Sofia Simba naye ajitangaza kupambana na mafisadi

Aha aha kafulia huyo tia maji tia maji uchaguzi waja hana lolote,yeye c ndio mtetez wa mafisadi mwakani imekula kwenu
 
Ndugu MkuyuMkubwa,

Enzi za Mkapa to be honesty alikuwa alikuwa Dictator full hakupenda kuambiwa wala kukosolewa hukuona alivyo mfanyia Gen Ulimwengu, waambie watu wakupe full story yule bwana ni nyoka wa roho ngapi sijui na alituchabanga kweli pamoja na kuinua uchumi wetu ila mambo yake bwana ukiyapata utakoma mwenyewe we kwanini wanamtaka ajitokeze na kujibu tuhuma aone cha mtemakuni anajijua moto utamwakia mbaya tena kuanzia kwa waandishi wa habari, Democracy ndio imeanza kutokea kipindi hiki bali viongozi wetu hawajajua ni jinsi gani na ni namnagani kuliongoza hili taifa kwa alama za nyakati zilizopo na zijazo
 
Mimi nawashangaa mnaopinga sofia simba kusema anapambana na mafisadi. kwani hao waliojibatiza mgambo wa kupambana na ufisadi wamepata wapi uhalali wa kusema wanachukia ufisadi?....unahoji kwanini sofia simba aseme leo, alikuwa wapi? kwani akina Mwakyembe, Annae Killango, Olesendeka, Mengi na wenzao walikuwa wapi nchi yetu ikiuzwa na mkapa waone leo?

Huyu mama una mahusiano nae nn mkuu? By the way karibu JF! Hatusemi kaanza lini ila kwa matendo yake na jinsi alivyowatetea Rostam na Manji wakati wa sakata lao na Mengi leo akisema anapinga UFISADI kweli kama ni kuokaka basi yeye ni peponi tu! Lakini kama kweli kaokoka basi hayapinge yale aliyosema wakati Mengi alipotuhumu Mafisadi papa!
 
Huyu mama huwa anatia kichefuchefu ile mbaya kutokana na maneno yake ya mtaani uwanja wa fisi tena yasio na tbs,mie simo ati!!
 
Kweli inatisha, kumbe chaguzi zikikaribia watu wetu hawa huwa wanatufanya waajinga, walianza kina makamba walienda hadi kwa mama ake sita!!!Du
 
Huyu mama ni m-pambanaji na amedhamiria kupinga ufisadi kwa msio mjua mama Simba hanunuliki ni mtu wa msimamo na hateteleki.

Tatizo ili mtu awe mpinga ufisadi lazima awe na surname Mwakyembe, Selelii, Kilango, sendeka, kimaro et al. Mnaibinafsisha vita ya ufisadi kalabagho!

ulisha mgonga nini? Usitetee ujinga
 
Huyu mama ni kikaragosi cha mafisadi na hao ndio waliompa hela za kuhonga wakati wa uchaguzi wa wanawake wa CCM. Leo hii anakuja na gia mpya kuwa hawezi kuchukua MSHIKO toka kwa mafisadi wakati wafadhili wake wakuu kisiasa ni MAFISADI PAPA!! Hawa ndio mawaziri FAKE wa mkwere!!
 
Sofia ulikuwa wapi siku zote??????? mbona mnapenda kuwageuza watanzania kama hazimo kabisa na hizi comedy zenu??!!!!
 
Hivu huyu mama hana washauri??

Ukisoma huo utumbo aliouongea hapo kwa kweli utagundua kuwa aliamua kukurupuka tu bila kushauriwa hicho anachotaka kwenda kukiongea, na kama anao hao washauri basi na wao ni vilaza haswaa maana huwezi ukajisimamisha mbele ya umati wa watu ukaanza kujigamba kuwa MIMI SOFIA SIMBA NI MWANAMKE PEKEE AMBAYE NIPO KWENYE MAPAMBANO NA MAFISADI whats are talking about??

Huoni aibu we mama, do you know some calles ANE KILANGO MALECHELA?? nafikiri humfahamu so seat down then anza kucollect data ili umjua huyo Ane Kilango na ukishapata data zake na anapambana vipi na mafisadi urudi kwa wale waumini ukawaombe radhi kwa uongo wako uliowaongopea alafu pia uwaombe radhi viongozi wa dini kwa maneno mabovu uliyotoa juu yao. Wakuu wako tu wanahangaika kutafuta suluhu na hao viongozi wa dini then we unakurupuka kuwatolea maneno ya kashfa na vitisho.

Uongozi si kuimba TAARABU bwana inabidi uwe na kitu kinaita HEKIMA thats way kulikuwa na watu kama mfalme Suleyman.

Watch your steps unapotea mama
 
Tokea neno fisadi lishike hatamu hamna mtu aliyehukumiwa na kufungwa kwa ufisadi, kwa hiyo mimi naamini TZ hamna mafisadi na kama hamna mafisadi basi hii vita hewa na mafisadi ya nini???

sofia simba umechemsha mpaka maji yakaisha na sasa "umeunguza"
 
Kaazi kweli kweli.

Hii inakera na inatia hasira. Kwa mtaji huu wanatupoteza lengo, ni sawa na ujanja wa mijizi ambayo nasikia ikikimbizwa, akiona kafika kona na amepata upenyo mzuri, yeye pia huungana na wakimbizaji mwizi na kupiga kelele za 'mwizi, mwizi'.

Kama wamekosa la kusema bora wanyamaze.

TUSIDANGANYIKE!!!!!!!!!!!

Tiba
 
Huyu mama ni mnafiki kupita mfano....alipokuwa anawania hiyo nafasi ya uenyekiti alikuwa anatumia magari ya ofisi ya dr hosea kufanyia kampeni, pia alichukuwa pesa za kampeni zaidi ya milioni 200 just for uenyekiti wa uwt.... Hizo pesa alipewa na mfanyabiashara mmoja kwa sasa namuhifadhi ila ni mchaga...... Uongo mtupu...ukishaona nundu ya mwezio huwezi kujitoa
 
....Ahha!! Wakuu pengine neno 'MAFISADI' lina maana ya tofauti tunayo ijua sisi tuliyo wengi....otherwise towards 2010 we shall see lots of Sofia and the likes trying to test the Litmus paper....the funny thing is they all believe it will turn GREEN!!....
 
Lowassa naye alishaanza kuongea majukwaani kwenye harambee za makanisani. amewashauli makasisi kuachana na mambo eti ya siasa . Ameanzia kanisani tumsubili kwenye majukwaa maarufu ya kuomba kula mwakani. Kweli watanzania tumerogwa , mpaka tumesahau Richimond , mpaka ameanza kutuimbisha tena na masikio tumempa .
Mganga wake Lowassa alimwambia awe kivya kwa muda kadhaa tangu soo la Richimond . Watakuja zaidi ya sofia , mkapa kalamagi Rostam eti nao wanapinga ufisadi. mambo ya 2010 hayo tusubiri. lakini mimi nataka mabadiliko . Tujaribu chadema tuone wakina Richimond watakavyo haha kutafuta pa kujichimbia. mungu ibaliki Tz , wabaliki wapinga ufisadi waliojitokeza mapema hasa waliomwondosha lowassa na Wenzake.
 
Kweli Sofia ameisha kula nyingi mpaka bilion nzima inamaana hizo ndogo ndogo hazina shida . Je mmeo na kashifa za sukari , hukulapo nini? Funga safari nenda kapate ushauli huko Same Mashaliki . kwenye shingo mlimsafisha Mkapa . hata hivyo hakutakata labda mmuombe Mungu afe mapema ila siku zake zinahesabika , mpaka tujue ikulu ni sehemu gani. pa biashara au pakutoa huduma za jamii tena zenye utukufu. Ee mora tunusuru na majanga makubwa kupita yote , siku moja wakina karamagi , lowassa, Rostam ,mkapa, na wote waliomiliki meremeta, kagoda ,kiwira, wasurubiwe kama mwanawako . Ila si kwa mapenzi yako bali mapenzi ya watanzania wanaoteseka kwa kuishi maisha kama ya ahela kabla ya kifo chao . Amina
 
Back
Top Bottom