'Soko kuu la Ubungo' limeidhinishwa?

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
Kwa kipindi kirefu sana tumeshuhudia kuibuka kwa soko la bidhaa mbalimbali eneo la ubungo.Soko hili lilianza kama utani.Wachuuzi wa nguo walikuwa wanajipanga na nguo za kuuza kuanzia jioni upande wa mandela road kutazamana na Songas. Nao wachuuzi wa matunda walikuwa wakijipanga pembeni mwa eneo la stendi ya daladala.

Leo hii hatuzungumzii tena wachuuzi wachache.Ubungo imegeuka kuwa soko kubwa lenye biashara za kila aina kuanzia nguo, viatu, neti za=enye ngao, vitabu, cds, vyakula kama kuku, ndizi,chips, mihogo, matunda na samaki wabichi.

Soko hili huanza asubuhi hasa eneo la kuanzia darajani karibu na landmark hotel mpaka eneo linalotizamana na Songas.Kuanzia saa tisa jioni wachuuzi hufurika kuanzia darajani mpaka kwenye mataa, ndani ya kituao cha daladala mpaka mbele ya jengo la tanesco na eneo lote la kituo cha mafuta cha oilcom.

Madhara na usumbufu unaoletwa na soko hili ni mkubwa:
- Njia za waendao kwa miguu zinazibwa zote, waenda kwa miguu tunalazimika kupita katikati ya magari.
- Uchafu wa eneo husika.
- Uwezekano wa kutokea ajali kutokana na biashara kuwepo eneo lisilo rasmi.

Kwa ujumla, eneo hilo ni kero, lazima ujifikirie sana kabla haujaamua kupita hapo.
Biashara katika eneo hili hazifanyiki mafichoni hata kidogo, ni mahali pa wazi panapoonekana.Ninachojiuliza siku zote ni je, soko hilo limehalalishwa na mamlaka husika? waenda kwa miguu wapite wapi kama hili limeshakuwa soko?

Inasikitishwa kuona hali hii ikiendelea kana kwamba nchi haina wenyewe.Nafahamu kuwa wachuuzi wanaokwenda pale kuuza wanatafuta kipato lakini haiyumkiniki kuwa katika mazingira yale ya hatari namna ile na kwa kuwapatia taabu wapita kwa miguu ni sahihi.

Hivi manispaa ya Kinondoni ipo au imelala?:confused:
 
Hii iko wazi sana.
Kweli eneo hilo kwa sasa halifai, pamekuwa ni fujo, wizi, uporaji na kila aina ya ghasia.
Ni kweli wale vijana ni wajasiriamali, lakini serikali inatakiwa kuingiza mkono wake pale kwa kuhakikisha kuwa taratibu za matumizi ya maeneo zinafuatwa.
Mbaya zaidi lile ni eneo la mitambo ya umeme, hivyo risk inakuwa kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom