Soko la samaki la feri laungua majiko 48 yateketea.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
4178942.jpg

Picha inaonyesha jinsi gani moto ulivyoharibu miundo mbinu ya soko Thursday, March 04, 2010 2:58 PM
Soko la kukaangia samaki la Feri lililopo katika kivuko cha Kigamboni limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo. Soko la kukaangia samaki la Feri lililopo katika kivuko cha Kigamboni limeteketea usiku wa kuamkia leo , akizungumza shuhuda mmoja aliyekuwepo katika tukio hilo aliye jitaja kwa jina la Jafari Juma alisema kuwa soko hilo liliungua majira ya saa 4 usiku wakati wakaanga samaki wengi walikuwa tayari wameondoka.

Mmoja wa wakaanga samaki alikuwa anawahi kuondoka ndipo alipo chukua mafuta yaliyokuwa na uchafu wa samaki ambao tayari walikuwa wamekaangwa akarushia kwenye jiko ndipo mlipuko ukatokea mripuko huo umesababisha hasara ya Majiko 48 kuungua.

Kutokana na moto huo kuunguza soko hilo vibaka na baadhi ya wavuvi wameiba vitu mbalimbali vikiwemo vyuma chakavu vilivyo salia katika janga hilo.
 
MOTO WATEKETEZA SOKO LA SAMAKI FERI


pix.gif
MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza baadhi ya majiko ya kukaushia samaki katika soko la Feri lililoko Kivukoni jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
Akiongelea tukio hilo, Meya wa Wilaya ya Ilala, Abu Juma, alisema jana majira ya saa tatu na nusu usiku alipata tarifa za moto kuteketeza soko hilo ambapo alikwenda kushuhudia tukio na kukuta kikosi cha Zimamoto kikiendelea na uzimaji wa moto huo.
Alisema chanzo cha moto huo hakikufahamika mara moja isipokuwa alihisi baadhi ya watumiaji wa majiko katika soko hilo hawakuyazima baada ya kuyatumia, hususani jiko Namba Moja ambako moto unadaiwa kuanzia.


Jengo la soko hilo lilivyoteketea kwa moto.


Meya wa Wilaya ya Ilala Abu Juma (katikati) akijaribu kuelezea chanzo cha moto huo kwa waandishi wa habari.


Baadhi ya askari na raia wakishudia juhudi za kuuzima moto huo.


Shughuli ya kuuzima moto ikiendelea.​
 
Back
Top Bottom