Sofina/Janeth na Tuhuma za Rushwa

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Mimi imenishangazwa kusoma habari, kwenye gazeti la Nipashe, za Mh. Janeth Kahama kuwasilisha tuhuma za Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utawala Bora Mh. Sophia Simba (M) kutoa rushwa ya sh. 100,000/- kwa Mh. Rais badala ya kuziwasilisha kwa TAKUKURu. Lakini kingine ambacho kimenishangaza ni habari hiyo kueleza kwamba CCM wamesema kwamba ikibainika kwamba tuhuma hizo ni za kweli hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Mh. Sophia Simba. Kinachonishangaza ni kwamba siamini kwamba huyu Mh. Janeth hajui nani mwenye jukumu la kushughulikia masuala ya rushwa. Hata kama Taasisi hiyo iko chini ya Ofisi ya Rais haimaanishi kwamba tuhuma za rushwa zipilikwe kwa Rais. Je hawa Madakitari kina Hosea watakuwa wanalipwa vijisenti vya bure tu! Lakini kwa upande mwingine nimeshindwa kubaini kipengele cha sheria za makosa ambacho kinasema kwamba mtoa hurwa anatakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu; sijui kuna sheria ya makosa ya rushwa inayowahusu viongozi wa CCEM tu na ile ya raia wengine.

Habari hizi za rushwa kwenye uchaguzi wa viongozi katika jumuia za CCEM zilianza siku nyingi. Ilifika wakati Mh. Rita Mlaki akatangaza kususa kuendeleaa na kugombea uongozi; lakini jamaa wakampoza aendelee na baadaye kumtosa.

Kwa maoni yangu katika malalamiko haya mawili tayari TAKUKURU wanao watu wawili wenye hatia: (1) Anayelalamikiwa/Aliyalalamikiwa kutoa rushwa anaweza kuwa na hatia baada ya kuchunguzwa na kutiwa hatiani; (2) Aliyelalamika atakuwa na hatia iwapo itabainika kwamba aliyelalamikiwa hakujihusisha na kitendo cha kutoa rushwa, kwa maana nyingine atakuwa na hatia ya kusema uwongo kwa madhumuni ya kujinufaisha kwenye uchaguzi. Nashindwa kuelewa kwanini hadi sasa Dr. Hosea hajachukua hatua kwa tuhuma hizi kwani ushahidi uko wazi kabisa kuwatia hatiani mmoja wapo wa watuhumiwa hawa. Haiwezekani Mh. Mbunge akakurupuka tu na kusema hadharani kwamba fulani ametoa rushwa bila kuwa na ushaidi. Kwa nini basi tusiwatie adabu hawa wanaokurupuka kuwachafulia wenzao bila kuwa na ushahidi? Mbona mchezaji akimhadaa Refa kwa kutaka kufunga goli kwa mkono au kujiangusha ili apatiwe penalti hupatiwa sawadi yake, kwanini isiwe vivyo hivyo kwa hawa wanasiass?
 
Mnategemea wajinga kama hawa akina mama wawili ndio walete maendeleo Tanzania?

Inabidi CCM mufike mahali muamke, mtawavumilia hawa wanaoendeleleza migogoro mpaka lini?

Huyo waziri ana muda gani hata wa kutaka kuwa mwenyekiti wa jumuia ya chama? Mtu mmoja anakuwa mbunge, waziri, mwenyekiti wa jumuia, mjumbe wa halmashauri ya CCM nk. Huo muda wanautoa wapi? Ukienda kwenye majimbo yao unakuta yako hoi bin taabani.
 
Back
Top Bottom