Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

Amesema, kwa vile kuuza hisa kunahusisha kukusanya fedha from public, lazima pia na uthibiti, ili kulinda fedha za wananchi, yasije kutokea kama yale ya kampuni ya NICO, amesema hisa za kampuni ya NICO zimeondolewa sokoni, baada ya kubaini udanganyifu!.
 
mimi napenda sana kuwekeza kwenye ununuzi wa hisa ila tu bado sijapata elimu stahili na kila nikijitahd kusoma mwenyewe nakutana na maswali magumu ambayo siwez kujijibu sijui ninawezaje kupata elimu juu ya umiliki wa hisa.
 
Ili kulinda fedha za wananchi, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMCA), italidhibiti soko hili na kwa kuanzia, imewateua washauri maalum wa biashara wanaoitwa "nomads", kuipitia prospectus ya kampuni inayotaka kuingia kwenye soko dogo, ili kuthibitisha, hiyo biashara wanayoitafutia mtaji, ni biashara sala na itazalisha faida ili wanahisa wafaidike na uwekezaji wao!.

Akatolea mfano ukileta kapuni yenye bussiness plan ya kutafuta mtaji wa kuanzisha mradi wa kutafuta dhahabu Zanzibar, hautakubaliwa, kwa sababu inafahamika fika Zanzibar hakuna dhahabu!.
 
Amesema, masharti ya kuiingiza kampuni kwenye soko hili la kukuza wajasiliamali wadogo na wakati, ni pamoja na kuwa na mtaji wa kuanzia shilingi milioni 200 tuu!. Japo hapa hakufafanua kama initial capital hii ya mtaji wa milioni 200, ni hard cash, assets au hata ile "guarantee".

Hii inamaani ukiwa tuu na wazo zuri la biashara, hata kama huna hata senti tano, unakwenda kusajili kampuni, unaandaa "bussiness plan" kuonesha ukipata mtaji wa kiasi kadhaa, una take off!. Yaani "capital by guarantee". Unapatia huyo "nomad" hiyo bussiness plan yako, anaipitia, akijiridhisha italipa, unasajiliwa, unauza hisa, unapatiwa mtaji!.
 
Hii inamaanisha hata mimi na kikampuni changu cha PPR, nikiangalia assets zatu, zile equipments zetu tuu peke yake, zimeishazidi mtaji wa milioni 200!, inamaana sasa PPR inaweza kuwa listed, tukaanzisha TV yetu, na tukairusha jf hewani free to air 24/7!.

Au JF, ikaandaa business plan yake kuwa inataka kufanya nini, mfano tukianzisha gazeti, litakuwa hit!, tukianzisha TV na Redio, itafunga kazi, hebu imagine siku ya kipindi cha Mzee Mwanakijiji, Mchambuzi, kina Nguruvi 3 wakizichambua siasa za bongo!, who can afford to miss!, tukawa listed, tukapata mtaji, tukatake off, kuna TV gani nyingine bongo inaweza kushindana na sisi?.
 
Magabe amemalizia kwa kutoa wito kwa Watanzania, wenye vikampuni vidogo vidogo, kuacha ubinafsi, bali wa float shares wapate mitaji mikubwa, wapae kibiashara!.

Amesisitiza hii ni opportunity adimu, tuichangamkie!.

Kipindi kimekwisha!

Pasco
 
Mkuu Pasco hapo kwenye hiyo 200m ndipo kazi inapoanzia, kwani vijikampuni vyetu vidogovidogo initial capital (kwa mujibu wao) ni kiasi gani?
Mkuu Rock City, jamaa hakufafanua zaidi kuhusu huu mtaji wa kwanza wa milioni 200!.

Unaweza kuwa ni "capital by guarantee!" kuwa wewe mkulima, unamiliki kiwanja, una nyumba, una assets etc. Mfano mimi naweza kujifanyia "self valuation" kuwa "thamani ya Pasco wa jf kwenye markert value ni TZS Milioni 500"
 
Hii inamaanisha hata mimi na kikampuni changu cha PPR, nikiangalia assets zatu, zile equipments zetu tuu peke yake, zimeishazidi mtaji wa milioni 200!, inamaana sasa PPR inaweza kuwa listed, tukaanzisha TV yetu, na tukairusha jf hewani free to air 24/7!.

Au JF, ikaandaa business plan yake kuwa inataka kufanya nini, mfano tukianzisha gazeti, litakuwa hit!, tukianzisha TV na Redio, itafunga kazi, hebu imagine siku ya kipindi cha Mzee Mwanakijiji, Mchambuzi, kina Nguruvi 3 wakizichambua siasa za bongo!, who can afford to miss!, tukawa listed, tukapata mtaji, tukatake off, kuna TV gani nyingine bongo inaweza kushindana na sisi?.

Kiongozi hizi idea nna imani iko siku watazifanyia kazi na itabidi ulipwe......nimeipenda sana!
 
mimi napenda sana kuwekeza kwenye ununuzi wa hisa ila tu bado sijapata elimu stahili na kila nikijitahd kusoma mwenyewe nakutana na maswali magumu ambayo siwez kujijibu sijui ninawezaje kupata elimu juu ya umiliki wa hisa.

GFsonwin, naungana na wewe, Tanzania tuna tatizo kubwa sana la elimu ya uwekezaji!. Mfano kumetokea fursa kibao za making good big money, zikiwepo "debt conversions" "Government Bonds" EPA etc, benefisiaries wakubwa ni wenzetu wazungu na wahindi!. Mfano hili libenki letu kubwa la CRDB, limamilikiwa kama ifuatavyo

CRDB BANK LIMITED is owned by over 11,000 shareholders under the following major groups (by value of shares):
Private individuals
37.0
Co operatives
14.0​
Companies
10.2
DANIDA investment fund
30.0
Parastatals (NIC & PPF)
8.8
TOTAL
100.0
[FONT=Arial, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif][/FONT]
Katika umiliki huu, Wazungu wa Danida, wanamili 30% peke yao!, vyama vya ushirika ambao hiyo ndio ilikuwa benki yao, wanamili asilimia 14% tuu!. Makampuni makubwa yenye mitaji ya nguvu kama pensio funds, ambayo yangeweza kununua shares nyingi, ushirikiano wa PPF na NIC, wanamili asilimia 8% tuu!.

Utashangaa kukuta majority ya wamiliki wa hizo shares asilimia 37%, na yale makampuni yanayomiliki asilimia 10%, unaweza kujikuta karibu wote ni wahindi, wazungu na makampuni ya kigeni!.

Tunajidai tuu benki letu hili, huku wanaikula faida ya gawio la mamilioni ya faida ni wazungu, huku sisi wamatumbi tukiendelea tuu kuwandundulizia tujisenti twetu wao wakizidi kuneemeka!.

Ni kufuatia elimu hii duni ya mambo ya Hisa, DSE wamezindua kampeni kamambe ya uelimishaji!.

Pasco.
 
Hii nimeipenda, je hao SME's wanapaswa kujiunga kwanza na kituo cha uwekezaji kama vile TIC au vinginevyo?
No, hakuna shurti la kujiunga na TIC, sharti ni moja tuu, "uwe na business idea, au business plan inayotekelezeka, na mtaji wa milioni 200! bei ni capita by assets au guarantee!.
Pasco.
 
Bwana Magabe, anafafanua kuwa lengo la kufungua soko hilo dogo lenye masharti nafuu, ili Watanzania wengi zaidi wenye vipato vidogo na vya kati, waweza kupata fursa za kutajirika kupitia soko la hisa la Dar es Salaam.

Utatajirika bila biashara uliyowekeza kufanya vizuri? Faida kwenye hisa (i) Mgawo wa faida (dividend) (ii) Kuongezeka kwa thamani ya hisa (increase in intrinsic value) kwa kuangalia ufanisi wa mbeleni
 
Amesema, masharti ya kuiingiza kampuni kwenye soko hili la kukuza wajasiliamali wadogo na wakati, ni pamoja na kuwa na mtaji wa kuanzia shilingi milioni 200 tuu!. Japo hapa hakufafanua kama initial capital hii ya mtaji wa milioni 200, ni hard cash, assets au hata ile "guarantee".

Hii inamaani ukiwa tuu na wazo zuri la biashara, hata kama huna hata senti tano, unakwenda kusajili kampuni, unaandaa "bussiness plan" kuonesha ukipata mtaji wa kiasi kadhaa, una take off!. Yaani "capital by guarantee". Unapatia huyo "nomad" hiyo bussiness plan yako, anaipitia, akijiridhisha italipa, unasajiliwa, unauza hisa, unapatiwa mtaji!.

Hiyo ni nzuri sana, watu wengi huwa wanalalamika kwamba wana mawazo mazuri ila tatizo ni mtaji, huu utakua ni ufumbuzi wa hilo tatizo.

Angalizo, pawe na wataalamu wa kupima na kuangalia uhalisia na utekelezaji wa hayo mawazo kabla watu hawajavunja vibubu kurushia akiba zao huko.

Thanks mkuu Pasco
 
Last edited by a moderator:
Ni kitu kizuri ila Tuombee tu wajanja wa Mujini wasiingilie hilo deal, vinginevyo itakuwa majanga tu kama ilivyokuwa katika Mabilioni ya JK, EPA, Fedha za ICS, Stimulus Package....n.k
Nchi ngumu hiii !!!
 
Halafu nadhani DSE watengeneze utaratibu wa kuzifuatilia hizo kampuni zitakazo pewa hizo fedha kuona trend yake itakuwaje huko baadae, vinginevyo kwa jinsi ninavyojua Wajanja wa Mujini watatengeneza vikampuni vya chap chap ili mradi tu Wakwarue hizo pesa za mitaji ili waendelee kula Bata hapa mujini.

Wapo watu hapa mjini kazi yao ni hio tu, kunusa deal lipo wapi na kulichangamkia fastaaa
 
Utatajirika bila biashara uliyowekeza kufanya vizuri? Faida kwenye hisa (i) Mgawo wa faida (dividend) (ii) Kuongezeka kwa thamani ya hisa (increase in intrinsic value) kwa kuangalia ufanisi wa mbeleni
Mkuu Ndachuwa, kweli Watanzania ni masikini sana wa mawazo, ndio maana kila uchao, wazungu wanakuja kujivunia mihela na kuhamishia kwao!.

Hebe angalia, juzi nilikuwa Bahi, kuna Mgogo fulani alikuwa na ngombe 800 wake 4 akiishi nyumba ya tembe!, ana watoto lukiki, kazi yao ni kuchunga ng'ombe!. Sasa ameshauriwa kuuza ngombe 600, amejenga nyumba 4 za kisasa kwa kila mke, amenunua magari 4 ya kisasa kwa kila nyumba, yeye naye ana gari lake, ana trekta, ameajiri wafanyakazi, sasa watoto wanakwenda shule kwa magari!.

Mtu kama huyu angapatiwa alimu ya hisa, akawekeza kwenye hisa, saa anakaa miguu juu, anakula tuu gawio!.

Ziko familia chache za wabongo, wao walifunguka macho zamani, wakanunua hisa kwenye IPO, leo watoto wao na watoto wa watoto wao, tangu wanazaliwa, mpaka watakapo kwenda kaburini, tayari, ni matajiri wa kutupa, hawahitaji kufanya kazi to earn a living, wanaweza kuishi maisha ya raha mustarehe huku wakitumbua maraha bila kufilisika!, ila pia ndio kwanza, wanaendelea kumiliki hisa na hilo gawio wanalitumia kuendelea kununua hisa!.

Kama sisi maskini hatutaungana kumiliki uchumi wetu, amini asiamini, watoto wetu, na watoto wa watoto wetu, wataishia kuwa wapangaji milele ndani ya nchi yao!. Wenye nacho, wanaongezewa!, wasio nacho, wananyanganywa hicho kidogo walichonacho na kuongezwa kwa wenye nacho!.

DSE sasa, ndio imetupa fursa akini sisi nasi tuingie kwenye kundi la wenye nacho, kwa sisi masikini kichangia hivi hivi katika umasikini wetu, tuwezeshane, tuweze!.
Pasco.
 
Back
Top Bottom