Sofia Simba naye ajitangaza kupambana na mafisadi

Hizi ndizo siasa za Tanzania. Waziri Simba kudai anapambana na mafisadi kweli ni kichekesho cha karne. Lakini hatuwezi kushangaa maana alianza Makamba kujipeleka Urambo kujipendekeza kwa Sitta ili ionekane kuwa wako the same page.
Kwa mwendo huu wa Waziri Simba tutajikuta tunamsikia Osama Bin Laden akidai anapambana dhidi ya ughaidi duniani au yule bilionea wa Mexico (Mexican drug lord Joaquin "El Chapo" Guzman Loera) anapambana na Drug Cartels nchini Mexico.

Watanzania bado hawajasahau Simba alivyomzodoa Bw. mengi kuhusu fisadi papa. Upepo unaweza kugeuza mwelekeo lakini watanzania wa sasa hawabadiliki kufuata upepo.
 
Uliyotabiri (Tanzania Daima) J2 iliyopita na angalizo lako kwa wapambanaji (wapambanaji asili) wa ufisadi ndani ya CCM sasa yametimia.

Asante kwa utabiri wako na makala yako elimishi!
 
Huyu mama nadhani anatafuta njia ya kujikosha tu. Huu ni usanii kama anaoufanya Makamba wa kujidai anamfagilia Sitta, wakati alishiriki katika njama za kutaka kumng'oa. Ni vizuri kwamba wanaonyesha unafiki wao ili tuwafahamu zaidi. Sophia Simba hana moral authority ya kuzungumzia ufisadi kwani rekodi yake sio nzuri. Akanushe kwanza madai yaliyotolewa dhidi yake wakati anagombea uongozi wa UWT kwamba alitumia rushwa. Halafu afute kauli yake kuwa Mengi alichemsha alipowataja mafisadi papa. Huyu anafahamika kuwa mtetezi mkubwa wa mafisadi, na sijui kwa nini Kikwete mpaka leo anamwachia aongoze wizara nyeti ya Good Governance! Inashangaza sana.
Tusipoangalia hawa watetezi wakubwa wa mafisadi sasa hivi watajipachika ukamanda wa vita dhidi ya ufisadi na kuanza kuwaita makamanda wa kweli kuwa ndio mafisadi.
Leo nimesoma habari ya Lowassa kwenye MTANZANIA NA TANZANIA DAIMA nikacheka sana. Sasa mafisadi hawa wanabadilisha mbinu ili nao waonekane wanakemea mambo fulani maovu. Katika habari hiyo Lowassa eti anakemea udini na anataka tuwapuuze watu wenye nia ya kupandizika chuki! Hasemi lolote kuhusu ufisadi kwa kuwa anajua yeye na rafiki yake Rostam ni wahusika mkuu. Kwake yeye wanaopandikiza chuki ni wale wanaokemea ufisadi wao! Lakini anasahau kwamba tamaa yao ya kutaka kujilimbikizia mali kwa kuwanyonya wananchi ndiyo inapandikiza chuki zaidi kuliko kitu chochote....
 
Huyu mama ni mnafiki kupita mfano....alipokuwa anawania hiyo nafasi ya uenyekiti alikuwa anatumia magari ya ofisi ya dr hosea kufanyia kampeni, pia alichukuwa pesa za kampeni zaidi ya milioni 200 just for uenyekiti wa uwt.... Hizo pesa alipewa na mfanyabiashara mmoja kwa sasa namuhifadhi ila ni mchaga...... Uongo mtupu...ukishaona nundu ya mwezio huwezi kujitoa

Huyu Mama na yule mwenzie Mama Kahama wote walikuwa na pesa chafu!
Huyu akichukua za mafisadi papa na mwingine alichukua za mafisadi nyangumi! Ila mwinzie alimzidi kete kutokea kwenye mlango wa Mkulu!
 
Huyu mama ni m-pambanaji na amedhamiria kupinga ufisadi kwa msio mjua mama Simba hanunuliki ni mtu wa msimamo na hateteleki.

Tatizo ili mtu awe mpinga ufisadi lazima awe na surname Mwakyembe, Selelii, Kilango, sendeka, kimaro et al. Mnaibinafsisha vita ya ufisadi kalabagho!
.

Humjui Sofia Simba wewe.

Je angekuwa mpinga ufisadi basi asingeporomosha matusi na kashfa ikiwa pamoja na kutumia Usalama kumfedhehesha mgombea mwenzake Mama kahama.

Hakika mama huyu ninavyomjua mimi toka akiwa Mke wa Mh .... Pesa alizotumia kwenye kampeni ya UWT lazima awe amechota pahala. yeye mwenyewe hana ubavu wa kuzipata kwanza kwa biashara gani.

Huyu ni mwanasiasa kama alivyo makamba. Penye pesa nae yupo. hakuna kwaheri
 
Na asiye fisadi NCHI hii awe wa kwanza kumrushia jiwe mama huyu "jasiri".

Anza wewe na mawe yako!!

Huyu mama Akiwa Bungeni wabunge wenzie wakiwa wanapinga mfuko wa fisadi mama Mkapa (EOTF) Kuhamishwa Ikulu, yeye alisimama kidete kutete mfuko huo ili aondoke nao mama Mkapa akitoka Ikulu! Ndo na huyu Mama Salma amekuja na Mfuko wake mwingine WAMA!
 
Anza wewe na mawe yako!!

Huyu mama Akiwa Bungeni wabunge wenzie wakiwa wanapinga mfuko wa fisadi mama Mkapa (EOTF) Kuhamishwa Ikulu, yeye alisimama kidete kutete mfuko huo ili aondoke nao mama Mkapa akitoka Ikulu! Ndo na huyu Mama Salma amekuja na Mfuko wake mwingine WAMA!
Hapo ufisadi wake ni upi? Unazielewa taratibu, umiliki wa mifuko hii?
 
wala siomaneno yakehayo katumwa kama alivyotumwa ngomalemwiru. na bado watumwa sana.jana gwiji la mafisadi limeonekana katika luninga linachangia ujenzi wa kanisa na viongozi wa kanisa wanafurhia pesa ambazo wanajua fika zimetoka wapi. inasikitisha. imaumiza na inatesa sana. HIVKWELI MAFISADI WATAISHA KWELI????!!!!!
 
Nadhani sasa umefika wakati wa hao viongozi wa ki-dini wanapo-wa invite kushiriki katika mambo mbalimbali ya kiroho (kuanzia harambee hadi kusimikana wakfu).. viongozi wenye mienendo tata katika taifa letu kutoa pia muda kwa waumini wao kumuuliza maswali na kuhitaji ufafanuzi katika masuala mbalimbali yanayomuhusu...siamini kama kuna sehemu yoyote yenye halaiki ya watu kama huyu mama anaweza kufungua mdomo wake kuu ongelea ufisadi hapa nchini..kwani nani asiyejua kwamba hata position aliyo nayo aliipata kutokana na baraka/utashi wa mafisadi? ambapo katika awamu hii ya kwanza inayoelekea ukingoni ni wao ndio walii-umba lakini mungu saidia hawako nayo tena?
 
My Take:
Tumekwisha. Nasubiri Rostam na EL nao wajitokeze kulaani mafisadi na kujitaja kuwa wanapigana na ufisadi kwa namna yao. Very soon.[/QUOTE]


Shujaa MM

Utabiri wako kwenye makala ''Vita ya ufisadi bado tete'' Tanzania Daima ya J5 23/sept/2009 umetimia. Ni makala elimishi na ni angalizo si kwa wapambanaji asili wa ufisadi ndani ya chama tawala pekee bali kwa vyama pinzani na watanzania wote.

Asante kwa makala hiyo.
 
nini kilitokea katika kikao cha kamati kuu ya mwisho ya CCM jamani, mbona sasa kila mtu anajifanya anapinga ufisadi..kuna ajenda gani ya siri..
1. mmeona makamba alipoenda kujikosha kwa sita kule Tabora
2. Mzee Msekwa na kuwasupport wapiganaji wa CCM....
3. Mzee ruksa nae kurusha dongo kwa mafisadi kule jimboni kwa kilango........
4. hata Sofia nae..??

nikweli tusubir EL, RA, Mkapa nao waje wakemee ufisadi.....

"Tanzania itajengwa na mafisadi.." TUSIDANGANYIKE...

EL nae alikua handeni jana akajikanyaga kanyaga hakudhubutu kutamka neno mafisadi ila aliwaambia watu wasiwasikilize wanaotaka kuwavuruga. Sijui ni kina nani hao wanaotaka kuwavuruga.
 
Huu ni unafiki ambao hauna mfano,kwanza hiyo billion moja ameshapewa tayari angejuaje kama wanahongwa hela zote hizo?pili alitumia hela nyingi sana kwenye uchaguzi wa m/kiti wa wanawake alipata wapi hela ya kuhonga Dodoma?
 
Teh teh teh hee......
Kumbukeni kwamba Ameyatamka haya akiwa KANISANI.
SHAME ON HER.
 
Sasa itabidi neno fisadi lipatiwe definition mpya. Vinginevyo mafisadi watakua ni kina nani?
 
Kwanza kwa silika yake Sofia hana ubavu kabisa ya kukataa billioni moja!Kimaadili ni fisadi.Sina shaka juu ya hili.Kuwepo kwenye serikali ya Kikwete ni ushahidi tosha kwamba yeye ni fisadi!Asiye fisadi hawezi kuwepo kwenye serikali ya CCM.Kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?Tusidnganyane bwana.

Serikali ya CCM inaelekea kuwa na mbinu mpya za kujifanya inapiga vita ufisadi wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.Hili ndilo analolifanya Sofia.Hata Bwana Makamba nae alifanya hivyo hivyo kwa kumfuata Sitta Tabora.Kule alitoa matamshi ambayo yalinishangaza sana.Eti yupo pamoja na Sitta kwenye vita dhidi ya ufisadi.Salalee.Kazi kweli.Makamba apige vita ufisadi, dunia si itapasuka.

Watu hawa wanatapatapa tu,wasubiri tu doomsday yao!

Sitamuonea haya fisadi hata aje na bilioni - Simba

27 September 2009
Majira
Na Gladness Theonest


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bibi Sophia Simba amesema hatamwonea haya fisadi yeyote hata aende na shilingi bilioni moja.

Pia waziri huyo amewataka wanawake wa Tanzania na Taifa kwa ujumla kumwombea kwa kuwa ni mwanamke pekee aliye katika nafasi ngumu ya kupambana na mafisadi nchini.

Bibi Simba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga Kongamano la Wanawake Waombolezao kitaifa, lililofanyika katika kanisa la Sinza Christiane Centre jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa fisadi yeyote asitarajie kwenda kwake kwa dhana potofu inayotafsiriwa na wengi kwamba wanawake ni dhaifu na kumpa rushwa ya bilioni moja akitegemea kuwa kesi dhidi yake itasitishwa isiende mahakamani, kwani atakuwa anajidanganya.

"Wanawake wenzangu nikiwa kama mwanamke na kulingana na wadhifa wangu wa kusimamia utawala bora nchini, sitamwonea haya fisadi yeyote hata aje na bilioni moja ili tuyamalize. Hilo kwangu halitawezekana kwani natetea maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla," alisema Bibi Simba.

Aliwatoa hofu wanawake nchini kuwa serikali inafanya kazi kwa nguvu zake zote katika masuala mbalimbali hasa la kupambana na mafisadi baada ya sheria ya Takukuru kufanyiwa marekebisho.

Amewataka wanawake wote nchini kuiga mfano wake, kwa kukataa kutoa rushwa sehemu ambazo wanatakiwa wapate haki zao kama hospitalini na mahakamani.

Waziri huyo aliwaonya viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa kuachana na tabia hiyo ili kulinda amani ya nchi hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi mkuu.

"Nawaasa wanawake nchini na taifa kwa ujumla kuwapuuza viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa na dini, bali nawaasa wafanye kazi ya kuongoza watu kiroho na masuala ya siasa waachie wanasiasa," alisema Bibi Simba.

Aidha amewataka wanawake nchini kutokubweteka kwa kutegemea maendeleo yatawafuata mahali walipo bali pale wanapoona kuwa serikali inatoa fursa ya mikopo kwa wanawake wawe mstari wa mbele kufuatilia nafasi hizo.

Naye Mchungaji wa Kanisa hilo, Godfrey Emmanuel alisema akina mama na Taifa kwa ujumla hawana budi kusimama imara katika maombi ili kuwaokoa vijana ambao wamechakaa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya.

Kongamano hilo liliwakusanya wanawake wapatao 200 kutoka katika mikoa 26 ya Tanzania bara na visiwani na wengine kutoka nchi jirani za Kenya, Uganda na Congo.

mwisho.

My Take:
Tumekwisha. Nasubiri Rostam na EL nao wajitokeze kulaani mafisadi na kujitaja kuwa wanapigana na ufisadi kwa namna yao. Very soon.
 
Back
Top Bottom