Soka la bongo! Tutazidi kuwa wasindikizaji mpaka mwisho wa dunia!

Ndiyo mpira huo mkuu, hata huko Brazil na Ulaya timu zinazo heshimika sana na kutwaa ubingwa zishawahi kunyukwa zaidi ya mabao hayo.
 
mfumo wetu mbovu ndio unasababisha soka letu lisikuwe.

huwezi kuwa na wachezaji hao hao wa ligi kuu wanacheza mechi za mchangani kusaidia timu ndogo kule kupanda daraja,hapo hujengi unabomoa tu na kuwazibia nafasi wachezaji wachanga.TFF inatakiwa hiwazuie wachezaji wa ligi kuu kucheza mechi za mchangani na kama timu ya mchangani itakodisha mchezaji wa ligi kuu hio timu ivuliwe ushindi.

kitu kingine timu za secondary zijengewe mashindano ambayo yanatambuliwa rasmi na TFF. Sheria hiwekwe kwamba kila timu ya ligi kuu lazima ichukue wachezaji atleast wawili kutoka mashindano hayo katika usajili wake kila mwaka.
 
Wadau nimeona jana kipindi fulani hivi kwenye capital tv, wenzetu ghana wana kitu km hii coca cola cup, wanasaka vipaji. zile mechi zinaoneshwa live nchi nzima na watu wanawapigia kura wachezaji kupitia simu zao za mkononi, wachezaji wanachujwa mpaka wanabaki 14 tu, hawa wanaingia kwenye academy na ni ya mtu binafsi, kwa kweli kwa mtindo huu ndo maana wenzetu wanaendelea kwenye soka
 
TFF watakuwa wamekusikia mkuu!
 
Back
Top Bottom