Soko la Tandale kama dampo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
BAADHI ya wafanyabiashara katika Soko la Tandale, wameushutumu uongozi wa soko hilo kwa kushindwa kusimamia vyema usafi wa mazingira ya soko hilo, hali inayohatarisha maisha ya watumiaji wake.

Wakizungumza na HABARILEO sokoni hapo jana, wafanyabiashara walisema licha ya kutozwa ushuru wa kufanya biashara mahali hapo, shughuli ya usafi hasa uzoaji wa taka
imekuwa haipewi kipaumbele cha kutosha na wahusika.

“Ni kawaida kutozwa ushuru sokoni hapa kila siku iendayo kwa Mungu, lakini cha kushangaza uchafu umejazana tele kila sehemu, sasa sijui nini maana ya wao kututoza
ushuru huo huku usafi hawafanyiki,” alisemammoja wa wafanyabiashara wa viazi mahali hapo aliyejitambulisha kwa jina la Peter Mapunda.

Akizungumzia kukerwa na hali hiyo mwana mama anayeuza ndizi kwa jumla sokoni hapo aliyejitambulisha kwa jina moja la mama Shayo, alisema amekuwa akitozwa ushuru wa kushusha mzigo mahali hapo kila anapoingiza mzigo mpya, lakini hajawahi kuona
mazingira ya soko hilo yakiwa safi.

“Tunaweza hata tukapata magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na mengine, usafi hawafanyi wanachojali wao ni kututoza ushuru, ni vyema manispaa (Kinondoni) ikaliangalia jambo hili kwa makini na kulidhibiti kabla hatujapata madhara mahali hapa,” aliongeza
mama Shayo.
 
Back
Top Bottom