Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

Mimi nilinunua hisa za Twiga Cement kwa Tshs. 435 kwa kila hisa kabla ya kuingizwa DSE. Kwa sasa hisa moja ni Tshs. 1,960.

Tatizo ni kuwa hisa walizokuwa wanauza zilikuwa kidogo kuliko demand hivyo watu wote tulirudishiwa pesa zetu na kupewa only around 40 % ya hisa ulizotolea pesa. Gawiwo huwa linabadilika kila mwaka kutokana na maamuzi ya wakubwa na faida iliyopatikana.

Hakuna constant gawio kwa kila mwaka.
 
Wadau naomba kujua biashara ya hisa inakwendaje na jinsi gani naweza nufaika nayo, pia hisa za kampuni gan now zpo high kwa kuanzia
 
Wadau naomba kujua biashara ya hisa inakwendaje na jinsi gani naweza nufaika nayo, pia hisa za kampuni gan now zpo high kwa kuanzia

Kwa nini unaulizia hisa zilizopo juu DSE? Wewe unazo za kampuni gani? Kama huna basi, na unataka kufaidika (actually hata hasara unaweza kupata. Ref TOL Gases Limited) na hii biashara wakati kipato chako ni cha kawaida kama sisi basi wakati wa kununua hisa ni wakati wa IPO (initial Public Offering).

Wakati huu hisa zinakuwa hazijaenda kwenye secondary Market yaani DSE. Wewe utanunua kwa mawakala tu kama Banks.

Huku DSE kunahitaji utaalamu na unashauriwa uwaone washauri wako wa masuala ya uwekezaji.
 
Wadau naomba kujua biashara ya hisa inakwendaje na jinsi gani naweza nufaika nayo, pia hisa za kampuni gan now zpo high kwa kuanzia

Kwa nini unaulizia hisa zilizopo juu DSE? Wewe unazo za kampuni gani? Kama huna basi, na unataka kufaidika (actually hata hasara unaweza kupata. Ref TOL Gases Limited) na hii biashara wakati kipato chako ni cha kawaida kama sisi basi wakati wa kununua hisa ni wakati wa IPO (initial Public Offering). Wakati huu hisa zinakuwa hazijaenda kwenye secondary Market yaani DSE. Wewe utanunua kwa mawakala tu kama Banks.

Huku DSE kunahitaji utaalamu na unashauriwa uwaone washauri wako wa masuala ya uwekezaji.

Nmekusoma
 
Nidondoshee kdogo bas hayo ya nico yakoje

Gawio halitolewi, kampuni ina hasara, na mahesabu yao hayaeleweki (hayatolewi kwa wakati) mpaka BODI imepigwa mkwara na CMSA.

Sasa issue ipo kwa wale wanaotaka kuuza hisa zao DSE, kwani kibali kinachoruhusu kampuni kufanya biashara huko kimezuiwa
 
Jibu rahisi mngemshauri mleta mada akapate ushauru kwa "Brokers" badala ya kumkatisha tamaa na kampuni zilizofeli kama NICO na TOL.

Binafsi ningemshauri hisa kama za CRDB bado hazijapanda sana bei na "future prospect " ni nzuri kama hawajanunua Tanzania Government bond.

Kama wana Government Bond, anything can happen because mwelekeo wa GDP ya Tanzania haielekea Tanzania itakuwa na uwezo wa kulipa madeni yake.
 
kama upo dar nenda jengo la twiga ambapo ipo DSE na benki ya twiga bancorp bank HQ au IPS building pale posta mpya kuna ma brokers kibao wa hisa au wa ulizie orbit au chui watakushauri zaidi..
 
Jibu rahisi mngemshauri mleta mada akapate ushauru kwa "Brokers" badala ya kumkatisha tamaa na kampuni zilizofeli kama NICO na TOL.

Binafsi ningemshauri hisa kama za CRDB bado hazijapanda sana bei na "future prospect " ni nzuri kama hawajanunua Tanzania Government bond. Kama wana Government Bond, anything can happen because mwelekeo wa GDP ya Tanzania haielekea Tanzania itakuwa na uwezo wa kulipa madeni yake

You are right NDACHUWA, ndi maana ukisoma post no 2, ameambiwa awaone investmest advisors kabla ya kuingis DSE, na ni ushauri unaotolewa na CMSA pia kabla ya kununua hisa. Hilo suala ya kumuonyesha makampuni yaliyopata hasara ni la msingi sana kwani vyema mtu akijua pande mbili za shilingi kuna nini. na ndio maana amekuwa interested kujua zaidi kilichotekea.

Kuna watu wakisikia hisa wanajua ni suala la faida tu na hakuna hasara kitu ambacho ni very wrong. Cha msingi ni kuchagua hayo makampuni ka uangalifu na kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Kuhusu hisa za CRDB, ni kweli bado zipo chini sikatai, lakini ni vyema ukajua zimecheza kwenye hiyo bei kwa muda gani? Kuna watu wanataka kununua hisa, si ili wawekeze fedha zao na kupata magawio (dividends) bali waweze kuziuza ndani ya muda mfupi ili watengeneze faida, ndio maana akaambiwa kama yeye ni mmoja wao ni vyema akasubiri wakati wa IPO.

Nimesikia kuna kampuni ya RICHLAND RESOURCES (Tanzanite One- as it then was) inaingia sokoni, issue ni kwamba wananchi wa kawaida watamudu gharama (hisa moja itauzwa kwa sh.ngapi?)
 
Jibu rahisi mngemshauri mleta mada akapate ushauru kwa "Brokers" badala ya kumkatisha tamaa na kampuni zilizofeli kama NICO na TOL.

Binafsi ningemshauri hisa kama za CRDB bado hazijapanda sana bei na "future prospect " ni nzuri kama hawajanunua Tanzania Government bond. Kama wana Government Bond, anything can happen because mwelekeo wa GDP ya Tanzania haielekea Tanzania itakuwa na uwezo wa kulipa madeni yake

You are right NDACHUWA, ndi maana ukisoma post no 2, ameambiwa awaone investmest advisors kabla ya kuingis DSE, na ni ushauri unaotolewa na CMSA pia kabla ya kununua hisa. Hilo suala ya kumuonyesha makampuni yaliyopata hasara ni la msingi sana kwani vyema mtu akijua pande mbili za shilingi kuna nini. na ndio maana amekuwa interested kujua zaidi kilichotekea.

Kuna watu wakisikia hisa wanajua ni suala la faida tu na hakuna hasara kitu ambacho ni very wrong. Cha msingi ni kuchagua hayo makampuni ka uangalifu na kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Kuhusu hisa za CRDB, ni kweli bado zipo chini sikatai, lakini ni vyema ukajua zimecheza kwenye hiyo bei kwa muda gani? Kuna watu wanataka kununua hisa, si ili wawekeze fedha zao na kupata magawio (dividends) bali waweze kuziuza ndani ya muda mfupi ili watengeneze faida, ndio maana akaambiwa kama yeye ni mmoja wao ni vyema akasubiri wakati wa IPO.

Nimesikia kuna kampuni ya RICHLAND RESOURCES (Tanzanite One- as it then was) inaingia sokoni, issue ni kwamba wananchi wa kawaida watamudu gharama (hisa moja itauzwa kwa sh.ngapi?)[/QUOTE]

Hapo somo limeingia wadau,, thanks all
 
LEO nitazungumzia suala la dhamana. Dhamana ina wigo mpana sana ikihusisha aina zifuatazo: hisa, vipande, hatifungani na amana za serikali.

Katika mada ya leo nitapenda kuaangazia aina mojawapo ya dhamana ambayo ni hisa na wakati ujao nitazungumzia dhamana nyingine.

Mbali na kuzungumzia suala la hisa leo, wajasiriamali wanashauriwa kusoma baadhi ya vitabu ambavyo waandishi wameandika mada mbalimbali za ujasiriamali ikiwamo uwekezaji katika hisa.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 84 ya Watanzania wakiwamo wasomi na wengine ambao hawajabahatika kusoma hawajui au hawana elimu kuhusu kuwekeza katika hisa.

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba mada hii haijawekwa katika mitaala mbalimbali ya elimu. Kama ipo basi wale wanaostahili kuifundisha ama hawana uelewa mpana na uzoefu wa kuwawezesha wanafunzi wao kufahamu umuhimu wake katika medani za kiuchumi.

Hisa inaelezeka kwa namna mbalimbali, kwa ujumla wake hisa ni mali, rasilimali, kitegauchumi, hati miliki, biashara, dhamana ya mkopo, ni akiba, ni fedha iliyohifadhiwa, na ni mtaji.

Katika mtazamo wa kibiashara, hisa ni uwekezaji wa mtaji au fedha ambayo imewekezwa na mfanyakazi, mkulima, mfanyabiashara au mtu mwingine ambaye ameamua kununua hisa kutoka katika kampuni fulani kwa lengo la kupata faida kupitia gawio na ongezeko la bei ya hisa husika.

Uwekezaji katika hisa kama biashara nyingine unahitaji umakini na upembuzi yakinifu. Kufanya upembuzi wa wapi uwekeze fedha zako na wapi ununue hisa kwa msingi wa kupata faida.

Mjasiriamali au watu wengine wanaweza kufanya upembuzi yakinifu, lakini kama watu makundi niliyoyataja hapo juu wana uelewa wa kutosha na mbinu za kusoma taarifa mbalimbali za kampuni ambayo unakusudia kununua hisa. Kwa mfano, unapaswa kufanya upepenuzi yakinifu wa taarifa za fedha na hali halisi ya kampuni husika
katika soko la hisa.

Kwa upande mwingine, washauri wataalam wana ujuzi wa kufanya upembuzi yakinifu katika masuala ya uwekezaji kwenye soko la mitaji ambao wa wanapatikana kwenye masoko ya hisa katika jengo la Habour-view, mtaa wa Samora, jijini Dar es Salaam.
Ununuzi wa hisa unaweza kufanywa katika soko la awali mathalani pale kampuni inapotangaza kuuza hisa zake.

Baada ya kampuni kutangaza kuuza hisa, watu wananunua kwa thamani halisi, lakini baadaye zinauzwa katika soko la hisa ambako thamani ya hisa inabadilika kuendana na hali ya soko.

Tukiangalia upande wa kampuni, mpaka Agosti, mwaka huu kulikuwa na zaidi ya kampuni 16 zilizosajiliwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE). Kampuni 11 ni za kizalendo na kampuni sita ni za nje.

Kwa mujibu wa Emilian (2010), asilimia 0.39 tu ya Watanzania wamewekeza kwenye soko la hisa. Kutokana na tatizo hilo, bado ni tatizo kubwa kwa Watanzania na kwa jicho la pili ni fursa kubwa kwa wajasiriamali, wafanyakazi na wanafunzi kuwekeza katika hisa.

Uwekezaji katika hisa unachangamoto zake ikiwzmo kushuka kwa bei ya hisa, kukosa gawio, mfumuko wa bei, viwango vya riba, kukosa wanunuzi kutokana na ukwasi na hitilafu mbalimbali.

Kwa hali ya kawaida uwekezaji katika hisa una faida nyingi kuliko changamoto kwa mfano, kupata gawio baada ya kampuni kutengeneza faida, ongezeko la thamani ya hisa, punguzo la kodi ya zuio kwenye gawio.

Katika masuala ya hisa, hakuna kodi kwenye ongezeko la thamani, urahisi wa kuuza na kununua hisa, na ukiwekeza katika hisa unapata muda wa kufanya shughuli nyingine. Kwa upande mwingine hisa ni dhamana ya kupata mkopo, hisa ni urithi mzuri, ukijiwekea utaratibu wa kutenga asilimia fulani ya pato lako kutoka kwenye mshahara ama biashara kwa ajili ya kununua hisa ni uamuzi mzuri, na hisa pia ni utajiri.

Unapowekeza katika hisa jihadhari na makosa yafuatayo; kununua au kuuza hisa zako bila utafiti, kutokujua tofauti ya thamani ya bei, kununua kwa kuangalia jina na umaarufu wa kampuni, kutokua na malengo maalum, kununua kwa kuwa bei ni rahisi, kukosa maarifa au kutozingatia elimu ya fedha, hisa na uwekezaji, na kuwekeza fedha nyingi kwenye kampuni moja.
 
Mimi ninazo za NICO,frankly speaking it was a bad investment

"kununua au kuuza hisa zako bila utafiti, kutokujua tofauti ya thamani ya bei, kununua kwa kuangalia jina na umaarufu wa kampuni, kutokua na malengo maalum, kununua kwa kuwa bei ni rahisi, kukosa maarifa au kutozingatia elimu ya fedha, hisa na uwekezaji, na kuwekeza fedha nyingi kwenye kampuni moja..."nukuu!!
 
Samaritan, Kuna ada yeyote inatozwa mtu akihitaji ushauri toka kwa wataalam walioko hapo harbours tower?

Samahani mkuu, nimechelewa kujibu swali lako mambo ya mwaka mpya, nimeku PM namba ya jamaa mojawapo yuko Dar wasiliana nae atakupa maelekezo na kujibu maswali yako bila malipo.

Asante
 
Hi thread nimeipata cku zimeenda kidogo! Ila napenda kujua Kwa wale ambao wanamitaji midogo! Wafanye nini ili kuchangamukia hizi furusa!

Asante!!
 
Back
Top Bottom