono, anatoka jasho, nguo chafu, chini tope hajafanya usafi hopeless. ni bora tuuze na ikiwezekana wenye uwezo wajenge majengo mazuri ya kisasa ya masoko. hatuwezi kubakia na mambo ya kizamani ili kuwafurahisha machinga!
Kama nimeelewa vizuri, barua iliyoandikwa na manucipal ya Temeke imeweka wazi kuwa M/s Technical Developer alishinda zabuni ya kuendesha soko hilo. Hii ina maanisha kuwa, mwekezaji huyo alishindanishwa na wengine na akashinda zabuni hiyo. Vile vile, mwekezaji atatakiwa kujenga maduka kuzunguka soko kwa gharama zake mwenyewe na atalikodi soko hilo kwa wafanya biashara kwa kipindi cha miaka 8.
Kwa mtazamo wangu, hatua hiyo inaashiria kuwa;
1. Manucipal ya Temeke imeona ni rahisi kwao kutumia kampuni binafsi kuendesha soko, na wao kupata kodi kutoka kwake badala ya kulisimamia yenyewe. Hii ni njia mbadala ya kuendesha soko, na inakubalika endapo taratibu za kufanya hivyo zimetumika vizuri
2. Manucipal haina/haitaki kutumia pesa zake kujenga soko hilo (200mil). Nadhani ni uamuzi mzuri, hasa kama Manucipal ina lengo la kutumia pesa zake kuendeleza miundombinu mingine kama barabara, hospitali, n.k. badala ya kuziweka katika ujenzi wa soko
3. Muda wa miaka 8 uliotolewa si mwingi kiasi cha kuzua wasiwasi. Ni muda mfupi ambapo mwekezaji anatarajiwa kuwa amemaliza shughuli zake katika soko hilo. Inawezekana baada ya muda huo, mwekezaji mwingine au yule yule akapewa tena muda wa ziada wa kuendesha soko hilo (endapo atakuwa amefanya hivyo kwa ufanisi katika kipindi cha kwanza). Fursa hii inaipa Manucipal uwezo wa kuendelea kusimamia soko endapo itathibitika kuwa mwekezaji aliemaliza muda wake, hakuweza kufikia malengo yaliyotarajiwa na Manucipal
4. Ni namna ya serikali za mitaa kushirikiana na wananchi katika shughuli za maendeleo. Mwendelezaji wa soko ataisaidia Manucipal kuendeleza na kusimamia shughuli zake
5. Sioni madhara makubwa yanayoweza kuwakumba wafanya biashara katika soko hilo. Usumbufu utakaotokea unaweza ukawa katika kipindi cha ujenzi tu. Ila mwekezaji atawahitaji wafanya biashara hao kwa kuwa ndio wateja alionao sasa, kuliko kutafuta wengine wapya. Utaratibu atakaoutumia katika kuwapangishia sehemu za biashara upya unaweza kuwa suala la mjadala.
Nadhani serikali ikiwa inatumia njia kama hizi itaongeza ufanisi kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa serikali inajaribu kufanya kila kitu bila kushirikiana na wadau wengine. MAdhara yake ni kushindwa kwa miradi mingi (hata iliyo mizuri)
".....tz bwana........kama tumerogwa"
Hivi Mhe. Raisi anajua hili au kama kawaida funika kombe? Na hiyo bajeti waliyoweka ya soko imeenda wapi? Hivi Kikwete yupo kweli na anajali wa-Tanzania?
Msalie Mtume, Duh! kamanda kauli zingine zinatisha kwani hazina ukweli wowote na zinaashiria chuki...Lusajo, Kikwete hahusiki na kuuzwa kwa soko la Tandika na sidhani kama anahusika na chochote kinachoendelea ndani ya nchi yetu. Amewekwa pale Ikulu kama picha tu wakati mafisadi wakifanya mavitu yao. Wanauza soko hata kumtaja ni nani aliyeuziwa wanaogopa wanaitaja kampuni!!! Sasa hiyi kampuni si ina wamiliki? Kwa nini majina yao yasianikwe hadharani!? Kazi kweli kweli!!!
Lusajo, Kikwete hahusiki na kuuzwa kwa soko la Tandika na sidhani kama anahusika na chochote kinachoendelea ndani ya nchi yetu. Amewekwa pale Ikulu kama picha tu wakati mafisadi wakifanya mavitu yao. Wanauza soko hata kumtaja ni nani aliyeuziwa wanaogopa wanaitaja kampuni!!! Sasa hiyi kampuni si ina wamiliki? Kwa nini majina yao yasianikwe hadharani!? Kazi kweli kweli!!!
Lusajo, Kikwete hahusiki na kuuzwa kwa soko la Tandika na sidhani kama anahusika na chochote kinachoendelea ndani ya nchi yetu. Amewekwa pale Ikulu kama picha tu wakati mafisadi wakifanya mavitu yao. Wanauza soko hata kumtaja ni nani aliyeuziwa wanaogopa wanaitaja kampuni!!! Sasa hiyi kampuni si ina wamiliki? Kwa nini majina yao yasianikwe hadharani!? Kazi kweli kweli!!!